Monday, May 30, 2016

HABARI PICHA: BASATA, HAANNEEL WAZINDUA MATUKIO YA SIKU YA MSANII KWA MWAKA 2016

Mkurugenzi wa Kampuni ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka ambayo ni waandaaji wa Siku ya Msanii akimwongoza Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kutia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kuzindua matukio ya Siku ya Msanii (SYM, 2016) kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise mwishoni mwa wiki.   
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ndilo mbunifu na mmiliki wa maadhimisho ya Siku ya Msanii nchini Godfrey Mngereza (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi (Katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni mwendeshaji wa Siku ya Msanii ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka mwishoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 katika Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam.
Msanii maarufu wa kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akisaini kitabu cha wageni kabla ya kushuhudia hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise ulioko jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi. Vivian Shalua (Kushoto) akifuatilia kwa makini moja ya matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francoise mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Msanii wa Sanaa za Ufundi Gozbetha Rwezaula.
Marais wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini kutoka kushoto Symon Mwakifamba (Filamu), Adrian Nyamangale (Ufundi), William Chitanda maarufu kama MC Chitanda (Sanaa za Maonesho) na Addo November (Muziki) wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali ya uzinduzi wa matukio ya Siku ya Msanii mwaka kwa mwaka 2016
Kikundi cha Sanaa cha Safari kikitoa burudani kwenye hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam
Msanii maarufu wa Sanaa za Uigizaji na Filamu Ahmed Olutu maarufu kama Mzee Chiro akitabasamu na Msanii mwenzie Thecra Mjata wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio ya hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 

MH. JANUARY MAKAMBA ALIPOTEMBELEA JAMII YA WAFUGAJI WA KIMASAI JUZI JUMAMOSI

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya parakuyo ambao wengi wao wanatokea kwa familia za kifugaji   
akizungumza na baadhi ya wazazi katika kijiji cha parakuyo
Akisaliamana na Wananchi  waliojitokeza kumpokea kijijni hapo
Akivishwa Vazi rasimi la kiamasai
AKizugumza na wananchi wa Parakuyo