Thursday, December 15, 2011

AUNT EZEKIEL: MIMI SIO MTU WA KUOLEWA.


KATIKA hali ya kushangaza msanii anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel  amefunguka kuwa yeye si mwanamke wa kuolewa na katika maisha yake hana ndoto za kuja kuwa mke wa mtu.
Akipiga stori na paparazi wa ukweli hivi karibuni, Aunt alisema kuwa amefikia hatua ya kusema hivyo kwa kuwa anahisi kutopenda kuolewa.
Alisema, hali ya kuchukia maisha ya ndoa alikuwa nayo tangu alipokuwa mdogo na mpaka sasa anaamini suala la kuvishwa pete ya uchumba  na hatimaye kuolewa halipo.
“Ninachoongea namaanisha, ndoa ni kitu ambacho hakipo kwenye akili yangu tangu nilipozaliwa, sijatendwa na mwanaume yeyote ila imetokea tu hivyo,” alisema Aunt.

No comments:

Post a Comment