Thursday, April 22, 2010

kwa pamoja

wana wa kitaa wakifuatilia show mwanzo mwisho
Yuda skills akitoa burudani kama kawa


Dj Nyoka kwenye mashine na Dj kinyonga pe3mbeni


Mr Kitime akishow lavu na Dj Kinyonga (Kushoto) na Dj SB (kulia)


mtoto wa kitaa *The DON* nikishow lavu na warembo Marry na Lucy Huku Dj Kinyonga na Mr kitime wkakitoa campan.

Sunday, April 18, 2010Hawa ni masakala mobb....Kundi la adventure........ADVENTURE wakiwa kazini..

MASAKALA MOBB wakiwa kazini...
MAJAJI wakijadiliana mpango mzima wa matokeo.....
DJ SB akiwa na Mrembo LUCY katika mpango mzima wa kusherehesha shughuli nzima......

Hawa ndio CASH MONEY............

Huyu ni chief jaji akitangaza matokeo


FLEVA ZA KITAA........
Lile shindano lakumtafuta mkali wa kudanc katika kata ya kawe bado linaendelea na wakati huu limefikia mwisho wa mzunguko wa kwanza na makundi kibao tu yamesha sepa kiaina kwani wiki ijayondio makundi yaliyofanikiwa kupita ndio yanaingia katika raundi ya robo fainali
akiongea katika tamasha lenyewe mkurugenzi wa BONGO SHAKERS INTERTAINMENT ambao ndio wenye jukumu zima katika kuhakikisha suala hili linasimama vilivyo Mr Calos alituambia kuwa wamejipanga vya kutosha "tumejipanga vya kutosha kabisa kwani sasa tuna kibali cha kuandaa mashindano haya tanzania nzima na hapa tumeanza mtaa kwa mtaa,"
.....katika mashindano hayo yaliyoshirikisha makundi kibao ambayo mengine tayari yamesha toka kaitka mchujo uliopita.
makundio yaliyojifua wiki hii ni pamoja na Cash Money, Adventure, Ungaunga, Masaskala Mobb na Revolution Guys.
Pia katika tamasha hilo walikuwepo watu kibao katika kuhakikisha burudani inasonga mbele, watu hao ni pamoja na Matumaini, Yuda Skillz, Kinyonga na Taza boy, Bacho wa michano, Man dabi. pia tulitembelewa na Mr Kitime katika kushoo lavu kwa wana wa kitaa........
HIZO NDIO FLEVA ZA KITAA BANAA............ Nani anabishaaaaaaaaaa

Sunday, April 11, 2010

Miss Mwanza 2010 ni mpango mzima

Mzee Mzima The DON hapa nimekula poooz kitaacha kati!
MIRIAM GERALD ambaye nio mrembo wa tanzania aliyetokea mkoani MWANZA

Bw. JOHN DOTTO aliyeweka mikono mfukoni ndiye mkurugenzi wa Sisi Entertainmant ambayo ndio inayoandaa mashindano ya urembo mkoani mwanza

SHINDANO la kumsaka mrembo wa Mwanza 2010, sasa liko njiaani na linatarajiwa kufanyika Juni 4, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Yatch Club jijini mwanza, imefahamika.

Kampuni ya Sisi Entertainment ambayoi ndio inayosababisha mpango mzima imesema kwamba warembo zaidi ya 15 watakimbizana katika kuliwania taji hilo linaloshikiliwa na Miriam Gerald ambaye pia ni Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2009/10.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, Bw. John Dotto, maandalizi ya shindano hilo yameshaanza vyema kwa ajili ya kumpata Mrembo wa Tanzania.

“Tumejipanga kufanya shindano la kutoa warembo bora kama iliovyokuwa mwaka jana na kwa uhakika tunaweza kuchukua taji la taifa,” alisema Dotto katika taarifa hiyo na kuongeza: “Kauli mbiu ya mwaka huu: “Ni Utalii kwanza tukilenga watalii wa ndani.”

“…..Haiwezekani kutegemea watalii kutoka nje tu. Kwa mfano Mwanza ina sehemu nyingi za kutembelewa na watu kujifunza mambo mengi, tena kwa gharama nafuu zaidi,” ilisisitiza taarifa hiyo.

Dotto alivitaja vivutio vya utalii hivyo kuwa ni hifadhi ya wanyama ya Serengeti, hifadhi ya wanyama ya Kigosi-Moyowasi, Ziwa Victoria pamoja na visiwa vyake vya Rubondo na Sanani.

Alisema sehemu kubwa ya maandalizi itakuwa ni darasa la kutosha kabisa kutoka kwa watalaamu wa ushauri nasaha wanatakaowapa somo warembo wote ili kuishi katika hadhi wanavyostahili.

Kampuni ya Sisi Entertainment ikiwa chini ya udhamini wa Vadacom na Bia aina ya Redds’ kutoka TBL, ina rekodi ya kufanya vema kwenye mashindano ya urembo baada ya mwaka jana kuingiza warembo watano katika 10 bora ya shindano la taifa.

Warembo hao walitokea kituo cha Dar City Center, Kanda ya Ilala ikiwa ni shindano lililoandaliwa na Sisi Entertainment, na warembo wake waliopaa zaidi mpaka katika tano bora ya taifa ni Sylvia Shally na Glad Shao.

.......kama vipi.... tukutane pande hizo tukale SATO na SANGARA BANAA!

Saturday, April 10, 2010

SULE'S WEAR.

huyu ni mchora katuni wa ukweli kabisa wa tanzania daima anaitwa SAID MICHAEL a.k.a wakudata akionesha nembo ya wewe 2 mimi sina habari.
mtoto wa kitaa mwenyewe a.k. the don akiwakilisha nembo ya kaka mkubwa
nembo za t-shirt za kaka mkubwa sasa ziko mtaani. Nembo zina maneno kama MAJUKUMU HAYAPIGI HODI, MJINI CNG'OOKI, WEWE TU MIMI CNA HABARI ya wakudata wear na KAKA MKUBWA yenyewe ikiwakilisha. kwa anaehitaji anicheki kwenye+255 7194 086

KITAA CHETU.

mwangu wa kitaa CBH naye alihudhuria kucheki wadogo zake wanachokifanya banaaa. Hahahahahahahahahahaaaaaaaaa.
msanii wa kitaa naye hakuwa nyuma katika kuwakilisha.

Huyu ni DJ S'B alikuwa kama mc wa shughuli nzima.

msanii YUDA SKILLS alikuwepoo kwenye upnde wa kipaza.


mashbiki wakifuatilia shindano klwa umakini mkubwa.
Mmoja wa majaji anaitwa SHAFII aliyeshika mic akitoa maoni yake kwa washiriki wa shindano.
SABABISHA wakiwa kazini.


Hili ni kundi la PAPILI CAMP likifanya mambo.

Kundi la OBADAA LIKIINGIA NA STAIL YA KUBEBA MAITI.

Hawa wanaitwa FANTHOM SOULDER watoto wa kitaa cha kawe wakifanya mambo.


Huyu ni miongoni mwa majaji wa hili shindano anaitwa bw FRENK

Hili ni kundi la SABABISHA wakionyesha utundu wao.

Baadhi ya mashabiki waliokuwepo ukumbini wakifuatilia kwa umakini mpambano wa kimtaa.


Mmoja wa majiaji MONALISA akisoma matokeo...........Katika pitapita zangu za moja ya harakati za kimtaa kama kawaida mtoto wa kitaa a.k.a The DON si ndio nikagumia show moja kabambe mitaa ya kati pande za kawe hivi… ……unajua show ilikuwa ya nini!?...
……show ilikuwa ni ya mashindano ya kusakata dansi bana.. …yaani unaambiwa mtu nyomi kama kama kiwanja flani hivi cha mbele kumbe ni huku kwetu uswazi. Ma camp kibao kutoka mtaa tofauti tofauti na pande zite za jiji yalishriki.
Kwa mujibu wa mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo amesema wameamua kuingia mtaani kusaka vipaji kwa sababu wanaamini kabisa mtaani ndiko vilipojificha vipaji vya ukweli ambavyo haviwezi kuonekana kwa sababu havipewi nafasi kabisa. …..“tumeamua kuingia mtaani kusaka vipaji vya kudansi kwa sababu tunaimani kuwa huku ndio kuna vipaji vya ukweli kabisa ila haviwezi kuonekana kutokana na kukosa nafasi ya kushiriki mashindano makunwa makubwa”..
Aliongeza….. “…..Sisi kama BONGO SHAKERS ENTERTAINMENT tumejupanga vya kutosha kuwapata na pia tuna majaji wa ukweli ambao watatusaidia katika mpango mzima!”
….show ilikuwa ni ya kimtaa zaidi kutokana hata washiriki (madansa) wenyewe walionekana kuwa ni wageni sana kwenye genu.
Pia mtaani bana hapakosekani burudani mzeiya……. Wasanii wetu wa kitaa kama kawa waliwakilisha ipasavyo kwa kutoa ushirikiano kwa madansa kwa kupafom nyimbi kubao tu ambazo ni kali tu kwa kusikiliza ila hazipo on air ….si umajua kimtaa mtaa?! Ngoma zinasikiliziwa geto tu!....

Thursday, April 8, 2010
Leo mtoto wa kitaa nilikuwa pande za mwenge kwa washkaji zangu wakitaa kama mimi na tulipiga stori kibao tu kuhusu haya malaifu. Kama vipi kesho tutashea wote haya mating'a halafu tuoneeeeeeeeeee!

Tuesday, April 6, 2010

PIGO KWA MWANAHALISI.

Aaliyekuwa mhariri wa gazeti la mwanahalisi Ndg ASTERICO KONGA amefariki dunia jana jionni katika hospitali ya lugalo alipokuwa akipata matibabu yake ya kila siku.
Ndg. Konga alikuwa ni mwandishi na mhariri shupavu aliyekuwa akisimamia kwenye ukweli daima na pia alikuwa ni kiiongozi wa kuigwa katika kazi za uandishi na uhariri.
hili ni pigo kubwa na pengo lisilozbika kwa HALI HALISI PUBLISHER ambao ni wachapishaji wa magazeti ya mwanahalisi na mseto.
Sisi tulimpenda lakini mungu alimpnda zaid.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPOONI.
.....AAMEN........

Monday, April 5, 2010

mating'a ya pasaka

Baada ya mizunguko kibao ya hapa na pale katika mihangaiko ya dunia hii huwa natulia geto na kuendeleza kazi ambazo sikuzimaliza maofisini.
kaka mkubwa SALUM SULEIMAN a.k.a ALONE Mc the DON akiwa na B. TWANGALA wa clouds FM.
Washkaji kutoka River camp waliwakilisha vy kutosha kabisa pande zile za coco beach katika kuwarusha wadau wa burudani pasaka yote!
na hili ndio nyomi lililokuwepo pale coco.
Hapa ni mashabiki waliofurika coco beach katika kuisherehekea pasaka na wasanii kibao tu walipafom pale
mtu mzima Farid akiimba na mashabiki wake.
Mashabiki wakimshangilia Fid Q.
Farid kubanda a.k.a Fid Q akiimba na mashabiki wake waliofurika katika kumpa shavu pande zile za coco beach.
Kubanda Mwnza mwanza akiwasikiliza mashabiki wake kile wanachokihitaji kutoka kwake.
Mtu mzima Ncha kali akiwa sambamba na Farid kubanda wakati wakichana songi lao la shimi limetema.
Mtu mzima Dj Chioka akiwa klwenye moja na mbili akiwarusha wapenzi wa burudani waliofurika kwenye viwanja vya coco beach
Hapa ni Chege Chigunda akimkabidhi Dj Choka cd yake ambayo allitumia katiak kuwapa burudani mshabiki wake.

Sunday, April 4, 2010

Za ukweli!

Mwanaenu wakitaa hapa nipo na mkali wa kusugua cd a.k.a DJ CHOKA kabla hajaingia mtamboni katika moja na mbili kuwapa burudani wale waliofika pande za coco beach.
Hapa ni mtu mzima SALUM SULEIMAN a.k. ALONE Mc the DON akiwa na mkali wa krank QWCK RAKA pale coco beach.
Hapa ni SALUM SULEIMAN a.k.a Alone Mc the DON, akiwa na mjomba MRISHO MPOTO na mrembo wa mmoja wa filamu nchini anaiotwa MARRY pale coco beach.