Tuesday, May 29, 2012

JOYCE KIRIA- KUTOKA U'HOUSEGIRL MPAKA UTANGAZAJI


Na HERIETH MAKWETTA
'UGUMU wa Maisha ni Kipimo cha Akili'. Huu ni usemi uliozoeleka katika maisha ya kijamii hasa kwenye miaka ya sasa ambapo hali ya uchumi imekuwa ikizidi kuwa ngumu.
Katika ugumu wa maisha huo kuna walioshindwa kabisa kujikwamua hadi kukata tamaa. Lakini kuna ambao wameutumia ugumu huo kutafuta namna ya kujikomboa, ndiyo wanaozungumzia kwenye usemi huu.
Mmoja wa watu hao ni mtangazaji ambaye pia ni Mmiliki wa Local Media Entertainment, kampuni inayoendesha vipindi vya televisheni vya 'Wanawake Live' na 'Bongo Movie', vinavyorushwa na Kituo cha EATV, mwanadada Joyce Kiria.
Utumwa pasipo malipo sahihi na kutokuwa na uhuru wa maamuzi, vilikuwa sehemu ya maisha yake kwa muda mrefu. Ilikuwa ni baada ya kumaliza elimu yake ya msingi.
"Unajua natoka katika familia ya hali ya chini, hivyo nilipomaliza Darasa la Saba sikuwa na namna ya kuendelea na masomo," anasema.
"Nilianza kwa kufanya kazi za ndani za u-hausigeli, nilifanya kazi hii kwa miaka miwili. Sikuifurahia sana.
"Baadaye niliona nisonge mbele, niliiacha kazi hiyo na nikajiunga katika genge la mama ntilie, nilifanya kazi hapo kwa muda mpaka nilipoamua kuanza kuchoma chapati."
Hata hivyo anasema hakudumu na kazi hiyo kwani hakuwa akipatana na moto hivyo akatafuta kazi katika kiwanda cha mablanketi, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
"Nikafanya kazi kwa muda pale lakini baadaye nikapata nafasi ya kazi katika duka moja Kariakoo, jijini Dar es Salaam, hapo ilikuwa tayari imefikia mwaka 2000," anaongeza.
"Niliendelea na kazi yangu na baadaye nilipata mtaji wa kuniwezesha kufungua biashara yangu."
Anasema alianza biashara zake rasmi kwa kupigisha simu katika vibanda vidogo, mtaji ulikua na baadaye alifungua duka la vifaa vya shule na mapambo, lakini baadaye akairudia biashara ya nguo.
"Baada ya kufanikiwa kukuza mtaji wangu, niliingia tena katika biashara ya nguo, na nikaanza kununua nguo za jumla kutoka Dubai, Falme za Kiarabu," anasema.
"Siku moja nikaenda na kununua nguo mwenyewe huko Falme za Kiarabu. Nilirudi na kuona nguo hizo zimejaa sana Kariakoo na bei yake ipo chini, hapo ndipo mtaji wangu ukafa au kwa maneno mengine nifilisika."
Anasema baada ya kushindwa biashara akaamua kumwona, Amina Chifupa (sasa marehemu) ambaye alikuwa mteja wake wa nguo na kumweleza shida yake.
"Amina ambaye wakati huo alikuwa anafanya kazi redio ya Clouds akanishauri nianze utangazaji kwani aliona nina kipaji, hivyo nilianza kazi hiyo pale Clouds mwaka 2006. Mwaka 2008 nikaolewa," anasema.

KUVUNJIKA KWA NDOA YA AWALI
Joyce, ambaye sasa ni mke halali wa Henry Kilewo, ndoa yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2008 alipooana na Nelson Joshua 'DJ Nelly'.
"Muda mfupi baada ya ndoa nikaanza kuonja machungu yake, niliishi maisha ambayo sikuchagua, hii ilikuwa ni baada ya kuolewa," anasema.
"Niliamua kuachana na mume, unajua ilifikia hatua nilihisi ningeweza hata kuwekewa sumu katika chakula, yalikuwa ni maisha ya chuki.
"Hapo ndipo ukawa mwanzo wa kuyajua mengi ambayo niliamua rasmi kuanza kuyafanyia kazi nikiwa kama mwanamke niliyejitolea kutetea haki za wanawake."
Anasema alianza kwa kudai talaka ambayo ilikuwa ngumu kutolewa kwani ndoa aliyofunga ilikuwa ni ya Kikristo.
"Nilifanikiwa kupewa talaka yangu na hapo ndipo ukawa mwanzo wa kuanzisha kipindi cha Wanawake Live nikiwa na dhamira ya kweli ya kutetea Haki za Wanawake.

WITO WAKE KWA JAMII
Joyce ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro, anasema tatizo lililopo hapa nchini ni mfumo dume, ambao umekithiri.
"Mwanaume anasahau kutunza familia yake na kutokomea kusikojulikana, kwa sababu ya uchumi mdogo familia yake inaingia kwenye taabu, hali hii haivumiliki na ndiyo mwanzo wa kuvunjika kwa ndoa nyingi," anasema.
"Pia changamoto za kimaisha ni nyingi, wapo wanawake wenye kipato, lakini kutokana na mfumo dume wanalazimika kuacha kila kitu kikiwa chini ya waume zao ambao baadaye huwasaliti."
Anasema kupitia kazi yake ya sasa amepania kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili iachane na na mfumo huo kuweza kutoa haki sawa kwa wote.
Habari hii kwa hisani ya gazeti la Mwanaspot.

AIRTEL JIUNGE NA SUPA 5 ILIVYOPASUA ANGA MKOANI DODOMA

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu kwa Baltazar Theobald, mshindi wa kwanza aliyeweza kueleza vizuri jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa 5 wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Airtel Jiunge na Supa 5 ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mnenguaji mahiri wa bendi ya Mashujaa, Lilian Tungaraza ‘Internet’ akiongoza kundi la wanamuziki wa bendi hiyo kulishambulia jukwaa wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Family, Said Juma ‘Chege’ (kushoto) na Amani James Temba ‘Mheshimiwa Temba’ wakionyesha makali yao katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mpiga tumba mahiri wa bendi ya Mashujaa Musica aliyejiunga na bendi hiyo akitokea Twanga Pepeta, Sudi Mohamed ‘MCD’ akionyesha makali yake wakati wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Cyprian ‘ Chaz Baba’ ambaye naye amehama akitokea Twanga Pepeta, akiimba wakati wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Mji wa Dodoma waliohudhuria uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Msanii wa kundi la muziki wa bongo fleva la Tip Top Connection lenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam, Hamad Ally ‘Madee’ akichengua mashabiki wake waliojitokeza katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.


Na Mwandishi wetu

Huduma ya SUPA 5 imepokelewa kwa shangwe mkoani Dodoma huku dhamira yake ikiendelea kutimia baada ya umati mkubwa wa vijana kujitokeza ili kufahamu vyema huduma hiyo nafuu iliyozinduliwa wiki moja iliypota kwa lengo la kuwapa unafuu wateja wa Airtel ili kufurahia huduma tano nafuu.
Wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha la wazi katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wasanii wa muziki wa Dansi na Bongo Flava walitumbuiza na kufanya tamasha hilo kufana zaidi.
Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye utambulisho wa huduma hiyo mpya kabambe ni pamoja na bendi ya muziki ya Mashujaa, kundi la muziki wa kizazi kipya la Tiptop Connection na kundi la Wanaume TMK.
Akitambulisha huduma hiyo mbele ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando amesema, wateja wa kampuni hiyo watapata unafuu mkubwa wa gharama za kupiga simu.
“Huduma ya SUPA 5 inamuwezesha mteja wa Airtel kutumia mtandao wa facebook bure masaa 24, kuongea nusu shilingi na watu watatu, kupiga simu kwa robo shilingi kuanzia saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi na kutumia huduma ya internet bure usiku kucha” alieleza Bw, Mmbando.
Huduma ya SUPA 5 itaendelea kutambulishwa katika mikoa mbalimbali kwa kuwa huduma hiyo nafuu ni ya kudumu, mikoa inayotarajiwa kutembelewa kwa kufanyiwa utambulisho rasmi wa huduma hiyo ya Airtel Supa 5 ni pamoja na Morogoro, Iringa, Arusha, Mwanza na DSM.

USIKOSE USIKU WA HIP HOP


Monday, May 28, 2012

LULU AFIKISHWA MAHAKAMANI, KESI YAKE YA AHIRISHWA MPAKA JUNI 11.

Lulu akishuka kutoka katika Basi la Mahabusu
Lulu akiwa katika viti akisubiri kusomewa mashtaka.
Askari magereza wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.

CHADEMA YAZINDUA TAWI WASHINGTON DC.

 
Uongozi wa juu wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc  kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mh. Msigwa,  Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi,  Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirege Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
 
Mhe. Leticia Nyerere 
 
 Mhe. Maryam Msabaha 
Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc.
Baadhi ya wakereketwa wachukua kadi baada ya uzinduzi wa tawi la chadema Washington
 Mhe. Nassari Joshua (Dogo Janja) Akishanga mamia ya wana DMV waliofurika katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc
Mhe. Peter Msigwa akiandika masuali yaliokuwa yakiulizwa na baadhi ya wakireketwa 
  
Mwanachama wa chadema kutoka Boston Ma na kamanda Doto wakiuliza masuali tafauti  katika mpango mzima wa uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc uliofanyika jana Mei 27, kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University  Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania
Wana DMV wakisikiliza hutuba ya Mhe. Zitto Kabwe.
Picha zote na swahilivilla.blogspot.com

NEW TRACK, IKO 50/50 By UB SOUNDS FT KASALOO -

Hii ngoma imetengenezwa na Producerwa kike (Illuminatha)  anaegonga Hip.
Klick down and download 4 promo only.

BRAND NEW SONG, JEMBE By SENE TA.

Sene Ta

Sunday, May 27, 2012

MNYEKE AJIFUA KUCHAPANA NA FADHIL AWADH JUNI 9 MWAKA HUU

Bondia Iddy Mnyeke (kushoto) akiwa katika mazoezi na Vitor Njait, ikiwa ni sehemu ya mazoezi yake yanayoendelea katika kambi ya ngumi ya Ilala. Mnyeke anajiandaa na pambano lake na Fadhiri Awadhi linalotarajia kufanyika June 9, mwaka huu katika ukumbi wa Frensi kona Manzese Dar es salaam.
Picha na Super D

MISS DAR INTER COLLEGE KUPATIKANA JUNI 8 CLUB SUNCIRO

Mshindi wa Miss Dar Inter College (katikati) anaeshikilia taji hilo.

Na Mwandishi Wetu
SHINDANO la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012 linatarajiwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Sunciro, ulipo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam, imefahamika.
Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba warembo watakaoshiriki shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.
Alisema mpaka sasa warembo 12 kutoka vyuo vyaBiashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesharipoti kambini.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus,Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.
“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.

WASHINDI WA KILI WALIVYOKINUKISHA MTWARA JANA

Msanii aliyefunika vibaya katika tamasha la Kili Music Award mjiji Mtwara, Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Msanii anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Queen Darling  nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Gwiji la Muziki wa Taarabu nchini, na Mshindi wa Tuzo ya Mtumbuizaji bora wa Kike, Hadija Kopa akifanya makamuzi  katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Mkali wa Bongo fleva Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Mashabiki wakifuatilia burudani kutoka katika Jukwaa ambalo washindi wa Tuzo za Kili Music Award 2012 walikuwa wakitumbuiza kwenye uwanja Umoja  wa mjini Mtwara  jana.
Picha zote na Mpigapicha wetu.

NEW M-LAB RELEAS, UTANDARHYMES - GHETTO AMBASADOR & SONGA.

Artist: Ghetto Ambasador & Songa
Song: UTANDARHYMES
Produced by Duke
M-Lab
Tamadunimuzik.

Saturday, May 26, 2012

BIFU JIPYA KATI YA CYRIL, OMMY DIMPOZ.

CYRIL
BAADA ya msanii aliyevuma na wimbo 'Nai Nai' Faraji Nyembo 'Ommy Dimpoz' kumuua kwa maneno msanii Cyrill, sasa yamemrudi baada ya Cyrill naye kuongea yasiyofaa kumhusu Ommy Dimpoz.
Ommy Dimpoz alinukuliwa katika kituo kimoja cha redio akisema kuwa Cyrill ni msanii ambaye hafanyi shoo kabisa.
"Huyu jamaa amekosea kwa kwa kukimbilia katika vyombo vya habari na kuzungumza tu, siku nyingine ajipange kabla ya kufanya mahojiano yoyote, kwani ukiwa msanii wewe ni kioo cha jamii, haifai kuongea kila linalokuja kichwani mwako" alisema Cyrill.
Bifu hili jipya kati ya wasanii hawa limetokana na kuzuiwa kwa Cyrill kufanya show na BASATA siku ya Jumapili iliyopita pale Club Maisha akidaiwa hana kibali kwani ni raia wa Kenya. Ommy Dimpoz naye alikuwa na shoo yake siku hiyo Billcanas.
Baadaye Ommy Dimpoz alifunguka kwenye vyombo vya habari na kusema Cyrill anatangaza kuwa yeye ndiye kamfanyia fitna ili asifanye shoo hiyo, jambo alilokanusha. 

Friday, May 25, 2012

JANUARI MAKAMBA ALIPOTEMBELEA MAKAO MAKUU YA KAMPUNI YA SIMU YA AIRTEL.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  January Makamba (kushoto) akipokewa na Mkurugenzi Mtendai wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor,  alipofanya ziara kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilino\ wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  January Makamba (kushoto) akipokewa na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Chiruwi Walingo  alipokwenda kufanya  ziara ili kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya akiongozana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kushoto) katika ofisi za makamo makuu ya Airtel  wakati wa ziara yake kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kulia) na ujumbe wake wakati wa ziara ya naibu waziri huyo kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana

CAMP MULLAH WAPATA HARUFU YA MABILIONI YA CHRIS KIRUBI

Kundi la CAMPMULLAH la nchini Kenya
Chris Kirubi - Mmoja kati ya mabilionea wa Afrika
Nyota ya kundi la Hip hop la Campmulla la Kenya inazidi kung’aa. Juzi tu walipokea habari njema ambayo tayari imewaweka kwenye historia ya muziki wa Afrika Mashariki kwa kutajwa kwenye tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act Africa. Na sasa tajiri namba 31 katika orodha ya matajiri barani Afrika kwa mujibu wa Forbes Magazine anataka kuwapa shavu?? Si mwingine ni tycoon wa nchini Kenya Chris Kirubi ambaye ni mmiliki wa Capital FM ya Kenya. 
Ilikuwa ni baada ya leo kufanya interview Capital FM na Lora Walubengo,kama bahati vijana hao watano wakakutana na Mr. Kirubi kubadilishana story mbili tatu! Baada ya kuachana, Kirubi ambaye ni mhudhuriaji mzuri wa mitandao ya kijamii, akatweet, “@CampMulla Great meeting you guys, I think the future is very bright for you. We will work together. Just stay on course."
Ukiambiwa “we will work together. Just stay on cource” na mtu ambaye utajiri wake unafikia $300 Million! Lazima ushtuke kidogo, ushushe pumzi, utulie na kisha ucheke kimoyomoyo na kuimba ‘money, money, money’! 
Kwa umaarufu walionao CampMulla kazi zipo nyingi tu za kufanya na Chris Kirubi husasan zinazohusu kupromote biashara zake. Anamiliki jengo ambalo ni miongoni mwa majengo marefu na yenye thamani zaidi jijini Nairobi! Ni mmiliki wa shirika kubwa la bima, UAP Insurance na kampuni ya ujenzi ya Sandvik East Africa pamoja na michongo mingine!

HEPPY B'DAY DIVA (LOVENESS LOVE)

LEO ni siku ya kuzaliwa ya mwana dada DIVA kutoka Clouds FM. uongozi wa SULE'S INC. & ENTERTAINMENT na blog ya MTOT WA KITAA kwa pamoja wanamtakia mwanadada DIVA heri ya sikukuu ya kuzaliwa. "Mungu akupe maisha marefu yenye mafanikio"

VODACOM YAZINDUA PROMOSHENI YA WIKIENDI YA WAJANJA!

· Wateja wa Vodacom kupata nyongeza ya asilimia 50 kila wanapoongeza muda wa maongezi kuanzia Tsh 1000
· Nyongeza hii inaweza kutumika kwa ajili ya a kutuma ujumbe mfupi SMS, kupiga simu au kuperuzi internet.· Kujua Salio la nyongeza mteja anaweza kubonyeza *102*02#
Kampuni ya mawasiliano inayoongoza Tanzania, Vodacom leo imezindua promosheni kwa ajili ya wateja wake ambapo kuanzia leo hadi mwisho wa wikiendi watapata nyongeza ya asilimia hamsini kila mara wanapoongeza muda wa maongezi wa kuanzia Tsh1000. Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema promosheni hii imetokana na kuguswa kwa wateja na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya WAJANJA ambayo imeonyesha kupendwa na kutumiwa sana na wateja wao kwenye matumizi ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi SMS na kuperuzi kwenye internet.“Tunajivunia tunapowaona wateja wetu wakifurahi na kuendelea kutumia huduma zetu na hii promosheni inanuia kuwapa thamani zaidi yapesa zao wakati huu wa wikiendi ikiwa ni fursa kubwa kwa familia kufanya shughuli kadha wa kadha,” alisema Bwana Meza.Nyongeza hii ya salio ya asilimia 50 inaweza kutumika kwa kutuma ujumbe mfupi, kupiga simu na kuperuzi internet kupitia simu za mkononi na pia promosheni hii ni kwa ajili ya wateja wanaotumia Mpesa kununua muda wa maongezi. Wateja pia wanaweza kuangalia salio la nyongeza hii kwa kubonyeza *102*02#.

STOPA, IZZO B, VEEJAY NA OMMY DIMPOZ NDANI YA TRIPLE A BLUE FAME.

Arushaaaaaaa, sasa Stopa Rhymes,I zzoBizness, Ommy Dimpoz Veejay, May C na wasanii wengine kibaooooooo!!!! watakuwa kwa stage siku ya Ijumaa terehe moja mwezi wa sita mwaka 2012 Pande za Arachuga ndani ya Ukumbi wa The Triple A Blue Fame,performance za kueleweka ndani ya usiku huo unaoletwa kweny na Talet survivor a.k.a Deejay Tass toka Pro 24 Deejays!Come one come all..

Thursday, May 24, 2012

BREAKING NEWS!!!!!!! MBUNGE WA ROMBO APATA AJALI MBAYA BARABARA YA MOSHI ARUSHA.


Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini (pichani) kapata ajali mbaya sana muda si mrefu.
Ajali hiyo imemtokea akiwa safarini toka Arusha kwenda Rombo na ni eneo la Bomang'ombe mjini.Watu watatu akiwemo mamake mzazi wamekufa papo hapo.Mhe. Selasini amepekimbizwa Hospitali ya wilaya ya Hai pale Bomang'ombe; hali yake si nzuri.

STEVIN NYERERE AGAWA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KINONDONI


Stevin Mengele 'Steve Nyerer' kushoto akimkabidhi chandarua mtoto ali Husein  wakati alipokwenda kutoa misaada mbalimbali na kufanya utambulisho wa filamu yake mpya ya Nyerere
Stevin Mengele 'Steve Nyerer'  katikati akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Maunga Kinondoni Dar es salaam leo


Stevin Mengele 'Steve Nyerer' kushoto akimkabizi  maharage kwa mama mrezi wa kituo cha Maunga kilichopo Kinondoni Dar es salaam Bi. Zainabu Bakari alipokwenda kutoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali leo
Stevin Mengele 'Steve Nyerer' akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kwa ajili ya kutambulisha filamu yake ya Nyerere