Tuesday, January 29, 2013

MASUMBWI YALIYOFANYIKA TANDALE


Bondia Kalama Nyilawila kushoto akipambana na Athumani Pendeza wakati wa mpambano uliofanyika katika ukumbi wa CCM Tandale Dar es salaam jana Nyilawila alishinda kwa K,o raundi ya tatu

Bondia Hassan Mandula kushoto akimlushia makonde James Martini  wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Mandula alishinda kwa point

Bondia Charles Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Adam Ngange wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumb i wa CCM Tandale Dar es salaam jana Mashali alishinda kwa point.

Baazi ya wadau wa mchezo wa ngumi wakiwa na mabondia kutoka kushoto ni Kaike Silaju, Nassoro Choro,Selemani Kidunda, Thomas Mashali na Kibavu wakifatilia masumbwi
Picha zote na www.superedboxingcoach.blogspot.com

KICHUPA KIPYA KUTOKA KWA KEISHER FT DIAMOND - NIMECHOKA

MAHAKAMA YA MAPENZI - LINEX

Friday, January 25, 2013

KIJANA ISMAIL AFURAHIA KUHITIMU KIDATO CHA SITA TAMBAZA HIGH SCHOOL

Ismail akipozi na keki yake
Ismail (kushoto) akiwa na wahitimu wenzake
 Ismail (katikati) akiwa na Mama yake mzazi Naima Kilahama (kushoto) na mama yake mdogo Jamilah Kilahama

Friday, January 18, 2013

MPANGO MZIMA KUTOKA SULE'S INC & ENTERTAINMENT

Kama kawa kambi yetu ya maujuzi na mautundu + maujanja ya hapa taun iko pouwah na tuanaendelea kukimbiza mpaka kieleweke! wajanja wote wa tauni wanaijua hii kitu! 
SULE'S INC & ENTERTAINMENT The Home Of Creativity ndio sehemu pekee ya kupata haya mambo!

Thursday, January 17, 2013

BONDIA IDDY MNYEKE AJIFUA KUMKABILI SADIKI MOMBA FEBRUARY 14


Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu Ilala
BONDIA Iddy Mnyeke yupo katika maandalizi mazito ya kujiandaa na mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika  February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam
Bondia huyo kwa sasa ananolewa na kocha wa kimataifa wa Mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo wameweka kambi ili kumkabili Momba
Akizungumza Super D alisema kuwa amemwingiza kambini bondia wake ili aweze kumtengeneza vizuri kwa ajili ya mpambano wake na Sadiki Momba
Super D alisema kuwa mpambano huo utakuwa wa utangulizi kabla ya Deo Njiku na Omary Ramadhani kutwangana kugombea Ubingwa wa Taifa wa PST 
Kocha huyo alisema kuwa kambi yao itahakikisha inaendeleza ubabe baada ya bondia tegemeo wa kambi hiyo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kumdunda Saidi Mundi Kutoka Tanga
Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.
 michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.
 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

Monday, January 14, 2013

WANAFUNZI WA IFM WAMEANDAMANA MPAKA KWENYE OFISI ZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI.Wnafunzi wa chuo cha IF wakiwa wameandamana mpaka nje ya ofisi za mambo ya ndani kuwakilisha kero zao.

Wanafunzi ho wameandamana kwa kile walichodai kuwa wamechoka na uonevu wa muda mrefu kutoka kwa vibaka, hasa kwa waliopanga kigamboni, wamekua wakiporwa vitu vyao kama laptops na vingine vya thamani na mabinti kubakwa pindi warudipo katika hostel zao baada ya masomo ama nyakati za alfajiri wakiwahi chuoni.


HAWA MIKIDADI NDIO MISS MWENGE UNIVERSTY (MOSHI)


Hapa ni Miss & Mr Mwenge University

Sunday, January 13, 2013

MASHALI ALIVYOMGARAGAZA MKENYA

 
Bondia Bernad Mackoliech wa kenya na Mtanzania Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mchezo wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki Mashali alishinda kwa K,O raundi ya sita 

Bondia Mtanzania Thomas Mashali kushoto akiwa amemgalagaza bondia Bernad Mackoliech na kwenda chini akimsubili ili amwendelezee kipondo wakati wa mchezo wao wa kugombania ubingwa wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam na Mashali kuibuka na ushindi wa K,O katika raundi ya sita

Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamulu Thomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika mpambano huo wa ubingwa wa Afrika Mashariki

Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela akimvisha ubingwa wa Afrika Mashariki bondia Thomas Mashali baada ya kumpiga Bernad Mackoliech wa Kenya kwa K,O Raundi ya 6
picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, January 4, 2013

BONDIA LULU KAYAGE AJIANDAA KUMKABILI SALMA KIHOBWA WA MOROGORO


Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro

Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro

Bondia lulu Kayage 'kulia' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro 
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

ALIEPIGA PICHA NA LEMA HUKU AKIWA NA SARE ZA JESHI (JWT) ATIWA MBARONIYule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha Monduli ametiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari ila aliwahi kuwa JKT na akaacha, ila amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi wa Mererani wanamtambua kama mwanajeshi.
Maswali ya kujiuliza:
Inakuwaje raia anavaa nguo za jeshi kwa miaka mingi bila kuchukuliwa hatua, hayo mavazi kayapata wapi?
Je, Lema asingepiga picha naye angejulikanaje kuwa ni raia anavaa nguo za jeshi na kujitambulisha kama mwanajeshi?

Source:

Wednesday, January 2, 2013

BASATA WATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA SAJUKI

Yah: Salaam za Rambirambi
Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii wa tasnia ya filamu nchini Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki.
“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Sajuki ambaye mchango wake unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Tunaomba mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Imetolewa na
Ghonche materego
Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.KUTOKA NYUMBANI KWA SAJUKI (TABATA-BIMA) LEO MCHANA


Mke wa marehemu, Sajuki, Wastara Juma, akiwa mwenye simanzi kwa kumpoteza mumewe.

Bibi wa marehemu Sajuki akiwasili msibani leo.

 Baba mzazi  wa Sajuki akiwasiliana na ndugu na jamaa…
Sajuki amefariki dunia leo alfajiri akiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili ambapo alikuwa akitibiwa.

R.I.P SAJUKI, MUNGU AMKUPENDA ZAIDI (02.02.2013)


Sajuki, Enzi za Uhai wake

Leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.
Source: ITV Tanzania Facebook Page

SULE'S INC. & ENTERTAINMENT na Timu nzima ya Blog ya MTOTO WA KITAA tunatoa pole kwa Wastara Ndugu Jamaa na Familia Nzima Ya Sajuki.
...Allah Atawapa Wepesi Wa Mambo Insha'allah. 
...Inna Lillahi Waina Ilayh Rajiun. 

Tuesday, January 1, 2013

HARAKATI ZA KWENYE PANTONI USIKU WA LEO

Wwatu wakikimbilia kuingia kwenye pantoni 
Wadau wakiwa wametulia ndani ya pantoni
Uumati wa watu ukishuka kutoka kwenye pantoni upande wa posta wakitokea Kigamboni
Mtoto wa kitaa mwenyewe nilipata picha moko ndani ya Pantoni.
Picha hii imepigwa na Daniel Manupa