Monday, April 24, 2017

SHEREHE YA UBATIZO WA MTOTO ROSELYN HENRY KAPINGA KATIKA UKUMBI WA VIP WANYAMA HOTEL SINZA.

Cake maalum kwa ajili ya Ubatizo wa mtoto Roselyn Kapinga iliyoandaliwa na Aunt Agnes Makwati ikiwa tayari kwa kukatwa.
Aunt Eva (Doto) akiwa amembeba Roselyn kabla ya kuanza tukio la kukata Cake.
Mama wa Kiroho Aunt Esther Mbapila akitoa zawadi ya Roselyn kwa mama Roselyn
Cindy Makwati akimlisha cake Mama Roselyn kwa niaba ya Roselyn huku baba Roselyn akishuhudia tukio hilo.
Cindy akijiandaa kumlisha cake Aunt Agnes ambaye ni mama yake.
Babu Roselyn naye hakuwa nyuma katika kusherehekea Ubatizo wa mjukuu wake. Mtoto Roselyn Henry Kapinga alipata Ubatizo siku ya Jumatatu ya Pasaka ya tarehe 17/04/2017 katika kanisa la Mt. Petro Oysterbay jijini Dar es salaam na baadae kufuatiwa na sherehe fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa ndani katika Hoteli ya Wanyama Sinza jijini Dar es salaam.

Tuesday, April 11, 2017

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA TANO CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LEO MJINI DODOMA.

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Mwibara(CCM) Mhe. Kangi Lugola akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Fakharia Shomar Khamis (CCM) akiuliza swali katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi  akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha tano cha mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Dodoma.

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO, HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA TBC

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe (kulia), akipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Ayoub Ryoba, wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Hassan Abbasi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe (kulia), akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Ayub Ryobawakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017. 
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe picha za Viongozi mbalimbali waliowahi kuongoza TBC wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam 10 Aprili, 2017.

Monday, April 10, 2017

MSANII ROMA AFUNGUKA YALIYOMKUTA BAADA YA KUTEKWA KWA SIKU 3

Mwanamuziki wa Hip Pop, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu tukio ake la kutekwa na watu wasijulikana hivi karibuni. (PICHA NA VENANCE NESTORY)
Mwanamuziki wa Hip Pop, Ibrahim Mussa ëRoma Mkatolikií akionesha alama za makovu katika mkono wake wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu tukio la kutekwa na watu wasiojulikana hivi karibuni. (PICHA NA VENANCE NESTORY)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana alipokuwa ajibu maswali kuhusu tukio la kutekwa kwa Mwanamuziki wa Hip Pop ëIbrahim Mussa ëRoma Mkatolikií(katikati). Kulia ni Mke wa msanii huyo, Nancy Ibrahim Mussa. (PICHA NA VENANCE NESTORY)


Saturday, April 8, 2017

NAPE AKIZUNGUMZA NA WAPIGAKURA WAKE JIMBONI MTAMA

NAPE ALIPOFIKA JIMBONI KWAKE (MTAMA) NA KUZUNGUMZA NA WAPIGAKURA WAKE

Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, Nape Nnauye akihutubia wananchi jimboni humo, na kuelezea kisa cha yeye kuvuliwa uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na kitendo cha kitishiwa bastola alipotaka kuzungumza na wanahabari nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Msasani Dar es Salaam mwezi uliopita. 
(PICHA KWA HISANI YA MICHUZI Jr)