Monday, December 23, 2013

KASEBA AMCHAKAZA ALIBABA KWA K,O RAUNDI YA 4

http://1.bp.blogspot.com/-wPIEWnTbm8Q/UrdiSsKinsI/AAAAAAAAECA/5NaSAHTncn8/s1600/IMG_0236.JPG 
Bondia Japhert Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Alibaba Ramadhani wakati wa kugombania ubingwa wa Taifa uliofanyika Manzese Dar es salaam Kaseba alishinda kwa KO ya raundi ya nne ya mpambano huo.
Picha na superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, December 1, 2013

MABONDIA JAPHET KASEBA, ALIBABA KUZIPIGA DESEMBA 21 FRIENDS CORNER HOTEL DAR

http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2012/06/Kaseba.jpg
Japhet Kaseba
http://2.bp.blogspot.com/-_Y_l71REAdA/Upiv_Zr5QgI/AAAAAAAA7eo/7sQASsTpCVg/s1600/Alibaba+Ramadhan.jpg
Alibaba Ramadhan

 Na Mwandishi Wetu
Mabondia Japhet Kaseba wa jijini Dar es Salaam, na Alibaba Ramadhan wa jijini Arusha, wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 Decemba, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner hotel,kuzichapa katika pambano la ubingwa wa pst.

Pambano hilo liloandaliwa na Promota Ibrahim Kamwe chini ya  BigRight Promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kama Karage Suba na Fadhil Awadh, watakaozichapa kuwania ubingwa wa Mkoa katika uzito wa wealter Kg66 pambano la raundi kumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe, alisema kuwa  zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa, pia mahasimu wawili wa uzito wa juu Lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku Kheri (ndota) ikiwa ni marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi.

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni pamoja na Bondia Adam Yahaya (Baby Edo) atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku (Tyson) atacheza na Shah Kassim,  kukumbushia Enzi za akina Stanley Mabesi , Jocky Hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena Rajabu.

Wengine ni Issa Omar  atazipiga na Haji Juma wa Tanga, Moro Best atapigana na Shafii Ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengera.

Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huo na wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.

kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi kutoka Kampuni ya Kiwango Security na jeshi la polisi amblo limeahidi kutoa mchango mkubwa ili kufanikisha pambano hilo.

Friday, November 22, 2013

MOJA YA KAZI ZA KUTOKA SULE'S INC. & ENTERTTINMENT (SHOOTING KATIKA SEND-OFF PARTY YA DADA JULIETH MASAWE)

Sule Junior (kulia) na Alex Nyaganilwa wakiwa kwenye kamera kuhakikisha wanadaka kila tukio.
Julieth (kushoto) akiingia ukumbini sambamba na mpambe wake.
Kitu cha ndafu kama kawa
Julieth akikata keki
Kamati ya maandalizi ya sherehe ikinyanyua keki juu ishara ya umoja
Julieth Masawe akiwa na mumewe wakati wa Send-off
Watu wakiserebuka makwaito katika kufurahia sherehe.

SULE'S INC. & ENTERTTINMENT wanafanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na video production za matukio mbalimbali kama harusi, send-off, kichen party, mahafali na sherhe za aina zote.
WAPO KAWE MZIMUNI KARIBU NA KITUO CHA KANISANI 
Wasiliana nao kwa +255 719 694086 / +255 767 007515 /+255 715 379691

Wednesday, November 13, 2013

COUNTRY BOY NDANI YA AMBASADORS LOUNGE

 
Country Boy Ndani Ya Ambassadors Lounge Ijumaa Hii Tarehe 15.11.2013 Ni Birthday Party Yake Na Pia Anatambulisha Audio Na Video Ya Wimbo Wake "Watch Me" Feat Gnako,Host Wa Show Ni Kajala,Guest Performances By Mirror,Babuu Wa Kitaa,Chibwa,Tash Na Surprises Nyingine Zitakuwepo,Dj Steve B/Dj Skills,Dvj Ally B Na Dj Masu On The Set,Entru 10,000 shs kuanzia Saa 3 Usiku

Friday, October 25, 2013

Thursday, October 24, 2013

KICHUPA CHA MWANAMBUZI KIPO TAYARI, MDAU KAA MKAO WA KUKITAZAMA SIKU YEYOTE KUANZIA LEO

Video hii ya wimbo wa Mwanambuzi ulioimbwa na msanii Wynem, imefanyika katika production ya Sule's Inc. Chini ya Director, Sule Junior (Salum Suleiman)

Thursday, October 17, 2013

BONDIA, CHUGA BOY ALIVYO MSAMBALATISHA ISMAIL KAJIMA


Bondia Amani Bariki 'Chuga Boy' kushoto akipambana ya Ismail Kajima wakati wa mpambano wao uliofanyika Mbezi kwa Msuguli katika ukumbi wa Samunge Dar es salaam siku ya kusherehekea sikukuu ya Idi Chuga boy alishinda kwa pointi.

Bondia Amani Bariki 'Chuga Boy' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ismail Kajima wakati wa mchezo wao uliofanyika mbezi kwa msuguli ukumbi wa Samunge Dar es salaam wakati wa kusherehekea sikukuu ya Idi Chuga Boy alishinda kwa point mchezo huo.

Chuga Boy akitangazwa mshindi wakati wa mpambano huo
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, October 2, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA PANANDI PANANDI ILALA OKTOBA 26


Kocha wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto) akiwaelezea jambo masahabiki wa mchezo wa ngumi kuhusu DVD zinazoonyesha mafunzo mbalimbali ya Mchezo huo.

Na Mwandish Wetu

MPAMBANO mwingine wa masumbwi kufanyika katika ukumbi wa panandi panandi Oktoba26 mpambano huo wa mchezo wa masumbwi utakaokuwa chini ya uratibu wa Kinyogoli Fondition utawakutanisha mabondia mbalimbali wenye majina na wanaotamba kwa sasa katika anga za masumbwi nchini.
Akizungumzia mchezo huo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka kambi ya ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano huo utawakutanisha bondia Yakubu Maganga atakae zichapa na Ubwa Salumu katika uzito wa kilo 75 huku Seif Ali akipambana na Hassani Labanda pamoja na mipambano mengine ya masumbwi itakayo wakutanisha mabondia mbalimbali Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama.Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi

Monday, September 30, 2013

J DEAL FT G'NAKO - NIIMBIE (Official Audio Release)

Download "Niimbie" wimbo toka kwa mkali ya R&B, J Deal au ukipenda "Jacob Deal" akiwa na Gnako the A City Kankara aka WaraWara. Wimbo ni category ya R&B toka studio za Noizmekah Arusha chini ya Producer Defxtro, kuusikiliza bofya HAPA na kwa mawasiliano zaidi check na J Deal kupitia +255 718 515 772

JIMMY MASTER FT KISUKE & SPAC DAWG - BADO NASO

Download "Bado Nahaso" wimbo wa JimmyMaster akiwa amemshirikisha Kisuke Matoke & SpacDawg mzigo toka studio za Noizmekah Arusha bofya HAPA kuisikiliza ngoma na kwa mawasiliano zaidi check na Jimmy Master aka Mnyampaa kwa nambari +255 655 499 318 powered by www.vmgafrica.com