Friday, December 9, 2011

ZITTO KABWE :WABUNGE WOTE WALIOPOKEA POSHO WAMEVUNJA SHERIA YA UTAWALA WA BUNGE


Alisema hayo jana katika tafrija ya miaka 50 ya ushirikiano wa Shirika la Uingereza la Maendeleo Kupitia Shughuli za Kujitolea (VSO) na Tanzania iliyofanyika Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yanayofikia kilele leo. “Nitasimama kidete kuhakikisha posho zilizoongezwa zinarejeshwa katika akaunti ya Bunge ili kulinda maslahi ya umma. “Wote waliozipokea wamevunja Sheria ya Utawala wa Bunge ya mwaka 2008, kifungu cha 17 inayotaka malipo ya posho zote yatolewe kwa maandishi na kusainiwa (kuidhinishwa) na Rais.Wanapaswa kuzirudisha na kuonesha stakabadhi kuwa wamefanya hivyo.” “Huo ndio ukweli kwa sababu Rais hajaziidhinisha. Bunge ndio linalotunga sheria hivyo halipaswi kuwa kiongozi wa kuzivunja,” alisema. Alisema kuwa wabunge hawana budi kuchagua moja kati ya mshahara na posho, vinginevyo watakuwa wanaendekeza maslahi binafsi tofauti na ilivyokuwa wakati nchi ilivyopata Uhuru ambapo wawakilishi wa wananchi walilipwa posho bila mshahara na kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Alisema kikao cha wabunge cha mwaka 1978 Chake Chake, Zanzibar kilipitisha mshahara na kufuta posho baadaye mwaka 1985. “Sasa mambo yaligeuka baada ya kuanza kwa vyama vingi ambapo posho zilianza kutolewa sambamba na mshahara lakini sheria haielekezi hivyo,” alisema. “Ndio maana sisaini mahudhurio. Sitaki kuingiziwa posho kwenye akaunti na kujitetea kuwa ziliingizwa automatically kwenye akaunti. “Wote wanaozipokea na kujitetea kuwa wanazipokea kwa kuwa wanazikuta kwenye akaunti wanazipenda na kuzitaka kwa sababuwanafahamu utaratibu kuwa ukisaini unawekewa,” alisema Zitto.

No comments:

Post a Comment