b..

B1

Wynem

animation

Thursday, December 15, 2011

KAMBI YA NGUMI ILALA YAMUHAKIKISHIA UBWA SALUM KUIBUKA MSHINDI WA MPAMBANO WAKE DESEMBA 25.


KAMBI ya mchezo wa Ngumi ya Mkoa wa kimichezo wa Ilala Dar es Salaam, inamuandaa bondia Ubwa Salum kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Mustafa Dotto, litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu.
Pambano hilo la utangulizi litakuwa la uzito wa Light la raundi sita litakalopigwa katika Ukumbi wa Heinken Mtoni Kijichi.
Akizungumza na na mwandishi wetu Kocha Msaidizi wa Kambi Ilala, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa pambano hilo litakuwa kati ya mapambano yatakayotangulia katika pambano la Nani Zaidi litakalowakutanisha Maneno Osward pamoja na Rashid Matumla. lililoandaliwa na Shabani Adios 'Mwayamwaya' siku ya sikukuu ya Xmas
“Tunamuandaa bondia wetu ili aweze kujiweka vizuri na pambano lake, hivyo tunatarajia kuwa atafanya vizuri kutokana na maandalizi” alisema.
Alisema kuwa pambano la Matumla na Osward litakuwa la uzito wa Middle katika raundi 10.
Super D alisema kuwa mabondia hao wameshawahi kukutana mara tatu mpaka sasa ambapo Matumla alishinda mara mbili na Osward alishinda mara moja.
Alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa kali na la aina yake kutokana na historia ya mabondia wote katika mchezo huo.
“Pambano kati ya Osward na Matumla linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na kuwa mabondia wote ni wazuri na wana uwezo mkubwa ulingoni” alisema
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
"Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi", alisema Super D 

No comments:

Post a Comment