Wednesday, July 28, 2010

KALALE PEMA MPENDWA WETU PRIMITIVA

PRIMITIVA PANKRASI

Aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Primtiva Pankrasi, amefariki dunia juzi mchana katika hospitali ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya kawaida ‘Check up’ kama kliniki ya ujauizito.
Imeelezwa kuwa Primtiva kabla ya kufikwa na mauti alipatwa na presha ya ghafla na kupoteza uhai wakati madaktari wakihangaika kunusuru maisha yake lakini haikuwa bahati kwani sisi tulimpenda sana lakini mungu alimpenda zaidi.
Primitiva anataraiwa kuzikwa kesho jioni majira ya saa kumi katika makaburi ya kinondono.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPOONI - AAAMEN.