Monday, March 7, 2011

BAADA YA MAFISADI KUSHINDWA KULINYAMAZISHA GAZETI LA DIRA SASA LIPO MTAANI.


Na mwandishi wetu

MBINU chafu za kulinyamazisha gazeti la Dira Mtanzania zimeanza kuchukuliwa na watu wanaotajwa kuwa mafisadi kutokana na kulihujumu na hivyo kusababisha kutochapwa wiki iliyopita.
Dira Mtanzania hutoka kila Jumatatu, lakini kuingiza mkono kwa mmoja wa mafisadi kulisababisha gazeti hili kushindwa kuingia mitaani wiki iliyopita.
“Huu ni mkakati maalum. Gazeti lenu linaonekana kuandika habari za kuwashambulia mafisadi. Kuna mipango ya kuhakikisha linaondolewa kabisa machoni mwa wasomaji kwa sababu linazidi kuwachafua,” kilisema chanzo chetu cha habari kilicho karibu na mkakati huo.
Chanzo hicho kilisema kuwa mafisadi wameunda mkakati maalum kuhakikisha wanasafishika mapema kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao, kwani wengi wao wana ndoto za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi. Katika kufanikisha suala hilo, baadhi ya vyombo vya habari vimeshirikishwa na vile ambavyo haviko mikononi mwao, vinaundiwa mkakati wa kuondolewa sokoni kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuvitisha kwa kuvifungulia mashtaka ya madai ya mabilioni ya shilingi.
Kwa kipindi kirefu gazeti hili limekuwa likiandika habari za kifisadi, ikiwa ni pamoja na kupigia kelele za kuitaka Serikali kutoilipa shilingi Bilioni 94 kampuni ya kitapeli ya Dowans iliyoshinda kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa kibiashara.
habri kamili ipo kwenye gazeti la Dira ya mtanzania

No comments:

Post a Comment