Saturday, December 31, 2011

RAIS KIKWETE, LEO AMUAPISHA BALOZI SEFUE KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI, BADALA YA LUHANJO

00.jpg
 Balozi Ombeni Yohana Sefue, akiwa ukumbini wakati akisubiri kuapishwa rasmi kushika madaraka ya Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
0.jpg
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia katika ukumbi wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, aliyeapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo.
001.jpg
 Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo (kushoto) akimkabidhi nyaraka za serikali maalum kwa kuapishiwa na Biblia, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ili kuanza kuapishwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salam leo.
002.jpg

 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo.
003.jpg
 Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Nyaraka za Serikali, Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Ombeni Yohana Sefue, mara baada ya kumuapisha rasmi, leo Ikulu Dar es Salaam.
004.jpg
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
005.jpg
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue na Balozi Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
006.jpg
 Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
007.jpg
 Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa katibu Mkuu kiongozi Ikulu Dar es Salaam leo.
008.jpg
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, akihojiwa na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue Ikulu Dr es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani- OMR

Monday, December 26, 2011

MANENO OSWARD VS RASHIDI MATUMLA AKUNA MBABE POINT 99 KWA 99 DROO

Bondia Rashidi Matumla (kushoto) akiwa chini baada ya kuteleza uku mpinzani wake Maneno Osward akimsubili kwa ajili ya kumpiga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo
Bondia Rashidi Matumla (kushoto) akiwa chini baada ya kuteleza uku mpinzani wake Maneno Osward akimsubili kwa ajili ya kumpiga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.
Bondia Maneno Osward (kushoto) akimuacha Rashidi Matumla chini baada ya kuanguka kwa kuteleza wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.

T'S SUNDOWN PARTY

Events World, Sule's Inc. & Entertainment and Blood Brothers is welcoming you to SUNDOWN PARTY - MACHWEO on the evening of 31st December 2011 at Coco beach - Tasi lounge, to watch and take memorable pictures of the last Sundown of 2011 together with Bongo movies, Bongo flavor, Hip hop artists and various other Tanzanian celebrities. WELCOME TO THE WORLD!! BE THE FIRST TO PARTICIPATE IN THIS NEW EVENT

Saturday, December 24, 2011

Thursday, December 22, 2011

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA VIFO VYA WANANCHI 13 WA DAR ES SALAAM WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA MAFURIKO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu 13 ambao wamepoteza maisha katika mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua ambazo zimekuwa zinanyesha tokea jana, Jumanne, Desemba 20, 2011.
Aidha, Rais Kikwete amempa pole Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba, makazi na mali nyingine za wananchi uliosababishwa na mvua hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu wa miundombinu.
Rais Kikwete pia ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusaidiana na taasisi na vyombo vyenye uzoefu wa maafa kushirikiana katika kuendelea kuokoa maisha ya watu, kusaidia waliozingirwa na mafuriko na kuwahifadhi na kuwasaidia wale wote waliopoteza nyumba na makazi kutokana na mafuriko hayo.
Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Sadiq: “Nimepokea kwa masikitiko habari za vifo vya wenzetu 13 ilivyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar es Salaam tokea jana. 
Amesema: “Nakutumia wewe rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili la mafuriko. Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo.  Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu.
“Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo.”
                      
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
DESEMBA 21, 2011
DAR ES SALAAM

Wednesday, December 21, 2011

WAKAZI WA MWENGE NA TEGETA KIMENUKAAA.


Huu ndio msongamano wa magari uliopo baaya magari kuzuiwa kupita katika daraja hilo

Sehemu ya daraja yenye ufa
Upande wa daraja uliolika na kingo zake zikiwa zimeharika
Wakazi wakitembea kwa miguu kukatiza daraja kwenda upande wa pili ili wapate usafiri

Daraja likiwa limewekwa kizuizi
Sehemu ya Daraja likiwa inaonekana kingo iliyomeguka
Baadhi ya magari yaendayo Tegeta, Bunju na bagamyo yakiwa yameguza baada ya kushindwa kupita kwenye daraja hilo

Baadhi ya wakazi wakiwa wanapishana katika daraja hilo.

UKUTA WA UWANJA WA YANGA WAANGUSHWA NA MAFURIKO

Uwanja wa Kaunda unaomilikiwa na timu ya Yanga uliopo maeneo ya Jangwani ukiwa katika hali mbaya baada ya kukumbwa na mafuriko na sehemu ya ukuta wake kuanguka.
Baadhi ya maeneo ya Jangwani ambayo yamekumbwa na mafuriko.
Wakazi wa Jangwani wakiwa wanahamisha mali zao kukwepa adha ya

Monday, December 19, 2011

kafulia KAFULILA ATIMULIWA NCCR..POSHO MPYA HATAIFAIDI TENA

David Kafulila
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi.
Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki, Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.
Dalili za Kafulila kufukuzwa zilijionyesha wazi juzi baada ya wazee wa chama hichi kupitia kwa Katibu wao wa Taifa, Ernest Mwasada kuitaka Nec kumfukuza (Kafulila kwa kuwa ndiye chanzo cha migogoro yote inayoendelea ndani ya chama. 
“Hizi vurugu zinachochewa na Kafulila ambaye ndiyo mfadhili na kiongozi wa waasi wa uchochezi huu. Menejimenti inapaswa kumwangalia sana, huyu ni hatari ndani ya chama hastahili kabisa kukaa na jamii yoyote inayopenda amani,” alisema Mwasada.Hata hivyo, Kafulila juzi alikanusha akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba, Katibu wa Taifa wa chama hicho anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye amekosana naye.“Ni hivi, Katibu wa Wazee wa Chama anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye hatuelewani na juzi alifanya kikao kilichoeleza mambo mengi mabaya dhidi yangu," alisema Kafulila na kuongeza.“Huyo Katibu wa Wazee amelishwa maneno na Ruhuza kwani ndiye mwajiri wake ambaye anafanya kazi maalumu ya kumchafua Kafulila na alifanya hivyo kwenye semina ya wenyeviti na makatibu wa chama 19 iliyomalizika jana (juzi) jijini Dar es Salaam.”Kafulila alisema kazi ya Ruhuza ni kuwanywesha sumu viongozi wa chama kuwa yeye (Kafulila) ni mkorofi badala ya kuendesha semina kuhusu mambo ya msingi ya kukijenga chama.

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MABALOZI WAPYA IKULU DAR ES SALAAM LEO


 Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Phillip  Marmo, kuwa Balozi wa China, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Marmo awali alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
 Mabalozi wapya waliofia Ikulu Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, wakisubiri kuapishwa.
 Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Batilda Buriani,  kuwa Balozi wa Kenya, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Batilda awali alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). 
 Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Deodorus Kamala, kuwa Balozi wa Ubelgiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Kamala, awali alikuwa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Ally A. Saleh, kuwa Balozi wa Oman, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Saleh, awali alikuwa ni Balozi Mdogo wa Dubai.
 Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Shamim Nyanduga, kuwa Balozi wa Msumbiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana huu, Ikulu Dar es Salaam. Nyanduga awali alikuwa ni Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Samim Nyanduga, akipongezwa na Mumewe, baada ya kuapishwa rasmi kuwa Balozi wa Msumbiji, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Nyuma yao ni wanafamilia wa Familia hiyo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda (kuli) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakizungumza jambo, baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya baada ya kuapishwa rasmi leo Ikulu Dar es Salaam.