Monday, August 21, 2017

RAIS JOHN MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA JCA NA BALOZI WA JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

NSSF YATOA MKOPO WA BILIONI 8.9 KUFUFUA KIWANDA CHA USINDIKAJI WA NAFAKA MWANZA

Mwanza, Agosti 20, 2017: Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa mkopo wa Tshs bilioni 8.99 kwenda kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ya Tanzania kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji wa nafaka katika jiji la Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za mfuko huo kutekeleza kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda hapa nchini.

Mkopo huo unalenga kuiwezesha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuweza kuvifufua vinu vyake viwili vya usindikaji wa mazao ya mpunga na mahindi vilivyopo mkoani humo kwa  kununua vifaa na mitambo mipya na hatimaye kuanza uzalishaji baada ya kusimamisha uzalishaji huo mapema miaka ya 1990.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya hundi ya mkopo huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alitoa wito kwa Wizara yenye dhamana ya kulimo hapa nchini kuisimamia vyema bodi hiyo kiutendaji ili iweze kuijendesha kwa ufanisi utakaoiwezesha kurejesha mkopo huo unaotarajiwa kulipwa ndani ya kipindi cha miaka sita (6) ikijumlisha kipindi cha mpito yaani (grace period) ya mwaka mmoja. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (wa pili kushoto) Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia) ikiwa ni mkopo kutoka Shirika hilo kwenda bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji wa nafaka kilichopo jijini Mwanza. 

"Mbali na Wizara yenye dhamana ya kilimo, pia niwaombe sana uongozi wa mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa mkoa kutambua kuwa ufanisi wa kiwanda hiki unategemea sana uwepo wa malighafi ya kutosha hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha uwiano kati ya uzalishaji wa malighafi na uzalishaji wa kiwanda vinakwenda sambamba,'' alisisitiza. 

Alilipongeza Shirika la NSSF  kwa uwekezaji wa viwanda vyenye tija kiuchumi ndani ya muda mfupi ambapo kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita hadi sasa shirika hilo limewekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kiwanda cha kutengeneza viuadudu vya kuua vimelea vya mbu kiitwacho Tanzania Biolarvicide Limited kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.

"Uwekezaji wa NSSF pia unaonekana kwenye bodi ya nafaka na Mazao mchanganyiko ya Tanzania, Mkoani Dodoma, viwanda vipya vya kuzalisha sukari Mkulazi, mkoani Morogoro, kiwanda cha chaki Maswa (Maswa Chalk & General Enterprises) ambacho kipo Simiyu...hongereni sana!'' alipongeza. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa hundi hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba (kushoto) huku wadau wengine wakishuhudia.

Waziri Mhagama alitumia wasaa huo pia kuwataka  waajiri wasiolipa michango ya wanachama kuwasilisha michango hiyo kwa wakati na kwa usahihi kwani  kutofanya hivyo ni kosa kisheria na  kuanwanyima haki wanachama hao huku akisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wale wasiotekeleza sharia hiyo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alimuhakikishia Waziri Mhagama kuwa mbali na kuisimamia kwa ukaribu bodi hiyo ili iweze kurejesha mkopo huo, wizara yake imejipanga kuhakikisha kwamba miradi yote ya kilimo inayohusisha uwekezaji kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini inasimamiwa kwa umakini, ufanisi na weledi mkubwa ili kulinda pesa ya wanachama wa mifuko hiyo.

"Kwa kutambua kwamba ufanisi wa viwanda hivi unategemea zaidi kilimo kuna mipango na mikakati mizuri kuhakikisha mnyororo wa thamani unaohusika kuzalisha malighafi za viwanda hivi haukatiki,'' alisema Waziri Tizeba.
Kabla ya makabidhiano hayo Waziri Mhagama alipata wasaa kukugua mitambo ya kinu cha kukoboa mchele kinachotarajiwa kufufuliwa kupitia mkopo huo ambapo Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (mbele) alimuhakikishia Waziri Mhagama na wadau wengine kuwa kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutawezesha jumla ya tani 96 za mchele kukobolewa kwa siku kupitia kinu hicho.

Alitaja baadhi ya mipango na mikakati hiyo kuwa ni pamoja na ujio wa Mpango maalumu wa kuandaa mbegu bora unaotekelezwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Bill Gates. Alikili kuwa kwasasa taifa linakabiliwa na uhaba wa mbegu bora unaotakona na utegemezi wa mbegu hizo kutoka nje ya nchi huku taifa likizalisha asilimia 35 tu ya mbegu hizo.

Waziri Tizeba alitumia fursa hiyo kutangaza uamuzi wa serikali kutoa bei elekezi kwenye pembejeo za mbolea ili kudhibiti uuzwaji kwa bei holela wa bidhaa hiyo muhimu ambapo kila mfanyabiashara alikuwa akiuza bidhaa hiyo kwa bei inayotokana na utashi wake.

"Mbolea zinahusika ni zile za kukuzia na kupandia yaani UREA na DAP ambapo kuanzia leo bei elekezi itakuwa inatangazwa kulingana na maeneo husika. Tunataraji kuwa uwepo wa bei elekezi utasaidia kupunguza bei ya mbolea hususani ya UREA kwa asilimia  zaidi ya 15 kwa mfuko,'' alisema.
Hatimaye hundi hiyo ikafika kwa Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (wa tatu kushoto). Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba (wa pili kushoto), Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw. Stanislaus Mabula (katikati) na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia).

 Alitolea mfano kuwa katika baadhi ya mikoa bei ya mbolea ilifika hadi Sh. 100,000 lakini chini ya mfumo wa bei elekezi haitazidi sh. 56,000 kwa mfuko huku maeneo mengine ikiwa chini zaidi ya bei hiyo.

Mapema, akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara alisema kuwa mbali na lengo la kutunza thamani ya michango ya wanachama, uwekezaji unaofanywa na shirika hilo pia unalenga kuchochea ukuaji wa shughuli mbali mbali za uchumi na kijamii ambazo pia huongeza ajira, kipato na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania walio wengi na mwishowe kuongeza wanachama wa mfuko.

"Mkopo huu utapelekea kufufua kiwanda ambacho kitaleta ajira Zaidi ya 340 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 23,000 ambazo hazitakuwa za moja kwa moja.Hii itachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na pia kuongezeka kwa wanachama wa Mfuko,'' alibainisha. 
Muonekano wa sehemu ya mitambo ya kiwanda hicho cha kukobolea mchele kilichopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza. 

Prof.Kahayrara alisisitiza kuwa Uwekezaji huo unafanywa kwa  kuzingatia Sera ya Uwekezaji ya Shirika na Mwongozo wa Uwekezaji kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii unaotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kushirikiana na Mdhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Akitoa taarifa za kiwanda hicho,Mtendaji mkuu wa  bodi ya nafaka  na mazao mchanganyiko ndugu  John Maige alisema  mkopo huu utaongeza kiwango cha usagaji wa mahindi hadi kufikia tani 250 kwa  siku na ukoboaji wa tani 96 za mchele kwa siku pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa vyakula vya mifugo kwa Masoko ya ndani na nje ya nchi.

 "Mkopo huu pia utawezesha kuwepo kwa soko la uhakika kwa wakulima wa mahindi na mpunga hapa nchi na nitumie fursa hii kuipongeza serikali kwa hatua ya kuzuia usafirishaji wa mazao ghafi nje ya nchi.'' alipongeza Maige huku akiongeza shukrani zake kwa Mfuko wa NSSF kwa uamuzi wa kuwekeza kwenye kufufua kiwanda hicho.
Na huu ndio muonekano wa kiwanda hicho kwa nje.
Na hapa ndipo kitakapojengwa kinu cha kusagia mahindi! Baada ya kukagua kinu cha kukobolea mpunga Waziri Mhagama na wadau wengine walipata wasaa wa kutembelea eneo lingine la kiwanda hicho ambapo kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige ndipo kitakapojengwa kinu cha kusagia mahindi chenye uwezo kusaga mahindi hadi kufikia tani 250 kwa siku. 
Ukafika wasaa wa kufafanua mradi huo. Kwa mujibu wa Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (aliesimama)mkopo huu utaongeza kiwango cha usagaji wa mahindi hadi kufikia tani 250 kwa siku na ukoboaji wa tani 96 za mchele kwa siku pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa vyakula vya mifugo kwa Masoko ya ndani na nje ya nchi. Vinu hivyo vinavyofufuliwa kwa mkopo wa NSSF vilisimamisha uzalishaji wake tangu mapema miaka ya 1990 baada ya kushindwa kujiendesha.
Ikawa ni pongezi tu kwa NSSF na Serikali kwa kufanya kile kilichoshindikana kwa miongo ya miaka!Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw Stanislaus Mabula akitoa shukrani zake kwa naiba ya wananchi wa jimbo hilo pamoja na wakazi wa Mwanza kwa ujumla. Pamoja na faida nyingine nyingi, kufufuliwa kwa kiwanda hicho kunatajwa kuwa kutazalisha ajira zaidi ya 340 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 23,000 ambazo hazitakuwa za moja kwa moja.

Sunday, August 20, 2017

BONDIA SELEMANI SIMBA HAPANIA KUTOA KICHAPO KWA MABONDIA KUANZIA AGOST 26 VIJANA


Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa ngumi za kulipwa kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' amendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya mpambano wake wa Agost 26 utakaofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni ambapo atapambana na Kallage Ramadhani bondia anaenolewa na kocha mkongwe katika ngumi Rajabu Mkamba

Akizungumzia mpambano wake Simba amesema kuwa amekuja Dar kwa ajiri ya kupambana na kuwapiga mabondia wote watakaopambana nae wakati wowote ule bondia huyo mpaka sasa kashapigana mapambano mawili kati ya hayo mawili kashinda moja na kudundwa moja

akizungumzia matarajio yake katika masumbwi amesema anatamani kufika mbali zaidi kama Ibrahimu Class 'King Class Mawe' walivyofanikiwa kufika mbali na mpaka sasa kuwa bingwa wa Dunia

katika mpamano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya ubingwa kati ya bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'  na Baina Mazola 'Simba Mazola'
mapambano mengine ya siku hiyo ni sajo bosco Jr atakumbana na juma rashidi mdobi na Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile:-

Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez, Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi

Monday, August 14, 2017

Roma - Zimbabwe [Official Music VIdeo]

RAIS WA MISRI AWASILI NCHINI LEO KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi akishuka kwenye ndege yake baada ya kuwasili nchini mchana huu, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Misri Mhe. Abdel Fattah el-Sisi akisalimiana na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili nchini hivi punde kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake,  Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere, Jijini Dar es salaam mchana huu, ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili Agosti 14-15, 2017.