b..

B1

Wynem

animation

Monday, December 19, 2011

kafulia KAFULILA ATIMULIWA NCCR..POSHO MPYA HATAIFAIDI TENA

David Kafulila
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David kafulia na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe.Uamuzi huo ulitolewa kwenye kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Poroin jijini Dar es Salaam jana, ambao ulitawaliwa na vurugu mpaka polisi wakaitwa ili kuongeza ulinzi.
Baada ya uamuzi huo kutolewa Kafulila alikwenda kupiga magoti mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia huku akibubujikwa machozi na kuomba radhi akisema: “Naomba radhi, nimekosa mnisamehe...”Baada ya hapo Mbatia alisimama na kumwombea msamaha kwa wajumbe wa kikao hicho, lakini walikataa na kumweleza (Mbatia) kuwa akisamehewa watarudisha kadi zao za uanachama.“Hatutaki, Kafulila hatufai anakiharibu chama na akisamehewa sisi tutarudisha kadi zetu za uanachama ili ubaki naye kwenye chama...,” walisikia wajumbe hao wakisema kwa sauti ya juu.Wanachama wengine waliofukuzwa ni, Ally omari, Mbwana Hassan, Josam Rugugila, Lucy Kapya, Jamwe Batifa na Hashim Rungwe ambao walikuwa viongozi wa chama hicho.
Dalili za Kafulila kufukuzwa zilijionyesha wazi juzi baada ya wazee wa chama hichi kupitia kwa Katibu wao wa Taifa, Ernest Mwasada kuitaka Nec kumfukuza (Kafulila kwa kuwa ndiye chanzo cha migogoro yote inayoendelea ndani ya chama. 
“Hizi vurugu zinachochewa na Kafulila ambaye ndiyo mfadhili na kiongozi wa waasi wa uchochezi huu. Menejimenti inapaswa kumwangalia sana, huyu ni hatari ndani ya chama hastahili kabisa kukaa na jamii yoyote inayopenda amani,” alisema Mwasada.Hata hivyo, Kafulila juzi alikanusha akisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba, Katibu wa Taifa wa chama hicho anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye amekosana naye.“Ni hivi, Katibu wa Wazee wa Chama anateuliwa na Katibu Mkuu ambaye hatuelewani na juzi alifanya kikao kilichoeleza mambo mengi mabaya dhidi yangu," alisema Kafulila na kuongeza.“Huyo Katibu wa Wazee amelishwa maneno na Ruhuza kwani ndiye mwajiri wake ambaye anafanya kazi maalumu ya kumchafua Kafulila na alifanya hivyo kwenye semina ya wenyeviti na makatibu wa chama 19 iliyomalizika jana (juzi) jijini Dar es Salaam.”Kafulila alisema kazi ya Ruhuza ni kuwanywesha sumu viongozi wa chama kuwa yeye (Kafulila) ni mkorofi badala ya kuendesha semina kuhusu mambo ya msingi ya kukijenga chama.

No comments:

Post a Comment