Monday, December 31, 2012

MJANJA MJANJA - MIDZOO FT KITALE (OFFICIAL VIDEO)


KABATI ALL STARS- IRINGA BILA UKIMWI INAWEZEKANA


NGOMA MPYA YA KUNDI LA DADY DADYZ KUTOKA ARUSHA - MZURI


BAADHI YA PICHA ZA MKUTANO WA WANACHAMA WA TASWA ULIOFANYIKA BAGAMOYO


Baazi ya wanachama wa TASWA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete 

Katibu Mkuu wa TASWA Amir Muhando akitoa neno la shuklani kwa wajumbe waliohuzulia mkutano wakati wa kufunga mkutano huo
 
Mjumbe wa mkutano huo, Rajabu Mhamila 'Super D' akijitambulisha kwa mgeni rasmi

Baazi ya wanachama wa TASWA wakisikiliza mada mbalimbali
Picha na www.burudan.blogspot.com

HUYU NDIYE MSHINDI WA TAJI LA UNIQUE MODEL 2012

Mshindi wa taji la UNIQUE MODEL 2012, Catherine Masumbigana akiwa katika pozi la picha mara baada ya kutangazwa mshindi. shindano hili lilifanyika Ijumaa desemba 28, katika ukumbi wa New Maisha Club. 

Monday, December 24, 2012

NISHAN NA SHANI TAMADUNI MUZIK (FREESTYLE)

Kwa hili tunapenda kuipongeza timu nzima ya Tamaduni muziki maana hivi ni vipaji ambavyo wengi hawajaviona lakini kupitia Tamaduni muziki hata sisi wadau tumeweza kuviona na kuvitambua wasanii wapya hasa wa HIP HOP wenye vipaji vya kutisha. 
Timu ya SULE'S INC. & ENTERTAINMENT na Blog ya MTOTO WA KITAA tunatoa pongezi na tunaahidi kutoa sapoti ya kutosha kwa hili. 

CLUB BILICANAS  YAJA NA TOTO SHOO KRISMAS YA KESHO

Na Mwandishi Wetu
KATIKA kusherehekea sikukuu ya Krismas, Club yenye hadhi ya kimataifa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Bilicanas, kesho inatarajiwa kuwapa burudani kabambe mashabiki wa muziki wa disko wakiwemo watoto.
Mmoja ya viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omary alisema amesema leo kwamba  kwamba, kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo ndiyo maana wameandaa burudani kabambe ili kutoa fursa kwa watu wa rika lote kusherehekea kwa furaha.
Alisema shamrashamra hizo zitaanza usiku wa leo ambapo kutakuwa na usiku wa Kwaito ‘Kwaito Special’ uliongozwa na kundi la Wakli Dancers.
Omary alisema, kesho (jumanne) mchana kutakuwa na Watoto Shoo ambapo pamoja na muziki wa disko watoto watakaojitokeza ukumbini hapo wataburudika na Father Krismas ambaye atamwaga zawadi ambapo kiingilio kitakuwa sh 2,000 kwa kila motto huku wakubwa watakaoambatana nao watalipa sh 3,000.
“Usiku wa Krismasi utakuwa na shamrashamra nyingi ambapo watakaongia kila mmoja atapata mvinyo mwekundu au mweupe, hii kiingilio kitakuwa sh 10,000 kwa kila mmmoja,”alisema.
Aidha, Omary aliongeza kwamba siku ya boxing Day ukumbi huo utaendelea kupambwa na burudani mbalimbali ambapo kiingilio kitakuwa sh 5,000 kwa kila mmoja.

PLAYA HATERS - JANB FEAT EMMIE

TPBC KUMALIZA MWAKA 2012 NA MAFANIKIO LUKUKI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DESEMBA 24, 2012
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inamaliza mwaka 2012 na mafanikio lukuki ikiwa imeweza kuiletea nchi ya Tanzania mapambano makubwa ya kimataifa zaidi ya matano. 
Haya ni mafanikio ambayo yanapaswa kusifiwa na watanzania wote wapenda maendeleo kwani kutokana na mapambano hayo nchi imeweza kujulikana kimataifa, vivutio vyake vya utalii vimeweza kujulikana, nchi imeweza kuwatengenezea vijana ajira, na kuweza kupunguza uhalifu kwa kuweza kuwapa vijana kazi kwani kukaa kwao bure ni kishawishi tosha cha kutumia nguvu zao kwa shughuli ambazo sio za maendeleo. 
Katika mwaka unaoishia Desemba 31, 2012, TPBC imeweza pia kuwapeleka nje mabondia zaidi ya 15 wakiiwakilisha nchi ya Tanzania ambako waliweza kuitangaza nchi ya Tanzania vizuri na kuwavutia wageni wakitalii na kuwekeza katika nchi hii inayojulikana kama kisiwa cha amani katika bara la Afrika.
Aidha, TPBC imeweza kuhudhuria mikutano mitatu mikubwa ikiwa ni pamoja na mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) katika jiji la London, Uingereza na ule wa mwaka wa  Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Bahamas.
Kadhalika TPBC iliwakilishwa kwenye mkutano wa 30 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chana cha Ngumi  Cha Marekani (IBF/USBA) uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii nchini Marekani pamoja na ule wa Baraza la Ngumi la Dunia (WBC) uliofanyika pia katika mjiji la Las Vegas, nchini Marekani.
Hapa nyumbani , TPBC iliweza kutoa vibali na kusimamia mapambano mengi yaliyofanyika katika miji ya Tanga, Dar-Es-Salaam, Morogoro, Songea, Mbeya, Morogoro na Arusha na kuweza kuwapatia mabondia wengi  wa kitanzania mikanda ya Kanda, Taifa na Afrika ya Mashariki, Kati na bara la Afrika.
TPBC inawashukuru na kuenzi  michango ya mapromota wote waliochangia kuandaa mapambano haya wakiwa ni pamoja na:
Kitwe General Traders, Kaike Siraju Boxing Promotions, Kyando Boxing Promotions, Mwanzoa Boxing Promotions, International Boxing Promotions, Selemani Siminyu, Green Hills (T) Limited na wengine wengi.
Aidha TPBC inapenda kuishukuru TPBO chini ya Abdalla Mwaipaya Ustaadh kwa ushirikiano wake katika kuendeleza ngumi za kulipwa Tanzania.
Tunapenda pia kuwashukuru wadau wote waliochangia kwa njia moja au nyingine kama vile vyombo vya habari, mamlaka za miji na miji na majiji, jeshi la polisi, kumbi zote za burudani zilizotumika kuandaa mapambano haya na wadau wengine wengi.
Pia tunaishukuru serikali kupitia Msajili wa Vyama (Mambo ya Ndani), Mkurugenzi  wa  Maendeleo  ya Michezo na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ushirikiano wao katika kusaidia kuendeleza ngumi za kulipwa nchini.

Tuesday, December 18, 2012

MAZOEZI YA UNIQUE MODEL KUANZA WIKI HII

Photo: DONT MIC 28 DEC @ NEW MAISHA CLUB www.uniqueentertz.blogspot.com
Washiriki wanaowania taji la mwanamitindo mwenye sifa za kipekee Unique model 2012 wanatarajiwa kuanza mazoezi ya miondoko ya kimaonyesho alhamisi hii katika hoteli ya Lamada iliyopo jijini Dar.
Jumla ya washiriki kumi na mbili wataanza mazoezi hayo kwa nia ya kujifua kimazoezi ya kutembea miondoko ya kimaonyesho na dansi ili kuukabili mchuano mkali uliopo baina ya washiriki hao.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi mratibu wa shindano hilo Bw. Methuselah Magese amesema kuwa washiriki wapo katika hali ya ushindani sana na mwaka huu namshukuru mungu wamejitokeza wanamitindo wengi wenye sifa ukilinganisha na mwaka 2010 hii inaonesha kiwango cha ubora wa shindano kinapanda juu.
Magese aliyataja majina ya washiriki hao ni Janecy Maluli,Judith Sangu,Vestina Charles,Catherine Masumbigana,Darling Godfrey,Amina Ayoub,Elizabeth Pertty,Lulu Mramba ,Sadory Kendra,Elizabeth Borniface na Zeenarth Habib,
Mwalimu wa dansi ya washiriki Denis Lucas amejiandaa vyakutosha kuhakikisha kuwa washiriki hao wanatoa burudani ya dansi amabayo haijawahi kutokea ambapo watu watapata mengi ya kukonga nyoyo zao kwa kiingilio cha elfu kumi na tano tu.
Mwalimu wa miondoko atakuwa mwanamitindo mwenye uzoefu na majukwaa ya mitindo nchini Tanzania ambae ametajwa kwa jina la Wancy Nells ambae amejipanga kuwanoa vema wanamitindo hao tayari kwa fainali.
Fainali za Unique model 2012 katika kumtafuta unique model of the year 2012 zifanyika tarehe 28 mwezi huu katika ukumbi wa maraha New Maisha club uliopo oysterbay jijini Dar.
 Shindano hili limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general Traders,sophanaa investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie blog,Lmada Apartments & Hotel,mtaa kwa mtaa blog,Fabak fashins,Genessis health center na Yung don Records,Paka wear,Mtoko Design na Unique Entertainment Blog.

Monday, December 17, 2012

BAADA YA KUDONDOKA JUKWAANI, SAJUKI AKIRI KUWA HALI BADO SIO SHWARI
MSANII wa filamu nchini, Sajuki alidondoka jukwaani juzi wakati akijaribu kuwasalimia mashabiki wake waliofurika kumtazama kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Sajuki  ambaye jina lake halisi ni Juma Said Kilowoko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupungukiwa dawa na kulazimika kwenda kutibiwa nchini India.
Mwingizaji huyo alipanda jukwaani katika tamasha la lililowahusisha wasanii wa filamu na muziki, lakini ndoto yake ya kusalimia mashabiki wake hakuwezekana.
 Mara baada ya kukabidhiwa kipaza sauti Sajuki alitamka neno moja ”ahhh" na kudondoka chini na wasanii wenzake walimsaidia kuinuka na kumuondoa jukwaani hapo.
Akizungumza na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki alisema hali yangu si nzuri kwani nahishiwa nguvu na anahitaji matibabu zaidi.
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa, sijisikii vizuri,” alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi.
Hata hivyo, mashabiki wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali hiyo na kushutumu wasanii walioamua kumtumia ili wapate fedha ihali mwenzao ni mgonjwa.
“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu huyu mtu anaumwa, badala ya kumwacha apumzike wenyewe wanamzungusha bila ya kujali afya yake,” walisema mashabiki hao.

KICHUPA KIPYA KUTOKA KWA KLEX MAN - WINE YO BODY

NYALANDU AFUNGUKA KUHUSIANA NA TUHUMA ZA KUMILIKI KITALU CHA UTAALII

SIKU moja baada ya kuchapishwa kwa habari kwamba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu anamiliki kampuni inayojishughulisha na masuala ya kitalii ya Nitoke Safaris, kiongozi huyo amejitokeza na kuweka bayana umiliki wake huo.
Akizungumza kwa simu kutoka Mwanza jana, Nyalandu alisema kampuni hiyo iliyoanzishwa Aprili, 2009 ikiwa ni mali ya familia ilisitisha kazi zake tangu Mei mwaka huu baada ya kula kiapo cha kuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo.
“Baada ya kuapishwa Mei mwaka huu tulifikia makubaliano mimi na familia yangu kwamba kampuni hii isitishe shughuli kwa kuhofia mgongano wa kimasilahi,” alisema Nyalandu na kuongeza:
“Tangu wakati huo hakuna kazi iliyowahi kufanyika katika kampuni hiyo, hata aliyekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni hiyo ambaye pia alikuwa akisimamia Jarida la Tutoke (Tutoke Magazine), Gloria Mshana alilazimika kutafuta ajira sehemu nyingine.”
“Kufuatia uteuzi wangu wa  kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na kwa kuzingatia uwezekano wa kuwapo mwingiliano wa kimasilahi, niliamua kusitisha shughuli zote za kibiashara za Nitoke Safaris Ltd na Tutoke Magazine, baada ya kuapishwa…  Jarida la Tutoke lilichapisha toleo lake la kwanza Septemba 2009 na toleo lake la mwisho lilichapishwa Novemba 2011.”
“Nilichukua hatua hii ili nipate fursa na uwezo wa kusimamia sekta ya utalii nchini kwa haki na umakini kwa wadau wetu wote wanaojishirikisha na biashara ya utalii nchini. Kuhusu ofisi, waziri huyo alisema kampuni hiyo ilishahama katika Jengo la PPF Complex Suit, namba 24 Barabara ya Mzingo tangu mwaka 2011 na kuhamia katika eneo la Kijenge kabla ya kuzifunga miezi saba iliyopita.
Juzi, gazeti la Mwananchi liliandika baada ya kufanya uchunguzi na kubaini kuwa Nyalandu anamiliki kampuni hiyo na mkewe  Faraja, huku kumbukumbu za Wakala wa Usajili wa Kampuni na Leseni (Brela), zikionyesha kila mmoja ana asilimia 30 ya hisa.
Kampuni hiyo ilisajiliwa Aprili 24, 2009 na kupewa nambari 70735, wakati huo Nyalandu akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini, wadhifa alioupata kuanzia mwaka 2000. Alipoulizwa kuhusu madai hayo juzi, Waziri Nyalandu alisema tayari alishajitoa na kufafanua kwamba kama ambavyo haipendezi yeye kumiliki kampuni ya utalii akiwa waziri wa wizara hiyo, haitapendeza pia waziri wa habari kumiliki gazeti.
“Huwezi kuwa Waziri wa Utalii na ukafanya biashara ya utalii, katika kampuni hiyo mimi nilishatoka kitambo,” alisema bila kufafanua zaidi.

Sunday, December 16, 2012

KALA JEREMIAH KUTOKA NA ALBUM YAKE MPYA

Baada ya kufanya vizuri katika baadhi ya redio na televisheni kwa ngoma yake ya Dear GodKala Jeremiah sasa ameweka wazi kwamba siku ya tarehe 20 mwezi huu anatarajia kutoka na album yake mpya inayokwenda kwa jina la Pasaka.

Wednesday, December 12, 2012

WASANII WA BONGO BADO WAENDELEA KUJIACHIA BILA KUJALI CHOCHOTE


Ama kweli mwisho wa dunia umekaribia! Chipukizi wawili wa filamu za Kibongo, Tabasamu Mohamed na Neema Ibrahim, wamekutwa ‘laivu’ wakifanya mambo ya chumbani hadharani.
Awali wasanii hao walishuhudiwa wakiwa ‘klozi’ ambapo walikwenda ‘kupozi’ chini ya mti na kuanza ‘kudendeka’ kabla ya kuzama katika hatua mbaya zaidi ya kutomasana na kuvuana nguo bila kujali kuwa ilikuwa mchana tena hadharani.

Monday, December 10, 2012

RAY C AMHUKURU RAIS JAKAYA KIKWETE KWA KUMSAIDIA MATIBABU


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila 'RAY C' akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu aliompatia ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.
(Picha na Freddy Maro)

Na Mwandishi Wetu

Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

Sunday, December 9, 2012

MARQUEZ AMSHINDA PACQUIAO KWA KNOCK OUT (K.O)

Bondia  PACQUIAO akiwa chini baada ya kupewa makonde mazito na mpinzani wake MARQUEZ.

Wednesday, December 5, 2012

VIDEO MPYA YA DULLY SYKES FT OMMY DIMPOZ & DIAMOND - UTAMU

LULU AFIKISHA MIEZI NANE (8) MAHABUSU


KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu), dhidi ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba, inaendelea kupigwa kalenda kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo iliahirishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Mbando. “Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii haujakamilika, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” alidai Wakili wa Serikali, Kenneth Sekwao.
Hakimu Mbando alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Desemba 17 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa. shitakiwa anatetewa na mawakili, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatara na Fulgence Masawe.
Lulu yuko rumande kwa miezi nane sasa kutokana na makosa ya mauaji na kukosa dhamana, anadaiwa kwamba Aprili 7 mwaka huu maeneo ya Vatican, Sinza, alimuua Steven Kanumba.
Kuchelewa kukamilika kwa upelelezi kumeanza kuzua mjadala kwa watu mbalimbali wanaofika kusikiliza kesi hiyo, wakidai kwamba hawajui matukio gani nchini ambayo upelelezi wake unaweza kufanywa kwa haraka.
“Nashindwa kuelewa, kila siku upelelezi bado, kuna upelelezi gani katika kesi hii wa kumaliza mwaka mzima, kila kesi ina mazingira yake ya kuchelewesha upelelezi lakini hii…” alihoji msikilizaji huku akitoka katika chumba cha mahakama.

Tuesday, December 4, 2012

VIDEO MPYA YA DIAMOND - NATAKA KULEWA

MASHAIRI (LYRIX) YA WIMBO WA MISS TANZANIA - SOLO THANGTongwe Records Presents to y’all Hip Hop fans worldwide Solo Thang A.K.A TRAVELLAH
(Miss Tanzania Produced by J-Ryder) 

Verse 1 

Baba Yake Alikua Mkoloni Kipindi Huyu Miss Mwali 
Mchonga Alikata Utepe Lakini Hakuvinjari 
Sababu Alikua Busy Kumlinda Na Geti Kali 
Kumbe Wenzake Wanabinjuka Kushtuka Akakaa Mbali 
Demu Alikua Na Heshima Kabla Haijatangwazwa Rukhsa 
Chukua Chako Mapema Ukimkonyeza Tu Umegusa 
Ana Kifua Kimebetuka Sio Maziwa Ni Madini 
Kayaacha Wazi Watu Wanashika Hapo Ndio Anaponiudhi Mimi 
Watu Wanagonga Tu Ikulu Tena Kwa Mitindo Huru 
Kavu Kavu Bila Kinga Hajali Vinavyodhuru 
Kawa Shangingi Na Amedata Hana Uwoga Wa Kunguru 
Anapenda Sana Chapaa Haimtoshi Kodi Na Ushuru 
Ana Kijungu Matata Laini Kama Nyanya Masalo 
Anatingisha Afrika Nzima Na Mzigo Kilimanjaro 
Usimchezee Kwa Vidani Sio Pete Sio Hereni 
Anamiliki Tanzanite Kama Ardhi Ya Mererani 
Sura Dhahabu Inaita Kama Amezaliwa Geita 
Tatizo Ndio Kicheche Kila Mwanaume Ndio Amepita 
Hata Benja Hakutoka Kapa Huyu Demu Hajatulia 
Kama Rushwa Ndio Kikwapa Ananuka Na Kunukia

Chorus

Miss Tanzaniaaaa 
Nakupenda Ila Hujatuliaa 
Vitendo Vyako Sitojivunia 
Sifa Yako Kubwa Umefulia 
Miss Tanzania 

Verse 2 
Bora Angebaki Kuwa Modo Kama Flavian Matata 
Ila Demu Amejiachia Kisa Anaendekeza Bata 
Sitachoka Kuwakilisha Jinsi Anavyoniacha Hoi 
Juzi Juzi Kaopolewa Na Handsome Boy 
Kabla Hapo Shoga Zake Wote Kashawaona Mabwege 
Sababu Hawana Dira Na Yeye Ameshahongwa Ndege 
Anafaa Kua Miss Dunia Maandalizi Longolongo 
Tatizo Anakula Sana Akijamba Ni Songosongo 
Mara Ghafla Kanenepa Kumbe Mimba B.O.T 
Kumbe Demu Aligawa Epa Watu Wamepiga Hafu Jii 
Alizugwa Na Akaunt Hewa Kuwadi Bwana Bilal 
Mara Mdomo Nae Kazimwa Bila Hata Picha Ya Kaburi 
Kinachomponza Huyu Shawty Utulivu Sifuri 
Ila Hakuna Anaepinga Kwamba Huyu Demu Ni Mzuri 
Mixer Siasa Na Biashara Demu Ameshakua Chotara 
Mishe Za Dar Akimaliza Mjengoni Anakwenda Lala 
Kadri Miaka Inavyokwenda Demu Anazidi Fulia 
Kumbe Weupe Ni Mkorogo Ona Mwili Sasa Umefifia 
Demu Kazidi Umalaya Wacha Mabwana Wamteme 
Haogopi Kuliwa Mtungo Kisa Nagawa Umeme

Verse 3

Wadaku Walishamfuma Anakula Denda Na Richmond 
Dowans Akazidi Kete Akamvisha Pete Ya Diamond 
Binti Maskini Akanasa Bwana Mshenga Ndio Lowasa 
Shemeji Hataki Hata Picha Ndio Tabia Gani Sasa 
Ndoa Ilifungwa Kwa Vifijo Vigogo Wakala Piza 
Keki Nzima Wale Wao Share Yetu Si Ni Giza 
Sio Hayo Demu Ana Mengi Ya Kuchukiza 
Mali Ghafi Ashazinadi Forsale Anajiuza 
Mtaani Ilivuma Rumor Demu Kawa Mama Huruma 
Uchumi Umefungwa Drip Maemdeleo Ndio Kali Homa 
Mali Asili Ndio Kitasa Kila Ufungo Ndio Unapita 
Toka Alipovunja Ungo Nusu Karne Imeshapita 
Mapenzi Kafanya Mradi Anamegwa Na Mafisadi 
Amani Kwa Time Bomb Binti Amekumbatia Radi 
Vitendo Vyake Vibaya Vinafanya Adharaulike 
Tabia Katiba Sio Msahafu Ndio Useme Isibadilike 
Mikosi Inayomkuta Ndio Kwanza Anatabasam 
Hajali Waliomzunguka Kama Nao Binaadam 
Mbagala Walimbaka Mpaka Akamwaga Damu 
Na Juzi Gongo La Mboto Kaanza Kujamba Mabomu

Monday, December 3, 2012

BAGAMOYO, MKOA WA PWANI WAHAMASISHA NGUMI KWA KISHINDOMKOA


Bondia Zumbe Kikuru kushoto akipambana na Toma Kato wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita Kikuru alishinda kwa  K'O raundi ya pili 

Mashabiki waliojitokeza kushudia mpambano wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Refarii wa mpambano wa masumbwi Said Chaku katikati akimwinua mkono juu bondia Obete Ameme baada ya kumtwanga mpinzani wake katika raundi ya kwanza kwa K,O uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Picha Zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini anaefundisha Timu ya Ashanti pamoja na timu ya Mkoa wa Ilala Kimichezo Rajabu Mhamila 'Super D' amevutiwa na mashabiki wa mchezo huo mkoa wa Bagamoyo Pwani
Baada ya kuvutiwa na umati mkubwa uliojitokeza katika mpambano uliofanyika Bagamoyo mkoa wa pwani mwishoni mwa wiki iliyopita mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way ambapo uliudhuliwa na mashabiki wengi wa bagamoyo
Kocha huyo anaefundisha kwa njia mbalimbali ikiwemo DVD amevutika kwa wapenzi wa ngumi bagamoyo kuchangamkia DVD hizo zenye kuelimisha mchezo wa masumbwi pamoja na kujua shelia mbalimbali za ngumi Duniani
Mpambano huo ulioandaliwa na Sharif Muhsin na kuratibiwa na bondia wa siku nyingi Said Yazidu umefungua ukurasa mpya kwa wakazi wa bagamoyo kuukubali mchezo huo na kuendelea kuupenda na kuwapa sapotimabondia wanaowakilisha Bagamoyo
Baazi ya mabondia waliopigana katika mpambano huo ni Maneno Zele alipata kichapo kutoka kwa Baisa Juma wakati Zumbe Kikuru alimtwanga kwa K,O Tomo Kato katika raundi ya kwanza huku Kadani Rhamwana alimchapa Ndumbo Hassani kwa point 
Mpambano huo ni wa pili kufanyika kwa mwaka huu umendelea kuwa chachu ya kupata vipaji vipya vya mchezo wa ngumi hapa nchini

Saturday, December 1, 2012

BASATA KUANZA KUSHUGHULIKIA WASANII WANAOKIUKA MAADILI


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego akizungumza jambo wakati akifunga jukwaa la sanaa, Kushoto kwakwe ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kazi na Ajira ,  Haji Janabi.

Na Mwandishi wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaagiza viongozi wa Mashirikisho ya sanaa hapa nchini kufuatilia kwa karibu matukio ya ukiukwaji wa maadili yanayoendelea katika Sanaa hivi sasa na kuchukua hatua kwa wnaobainika kufanya hivyo.
Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego,  mbali na BASATA kuwakemea vikali wasanii wanaotumia majukwaa kwa kuidhalilisha Sanaa wao wenyewe na watazamaji pia limeyataka mshirikisho kushirikiana na vyama vyao kuwaita wale wote watakaohusika na uvunjwaji wa maadili ili kuwakanya katika hatua ya kwanza na kama wasipoacha tabia hizo Baraza litawafungia kujishughulisha na kazi ya Sanaa  hapa nchini.
“Shirikisho la Muziki tumeliagiza kuangalia tungo za wanamuziki zenye maneno yenye lugha isiyofaa, Shirikisho la Sanaa za Ufundi limeagizwa kuwachukulia hatua wasanii wachoraji na wachongaji wanaotengeneza Sanaa zinazokiuka maadili. Aidha Shirikisho la Sanaa za Maonyesho waliagizwa kufuatilia wasanii wote wanaocheza bila staha majukwaani. Na mwisho Shirikisho la Filamu tumeliagiza kuwaita, kuwaonya na kuwachukulia hatua wasanii wote katika fani ya Filamu wanaovaa nusu utupu bila kuzingatia husika katika kazi za Sanaa,” amesema Ghonche.
Aidha Baraza limewaagiza wamiliki wa kumbi zote za burudani kuzingatia maadili pale ambapo Sanaa zitakuwepo jukwaani na kwamba baraza halitasita kuufungia ukumbi wowote utakaokiuka agizo hilo.
“Pia tunaviomba vyombo vya usalama kuhakiki muda wa vibali vya maonyesho na bila kuchelewa kuwachukulia hatua stahiki wasiozingatia muda wa maonyesho. Na tunawakumbusha wamiliki wa vyombo vya Habari na Wahariri kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wasimamizi wa sanaa kwa kutokurusha wala kutangaza maonyesho ambayo kwa njia yoyote yanachangia mmomonyoko wa maadili ya Taifa letu,” alisema Ghinche.
 Kwa suala hili, Baraza linaziomba mamlaka zinazohusika na usimamizi wa uendeshaji wa vyombo vya habari nchini kuingilia kati na kuvichukulia hatua vyombo vya habari ambavyo kila siku vimekuwa mstari wa mbele kueneza wimbi la mmomonyoko wa maadili hapa nchini na kushusha hadhi ya Tasnia/Sekta ya Sanaa nchini.

Sanaa ni kazi na Sanaa ni kioo cha Jamii.

NGOMA MPYA KUTOKA NOISE MAKER - DARASA HURU YA MEKACHEKA Ft NAKAAYA