Thursday, September 15, 2016

Alikiba kutumbuiza Tuzo za MTV Mama Okt. 22

Mwandishi Wetu
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Salehe ‘Alikiba’, ametajwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza wakati wa utoaji tuzo za MTV Mama zitakazofanyika Oktoba 22, mwaka huu Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Meneja wa msanii huyo, Seven Mosha, msanii huyo amechaguliwa kufanya shoo hiyo pamoja na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali Afrika na Ulaya. 
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome jijini humo ambapo wasanii wengine watakaotumbuiza ni Yemi Alade, Nasty C, Babes Wodumo na wengine wengi. 
Kwa mwaka huu tuzo hizo zina vipengele 18 ambavyo wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika watawania.

Tuzo hizo kwa mara ya kwanza zilifanyika 2008 na zimekuwa na mafanikio makubwa kutokana na wasanii wanaopata tuzo hizo kuwa na vipaji vya kipekee na hadi sasa waandaaji wa tuzo hizo wanatambua vipaji 2Face Idibia, Big Nuz, Cassper Nyovest, Davido, D'Banj, Flavour, Fally Ipupa, Mafikizolo, Lira, Nameless, Lupita Nyong'o, Clarence Peters, Diamond Platnumz, P-Square, Tiwa Savage, Cabo Scoop, Yemi Alade na wengineo.