Thursday, November 17, 2016

BARAZA KUU YA UWT - IRINGA LAMPONGEZA MWENYEKITI WA CCM MKOA KWA KUFANIKISHA USHINDI WA RAIS DKT MAGUFULIMbunge wa  viti maalum Mary  Chatanda  akisalimia katika kikao cha baraza  kuu la UWT mkoa wa Iringa 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu akifungua  baraza  kuu la  UWT  mkoa wa Iringa 
Marcelina Mkini mwenyekiti wa UWT  Mufindi  akitoa pongezi kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kulia  katikati ni mwenyekiti wa UWT mkoa  Zainab Mwamwindi na  kushoto ni mjumbe wa baraza hilo Hafsa Mtasiwa 
Wajumbe wa baraza kuu ya UWT  mkoa wa Iringa 
Msambatavangu  akiagana na wajumbe wa baraza   kuu la UWT mkoa  wa Iringa kutoka  kulia ni Mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini , mbunge wa  viti maalum  mkoa wa Iringa Ritta Kabati na Rose Tweve 
Wajumbe wa baraza  kuu la  UWT  mkoa wa Iringa  wakimpokea mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu  wa tatu kushoto  akilakiwa na mbunge Rose Tweve  kushoto ni mwenyekiti wa UWT mkoa na mbunge wa  viti maalum Zainab Mwamwindi  na wa  pili  kulia ni mbunge Ritta kabati  akisalimiana na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina mkini  huku kulia ni katibu wa UWT mkoa 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu wa tatu  kushoto akiwa na viongozi  mbali mbali wa mkoa 
Mwenyekiti wa UWT  mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi akitoa salam za utangulizi
Na matukiodaimaBlog 
BARAZA  kuu  la  umoja  wa wanawake  mkoa  wa Iringa limempongeza mwenyekiti wa chama  cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa  kuwa  kiongozi  wa mfano ndani ya  mkoa na nje ya  mkoa wa Iringa na  hivyo  kumwomba  kugombea  tena nafasi  hiyo ya  uenyekiti mwakani 2017.
Akitoa pongezi  hizo  leo  wakati  akishukuru kwa niaba ya wajumbe wa baraza kuu la UWT  mkoa  lililokutana  kwenye  ukumbi wa CCM wilaya ya  Iringa mjini ,mwenyekiti wa  UWT wilaya ya  Mufindi Marcelina  Mkini ambae  pia ni mjumbe wa Halmashauri  kuu ya CCM Taifa (NEC)  alisema  kuwa  ushindi mkubwa ambao CCM iliupata katika  uchaguzi mkuu mwaka jana  uchaguzi  uliomwezesha Rais  Dkt  John Magufuli  kushinda kwa  kishindo dhidi ya  wapinzani  wake ni pamoja na kazi  nzuri  iliyofanywa na Msambatavangu katika  kampeni  za uchaguzi mkuu .
Mkini  alisema  mkoa  wa Iringa kwenye  uchaguzi huo  uliweza  kufanya  vizuri kwa kushinda  majimbo 6 kata ya 7  yaliyopo ndani ya  mkoa  wa Iringa na kuwa  pamoja na kila  mmoja  kushiriki katika  kupigania ushindi  huo wa chama  ila  wao kama  wanawake  hawanabudi  kumpongeza mwanamke mwenzao ambae ndie mwenyekiti wa chama  mkoa kwa  kuonyesha Taifa  kuwa  wanawake  wanauwezo wa  kuongoza .
'' Naomba  kuchukua nafasi hii kwa niaba ya  wanawake  wenzangu  kukupongeza  sana mwenyekiti  wetu wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu  umeonyesha  mfano  mzuri kuwa unaweza kuongoza .......nakumbuka  wakati wa kampeni  wewe  ulisimama  kidete   kuhakikisha  chama kinashinda  kwa  kishindo  mbali ya figisu figisu zilizokuwa zikielekezwa kwao  ila hukuteteleka ''
Mbali ya mwenyekiti  kufanya  vema katika  kampeni  za 2015  ila  hajaacha  kuitumikia vema  jamii ya  mkoa wa Iringa ikumbukwe mkoa  umepata  misiba miwili mikubwa  ukiwemo wa  aliyekuwa mwenyekiti  mstaafu wa CCM  mkoa Tasili Mgoda na mwasisi wa maendeleo ya   wilaya ya  Mufindi Joseph  Mungai shughuli  zote  zimeratibiwa  vema na Msambatavangu tena  pasipo  ubaguzi  wowote .
'' Mwenyekiti   wetu  anafanya kazi  vizuri  ndani ya  mkoa  wetu  tena  pasipo ubaguzi wowote  na ni mtetezi  mzuri  sana kwa  wanawake  ndani ya  mkoa na hanaga unafiki kabisa  kwani  yeye  siku  zote  husema  kweli  tupu ''
Mkini  alisema   kuwa   kutokana na  utendaji  kazi wake mzuri  ndani ya  chama  wao  wanaona  bado  mwenyekiti huyo anauwezo  wa  kuwavusha wana CCM kwa miaka  mingine mitano ijayo  hivyo  kumshawishi  kuingia tena ulingoni  mwakani 2017 katika  uchaguzi  mkuu wa  viongozi ngazi mbali mbali za  chama.
Mwenyekiti  wa UWT  mkoa  wa  Iringa Zainab Mwamwindi akisoma tamko la  UWT  mkoa  wa Iringa kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt  Magufuli  alisema  kuwa   wao kama  wanawake wa CCM  wameendelea   kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt Magufuli na  kuwa  kubwa  zaidi  ni jinsi  Rais alivyoweza  kujibu maswali ya  watanzania  kupitia   mkutano wake  wahariri  wa  vyombo   mbali mbali  vya habari  hapa nchini.
.Kwa  upande wake  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa ,Msambatavangu  pamoja na  kupongeza  pongezi za baraza  hilo  dhidi yake  na  zile za Rais alisema atahakikisha pongezi za  wanawake hao zinamfikia Rais Dkt Magufuli  huku  akisisitiza  wanawake  kuendelea  kuongoza  nafasi zao kwa kujiamini  zaidi badala ya  kutanguliza  uoga usio  wa lazima .
Alisema  wakati  chama kinajiandaa kwa  chaguzi zake mwakani ni vizuri  wanawake  kuanza  kujipima ama  kuwapima  wale ambao wanaingia kuwania nafasi mbali mbali ili  kupata  viongozi wenye  uwezo wa kuwatumikia  wananchi hasa katika  kipindi   hichi  cha kujenga chama  chenye  nguvu na  uongozi wenye  uwezo wa kuendana na kauli  mbiu ya  Rais ya hapa Kazi  tu.
Kwani  alisema  wapo baadhi ya  watu  ndani ya  CCM kazi yao ni  kusubiri uchaguzi hadi  uchaguzi  kufanya kazi  za chama na kuwa  wanachama hao hawapo kwa  ajili ya  kuwatumikia  wananchi bali  wapo kwa ajili ya  kutumikia matumbo yao jambo ambalo halikubaliki  kwa uhai na  nguvu ya CCM .
Mwenyekiti   huyo  alisema   hivi  sasa  wananchi  wanauelewa mkubwa  juu ya siasa   na uongozi  hivyo ni lazima  wanaopewa nafasi za  kugombea  ni lazima  wawe wanakubalika katika  jamii  inayowazunguka   vinginevyo  chama  kinaweza  kuyumba iwapo  watu  wasio na sifa  watapewa nafasi za  kugombea hivyo  ni  vizuri  kuanza  kuwatafuta  watu  wanaofaa ambao hawapo  ndani ya  CCM kujiunga na CCM ili mbeleni  waje kugombea kupitia  CCM.
Kwani  alisema  hivi  sasa kote  duniani ni  vema  viwili  pekee  ndivyo vimebaki kuitwa  vyama tawala na  vyama  hivyo ni  nchini China na Tanzania pekee ila maeneo  mengine  yote  vyama  tawala  imeondolewa madarakani    kwa  kuwa CCM lengo lake ni  kuendelea  kuongoza ni  vizuri kila mwanachama na kila kiongozi  kuhakikisha anawajibika   vema kwa  wananchi kama ambavyo mwenyekiti wa chama Taifa Rais Dkt Magufuli anavyoliongoza Taifa kwa  faida ya  watanzania na  vizazi vijavyo.

Sunday, October 2, 2016

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM JANA

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo katika mti alioupanda eneo la JKT Mgulani Barabara ya kilwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika eneo la JKT Mgulani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika jiji la Dar es Salaam zilifanyika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika JKT Mgulani, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini Dar es salaam inayokwenda kwa jina la MTI WANGU iliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiunga na mtandao kwenye eneo la Gymkhana ambalo huduma ya WI-FI inapatikanika bure kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
...................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jana tarehe 1 Oktoba 2016 ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti inayojulikana kama Mti wangu Jijini Dar es Salaam.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kilwa – Kurasini katika wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola mkoani Dar es Salaam ambavyo vimepewa jukumu la kutunza miti hiyo iliyopandwa ili isiharibiwe vihakikishe vinatekeleze jukumu ili kikamilifu ili kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa inakuwa vizuri ili kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Majiji bora katika utunzaji wa Manzingira.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa kampeni hiyo ambayo ameizindua Jijini Dar es Salaam inatakiwa ifanyike nchini kote kama hatua ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa vyanzo vya maji kote nchini.

Amesema kuwa jitihada za kupanda miti nchini zinatakiwa kuimarishwa maradufu kwani zitasaidia katika uhifadhi wa mazingira hususani katika suala zima la kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Makamu wa Rais katika hotuba yake ameeleza kuwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuongezeka hewa ya ukaa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na ongezeko la viwanda na idadi kuwa ya watu hivyo jitihada za pamoja kati ya serikali,taasisi binafsi,asasi za kiraia na wananchi zinahitajika katika kutunza mazingira na kupanda miti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pia amepongeza jitihada za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji na uimarishaji wa mifumo ya maji katika barabara itakayosaidia kurahisisha umwagiliaji wa miti iliyopandwa.

Amesema anafaraja na matumaini makubwa kuwa kampeni aliyoizindua ya upandaji miti itakuwa endelevu na miaka michache ijayo italifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio na mfano wa kuigwa na mikoa mingine kwa kuwa na mwonekano mpya na wa kuvutia.

Baada ya kuzindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais ambaye aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu Rais Mazingira na Muungano January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alifanya ziara fupi ya kutembelea na kukagua mifumo wa maji katika barabara ya Nyerere na Ally Hassan Mwinyi itakayotumika kumwagilia miti iliyopandwa pamoja na kuongeza na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Gymkana.


PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Thursday, September 15, 2016

Alikiba kutumbuiza Tuzo za MTV Mama Okt. 22

Mwandishi Wetu
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Salehe ‘Alikiba’, ametajwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza wakati wa utoaji tuzo za MTV Mama zitakazofanyika Oktoba 22, mwaka huu Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Meneja wa msanii huyo, Seven Mosha, msanii huyo amechaguliwa kufanya shoo hiyo pamoja na wasanii wengine kutoka nchi mbalimbali Afrika na Ulaya. 
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome jijini humo ambapo wasanii wengine watakaotumbuiza ni Yemi Alade, Nasty C, Babes Wodumo na wengine wengi. 
Kwa mwaka huu tuzo hizo zina vipengele 18 ambavyo wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika watawania.

Tuzo hizo kwa mara ya kwanza zilifanyika 2008 na zimekuwa na mafanikio makubwa kutokana na wasanii wanaopata tuzo hizo kuwa na vipaji vya kipekee na hadi sasa waandaaji wa tuzo hizo wanatambua vipaji 2Face Idibia, Big Nuz, Cassper Nyovest, Davido, D'Banj, Flavour, Fally Ipupa, Mafikizolo, Lira, Nameless, Lupita Nyong'o, Clarence Peters, Diamond Platnumz, P-Square, Tiwa Savage, Cabo Scoop, Yemi Alade na wengineo.

Monday, August 29, 2016

MABONDIA NASIBU RAMADHANII NA IDDI ATHUMANI WASAINI KUZIPIGA NOVEMBA 9 MABIBO

Bondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na Iddi Athumani 'Mchina' baada ya kutiliana saini ya kupambana novemba 9 Mabibo Dar es salaam katikati ni Promota wa mpambano uho Abdallah Kamanyani.
Mabondia Nassibu Ramadhani wa pili kushoto na Iddi Athumani kulia wakiwa na promota wao Abdallah Kamanyani katikati kushoto ni kocha wa Nassibu Cristopher Mzazi na wa pili kulia ni kocha wa Athumani Yusuph Komba
Mabondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na Iddi Athumani baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga novemba 9 mabibo Picha na SUPER D BOXING NEWS
IDDI ATHUMANI 'MCHINA'
NASSIBU RAMADHANI
Bondia Iddi Athumani 'Mchina' kushoto akitia saini ya kuzipiga na Nassibu Ramadhani Novemba 9 mabibo Dar es salaam Picha zote na SUPER D BOXING NEWS

Saturday, August 27, 2016

WATANZANIA WALIOSOMA CHINA KUPATA UONGOZI MPYA


Mwandishi Wetu
Chama cha watanzania waliosoma China- CHINA ALLUMNI ASSOCIATION OF TANZANIA (CAAT) hii leo tarehe 27 August, 2016 kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wake wapya.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rombo Green views Hotel sinza Dar es salaam kuanzia saa saba kamili mchana nakufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza viongozi wapya na kuwaaga viongozi waliomaliza muda wao.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa uchaguzi wa chama hicho GUSTAV SANGA uchaguzi huo utawaweka madarakani viongozi hao miaka mitatu kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Chairperson, Secretary, Treasurer, Director of Statistics, media and information, director of Art, culture and heritage pamoja na Director of Education, Science and Technology
SANGA pia amewakaribisha watanzania wote waliomaliza China kujiunga katika chama hicho ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea ikiwemo kuishauri serikali masuala yahusuyo TANZANIA- CHINA.

Chama hicho cha watanzania waliosoma China kina miaka sita tangu kuanzishwa kwake na kina wanachama tangu waliosoma china miaka ya1980 kwa ngazi ya shahada , astashahada na shahada ya uzamivu.

Tuesday, July 12, 2016

Thursday, June 16, 2016

MABONDIA GALILE NA MAPAMBANO KUMALIZA UBISHA JULAY 24 MUSOMA BAR

Mdau wa masumbwi nchini Jumanne Mbwembwe akiwainua mikono juu mabondia Imani Mapambano kushoto na Seleman Galile kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa julay 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika 
Mabondia Iani Mapambano kushoto na Selemani Galile wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa julay 24 katika ukumbi wa musoma bara tasndika
Mabondia Imani Mapambano kushoto akitunishiana misuli na Selemani Galile baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga julay 24 katika ukumbi wa musoma bar tandika

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Imani Mapambano na Selemani Galile wamesaini mkataba wa kuzipiga Julay 24 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika Dar es salaam
akizungumza baaya kusainishwa kwa mabondia hawo mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' 
Amesema amewasainisha mabondia hawo baada ya kutambiana mara kwa mara kadri wakutanapo
hivyo 
nimeamua wapambane julay 24 katika ukumbi wa musoma bar ili kumaliza ubisha wao 
mpambano uho utakuwa wa ubingwa wa Taifa utakaosimamiwa na TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'Ustadhi' 
Aliongeza kwa kusema kuwa mipambano mingine ya utangulizi watatangaza kadri watakavyo ingia mikataba na mabondia mbali mbali  

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.


Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

Friday, June 3, 2016

NGUMI ZA KIMATAIFA KUPIGWA KESHO UWANJA WA NDANI WA TAIFA JUNI 4

Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Msafili Haule baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4.
Promota wa mkanda wa ubingwa wa Dunia wa U.B.O Juma Ndamile kushoto akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza mpambano uho pamoja na upimaji uzito kwa mabondia wengine ni Kulwa Makaranga na bondia Cosmas Cheka atakaegombania ubingwa wa Dunia na Chrispin Moliyati mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4.
Bondia Lulu Kayage kushoto akitunishiana misuli na mpinzani wake Will Enelesi wa Malawi mpambano wao utafanyika juni 4 katika uwanja wa ndani wa Taifa 
Bondia Ashiraf Selemani kutoka Zanzibar  kushoto akitunishiana misuli na ElickGogodo wa Malawi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akitunishiana misuli na Mussa Ajiba baada ya kupima uzito kwa ajili ya Mpambano wao utakaofanyika kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa
Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Msafili Haule baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4
Mabondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Msafili Haule baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambao wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jumamosi ya juni 4 

Picha zote na SUPER D BOXING NEWSNa Mwandishi Wetu
BONDIA Cosmas chka anapanda uringoni kugombania ubingwa wa Dunia wa U.B.O kwa kupambana na Chrispin Moliyati kutoka Malawi mpambano wa raundi 12 wakisindikiza na mabondia chipkizi ambapo bondia kutoka katika kambi ya 'Super D' Vicent Mbilinyi ata kabiliana na bondia kutoka kambi ya akina ukoo wa Matumla Msafili Haule watazipiga katika uzito wa kg 63 mpambano wa raundi 6.
Mipambano mingine ya kimataifa yaa wakutanisha mabondia wa kike Lulu Kayage wa Tanzania atakaezipiga na Will Eneles kutoka Malawi
wengine ni Japhert Kaseba atazidunda na Amour Mzungu kutoka Zanzibar na Ashiraf Selemani kutoka Zanziba atakumbana na Elick Gogodo wa Malawi katika mchezo wa uzito wa juu kabisa wakati Alphonce Mchumiatumbo atakabiliana na Mussa Ajibu kutoka Malawi mpambano wa raundi sita

siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazo sindikiza mapambano hayo ya kimataifa ya mchezo wa masumbwi pia ngumi zitaanza mapema kuepusha usumbufu unaojitokezaga kwa wapenzi kuchelewa majumbani mwao kwa ajili ya mchezo wa masumbwi

siku hiyo pia kutakuwa na ugawaji wa zawadi kwa mabondia watakaocheza vizuri na kuonesa nidhamu ya mchezo wa masumbwi ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutamba sheria za mchezo uho nyingine zitakuwa zikiuzwa kwa galama nafuu kwa mashabiki watakaofika siku hiyo.

Monday, May 30, 2016

HABARI PICHA: BASATA, HAANNEEL WAZINDUA MATUKIO YA SIKU YA MSANII KWA MWAKA 2016

Mkurugenzi wa Kampuni ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka ambayo ni waandaaji wa Siku ya Msanii akimwongoza Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kutia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kuzindua matukio ya Siku ya Msanii (SYM, 2016) kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise mwishoni mwa wiki.   
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ndilo mbunifu na mmiliki wa maadhimisho ya Siku ya Msanii nchini Godfrey Mngereza (Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi (Katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni mwendeshaji wa Siku ya Msanii ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka mwishoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 katika Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam.
Msanii maarufu wa kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akisaini kitabu cha wageni kabla ya kushuhudia hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise ulioko jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi. Vivian Shalua (Kushoto) akifuatilia kwa makini moja ya matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francoise mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Msanii wa Sanaa za Ufundi Gozbetha Rwezaula.
Marais wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini kutoka kushoto Symon Mwakifamba (Filamu), Adrian Nyamangale (Ufundi), William Chitanda maarufu kama MC Chitanda (Sanaa za Maonesho) na Addo November (Muziki) wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali ya uzinduzi wa matukio ya Siku ya Msanii mwaka kwa mwaka 2016
Kikundi cha Sanaa cha Safari kikitoa burudani kwenye hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam
Msanii maarufu wa Sanaa za Uigizaji na Filamu Ahmed Olutu maarufu kama Mzee Chiro akitabasamu na Msanii mwenzie Thecra Mjata wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio ya hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016