Tuesday, September 27, 2011

MATUMLA NA FRANSIS MIYAYUSHO WATUNISHIANA MISHULI

 Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) naMbwana Matumla kulia wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa Mabara (UBO) Dar es Salaam , utakaofanyika mwishoni mwa mezi ujao katikati ni mratibu, Mohamed Bawazir.

Monday, September 26, 2011

MAGESE AINGIA KWENYE GEMU LA MUZIKI

Sikiliza ngoma yake aliyoipa jina la KIDOGO akiwa amemshirikisha Asarh 
isikize na kudownload (FOR PROMO ONLY)

NGOMA MPYA YA JCB - DUNIA KIZANI

klick (bofya) hapo chini kwa kusikiliza na kuudownload for promo only!

Sunday, September 25, 2011

JCB AACHIA DUNIA KIZANI.

Msanii kutoka Arachuga a.k.a Arusha pale kona za kijenge ya juu, JCB anatarajia kuachia ngoma yake mpya hivi karibuni
Akipiga stori na mtoto wa Kitaa JCB alisema "kaka mimi naamini watu kama wewe ni wa muhimu sana katika hili gemu letu la muziki maana harakai zako zinaonekana kaka!" pia katika kuuzungumzia muziki JCB alisema "kaka natarajia kuachia ngoma yangu mpya inaitwa DUNIA KIZANI , Ngoma hii nimeifanya pale kwa Lamar na pia katika ngoma hii nimemshirikisha mtu mzima Hardmad.

Friday, September 23, 2011

CHEK VIDEO YA JAFARAI ft WYREJaffarai - MCHARUKO (Official Video HQ)

AJALI YA MBEYA

Polisi wakiangalia gari aina ya roli lenye namba IT.9518, lililopata ajali baada ya kugongana na gari jingine na hivyo kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu watembea kwa miguu na kuvunja nyumba
Gari lenye T.438 BRT aina ya Landovermali ya mchungaji Nduka wa kanisa la Uinjilist Mbalizi. Ambalo liligongana na Lori hilo.
Taswira ya mbele ya Lori hilo lililosababisha hasara kumbwa.

Picha zote na Latest News Tz


Wednesday, September 21, 2011

BASATA YAHIMIZA USAJILI WA KUMBI NA WASANII


 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, BASATA Bw.Angelo Luhala (Kulia) akisisitiza jambo wakati akiongea na wasanii juu ya umuhimu wa wadau wa sanaa kujisajili kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu makao makuu ya Bara hilo. Alizungumzia pia ya haja ya wasanii kulinda haki zao. 
Mkuu wa Kitengo cha Matukio, BASATA Bw.Omary Mayanga (Kushoto) akizungumzia juu ya haja ya wasanii kuzingatia mikataba kwenye kazi zao katika Jukwaa la Sanaa Jumatatu wiki hii. Katikati ni Bw.Luhala na Kaimu Mratibu wa Jukwaa la Sanaa Bi. Agnes Kimwaga.
Mdau Kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akichangia mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.

Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wamiliki wa kumbi za burudani nchini kuhakisha wamezisajili huku likitoa wito kwa wasanii na wadau wa sanaa nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kujisajili.
Akizungumza kwenye programu ya kila wiki ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz), Mwenyekiti wa kamati ya usajili, BASATA Bw. Angelo Luhala alisema kwamba, kwa mujibu wa sheria suala la kujisajili ni la lazima.
“Naanzia kusema hapa, kila anayefanya kazi yoyote ya sanaa ni wajibu ajisajili, kujihusisha na shughuli za sanaa bila kujisajili ni kuvunja sheria,kanuni na taratibu za nchi” alisema Luhala.
Alizidi kueleza kuwa, kwa mujibu wa sheria ya nchi namba 23 ya mwaka 1984 Baraza limepewa mamlaka ya kusajili na kusimamia sekta ya sanaa nchini, hivyo mtu yeyote anayefanya shughuli za sanaa anapaswa kusajiliwa na kupewa kibali cha kufanya shughuli hizo.
Aliongeza kuwa, sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, hivyo kila anayefanya kazi ya sanaa hana budi kutambuliwa na serikali na Baraza kwa niaba ya serikali limepewa kazi hiyo.
Kwa mujibu wa Bwana Luhala wadau wanaopaswa kujisajili BASATA ni pamoja na wasanii wa fani zote, wakuzaji sanaa (mapromota), vikundi vya wasanii, kumbi zote za burudani, wafanyabiashara wa sanaa, vyama na asasi mbalimbali za sanaa.
Akizungumzia faida za kujisajili, Bw. Luhala alisema ni pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi, kutambuliwa na serikali, kupata utambulisho wa Baraza katika mahitaji mbalimbali, fursa za kushiriki maonyesho, taifa kuwa na takwimu sahihi za wadau wanaojihusisha na shughuli za sanaa na faida nyingine..
“Kuna watu wanajiuliza kwa nini wasajiliwe, lazima ieleweke kwamba, kila anayejihusisha na shughuli za sanaa lazima atambuliwe na serikali. Hapa ndipo tunapata takwimu pia” alisisitiza Bw. Luhala.
Wadau mbalimbali waliohudhuria programu hiyo walionekana kuwa na shauku kubwa kwani mbali na suala la usajili, Baraza lilitoa elimu kwa wasanii juu ya kulinda haki zao ikiwa ni pamoja na wasanii kutakiwa kujisajili kwenye chombo kinacholinda Hakimiliki na shiriki cha Cosota.

Tuesday, September 20, 2011

iP SPORTS YAKAMILISHA UTENGENZAJI WA JEZI ZA MICHEZO

Katibu mkuu wa iP Sports club iliyo na maskani mitaa Msasani Jijini Dar es Salaam-Dimo Debwe akiwaonyesha jersey Kwa wadau,wapenzi na Mashabiki wa Club iyo ili kuchangia mawazo yao katika Jersey hiyo. image Profession Sports Club iliyotambuliwa na kusajiliwa na Balaza la Michezo Tanzania (BMT) ni club ya michezo mbali mbali ikiwemo Football,Video Game,Swimming,Longtennis and Short tennis,Bicycle n.k.. kwa upande Mpira wa miguu tayari tumeshacheza mechi za kirafiki na Simba B, Azam B, Tanzania Bloadcasting Coproration (TBC), Independent Television-IPP Sports Club, Sahara Communications-Star TV na nyingine nyingi sana. Picha nikiwa na mtoto Machachari Ahmed Mohamed Omar, 
 Athumani Uwakika na Hussein Hoza wachezaji wa iP Sports

MWANAUME AOTA MATITIBAADA YA KUTUMIA DAWA ZA UKIMWI

BAADHI ya wanaume wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa za kurefusha maisha wamejikuta wakivimba matiti yao na kuwa makubwa kama ya wanawake. Vilevile, wanawake wanaotumia dawa hizo wanalalamika kukutwa na matatizo kadhaa ikiwa ni pamoja na ulemavu.
Joseph Mkanda (43) amekumbana na tatizo la dawa hizo ikiwa ni pamoja na kuvimba matiti.  Mwanzoni alihisi ni kutopata chakula bora, lakini akagundua kwamba ni aina za dawa anazotumia.
“Naona aibu sana kutoka nje ya nyumba yangu, kwani nimepata matiti kama mwanamke….  Naona watu wakiniona watanicheka,” anasema mwananchi huyo ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Mtwara.
“Nilipokwenda zahanati ya kijijini nikaambiwa hilo ni jambo la kawaida kwa watu walioathirika na Ukimwi, hivyo sijui la kufanya wala pa kwenda,” anasema Mkanda.
Mwanamke Salima Omar (36) mwenye watoto saba  kutoka Mtwara anasema mwili wake umekumbwa na matatizo kibao tangu aanze kutumia dawa hizo.  Mmoja wa watoto wake wa kike alifariki mwaka 2006 muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwake.
Hata hivyo, Salima ambaye ni mke wa Hassan, na ambaye mwili wake umejaa vipele, na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, anaamini hali hiyo inatokana na kutopata lishe bora.
“Madawa haya ni makali mno, usipokula vizuri ni lazima yataivuruga afya yako,” anasema na kuongeza kwamba kuna siku analazimika kuyatumia madawa hayo bila kula chochote hususan anapokuwa mgonjwa sana
Mwanamke huyo anasema kuna wakati hayatumii madawa hayo kutokana na ukosefu wa fedha ya chakula, kwani mumewe ni fundi wa baiskeli na yeye (Salima) hupoteza fedha anazopata kwa kunywea pombe.  Hali hiyo  imemsababishia kuuza mbuzi wote wa familia yake ili kumudu maisha.
Kama zilivyo familia nyingi katika Wilaya ya Mtwara ambazo zinakabiliwa na upungufu wa chakula tangu mwaka 2007, Salima naye yuko katika mkumbo huo.
Vilevile, licha ya kuwa mwathirika, mwanamke huyo bado anaendelea kuzaa.  Miezi mitatu iliyopita alizaa mapacha ambapo mmoja wao alifariki na mwingine hali yake ni mbaya.
Hata hivyo, wataalam wa tiba wamewashauri wanandoa hao kuacha kuzaa, jambo ambalo huenda wakakubaliana nalo.

Sunday, September 18, 2011

KITU CHA OFFSIDE TRICK

THE FIRST TIME EVER IN READING BONGODEEJAYS PROUDLY PRESENT OFFSIDE TRICK FEATURING RUSHA ROHO NITE!!! Yes all my Africans we back.......!SAt 1st OCT 2011 @ FACE CLUB RG1 7JE.READING xxxxxx

ATRACTIONS We will be giving away free bottle of Champagne FOR THE BEST DRESSED GENTLEMAN & LADY ON THE NITE

WAKAZI WA MWANZA WAVUNJIWA NYUMBA ZAO..!!

Zaidi ya wakazi 100 wa MTAA WA MIEMBE GIZA – KATIKA MLIMA WA KISEKE WILAYANI ILEMELA JIJINI MWANZA WAMEAPA KUTOHAMA KATIKA ENEO HILO KUTOKANA NA MWENYEKITI WA MTAA WA MIEMBE GIZA BWANA KAMANI KUVUNJA MISINGI YA NYUMBA 35 NA NYUMBA ZAIDI YA 100 WALIZOKUWA WAMEJENGA HIVYO KUWASABABISHIA HASARA NA UPOTEVU WA MALI ILE HALI BAADHI YA NYUMBA WANAZODAI KUWA NI ZA MATAJIRI ZIKIBAKIA KATIKA ENEO HILO BILA KUVUNJWA.
Wakizungumza na blogu hii katika eneo la tukio wananchi hao wamesema kuwa mnamo mwezi September 3 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni Mwenyekiti wa mtaa huo bwana Kamani akiongozana na watu wake kwa kutumia nguvu alibomoa nyumba na misingi ya nyumba za wakazi hao hali ambayo wanadai ni makosa na haikuwa sahihi. Kupitia amri ya mwenyekiti wa kitongoji hicho nyumba nyingi zimebomolewa, mali kuharibiwa na nyingine kupora huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiachwa hawana mahala pa kujisitiri.

Monday, September 12, 2011

TEMEKE KINONDONI NANI ZAIDI KATIKA MASUMBWI

Issa sewe

Na Mwandishi Wetu Kambi ya Ilala

MABONDIA Mbwana Matumla wa Temeke na Francis Miyeyusho wa Kinondoni Dar es Salaam wanatarajia kupanda ulingoni katika pambano la kudhihirishiana ubabe kati ya mabondia wa Temeke na Kinondoni litakalofanyika Oktoba 30 mwaka huu.
Pambano hilo pia litafuatiwa na lingine kati ya Ramadhani Shauri wa Kinondoni dhidi ya Issa Sewe wa Temeke ambapo yote yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Msaidizi wa Kambi ya Kinyogoli Foundation ya Dar es Salaam, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema mapambano hayo yameandaliwa na Promota Mohamedi Bawaziri kuhamashisha mchezo huo.
"Mabondia wote wameanza mazoezi na kwa upande wa Temeke wapo kambini chini ya Kinyogori Foundation chini ya kocha Habibu Kinyogori akishirikiana na mimi na tunawaandaa kucheza ngumi za kisasa sio kurusha ngumi bila mpangilio.," alitamba Super D
Alisema pambano kati ya Matumla na Miyeyusho litakuwa  la uzani wa Bantam Weight kilogramu 54 ambapo Shauri na Sewe watacheza kilogramu 58, uzito mwepesi (Light Weight).
Alisema licha ya kuhamasisha, kumekuwepo na tambo za mda mrefu kati ya mabondia wa Kinondoni, na wenzao wa Temeke ambapo mashabiki watajionea mapambano hayo.
Kocha huyo alisema mapambano hayo yatasindikizwa na mengine kutoka kwa mabondia wa Temeke na Kinondoni ambapo pia kutakuwepo na burudani mbalimbali zitakazotangazwa baadae.

--
Super D Boxing Coach

WASOMI WATAKIWA KUFANYA TAFITI KWENYE SANAA

Mhadhiri wa Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Profesa Elias Jengo akitoa historia fupi ya Idara hiyo toka ianzishwe.Kulia ni Mgeni rasmi na Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego.
Profesa Elias Jengo (Katikati) akimuonesha Katibu Mtendaji wa BASATA,Bw.Materego (Kulia) moja ya kazi za Sanaa zilizoandaliwa na wanafunzi wa Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kundi la Parapanda Art,Mgunga Mwamnyenyelwa (Kulia) akiwafafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee waliofika kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Idara ya Sanaa.
Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ambaye ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw.Materego akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.


Na Mwandishi Wetu
 
Wasomi nchini wametakiwa kujikita kwenye tafiti na kuandaa machapisho kuhusu tasnia ya sanaa nchini kwani kumekuwa na uhaba mkubwa wa vitabu na takwimu katika eneo hilo.
Wito huo umetolewa wiki hii na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw.Ghonche Materego kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 toka kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu hicho na kufanyika kwenye viwanja vya idara hiyo.
“Tunahitaji kujenga uwezo wa wanafunzi wetu ili kuwa na wataalamu waliobobea katika utafiti,hasa ukizingatia kuwa tafiti katika tasnia mbalimbali za sanaa hapa nchini bado siyo za kutosha sana” alisema Materego.
Aliongeza kwamba,kukosekana kwa machapisho na utafiti kwenye tasnia hii ni chanzo cha wasanii kukosa taaluma muhimu kwa maendeleo na ubora wa kazi zao lakini pia kukosa urithishwaji wa taaluma hii kwa vizazi vijavyo.
“Tunahitaji kuongeza machapisho yanayotokana na wataalamu wetu na kutoka Idara hii,ili kuwawezesha wasomi na wasanii wetu kupata maarifa yanayotokana na mitazamo na falsafa zetu kama wanataaluma wa Kitanzania na Kiafrika” alisisitiza Materego.
Katika hili aliweka wazi kuwa,kuongeza idadi ya wasomi bila kujikita katika utafiti na kuandaa machapisho ya tasnia hii si maendeleo yanayojitosheleza.
Awali akitoa historia ya Idara hiyo,Mhadhiri wa Sanaa Profesa Elias Jengo alisema kwamba ilianza kwa kutoa taaluma ya Sanaa za Maonyesho mwaka 1966 huku ikiwa na wanafunzi wachache sana kabla baadaye Machi 1975 haijabadilishwa na kuwa Idara ya Sanaa,Muziki na Sanaa za Maonyesho.
Aliongeza kwamba,kwa sasa Idara hiyo ina jumla ya wanafunzi kati ya 50-70 huku ikiwa na mafanikio mbalimbali ya kujivunia katika tasnia ya Sanaa.
 
Kampuni ya Sule's inc. & Entertainment ikishirikana na Image Profession nakuletea maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru katika soka! 

KAA TAYARI!!!!

Monday, September 5, 2011

JOYCE KIRIA AOLEWA TENA KWA MARA YA PILIBw Henry John Kileo na Bi Joyce Kiria Walipofunga ndoa yao jana Jumapili(JANA) na baadae ilifanyika bonge la pati katika hoteli ya Atrium pande za Afrika Sana - Sinza.
NI mara ya pili kwa Joyce kilia kuolewa ndani ya kipindi cha muda mfupi baada ya kutalakiana na mumewe wa ndoa ya kwanza Dj Nelly...tears to nelly duuu.

BEACH MOJA HIVI MITAA YA KATI

Sunday, September 4, 2011

WIMBO MPYA WA SAGNA (YAMENISHINDA)


Huu ni wimbo mpya kabisa wa msanii wetu SAGNA unaitwa YAMENISHINDA. Wimbo huu ni mwendelezo wa story iliyopo katika wimbo wake uliopita wa MGANGA. Mwanzo tulipanga kuu release kwenye radio stations Jumatatu ya wiki ijayo ila kuna mabadiliko kidogo sasa unaweza kuanza kupigwa muda wowote.
Video za nyimbo zote mbili MGANGA pamoja na YAMENISHINDA zinakuja very soon.

SAGNA - YAMENISHINDA


CREDITS:
Track Name: YAMENISHINDA
Artist : SAGNA
written by: SAGNA, JOSEFLY & KID BWOY
arranged by: KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
SEPTEMBER 2011


IMAGE PROFESSION WAANDAA MASHINDANO YA UCHORAJI

Kampuni ya IMAGE PROFESSION ya jijini Dar es Salaam imejitokeza na kuandaa mashindano ya vipaji vya uchoraji katika mashule ikiwa ni pamoja na vyuo vyote nchini Tanzania. Hii ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya UHURU wa Tanzania