Saturday, October 30, 2010

WASANII WA BONGO WAOMBA UCHAGUZI MKUU KESHO UFANYKIE KWA AMANI.

JOHN KITIME : Ewe Mwenyezi Mungu, tunakuomba utuongoze katika uchaguzi huu mkuu tuwaepuke wale wagombea wote wenye dalili za uchochezi, tupate viongozi wema kwa manufaa ya taifa.
ISIHAKA KIBENE : Tunaomba Mungu atufanye tuwe na amani na utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi, tukubaliane na matokeo yoyote huku tukimchulia kiongozi atakayepita kuwa ndie baba yetu.
JACOB STEPHEN ‘JB’: Mungu baba tazama Tanzania yako, umeiwekea mkono wako wenye nguvu siku nyingi na kuonekana ni kisiwa cha amani. Unapozungumzia amani duniani Tanzania ni mfano wake, bariki uchaguzi mkuu huu amani iendelee kutawala, shetani asipate nafasi. Ninaomba katika jina la yesu kristo Amen.
PRINCE MUUMIN MWINJUMA : Ewe Mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi, naamini wewe ndiye unayepaswa kuabudiwa kwa haki na kuombwa mazuri na mabaya, nami naomba kwako mazuri kwa niaba ya Watanzania wote. Tunakuomba utujaalie amani, utulivu na upendo wa kweli baina yetu wakati huu tukielekea kwenye uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi pia, ewe Mola tunakuomba tutilie wepesi kutakapokuwa na ugumu. Amin.
SAID FELLA : sisi vijana tujitokeze tukapiga kura kumchagua kiongozi atakayetufaa, Mungu atuongoze tuishi kwa amani hata baada ya uchaguzi, na hao waangalizi wa Kimataifa waliokuja wakae na kuondoka kwa amani.
STEVEN KANUMBA : Amani ni jambo tunalotakiwa kulienzi na kulikumbatia mno katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu kwani shetani huwa hachezi mbali, Mungu ibariki nchi yangu. Amen.
Baada ya wadau kusema hayo kila mtu yamemwingia barabara akilini na nahisi sina cha kuongeza zaidi ya kuungana nao kuuombea uchaguzi wetu uwe huru wa haki na uliojaa amani ili tuendelee kuishi salama hata baada ya matokeo ya kura zetu.
IRENE UWOYA : Tudumishe amani tuliyoachiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika kipindi hiki cha uchaguzi jamani na hata hapo baadaye.
20%: Naiombea Tanzania isimwage damu, ndio maana siku ya uchaguzi naenda kupigia kura nyumbani Kimanzichana kusikokuwa na vurugu, lakini wapiga kura muwe na maamuzi sahihi.
LADY JAYDEE : Mungu ibariki Tanzania na Watanzania wote, uchaguzi wa viongozi uende kwa amani na upendo, kadhalika nawakaribisha wote Thai Village, Masaki jioni ya Jumapili ya uchaguzi kuburudika na Machozi Band.
MZEE YUSSUF ‘Mfalme’: Mungu alete kheri katika uchaguzi wetu, uwe ni uchaguzi huru wenye haki, amani na maelewano kwetu sote. Amin.
AFANDE SELE : Mungu wetu muweza wa yote, awape mioyo safi viongozi wa tume ya uchaguzi ili wasimame katika haki kwa kumtangaza mshindi aliyechaguliwa na wengi kihalali.

Sababu sauti ya wengi ndiyo sauti ya Mungu mwenyewe, atusimamie Watanzania tuweze kuvumiliana baada ya uchaguzi kwa kuheshimu matokeo yatakayozingatia haki na ukweli ili amani ya taifa letu iendelee kudumu.

Nasema hivi kwa sababu historia inaonyesha kwamba katika nchi nyingi barani Afrika amani yake huvunjika wakati wa uchaguzi kwa kutotenda haki dhidi ya chaguo la wapiga kura mfano; Kenya, Zimbabwe na kwingineko.

Mungu wetu ni Mungu wa haki na pasipokuwa na haki, ataliacha taifa mikononi mwa shetani ambaye ndiye baba wa machafuko. Vilio, vita na mabalaa yote yataivamia nchi yetu pendwa.
Wote hawa kesho watapiga kura huku kila mmoja akimchagua yule nayeona anafaa kushika hatamu ya nchi.Hayo ndiyo maoni ya wasanii wa hapa Bongo hivyo ni jukumu letu Watanzania wote kufanya uchaguzi wa amani usioangalia udini na ukabila kwani Amani tuliyonayo Tanzania ni tamu sanaaaaa ilinde ikulinde. Wanausalama nao wako makini hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kulina amani yake fuata maelekezo ya uchaguzi, usijionyeshe unashabikia chama gani usivae wala kujinakshi kwa rangi za chama fulani washawasa atafanya kazi yake.
Fanya fujo uone kama hutoleta ubazazi kamwe dhahmayoyote haitokukuta. 

WAISLAMU WAOMBEA DUA UCHAGUZI MKUU T.Z .2010.


Mkuu wa Chuo cha Alnnajah cha Sheria za Kiislam Sheikh. Fahmi Lubwaza akizungumza wakati wa duwa ya kuombea uchaguzi mkuu katika msikiti wa Ilala Kota Dar es salaam
Ustaadhi akisoma wasiilat shaafi

CCM YAHITIMISHA KAPENI ZAKE LEO KI HIVI.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM,Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani leo kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwahutubia wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi waliofurika katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar leo wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni za chama hicho.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwa wanaCCM kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni hii.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viweanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani leo.
Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika katika viwanja Jangwani kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM iliyofanyika jioni hii.

DR JAKAYA KIKWETE AHUBIRI AMANI NA KUWAONYA WATANZANIA WANAOENDEKEZA NA KUKUMBATIA UDINI!!

Jakaya Kikwete akiongea katika mkutano wake na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Anatouglou jijini Dar ambapo alihojiwa maswali mbalimbali juu ya mustakabali wa nchi endapo atachaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu nyingine Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unafanyika Kesho Oktoba 31 nchini kote. Katika mahojiano hayo RaisDr. Jakaya Kikwete amewatahadhalisha watanzania kufanya maamuzi pasipo kuhubiri wala kuzingatia udini kwani kuzungumzia udini ni hatari na ni jambo litakaloigawa nchi kwa kiwango kikubwa na hakuna wa kutuokoa kwani hatuna pa kukimbilia kwakuwa nchi hii ni yetu hivyo tunatakiwa kuilinda na kuiheshimu ili tuishi kwa amani (Picha na Ankal Issa Michuzi)
Jakaya Kikwete na mgombea mwenza Dr Mohamed Gharib Bilali wakiondoka ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar baada ya kuongea na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo.
Wahudhuriaji wakimsikiliza JK kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar usiku usiku wa kuamkia leo
Wahudhuriaji wakimsikiliza Jakaya Kikwete kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar usiku usiku wa kuamkia leo
Wahudhuriaji wakimsikiliza Jakaya Kikwete kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu akimuamkia Dk. Mohamed Ghalib Bilali kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jakaya Kikwete na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Jakaya Kikwete akiwashukuru watangazaji wa TV mbalimbali waliokuwa wakimhoji kwenye mkutano na waandishi usiku huo kwenye ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Jakaya Kikwete akisalimiana na waandishi na wageni waalikwa kwenye mkutano wake na waandishi ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Hassan Mhelela wa BBC London akimhoji mgombea mwenza wa urais Tanzania bara Dk. Mohamed Gharib Bilal baada ya mkutano wa JK na waandishi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar
Hassan Mhelela wa BBC London akimhoji Makamu Mwenyekiti wa CCM Mh. Pius Msekwa baada ya mkutano wa JK na waandishi wa habari
Fundi mitambo mkuu wa Clouds TV Mehboub al Hadad akiwa kazini ambapo kituo hicho kiliungana na vingine kurusha mkutano wa JK na waandishi live
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza JK akijibu maswali usiku wa kuamkia loe katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar

KIKWETE AZUNGUMZIA SUALA LA MADINI.Hapo juu ni sehemu tu ya mahojiano aliyoyafanya Mgombea Urais kwa chama cha CCM,Dk Jakaya Kikwete usiku usiku wa jana (ijumaa 29/10/2010), kilichohusu suala la madini,Jk ameyasema hayo LIVE alipokuwa akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari ndani ya ukumbi wa Anatoglo,jijini Dar.

JK AFAFANUA SUALA LA AFYA KWA WATANZANIA

Thursday, October 28, 2010

The African artists have represented to the fullest. Rockstar 4000

 Ally Kiba akiwa kwenye pozi, habari nilizozipata ni kwamba Kiba anafanya vizuri na watu wameipenda sauti yake, mungu akujalie ndugu yangu uyafikie malengo.

Navio kutoka Uganda.

Amani kutoka Nairobi-Kenya

2 Face kutoka Nigeria.
 Ally Kiba akipigwa msasa kwenye kinanda na msanii kutoka Nigeria 2Face Idibia

Habari nilizozipata jana wasanii hawa walimaliza kurekodi wimbo huo wa Africa na sasa kilichobaki ni kuanza kushoot video hiyo, kama ulivyoona picha za juu wakiwa kwenye location tofauti tofauti.

Ally Kiba na wasanii wenzake wakiwa kwenye location wakifanya video hiyo.

ILIVYOKUWA KWENYE MKUTONO WA CHADEMA JANA JIJINI ARUSHA.

Umati Mkubwa wa watu uliofurika katika Viwanja vya NMC Arusha jana ukisikiliza Sera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA zilizokuwa zinatolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa (hayupo pichani) Bw, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Hai alipokuwa amelitembelea Jimbo la Arusha Mjini ili kuhamasisha kampeni za Chama chake wakati huu ambapo zimebakia siku chache kabla ya kupigwa kura za Uraisi, Ubunge na Udiwani Nchi nzima hapo Oktoba 31. katika Mkutano huo Mgombea wa nafasi ya Ubunge kwa Jimbo la Arusha Mjini Bw, Godbless Lema pamoja na Madiwani wote wa Chama hicho walipata nafasi ya kunadi Sera na kuomba kura
Wananchi wengi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Pamoja wa Mgombea Ubunge Jimbo la Hai na Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini wanaonekana wakiitikia Sera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati wakisikiliza hutuba iliyokuwa inatolewa na Mwenyekiti wa Chama hichoTaifa Bw, Freeman Mbowe
Umati mkubwa wa watu ukiwasindikiza wagombea Ubunge kwa Majimbo ya Hai na Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakati walipokuwa wanaondoka katika Viwanja vya NMC Arusha jana baada ya kumaliza kuhutubia - Picha zote kwa Hisani ya Arusha Mambo.

REGGAE CONCERT IN DAR ES SALAAM (29TH OCT 2010)

I-Noch brings you the Live performance “Explosive Zion “ a Reggae Live concert with Zanz-B from Jamaica supported by local Ragga , Raggae and Dance Hall artists .

Performances from
Jhikoman and Afrikabisa Band, Saganda and Hardmad accompanied with “Zemkala Band”                                          
Venue: Makumbusho Cultural Center Date: 29th October 2010 Time : 7pm till dawn.
 
"Tickets Available at the Gate."

Tuesday, October 19, 2010

ZITTO KABWE AFANYA HARAMBEE SUMBAWANGA

Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe akiendesha harambee ya kumchangia fedha za kuweka mawakala wa mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Mwalimu Norbart Yamsebo (chadema) ,katiba harambee hiyo zaidi ya shilingi 800,000 zilipatikana huku yeye Kabwe akiuza kwa manadi kombati yake iliyonunuliwa kwa shilingi 200,000
Bw Zitto Kabwe akiendesha harambee ya kumchangia fedha za kuweka mawakala wa mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Mwalimu Norbart Yamsebo (chadema) Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe( kulia) akisaidia kuhesabu fedha zilizochangwa jana katika viwanja vya mkutano wa kapeni vya Sumbawanga mjini wakati wa kampeni zake
Maelfu ya wananchi wa jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa wakimsikiliza naiu katibu mkuu Taifa wa Chadema Zitto kabwe wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo Mwalimu Norbart Yamsebo ( Chadema) katika kampeni zake mkoani Rukwa jana Askari polisi ,magereza na mgambo wakilinda mkutano wa kampeni za Chadema ambao alikuwa akihutubia naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe jana viwanja vya Sumbawanga mjini Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe (kulia) akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa Mwalimu Norbart Yamsebo jana wakati wa kampeni za Chadema mjini Sumbawanga. Picha zote na Francis G