b..

B1

Wynem

animation

Friday, July 31, 2015

NGUMI KUPIGWA TENA VIJANA KINONDONI SEPTEMBA 6


B0NDIA Mbena Rajabu atapanda tena uringoni kuzidunda na Twaribu Mchanjo mpambano utakaofanyika Septemba 6 katika ukumbi waVijana Kinondoni kugombania ubingwa wa Taifa wa uzito wa kg 57

mpambano uho unaoratibiwa na Ibrahimu Kamwe utakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yatakayowakutanisha mabondia mbalimbali nchini ambapo bondia Abdallah Pazi atazidunda na Ambokile Chusa na Georger Alen wa Muheza Tanga atazipiga na Mwinyi Mmzengela  wakati Epson John wa Morogoro atazidunda na Mohamed Alkaida 

Kamwe aliongeza kwa kusema mpambano uho ameuandaa kwa kuakikisha wanakuwa na mabondia wengi ambao watakuwa mabingwa na kuwakilisha nchi katika mapambano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar, Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez, Mike Tyson, Mohamed Ali, Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

BASATA YAMFUNGIA SHILOLE KUJISHUGHULISHA NA KAZI ZA SANAA KWA MUDA WA MWAKA MMOJA

Mmoja kati ya matukio ya aibu aliyoyafanya, Shilole,alipokuwa nchini Ubelgini



Friday, July 24, 2015

UANDIKISHAJI WA BVR KAWE WAENDELEA VIZURI

Msimamzi wa uandikishaji (BVR) katika kituo cha kawe mzimuni -shule ya msingi, Prisca Haule akimuelekeza mmoja wa wakazi wa kawe jinsi ya kukaa vizuri ili kupiga picha kwa ajili ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura. Zoezi hili la uandikishaji linaendelea katika maeneo yote ya jiji la Dar.
Mkazi wa kawe, Godfrey Matali akijiandikisha katika hatua za awali katika uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Baadhi ya wakazi wa Kawe wakiwa katika mstari wa kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura. Kituo hiki kinasimamiwa na ndugu Ally  kwa kushirikiana na Prisca Haule, Utulivu upo wa kutosha na kazi inasonga vizuri. 
Picha zote na Mpigapicha Wetu

Tuesday, July 21, 2015

MISS KILIMANJARO AMBASSADOR YATOA MSAADA KWA FAMILIA ZA VIJIJI VYA RAU NA URU

Mkurugenzi wa Shindano la Miss Kiliamnjaro AmbassadorJackline Chuwa akikabidhi msaadawa nguo na viatu kwa wakazi wa vijiji vya Ulu na Rau vilivyopo karibu na mji wa Moshi kwaudhamini wa kampuni ya Dream for Life iliyopo mkoani Kilimanjaro.
Warembo wa Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 wakiangalia wenzao wanaochuana katika mchezo wa kuvuta kamba,kukimbia na kucheza muziki,ambapo warembo hao waliwashinda wafanyakazi wa Dream for Life.
Washiriki wa Miss kilimanjaro 2015 wakiwa na baadhi ya watoto wa Uru na Rau Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro
Warembo wanaowania taji la Miss Kilimanjaro Ambassador 2015 wakishindana kuvuta kamba na Wafanyakazi wa kampuni ya Dream for life.

Friday, July 10, 2015

WANANCHI TUMIENI OFISI ZA NACTE MIKOANI

Dkt.Nkwera


Na Mwandishi Wetu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi – NACTE imefungua ofisi tano za kanda ikiwa ni sehemu ya mkakati wa wizara ya kuwekeza katika eneo la usimamizi wa sekta ya elimu nchini ili kuongeza ufanisi na kufikia matokeo makubwa sasa (BRN).

Ofizi hizo na makao yake makuu kwenye mabano ni Kanda ya Kaskazini (Arusha), Kanda ya Ziwa (Mwanza),   Kanda ya Kusini (Mbeya), Kanda ya Kati (Dodoma) na Zanzibar.

Akizingumza na mwandishi maalum wa habari hii JIJINI Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Primus Nkwera amesema kuanzishwa kwa kanda hizo ni wazi kutaongeza ufanisi na usimamazi wa elimu ya ufundi nchini ambayo ukuaji wake umekuwa ni wa kasi.

Dkt.Nkwera amesema serikali inatambua uhitaji na mchango wa elimu ya ufundi katika kutoa fursa kwa vijana kupata mafunzo ya stadi za kazi kwenye fani mbalimbali na hivyo kuwezesha upatikanaji wa nguvu kazi inayohitajika na kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri.

Amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaendelea kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya kuhakikisha ubora wa elimu nchini unasimamiwa vema na unalindwa hiyo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na watoa huduma kwenye sekta ya elimu wasiokuwa makini

“Tumeanzisha ofisi hizi za kanda ili kuwa karibu na wadau ikiwemo wananchi na watoa elimu ya ufundi tukiamini kuwa usimamizi wa karibu utasaidia kulinda hadhi na ubora wa elimu ya ufundi na pia kuwa na mfumo wenye kutoa majawabu ya haraka na kwa wakati ya changamoto pale zinapojitokeza.”Alisema Dkt.Nkwera

‘Ni shabaha ya serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha viwango vya ubora wa elimu yetu katika ngazi mbalimbali unakuwa imara na wenye kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kujiajiri ili kuiwezesha sekta ya elimu kuendelea kutoa mchango uanokusudiwa kwenye manedleoe ya kiuchumi na kijamii kupitia rasilimali watu. Kwetu sisi hili ni jambo la msingi na ambalo tutaendelea kuwekeza humo kulinda elimu yetu.”Aliongeza Dkt.Nkwera.

Dkt. Nkwera amesema pamoja na wizara kuwa na shabaha yake katika kuanzisha ofisi hizo za kanda za NACTE ofisi hizo zitachangia pia kutatua changamoto kadhaa ambazo wananchi wamekuwa wakikabiliana nazo katika kufikia huduma kutokana na kukosekana kwa ofisi mikoani.

Amesema utamaduni wa kutegemea ofisi zilizopo makao makuu Dar es salaam unapaswa kurekebishwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma katika sekta ya elimu kwa ukaribu zaidi jambo ambalo litawapunguzia pia gharama 

“Wizara inatambua ,kuwa mahitaji ya wananchi kwenye taasisi za elimu ni kubwa na hivyo itaendelea kuhamasisha taasisi zilizo chini yake kuwa na ofisi za kanda ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa huduma.”Alisema Dkt. Nkwera

Katika hatua nyengine, Dkt. Nkwera ameaigiza kuwa ofisi hizo za kanda za NACTE zitumike pia kuwahudumia wadau wa elimu ya juu ikiwemo wanafuzni wa elimu ya juu wakati Tume ya Vyuo Vikuu – TCU nayo inapojipanga kuanzisha ofisi za kanda.

Amesema wale wote wanaohitaji msaada na huduma  za Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) ikiwemo suala la uombaji udahili n.k wanaweza kufika kwenye ofisi za Kanda za NACTE ili kupata msaada wanaouhitaji badala ya kusafiri kwenda Dar es salaam zilipo ofisi za TCU

“Nataka wakati huu ambapo TCU inajipanga na yenyewe kuwa na ofisi mikoani, ofisi hizi za kanda za NACTE zitumike pia kuhudumia wanafunzi wa vyuo vikuu na wa taasisi za elimu ya juu nchini ikiwemo uombaji wa nafasi za kujiunga na vyuo na shughuli nyengine za TCU. Ni imani yangu kwamba agizo hili litafanyiwa kazi ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa muda na wa gharama wanaolazimika kufuata huduma za TCU Dar es salaam.”Alisema 

Dkt. Nkwera amewataka wakuu walioteuliwa kuongoza ofisi hizo kuhakikisha wanawatumikia wananchi na wadau kwa uadilifu ili lengo la Wizara la kuwa karibu na wananchi liweze kutimia na kutoa tija inayokusudiwa.