Friday, March 30, 2012

OFISI ZA TIGO MLIMANI CITY YAFUNGULIW

Waziri wa viwanda na biashara Dkt.Cyril Chami akikata utepe kuashiria uzinduzi huo leo kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tigo Bi.Hilda Damas
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo waliokuwepo katika ufunguzi huo wakiwa katika picha ya pamoja leo
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akipatiwa maelezo ya moja ya bidhaa za simu zilizopo
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt, Cyril Chami akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya tigo baada ya kuzindua ofisi ya huduma kwa wateja baada ya matengenezo makubwa mlimani city leo

Tuesday, March 27, 2012

TOMASI MASHARI AJIFUA KUMKABILI SELEMANI GALILE APRIL 9

Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9.
Bondia Tomasi Mashari akifanya Mazoezi leo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Selemani Galile litakalofanyika April 9.
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi yake ya  kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9

Monday, March 26, 2012

ILIVYOKUWA KWENYE MEDIA DAY (SIKU YA WAANDISHI WA HABARI)

Hii ndio ilikuwa meza ya waandishi kutoka Mwananchi!
Hapa waandishi kutoka mwananchi tukiwa kwenye mechi ya Vollyball
Mtu mzima Sule Junior nilikuwa fiti kwnye Boxing!
Tukisherehekea ushinndi.
Hapa na mwanangu Issah Habib tukishoo lav na kikombe chetu!
Kuanzia kushoto ni Henry Mdimu, Issah Habib na Danny Mzena wakishoo lav na kamera ya mtoto wa kitaa
Kuanzia kushoto ni Henry Mdimu, Danny Mzena na Dullah wakishoo lav na kamera ya mtoto wa kitaa
Kuanzia kushoto ni Issah Habib, Sule Junior na Jerome Risasi wakishoo lav na kamera ya mtoto wa kitaa
 
Issah Habib na Sule Junior 
 
Sule Junior na Allan Goshashi
Sule Junior na Jabir kuotoka Mwanahalisi
Waziri Sitta ambaye ndye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wanahabari
Foleni ya Chakula
Burudani kama kawa
Mzee wa Habari na matukio (kulia) akisakata dansi

Friday, March 23, 2012

IMAGE PROFESSION KUFUNGA MASHINDANO YA UCHORAJI KESHO.

KUFUNGWA KWA MASHINDANO YA UCHORAJI NA KUTOA ZAWADI
Siku ya Jumamosi tarehe 24/03/2012 kutakuwa na kufungwa na kugawa zawadi kwa washindi wa Mashindano ya Uchoraji yaliyobeba kichwa cha Habari cha Miaka 50 ya Taifa yakishindanisha Tasisii za Elimu kuanzia shule za awali , Msingi, Sekondari na Vyuo, mashindano yaliyoandaliwa na Image Profession.
Hafla ambayo itatanguliwa na maonyesho ya picha za washiriki wa shindano pamoja na kuonyesha picha za wachoraji wazoefu kuanzia saa 11 :00 (Saa Tano) asubuhimpaka saa 14 :00 (Saa Nane) Mchana kwenye Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa makabala na Chuo cha Fedha(I.F.M.)
Njoo ushuhudie Vipaji katika Sanaa za Uchoraji ,njoo uwape moyo Washiriki na pia uweze kujifunza mambo mengi yahusuyo sanaa hii ya uchoraji.
Pia Njoo ujuwe kichwa cha habari cha Mashindano ya Mwaka huu 2012.
WENU KATIKA UJENZI WA SANAA NA MICHEZO
Image Profession & iP Sports Club
22/03/2012

CHADEMA KUFANYA KAMPENI NA HELKOPTA ARUMERU MASHARIKI

Neville Meena na Mussa Juma, Arumeru
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilianza kutumia helkopta katika kampeni zake za kumnadi mgombea wake wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Habari ambazo gazeti hili limezipata zinasema helkopta hiyo itaendelea kutumika hadi siku ya mwisho ya kampeni na kwamba itakiwezesha chama hicho kufanya mikutano kati ya mitano hadi minane kwa siku.
Mkuu wa Operesheni wa uchaguzi wa Chadema katika jimbo hilo, John Mrema alisema kuanza kutumika kwa helkopta hiyo kutamwezesha mgombea wao kufanya mikutano mitano kwenye kata tano tofauti.
Mikutano ya jana ilifanyika katika vijiji vya Ngurdoto Kata ya Maji ya Chai, Ngabobo Kata ya Ngarenanyuki, Kijiji cha Sakila Kata ya Kikatiti na vijiji na kata za King’ori na Nkoanrua.
Helkopta hiyo ilianza kuonekana katika anga la Usa River, Arumeru jana asubuhi na hakukuwa na taarifa za awali kuhusu ujio wake kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikifanya katika kampeni nyingine zilizotangulia.
Helkopta hiyo yenye maneno makubwa CHADEMA, ilitumika wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho zilizofanyika katika Uwanja wa Shule ya msingi Leganga, Usa River Machi 10 mwaka huu na tangu wakati huo haikuwahi kuonekana tena hadi jana.
Dk Slaa na ardhi
Katikamikutano ya jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alimshambulia Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Gudluck Ole Medeye kwamba anahusika na kukodisha shamba la Valesca lililo Jimbo la Arumeru Mashariki kwa wawekezaji kwa bei ya kutupa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ngabobo, Ngurdoto na Sakila, Dk Slaa alisema ni aibu mawaziri wa Serikali ya CCM kuomba kura katika Jimbo la Arumeru Mashariki huku wakiwa ni waasisi wa mpango wa kugawa ardhi ya umma kwa walowezi wa kizungu.
Alisema Naibu Waziri huyo, ambaye ni mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, kabla ya kukubali kutolewa shamba hilo lenye zaidi ya ekari 400 ambalo Serikali itapata kiasi cha Sh2.4 milioni tu kwa mwaka walipaswa kuwakumbuka wananchi.
“Hivi kweli nyie wananchi wa Meru hamuhitaji ardhi hii na mngeshindwa kulipa Sh6000 kwa ekari moja ili muweze kulima, kama alivyouziwa mzungu? ” alihoji Dk Slaa.
Aliwataka wakazi wa jimbo hilo, kukubali mabadiliko sasa kwa kuchagua mbunge wa upinzani ili aweze kuhoji ardhi ya Meru ambayo kiasi kikubwa kimegawanywa kwa walowezi kutoka nje ya nchi.
Vituo bandia
Wakati hayo yakiendelea, tuhuma kwamba kuna vituo 55 vya bandia vilivyoandaliwa kwa lengo la kutumika kuiba kura kwenye uchaguzi huo, zinaonekana kugonganisha vichwa vya maofisa wa uchaguzi.
Tuhuma hizo ni zile zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa juzi kwamba kuna vituo 55 bandia 55 vya kupigia kura katika uchaguzi huo mdogo madai ambayo yalikanushwa na Msimamzi wa Uchaguzi wa Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi.
Juzi Kagenzi alipozungumza na waandishi wa habari alisema vituo halali ambavyo anavitambua ni 327 tu na hakukuwa na kituo ambacho kimeongezwa na kwamba hata kama ikitokea hivyo, itakuwa ni baada ya majadiliano na vyama vyote shiriki.
“Vituo vilivyopo ni 327 pekee, na kama ikitokea kituo kinakuwa na watu zaidi ya 500 ndipo kunaweza kuongezeka, lakini historia inajionesha kila uchaguzi mdogo unapofanyika idadi ya wapigakura inapungua,”alisema Kagenzi.
Lakini jana Kagenzi alikiri kuwapo kwa kasoro kwenye orodha ya vituo hivyo na kwamba alikuwa anawasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuwezesha kufanyika kwa marekebisho.
Maeleo ya Kagenzi yanatokana na ushahidi ambao gazeti hili liliupata kwa kuona orodha ya vituo hivyo, ambayo ilikuwa ikionyesha takwimu mbili tofauti za idadi ya vituo vya kupigia kura.
Katika orodha hiyo, safu ya idadi ya vituo vya kupigia kura katika kata 17 za jimbo hilo ilikuwa ikionyesha vituo 327, wakati safu ya mwisho ya orodha hiyo hiyo ilikuwa ikionyesha kuwapo kwa jumla ya vituo 382, likiwa ni ongezeko la vituo 55.
Waraka wa orodha hiyo unaonyesha kuwa katika Kata ya Akheri kutakuwa na vituo 20 idadi ambayo inayofautiana na iliyotolewa na tume ambavyo ni vituo 18.
Kata nyingine ambazo vituo hivyo vinaonekana kuongezwa ni Kikatiti vituo 22 badala ya 18, Kata ya Kikwe vituo 12 badala ya halali 11, Kata ya Kingori vituo 29 badala ya halali 26 na Kata ya Leguruki vituo 23 badala ya halali 20.
Kata nyingine ni Makiba vituo 21 badla ya halali 18, Majiya chai 24 badala ya 29 halali, Maroroni vituo 21 badala ya 17 halali, Mbuguni vituo 25 badala ya halali 21,Nkoarsambu vituo 10 badala ya 8 vinavyohitajika na Kata ya Ngarenanyuki ambako vimeongezwa vituo sita kutoka halali 20 hadi 26.
Orodha hiyo ambayo Kagenzi alithibitisha kwamba ilikuwa na makosa pia ina kasoro katika Kata za Nkoaranga ambako vituo vimeongezwa kutoka halali 17 hadi 22, Pori kutoka vituo halali 16 hadi 20, Nkwandua kutoka vituo 22 hadi kufikia 25 na Kata ya Seela - Sing’isi vituo hivyo viliongezwa kutoka halali 12 hadi 15.
Kata nyingine ni Songoro nyumbani kwa Mgombea wa Chadema, Joshua Nassari vipo vituo 15 na hakuna kilichoongezeka huku Kata ya Usa River ilikuwa na vituo 36, lakini vimeongezeka vitano na kufikia 41.
Kagenzi alisema alipowasiliana na idara ya teknolojia ya habari ya NEC kuhusu kasoro hizo walimwambia kwamba orodha ya awali haikuwa toleo la mwisho na kwamba wangefanya marekebisho ya kuondoa kasoro hizo.
“Wameniambia kwamba hiyo orodha ilikuwa ni working draft tu (rasimu ya kufanyiwa kazi), kwahiyo nimeomba hiyo orodha kamili ya mwisho, wakishanitumia nitaisambaza kwa vyama husika,”alisema Kagenzi jana.
Baadaye msimamizi huyo wa uchaguzi alisema wataalamu kutoka NEC walitarajiwa kuwasili Arumeru jana mchana kwa ajili ya kurekebisha kasoro hizo pamoja na kufanya maandalizi mengine kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo.
Hata hivyo, kauli ya Kagenzi ilikuwa ikipishana na ile iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Mallaba ambaye awali alisema hakukuwa na vituo vya nyongeza kama ilivyodaiwa na Dk Slaa.
Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Thursday, March 22, 2012

CHEKA VS MAUGO WAONESHWA MKANDA WA UBINGWA LEO

Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo Wametyambulisha rasmi mkanda huo ambao utashindaniwa Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa pambano hilo, Kaike Siraju alisema kuanikwa kwa mkanda huo kutaashiria kupamba moto kwa ambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo."Tunauanika mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda," alisema Kaike.Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo."Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D. 


VINEGA WALIVYOTIMBA MAHAKAMANI KISUTU JANA.

VINEGA wakiwa wanaingia Mahakama ya Kisutu
VINEGA wakiwa wanasikilizia kuitwa.
Picha ya pamoja ya vinega mara baada kumaliza ishu nzima ya mahakamani
VINEGA wakiwa kwenye gari kurudi MGENGE.

TAARIFA KWA UMMA:
JANA MAJIRA YA SAA 7 MCHANA VINEGA WENGI WALIKUWA PALE MAHAKAMA YA KISUTU ILI KUWEZA KUJUA NI MADAI GANI YALIYOWAFANYA WAITWE MAHAKAMANI...... 
MADAI AMBAYO KWA MUJIBU WA KARANI WA MAHAKAMA AMBAYE KESI HIYO ILIKUWA IMEFUNGULIWA JALADA NAMBA 294 KESI YA MADAI YA MWAKA 2011...
HAKIMU ANAITWA MOSHI NA KARANI WAKE ANAITWA GRACE ALIWAAMBIA VINEGA KUWA KESI ILIKUWA JANA JAMBO AMBALO SIO KWELI NA PILI KESI ILIFUTWA JANA.....
TUNAYO MASWALI MENGI SANA TUNAYOJIULIZA JUU YA MADAI HAYA AMBAYO MPAKA SASA VINEGA HAWAJAYAJUA.......
ISSUE IPO CHINI YA KITENGO CHA SHERIA NA MUDA SI MREFU TUTAUAMBIA UMMA WA WATANZANIA NINI KINAFUATA JUU YA MSALA HUU WALIOJITAKIA WAFU FM.....!!!!
TUNAPENDA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WADAU NA VINEGA WOTE WALIOKUJA KUTOA SAPOTI KWA MAGENGE YA MWENGE NA ANTIVIRUS KWA UJUMLA. TUNAJUA WENGINE WALISHINDWA KUJA KWAKUBANWA NA MAJUKUMU ILA HAKIJA ARIBIKA KITU KWANI BADO TUKO PAMOJA.