Thursday, March 31, 2011

WAZIRI NCHIMBI AANZA KUONGEA NA WASANII

Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi(pichani), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo atakutana na wasanii katika ukumbi wa BASATA kuanzia tarehe 31 Machi na tarehe 01 Aprili 2011.Waziri amepanga kuwaona wasanii kwa utaratibu ufuatao:-
31/03/2011 (Alhamisi) Saa 5:00 asubuhi 
Wasanii wa Sanaa za Picha Jongevu na Sanaa za Maonyesho
Saa 7:00 Mchana 
Wasanii wa Sanaa za Muziki na Sanaa za Ufundi
01/04/2011 (Ijumaa)Saa 3:00 asubuhi 
Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya
Izingatiwe kwamba Waziri atawaona wasanii wa muziki kwa siku mbili tofauti. Tarehe 31/03/2011 ataongea na wasanii wa Muziki wote isipokuwa wale wa Kizazi Kipya. Wasanii hao ni pamoja na wale wa Muziki wa Bendi, Taarab, Disco, kwaya na Muziki wa Asili.
Tarehe 01/04/2011 ataongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya tu. Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa hakikisheni wasanii wamepata taarifa na kuhudhuria kwa wakati.
Lengo kuu ni kuongelea maendeleo ya fani za sanaa.
Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI

VODACOM FOUNDATION YAKABIDHI MADARASA MAWILI MKOANI TABORA


Mkuu wa wilaya ya Urambo, Anna Magowa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ajili ya shule ya sekondari ya Kaliua iliyopo Wilaya ya urambo Mkoani Tabora, anaeshuhudia ni Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule, Madarasa hayo yalijengwa kwa thamani ya shilingi milioni 30.
Meneja wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom (Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule akiwasaidia kufanya usafi baadhi ya wanafunzi wa shule ya secondary ya Kaliua iliyopo Wilaya ya urambo Mkoani Tabora mara baada ya kufika shuleni hapo kwa lengo la kukabidhi madarasa mawili yaliyojengwa na mfuko huo kwa thamani ya shilingi Milioni 30.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya secondary ya Kaliua iliyopo Wilaya ya urambo Mkoani Tabora wakiwa wamekaa darasani mara baada ya Meneja wa Vodacom Foundation kuwakabidhi rasmi madarasa hayo yaliyojengwa na kampuni hiyo kwa thamni ya shilingi milioni 30.

Tuesday, March 29, 2011

LEO NI SIKU YA KUMKMBUKA MMOJA WA WAASISI WA HIPHOP NCHINI (FATHER NELLY)


Ni miaka mitano sasa toka Father Nelly alipotutoka duniani, Father Nelly ni mmoja kati nguzo iliyokuwa ngumu kabisa katika kundi laXplastaz na hip hop kwa ujumla, Na mpaka leo ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika gemu zima la hip hop.
NELSON CHRIZOSTOM BUCHARD aka Father Nelly, enzi ya uhai wake
 Hapa ndipo mwili wa braza Nelly ulipolazwa, 
 NELSON CHRIZOSTOM BUCHARD
ALIZALIWA: 18-02-1976
AKAFARIKI: 29-03-2006
"Heri yule afaye katika upatanishi maana atauona ufalme wa mbingu"
R.I.P 
Hili ndilo kundi ambalo marehemu Father Nellyalikuwa nalo kwa mda wote (Xplastaz)

HAPPY B'DAY MARAFIKI WA SULE JUNIOR KWENYE FACEBOOK.

MWANAHAMIS MWENDA
AMON MASHITA
APOSTLE ANGEL SHABA (EDNA)

Sule Junior na timu nzima ya mtotowakita .blogspot.com inawatakia sikukuu njema ya kuzaliwa mafans na marafiki wote wanaoisapoti blog hii!

TAARIFA YA WIZARA YA AFYANA USTAWI WA JAMII KUHUSU DAWA YA BABA WA LOLIONDO

TAARIFA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUPITIA TAASISI ZAKE ZA UTAFITI KUHUSU DAWA YA MCHUNGAJI MSTAAFU AMBILIKILE MASAPILA WA SAMUNGE- LOLIONDO, AMBAZO NI: MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA), TAASISI YA UTAFITI WA DAWA ASILI YA CHUO KIKUU CHA AFYA YA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI, (MUHAS) MKEMI MKUU WA SERIKALI (CGC), TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR) 
Taarifa ziliifikia serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.
Kufuatia taarifa hii, serikali iliielekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, ufanyike haraka uchunguzi kuhusu dawa hii na itoe ushauri Serikalini ipasavyo. Baada ya kupokea maagizo hayo, wizara iliteua wataalamu kutoka taasisi zake tukiwemo sisi, TFDA, NIMR, Muhimbili kwa maana ya MUHAS, Mkemia Mkuu na tulijumuisha wataalamu wa hapa wizarani, ili kuifanya kazi hiyo muhimu, akiwemo Msajili wa Tiba Asili na Mbadala.

BABU KAJU AACHIA NGOMA ALIYOFANYA NA CARLOS SANTANA

Alex Kajumulo "Babu Kaju"
Carlos Santana
Akiongea kwa njia ya simu kutokea nchini marekani Babu Kaju aliimbia blog ya mtoto wa kitaa kuwa sasa ameachia ngoma yake inayoitwa LIKE ME aliyo fanya katika studio zake mwenyewe (BABU KAJU RECORDS)  na kupigiwa gitaa na mtu mzima Carlos Santana. pia Babu kaju alisea wimbo huun ni maa lum kwa wale wanaowaonea aibu au kuwaogopa kuwatongoza wasichana pale wanapokutana nao kwa mara ya kwanza Hasa kwenye kumbi za starehe.
Babu Kaju aliosema hivi..... "WIMBO HUU NIMEUTENGENEZA NA KUPIGWA GITAA NA CARLOS SANTANA, PIA  NIMEITUNGA KWA SABABU YA WATU WANAO KWENDA KWENYE DISCO WANAMUONA MTU WANAMPENDA LAKINI WANASHINDWA KUONGEA NAYE."
CARLOS SANTANA ni mpiga gitaa maarufu sana duniania anaetokea pande za MEXICO. pia Babu Kaju alimalizia kwa kusema hiyo ngoima imeshaanza kupata air pla ya kutosha katika redio za nchini mexcico na jamaica na baadhi ya redio nchini marekani.

Sikiliza wimbo huu hapo pembeni kwenye playlist za mtoto wa kitaa.

Monday, March 28, 2011

20% AFUNGUKA NA KUSEMA MANI WALTER ALISTAHILI TUZO.


     http://1.bp.blogspot.com/-n1aU-6YDUOg/TZBLi-eDwzI/AAAAAAAADOI/pexPCqHZOQM/s1600/20%2Bpercent.JPG
Baada ya kushinda tuzo 5 za Kili Music Awards 2010/2011 na kuweka historia,amefunguka kuwa hakutegemea kama angeshinda tuzo zote 5 kwenye vipengele ambayo ameshiriki!  
"Sikutegemea kama ningepata tuzo hizo zote 5 kwani nilitegemea tuzo 2 kiuhakika....ya wimbo Bora wa Afro Pop na Mtunzi Bora wa Nyimbo,ila kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume,Muimbaji Bora wa Kiume na Wimbo Bora wa Mwaka - Tamaa Mbaya,kiukweli sikutegemea kabisa" 
Kuhusu Producer wake Man Water wa Combination Sound aka Combinenga kutopata tuzo ya Mtayarishaji/Producer Bora wa Muziki-2010,20% amesema kuwa Man Water alistahili coz kama yeye amepata tuzo zote 5 kupitia nyimbo ambazo Man Water amezitengeneza za Malumbano na Tamaa Mbaya,lakini tuzo imeenda kwa Producer Lamar toka FishCrab Studio haiko sawa kabisa...alifunguka 20% akiwa njiani kurejea Dar na akiwa kwenye basi akirudi,nyimbo zake ndio zilikua zinapigwa njia nzima bila hata ya kuwaambia wenye basi

20% amechukua tuzo hizo kupitia vipendele vifuatavyo;
1.Tuzo ya Mtunzi Bora wa nyimbo - 2010
2.Tuzo ya Wimbo Bora wa Afro Pop - Tamaa Mbaya
3.Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume - 2010
4.Tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka 2010 - Tamaa Mbaya
5. Tuzo ya Msanii Bora wa Muziki wa Kiume - 2010

GAZETI LAKO LA DIRA LEO LIPO MITAANI. PATA NBAKALA YAKO SASASunday, March 27, 2011

WANAHARAKATI WA HIP HOP (KIKOSI CHA MIZINGA) KUKINUKISHA MAISHA CLUB LEO.


Siku ya Jumapili ya leo (tarehe 27_) ndani ya NEW Maisha Club Kikosi cha Mizinga kikiongozwa na Kala Pina watazindua album yao inayoitwa MAISHA YANGU NYIMBO TOSHA,
Perfomance ya kutosha kabisa itasababishwa na wanahiphop kibao kutoka kila kona ya Africa mashariki. wanahiphop watakokinukisha ni pamoja na Back T kutoka RwandaKimya kutoka KenyaAY, FA, Madee, Godzilla, B.D.P, BoB Click, na wengine kibao
Sio Pakukosa kama wewe ni mwanaharakati wa ukweli

MAMBO YA KILI MUSIC AWARD HAYA!Dakika moja ya kusimama kuwaombea marehemu wa Five Star Moden Taarab.
Msanii C-Pwaa akikabidhiwa tuzo ya video bora ya muziki wa mwaka uitwao Action pia aliibuka na tuzo nyingine ya wimbo bora wa Ragga/dancehall uitwao Action
Wimbo bora wa asili Tanzania Shangazi ulienda kwa msanii wa vichekesho Mpoki
Wimbo bora wa RnB Nikikupata ulienda kwa msanii Ben Pol
Kushoto ni mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Combinations Sound aka Combinenga Man Water akipokea tuzo ya mwimbaji bora wa kiume kwa niaba ya 20% kutoka kwa mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd Juhyana Kusaga.
TUZO ALIZOCHUKUWA 20% NI
1.       Tuzo ya wimbo bora wa Afro Pop – Tamaa Mbaya
2.       Tuzo ya mtunzi bora wa nyimbo
3.       Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume
4.       Tuzo ya wimbo bora wa mwaka
5.       Tuzo ya msanii bora wa muziki wa kiume

Wimbo bora wa Hip Hop Karibu Tena ulienda kwa msanii Joh Makini
Mwimbaji bora wa kike tuzo ilienda kwa Lady JD

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB,Iman Kajura pamoja na Balozi wa Redd's 2010,Consolata wakikabidhi tuzo ya Msanii Bora wa Kike iliyokwenda moja kwa moja kwa Lady Jay Dee na kupokelewa na mdau aliejitokeza kumuwakilisha kutokana na kutohudhuria kwa msanii huyo.
Mtayarishaji bora wa nyimbo Lamar
Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikishwa tuzo ilienda kwa JCB na Jay Moe
Mwenyekiti wa Tanzania mitindo house, Khadija Mwanamboka akimkabidhi msanii wa kizazi kipya Linah tuzo ya msanii bora wa kike, pia Linah alichukua tuzo ya msanii mpya anayechipukia
Wimbo Bora wa Reggae, What u Feel Inside - Hardmad
Kushoto ni msanii Bonta, JayMoe, Ksingo, Nikki wa Pili na Ruben

Saturday, March 26, 2011

WASANII WA KUNDI LA FIVE STAR WALIOFARIKI WAOMBEWA DUAMkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Prof.Hermans Mwansoko naye akiongea jambo katika dua hiyo maalum ya kuwaombea marehemu.Wengine kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ghonche Materego na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Mh.Henry Clemensia.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Dtk.Fenela Mukangala akiongea na waumini pia wadau wa Sanaa waliofika katika Ukumbi wa Star Light Ilala jijini Dar es Salaam kuwaombea dua maalum Marehemu 13 wa Kundi la Five Star Modern Taarab waliofariki katika ajali iliyotokea wiki hii kwenye barabara ya Iringa-Morogoro.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni,Sanaa kutoka wizara hiyo,Bi.Ngowi.
Mratibu wa shughuli ya kuwaombea dua Marehemu,Mzee Chilo akitangaza utaratibu mbalimbali wa tukio zima.
Baadhi ya wasanii wa taarab wakisikiliza mawaidha kutoka kwa Sheikh Othman Zuberi (hayuko pichani) wakati wa dua hiyo.
Waumini wakiomba dua kwa marehemu.
Mmoja ya Wasanii waliopona kwenye ajali hiyo Ally Juma aka Ally J (Kulia) akiwa sambamba na Viongozi wa Bendi yake, Ferouz Juma (wa pili kutoka kulia) Mkurugenzi wa Bendi ya Five Star na Khamis Slim (Wa kwanza kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Bendi.

Na Mdau Alistide Kwizela wa BASATA

Shirikisho la Wasanii Tanzania (SHIWATA) Alhamisi ya wiki hii kwenye Ukumbi wa Star Light Ilala jijini Dar es Salaam liliandaa dua maalum ya kuwaombea wasanii 13 wa Kundi la Five Stars Modern Taarab waliofariki Dunia usiku wa Tarehe 21/3/2011 kutokana na ajali ya gari iliyotokea eneo la Hifadhi ya Wanyama ya Mikumi mkoani Morogoro.
Dua hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa,mashirika ya umma, masheikh, wachungaji na wasanii mbalimbali hususan wa taarab.
Miongoni mwa waliohudhuria dua hiyo maalum ya kuwaombea marehemu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh.Dtk.Fenela Mkangala,Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara hiyo,Profesa Hermans Mwansoko,Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni anayeshughulikia Sanaa,Bi.Angela Ngowi,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh.Henry Clemensia.
Akizungumza katika Dua hiyo,Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Dkt.Mukangala alisema kwamba,kifo cha wasanii hao ni pigo kubwa katika tasnia ya Sanaa lakini lazima wadau wa sanaa wajipange kuhakikisha kundi la Five Star linarudi katika hali yake na kuwa bora zaidi.
“Serikali itakuwa bega kwa bega katika kutoa ushirikiano wa dhati kwa kundi la Five Star kupitia idara yetu ya Utamaduni.Ni wajibu wa wadau wote wa sanaa kulisaidia kundi kwani katika ajali hiyo si tu lilipoteza wasanii hao 13 bali pia vyombo karibu vyote vya muziki” alisisitiza Dkt.Mukangala.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Mh.Clemensia aliwaasa wasanii kutunga nyimbo za kukemea madereva wanaoendesha magari yao kwa kasi na wasio zingatia sheria za barabarani.Aidha, alikiri kwamba, pengo la wasanii hao wa kundi la Five Stars haliwezi kuzibika kamwe kutokana na ukweli kwamba,kazi yao haina mbadala.
Awali kabla ya wageni kuzungumza,Sheikh Othman Zuberi aliongoza dua maalum ya kuwaombea marehemu ambapo naye hakusita kuasa juu ya wasanii kuzingatia maadili na kuvaa mavazi yanayo wasitiri badala ya kutumbukia kwenye mtego wa kutenda maovu kupitia kazi zao za sanaa.