Monday, March 12, 2012

MAN U YAREJEA KILELENI


MANCHESTER, England
MANCHESTER United imefanikiwa kurejea kileleni katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga West Brom mabao 2-0, wakati Manchester City ikipata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Swansea City. Man United ambayo ilikuwa ikishika nafasi ya pili kabla ya mechi ya jana kwa muda mrefu, imefanikiwa kupanda kileleni kwa tofauti ya pointi moja, ambapo kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi 67 wakati Man City ina 66 na timu zote zikiwa na mechi 28.Katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, Wayne Rooney ndiye aliyeipatia Man United mabao yote mawili katika dakika ya 31 kisha kumalizia la pili kwa penalti dakika ya 71. 
Kwenye Dimba la Liberty, Luke Moore ndiye aliyefunga bao pakee la Swansea katika dakika ya 83. Man City ilipigana kusawazisha bao hilo lakini hali ya mambo ilikuwa ngumu.

No comments:

Post a Comment