Monday, April 29, 2013

EXTRA BONGO YAZIDI KUWABAMBA MASHABIKI NDANI YA MEEDA SINZA JANA USIKU

Mkurugenzi wa Extra bongo Ally Choki akiimba mbele ya mashabiki wake (Hawapo Pichani) ndani ya Ukumbi wa Meeda sinza jana Usiku wakati bendi yake ilipokuwa ikiburudisha pande pande hizo
Kushoto ni mmoja wa marapa bora wa muziki wa dansi Totoo Ze Bingwa akirap ndani ya Meeda sinza wakati Bendi anayopigia mzigo Extra Bongo ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo na kulia ni Banza Stone a.k.a Generale akimpa big up.
Rapa bora wa Extra bongo Kabatano (Kulia) akigani moja ya jimbo zao bora huku akipewa sapoti na nguli wa muziki wa dansi Banza Stone mwana masanja wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza maeneo ya Sinza katika ukumbi wa Meeda jana usiku.
Wakata nyonga maarufu kwa sasa wa Extra bongo wakiongozwa na nyamwela wakiwapagawisha mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Meeda Sinza jana usiku

MBUNGE WA ARUSHA MJINI, GODBLESS LEMA APANDISHWA KIZIMBANI LEO

Wednesday, April 24, 2013

SHABANI MHAMILA 'STAR BOY' AJIFUA KUMKABLILI JIBABA MEI MOSI


Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Chalo Issa wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya ngumi Ilala Star Boy ana jiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba uatakaofanyika mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba .

Bondia Shabani Mhamila 'Star Boy' kushoto akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' mabondia wote wanajiandaa kwa ajili ya mashindano yatakayofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba 

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Shabani Mhamila 'Star Boy'  katika kambi ya Ilala iliyopo Amana CCM jana Sta Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Picha Zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu
BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' anaendelea kujifua kwa ajili ya kumkabili Yusuf Jibaba katika ambano la utangulizi wakati wa mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na  Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa
bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya  kujiandaa kumchakaza Jibaba ili
kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta Boy mwenye rekodi ya. won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga  Theodor Luanda
Frebruary 2,1996 na kutetea vema 

Thursday, April 18, 2013

BONDIA FADHILI MAJIHA ARUDI NA UBINGWA KUTOKA INDONESIA BAADA YA KUMDUNDA HERI AMOL

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akifuraia na bondia pendo Njau baada ya kumpokea bondia Fadhili Majiha (katikati) aliyerudi na kombe la ubingwa aliouchukua Indonesia wiki iliyopita  baada ya kumtwanga bondia Heri amol wa pili ni Japhet Kaseba mwingine ni Kanda Kabongo.

Wednesday, April 17, 2013

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU BI KIDUDE (FATMA BINT MBARAKA), KUZIKWA KESHO SHAMBANI KWAO ZANZIBAR

Mwanamuziki mkongwe katika Taarab Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude aliyefariki dunia leo asubuhi huko Bububu Zanzibar, alikokuwa anaugulia kwa kipindi sasa. 
Mwili wa Bi Kidude utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. 
Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102. 
Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni

BI KIDUDE KUZIKWA KESHO SHAMBANI KWAO ZANZIBAR
Bi Kidude anatatarajiwa kuzikwa kesho huko Zanzibar.

SULE'S INC & ENTERTAINMENT na Timu nzima ya Blog ya MTOTO WA KITAA ina toa pole kwa fwamilia, ndugu jamaa na marfiki na TAIFA kwa kufikwa na msiba huu
Mungu Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen

MKONGWE WA MUZIKI WA TAARABU NCHINI, BI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA.


Bi Kidude katika moja ya shoo zake enzi ya uhai wake
*********************

Bi.Kidude amefariki dunia mjini Zanzibar. Bi Kidude alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari Habari zaidi tutaendelea kuwaletea kile kinachoendelea.

Monday, April 15, 2013

MSARABA MWEKUNDU TAWI LA KISUTU WAPATA MSAADA WA VITI VYA WANAFUNZI


Meneja Masoko wa Kampuni ya Palray watengenezaji wa fenicha mbalimbali, Thomas Simpokolwe kulia akimkabidhi mwanafunzi wa chama cha msaraba mwekundu tawi la kisutu, Grace Raphael sehemu ya msaada wa viti kwa ajili ya kusoma masomo mbalimbali ya uokoaji kulia ni Mwenyekiti wa msalaba mwekundu tawi la kisutu Bw.Rashid Mkawa


Wanafunzi wa Msaraba Mwekundu Tawi la kisutu wakisaidiana kubeba madawati waliyo kabidhiwa
picha na www.burudan.blogspot.com

NEW SONG FROM JCB FT CHABA & BEN POL - I DONT CARE


HEKAHEKA MITAA YA KATI: JAMAA APOKEA KICHAPO BAADA YA KUSHINDWA KUMLIPA CHANGUDOA


Neema Samson (Changudoa) akiwa amemkaba mteja wake baada ya kushindwa kumlipa chake.

Joseph akizidi kupewa hali ngumu na Neema, pembeni wananchi wakianza kusogea eneo la tukio.

 Baada ya wananchi waliingilia kati zogo hilo baada ya kuona wanazidi kuvuruga amani mtaani kwao, waliamua kuwaweka mtu kati tayari kuwapeleka sehemu husika.

Wananchi waliamua kuwapandisha kwenye Bajaj tayari kuelekea kituo cha polisi.

Sunday, April 14, 2013

BREAKING NEWS!!!!!!!! ......SHULE YA SEKONDARI YA WAZO HILL INAENDELEA KUUNGUA

Tarfa zilizotufiki muda huu ni kwamba shule ya Sekondari ya Wazo Hill ya jijini Dar es Salaam inaendelea kuteketa kwa moto huku juhudi za kuuzima moto huo zikiendelea kufanyika.
......Wanahari wa Blog hii wapo njiani kuelekea katika eneo latukio.
...Tutaendelea kuwaletea kile kilichojiri.

Saturday, April 13, 2013

MTANDAO WA PR HABARI WAPATA MKOKO WAKE


Mwenyekiti wa  Mtandao wa kijamii wa http://prhabari.blogspot.com/, Spear Patrick akiwa amepozi na gari hilo

GARI HIYO INAVYO ONEKANA KWA NYUMA

Friday, April 12, 2013

NEW SONG (AUDIO) FROM LORD EYES - MAPITO

KING CLASS MAWE AJIANDAA KUMKABILI AMOSI MWAMAKULA MEI MOSI


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Abuu Mtambwe wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba 

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde naIbrahimu Toll wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi na Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba.

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kulia akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Ally Masaga wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika kambi ya Ilala Amana CCM Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake wa mei mosi dhidi ya Amos Mwamakula utakaopigwa katika ukumbi wa PTA Saba saba
 Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Monday, April 8, 2013

VIDEO YA USWAZ TAKE AWAY KUTOKA KWA CHEGE FT MALAIKA

DIWANI KATA YA BWILINGU, CHALINZE AAHIDI KUJENGA UKUMBI WA MASUMBWI linze


Bondia Martin Shekivuli kushoto akipambana na Abdull Ndosa wakati wa mpambano wao wa kirafiki ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mpambano huo ulitoka droo

Bondia Amour Mzungu katikati akipambana na Josefu Marwa wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kushoto ni refarii Ibrahimu Kamwe

Refarii Ibrahimu Kamwe akimnyoosha mkono juu Amour Mzungu kuwa mshindi wa mpambano huo dhidi ya Josefu Marwa

Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar katikati akizungumza mbele ya mabondia Issa Omari kushoto na Shabani Madilu kabla ya mpambano wao

Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar
 Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo, Ahmed Karama Nassar amesema yupo tayali kushilikiana na wadau mbalimbali ili iwezekane kupatikana ukumbi maalumu wa mchezo wa masumbwi Chalinze aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika mapambano ya ngumi yaliyopigwa katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala.
Nina tarajia kufikisha mbali mchezo huu kwa kuwa mmenishawishi kuupenda mchezo wa masumbwi mchezo unaopendwa na wengi na kukimbiwa na wadhamini wachache ata hivyo nimeandaa mpambano rasmi utakaochezwa Chalinze kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huu siku ya April 21 hivyo nawaomba wadau wote wa ngumi tuamie chalinze kwa mda hili tuweze kuhamasha mchezo huu
Ambapo siku hiyo kutakuwa na ushindani mkubwa wa mabondia kutoka Dar es salaam watacheza na mabondia wa Chalinze siku hiyo ata hivyo kwa kuonesha kwamba anajili na anathamini mchezo wa masumbwi ame aidi kutoa gari moja kwa ajili ya mashabiki na mabondia kwenda kushiriki mchezo uho wa April 21. M
bali na ahadi hiyo Diwani huyo ametoa pesa taslimu shilingi 1,50000 kwa ajili ya malipo ya baadhi ya mabondia waliokuwa awajilipwa na kuanza kudai kabla ya kupanda ulingoni na kuhamua kuchukua jukumu hilo la kuwalipa mabondia hao
Mmoja ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini Ibrahimu Kamwe  amesema kuwa yupo tayali kutoa ushilikiano wa hali na mali kwa kuanzia atachukua baahi ya vijana kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo wa masumbwi uliopangwa siku hiyo hivyo tupo pamoja unajua ngumi watu wanapenda kuangalia ili galama zake ni kubwa ata hivyo naona ajabu wadhamini kushindwa kujitokeza kuzamini mchezo huu unaopendwa na vijana wengi 
na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Ahmed Karama Nassar kwa kuanza kusapoti mchezo wa masumbwi sehemu uliyopo

Sunday, April 7, 2013

ILIVYOKUWA JANA PALE VIWANJA VYA LEADERS CLUB KWENYE BONANZA LA WANAHABARI

Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza na wanahabari wakati wa Bonanza maalum la waandishi wa habari 'Medi Day' lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni. Katika Hotuba yake Dkt Mwakyembe, alisema ''Nataka Niwe Waziri Bora wa Uchukuzi Tanzania, Na pia wananchi hawataki Cheo cha Mtu bali wanataka Maendeleo zaidi, na hata yule anafanya kampeni wa Urais kwa wakati huu tukiwa na Rais, anavunja sheria za nchi, asubiri hadi tukifikia kipindi cha kampeni ndiyo aanze kujinadi''. alisema Dkt. Mwakyembe.
Baadhi ya wanahabari waliohudhuria bonanza hilo wakifuatilia burudani Uwanjani hapo.
Mchezaji wa timu ya Blogers FC, Sule Junior 'MTOTO WA KITAA' akiwa tayari kwa Machi kati ya Blogers FC na DSJ.
Wachezaji wa timu ya Blogers FC wakipongezana wakati wa mapumziko
Wachezaji wa timu ya DSJ (wenye jezi za kijani) wakijaribu kuokoa mpira langoni mwao baada ya kupata mashambulizi makali kutoka kwa Blogers FC 
Mchezaji wa timu ya Blogers FC, Sule Junior 'Mtoto wa kitaa' (kulia) akijaribu kuokoa mpira katika lango lao wakati wa mechi yao na DSJ. Blogers FC iliichapa DSJ 7-6.
Kikosi cha timu ya Blogers Fc katika picha ya pamoja na kiongozi wao.
Sule Junior (kushoto) akishoo lav na Eddo Kumwembe mida ya misosi
Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo wakionyesha vitu vyao.
Mwmbaji wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki akifanya mambo
Waimbaji wa bendi ya Jahazi wakiongozwa na Mzee Yusuf wakifanya burudani.
BOFYA HAPA NA HAPA KWA PICHA ZAIDI