Thursday, March 3, 2011

ALEX KAJUMULO "BABU KAJU" MTANZANIA MWENYE MALENGO YA KUIKOMBOA BONGO FLEVA

Alex Kajumulo "Babu Kaju"
Babu Kaju akiwa na wasanii ndani ya studio yake
Na mwandishi wetu
Mwanaharakati wa siku nyingi katika masuala ya sanaa, michezo na  burudani  anaefahamika sana kwa jina la Alex Kajumulo a.k.a Kabu Kaju. Ameibuka na kusema kwamba kwa sasa ameamua kujikita sana katika kuikomboa sanaa ya muziki wa bongo kwa kua ameiona kama in aelekea kufa.
Babu Kaju aliyaseama haya wakati akifanya mahojiano maalum na mtoto wakitaa kwa njia ya simu  kutokea marekani anapoishi kwa sasa, babu Kaju alisema “ni muda mrefu sana tangu niondoke bongo (Tanzania) na nimekuwa nikifanya muziki huku nilipo (marekani) na nimekua nikiwasaidia baadhi ya wanamuziki lakini kwa sasa nataka nije bongo na kuwasaidi wanamuziki wote wa nyumbani kutokana kile nilichokiona kama muziki wa bongo unaeleke kufa hivyo mimi kama Mtanzania mwenye uchungu na snaa ya nchi yangu sina budi kurudi na kuikomboa”
Kwa sasa Babu Kaju ameshajiwekea mizizi nchini marekani kwani ameshafungua  studio ambayo ndio ipo kwa ajili ya kuindeleza harakati za sanaa. Pia Babu Kaju ni miongoni mwa wanaharakati wachache walioitoa mbali sanaa ya muziki bongo na hata michezo pia.
Kama utakumbuka kwa upande wa michezo  Kajumulo ndie alikuwa mtanzania wa kwanza kumiliki timu ya mpira wa miguu iliyokuwa inaitwa KAJUMULO FC ambayo kwa sasa inaitwa MORO UNITED baada ya kuiuza pia ndio mtanzania wa kwanza kuifadhili kwa kuipeleka timu ya taifa ya Tanzania kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Ghana
Wasanii waliopokelewa na kusaidiwa na Babu Kaju kwa namna moja ua nyingine walipofika nchini marekani ni pamoja na Mtoto wa dandu na Mr. II a.k.a Sugu
Babu Kaju natarajia kutua Nchini Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kutafuta wasanii watakao saini mkataba wa kufanya kazi na lebo yake ya Babu Kaju Record pia mwezi july Babu Kaju anatarajia kupiga shoo moja kali katika mji wa Kyela mkoani Mbeya. Shoo ambayo ni maalum kwa kuwasaidia wagonjwa wa Malaria.

No comments:

Post a Comment