Friday, March 29, 2013

PICHA ZA GHOROFA LILILOANGUKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO ASUBUHI

56789101214a2

Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia ambaye ameungana na wananchi wengine katika tukio hilo. 
1
Madaktari wa kujitolea wakimhudumia mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kifusi baada ya jengo linalomilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Nyumba la Taifa NHC na kampuni ya Aliraza Investiments Ltd ya jijini Dar es salaam huku mjenzi wa jengo hilo ikiwa ni kampuni ya ujenzi ya Luck Construction Ltd, mpaka sasa uokoaji unaendelea lakini ukionekana kusuasua kutokana na ufinyu wa eneo lenyewe na vifaa hafifu vya kuokolea, bado haijafahamika kwamba ni watu wangapi wamepoteza maisha katika ajali hiyo na wangapi wamejeruhiwa , magari ya kubebea wagonjwa yamekuwa yakipishana mara kwa mara wakati yakipeleka ama majeruhi ama watu waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata 

Wednesday, March 27, 2013

KIDO AMTAKA TENA MCHUMIATUMBO

Bondia mbavu nene Ramadhan Kido anamta tena mbavunene mwenzake Alphonce mchumiatumbo warudiane baada ya pambano lao la mwanzo lilofanyika uwanja taifa kuchapwa amepania kulipa kisasi ,”mchumiatumbo amenifanya nimeshindwa kulala kwa muda mrefu nikimfikiria yeye kanipigajepigaje jibu sipati,nimeamua kurudi tena ulingoni kwa kujipima na musa mbabe jumapili ya tarehe saba mwezi wa nne pale CCM Mwinjuma,mwananyamala hapahapa jijini dar es salaam ,najua musa ni bondia mzuri lakini siwezi kupoteza mara mbili mfululizo huu mwiko wangu nitahakikisha nafia ulingoni na ntajituma  kwa nguvu zangu zote na kuhakikisha nampiga ko mbaya,kwani siku hiyo ya tarehe saba april sitakuwa na huruma hata kidogo,lolote na litokee hata nikiua sawa tu nina uchungu sana na ngumi na nataka nimuoneshe mchumia tumbo nakuja kivingine,na nikipigwa katika pambano la mwananyamala ni bora niache ngumi

Monday, March 25, 2013

KAJALA ARUDI URAIANI, AMWAGA CHOZI BAADA YA KUKUTANA NA LULU

Kajala akishuka kutoka kwenye gari la magereza alipofika mahakamani.
Kajala akikumbatiana na Wema Sepetu mara baada ya kuachiwa huru
Kajala akimkumbatia mama yake
Kajala akimkumbatia lulu huku akihojiwa na vyombo vya habari.

SCHWARZENEGGER AMLILIA WEIDER

Mtunisha misuli maarufu (Bodybuilding), Joe Weider ambaye ndiye alimtambulisha mtu mzima Arnold Schwarzenegger pale Hollywood, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Anajulikani sana kutokana na umaarufu wake wa kujengawatunisha misuli na kuwaingiza katika mashindano tofauti sanah huku akiwa anamiliki jarida la Muscle and Fitness na Shape and Men's Fitness, majarida ambayo yalikuwa yakielekeza jinsi ya kuwa mtunisha misuli wa kimataifa.
Arnold Schwarzenegger ambaye aliwahi kuwa Gavana wa jiji la California "Yeye alitufundisha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii na mafunzo tuweze kuwa mabingwa," alisema gavava wa zamani wa California katika taarifa kwenye tovuti yake.
Aliendelea kusema "Nilipokuwa kijana mdogo katika Austria, nilipata msukumo kutokana na kusoma jarida lake la muscle magazines, na kuona picha zake ambazo zilinipa hamasa ya kuwa kama yeye na yeye ndiye aliyenifanya nikafika hapa nilipo.
Katika taarifa yake, Bw Schwarzenegger alisema Weider alikuwa ni mtu pekee aliyempa sapoti ya mojakwa mona katika kazi sake has a kwenye filamu kama  The Terminator, Total Recall and True Lies, na hata alipoamua kuingia kwenye siasa.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Weider, alisema kuwa Weider alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo ambayo ndiyo ya,esababisha kifo chake "Joe Weider, amefariki dunia kwa moyo wake kushindwa kufanaya kazi mjini Los Angeles"  Msemaje wake alisema.
Pia watu wengine waliomlilia Weider ni pamoja na Conan ambaye ni mtu maarufu na msomi, Conan alikuwa akimpa heshima Weider kwa kumuita "godfather of fitness."


Sunday, March 24, 2013

NATALIA ANAG'ARA KWENYE MUVI YA WORLD OF BENEFIT

NATALIA akiwa katika pozi tofasuti

Anaitwa Natalia Mossi, kinda mpya katika tasnia ya filamu ambapo kwa mara ya kwanza ataonekana katika filamu ya World of Benefit.
Mbali ya kujiingiza katika tasnia ya filamu Natalia ameshawahi kuwa model na kuonekana katika matangazao kadhaa ya biashara. 

MAFURIKO YATOKEA BAADHI YA MAENEO JIJINI DAR ES SALAAM

Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko baada ya mvua ya muda mfupi inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa Jiji la Dar wakipita katika eneo lililojaa maji mtaa wa tabata relini.

Thursday, March 21, 2013

UJIO MPYA WA MIX TAPE KUTOKA KWA JCB & MO PLUS 'MAKALA WA UKOO'

Coming soon ni "Makalla wa Ukoo" Mixtape check out tha tracklisting Hapa

1. MakallaWaUkoo & JCB ft Banx & Lavost-Be Yourself
2. MakallaWaUkoo & Chindo ft Keneh-Snitch
3. MakallaWaUkoo & Papaya ft Banx-Lookin for
4. MakallaWaUkoo & SlimDizzy-2000 BC
5.
MakallaWaUkoo ft Banx-Everywhere we go
6.
MakallaWaUkoo ft DomoKaya-Niende Wapi
7.
MakallaWaUkoo ft Donii-Blazee
8.
MakallaWaUkoo ft KJuu-Michano
9.
MakallaWaUkoo ft Nakaaya-Feeling
10.
MakallaWaUkoo ft SteveDaddy-Majaribu
11.
MakallaWaUkoo ft Vinega-Jishone
12.
MakallaWaUkoo -Sweetest
13.
MakallaWaUkoo-Criminal Minds

KEEP IT HIPHOP ALL DAY!!!

Wednesday, March 20, 2013

BAADA YA KUTOKA HOSPITALI, MSANII LIL-WYNE AWASHUKURU MASABIKI WAKE.After six days in hospital following his seizures last week, Lil Wayne has reportedly returned home. The rapper said he is "feeling a lot better", watching TV and laughing till he cries.

"Watching [the TV show] Highly Questionable on ESPN2 & [co-host] Papi got me kry'n laughing in dis [bitch]," Wayne tweeted on Tuesday afternoon. "Again thk u all for ur love and prayers. It was truly felt … pause."
Until Monday, Wayne was receiving treatment at Los Angeles' Cedars Sinai Hospital following a series of unexplained seizures. TMZ went so far as to report he had received last rites, though the site later deleted that part of its story.
In an interview with radio station Hot 97, Wayne's mentor, Birdman, dismissed claims his "son" had suffered a reaction to a codeine-laced cough medicine, known as "sizzurp". "It had nothing to do with drugs," Birdman said. "Honestly, it's [Weezy's] work ethic. How hard he works. How much dedication he gives to his music and his fans … [Wayne] just needs to get some rest and relax. He'll be back, normal, like everyone else."
Fans haven't seen Wayne since his seizures, but a new video shows the rapper just days – or maybe hours – before his crisis. The star had come to LA to appear in Nicki Minaj's new music video, and newly released behind-the-scenes footage has Wayne in high spirits, mocking and joking with Minaj. After Minaj reminds him he has to focus for the cameras, Wayne replies: "You don't have to tell me. This is my dream."

SOURCE: http://www.guardian.co.uk

BONDIA STAR BOY APANIA KURUDISHA ENZI


Na Mwandishi wetu

BONDIA Shabani Mhamila 'Star Boy' ameingia kambini kujiandaa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa
Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli 'Masta' akisaidiwa na  Rajabu Mhamila 'Super D' wamesema kuwa
bondia wao ameingia kambini juzi kujiandaa kumchakaza Jibaba ili
kuendelea kujiwekea sifa nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini rakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo uho kutokana na mabondia wengi awajui sheria na kanunu za mchezo huo Sta Boy mwenye rekodi ya .won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga  Theodor Luanda
Frebruary 2,1996 na kutetea vema
10 Februar1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa 
Super D
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa
katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mjapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe

Sunday, March 10, 2013

HABARI GROUP YAFANYA HARAMBEE NA KUFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA MILIONI SITA


Mratibu wa Kikundi ya HABARI Group Bi.Rabia Bakari akikabidhi risara ya kikundi hicho wakati wa uzinduzi 

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katikati akichangia katika harambee ya kikundi cha Habari Group ambao ni waanishi wa Habari waliojikusanya kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na pia kuhudumia jamii isiyojiweza kikundi hicho kinaendeshwa chini  ya jumuiya ya kukuza uchumi Ilala 'Jukuila' kikundi hicho kimezinduliwa March 8 Mlezi akiwa ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki wa pili kulia Udhinduzi huo umedhaminiwa na Mfuko wa Pesheni wa PPF pamoja na Hotel ya Lamaa kushoto ni mratibu wa hafla hiyo Bi, Rabia Bakar

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kushoto akiangalia baadhi ya dokomenti

Wana kikundi cha Habari Goup wakijitambulisha mbele ya mgeni rasmi.
Picha zote na www.burudan.blogspot.com

Saturday, March 9, 2013

NEW SONG FROM SOPRANO MUSIC - AMENISAHAUAWADH SALEHE: KIFAA CHA WORLD OF BENEFIT CHENYE MAKEKE MENGI!

Na Magreth Mgina
Awadh Saleh, si jina zito sana katika tasnia ya filamu lakini kwa wale ambao wameshashuhudia uwezo wake katika kazi ya uigizaji wa filamu wanakiri kwamba ni kifaa kinachoweza kuwatingisha nguli wengi wa tasnia hiyo.
Mbali ya umbo lake lenye muonekano wa kina Roberto de Niro, Antonio Banderas na wengineo, Awadh ana vitu vingi vilivojificha ambavyo hujitokeza wakati wa kazi tu. Staili ya uigizaji wake, umakini wa kuisoma na kuielewa script na jinsi anavyoweza kubadilika kwa kila muigizaji anayekutana naye ndivyo vitu vinavyodhihirisha uwezo wake katika tasnia hii ya filamu.
Awadh Saleh ni miongoni mwa washiriki wa filamu ya World of Benefit iliyowakutanisha nguli kama Mzee Chilo, Mama Mjata, Rose Ndauka na Hemed Suleiman Phd. Ameweza kuonesha uwezo mkubwa ndani ya filamu hiyo kiasi cha kuwashangaza nguli hao.
Pia ndani ya filamu ya World of Benefit, Awadh amekutana na wasanii damu mpya kama vile mwanamuziki Ali Timbulo, visura Tutti Rahman, Miriam, Latipher Mkuu na Natalia.   
Wengi watapata fursa ya kushuhudia makeke yake ndani ya filamu ya World of Benefit ambayo imemalizika kuchukuliwa picha hivi majuzi na sasa iko katika editing.


Wednesday, March 6, 2013

MWENYEKIT WA JUKWAA LA WAHARIRI, ABSOLOM KIBANDA AVAMIWA NA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, na Mhariri Mkuu Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.
Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu.
Kwa hisani ya Michuzi Blog