Thursday, August 29, 2013

DIAMOND MPA ZAWADI YA GARI MZEE GURUMO

1
Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini
 2
Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo 
3
Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari 
5
Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari 
6
Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari 
17
Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari 

Saturday, August 24, 2013

MAMBO YA FIESTA HAYA, LINA NA AMINI


Wasanii lukuki wa muziki wa kizazi kipya usiku wa jana wamewapatia burudani wakazi wa Tabora kwenye show ya Fiesta iliyofanyika kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi. Miongoni mwa mambo yaliyozalisha shangwe la kufa mtu ni pamoja na Amini kumbusu mdomoni mpenzi wake wa zamani Linah waliyependa naye kwenye stage.

Thursday, August 22, 2013

Twanga Pepeta, Roma Mkatoliki kupamba Tamasha la wafanya mazoezi la Vita Malt kesho.

Mkufunzi wa kimataifa wa maswa ya mazoezi ya viungo bwana SAAS akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya tamasha kubwa linalowakutanisha wafanya mazoezi kote nchini na familia zao linalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar Es Salaa ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kujumuika pamoja na kufanya mazoezi ya pamoja sambamba na hilo pia burudani toka kwa bendi ya Twanga pepeta na Roma Mkatoliki na baa za kisuma na Fyatanga zitakuwepo kuchoma nyama kwa kipindi chote,Katikakati ni Meneja wa Vitamalt Plus Consolata Adam na Meneja mawasiliano na mahusiano wa Tbl Edith Mushi.


Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi na litakalofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Vinywaji visivyo na Vileo katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Consolata Adam alisema, wameamua kuandaa bonanza hilo ili kuwakutanisha pamoja wafanya mazoezi wote, ambao mara nyingi wanafanyia katika vituo maalumu (gym).
Consolata alisema, bonanza hilo la aina yake kwa Dar es Salaam litafanyika katika Viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama kuanzia saa 12 asubuhi hapo kesho (Jumamosi).
“Tumeamua kuandaa bonanza linalowakutanisha wanamichezo mbalimbali hasa wafanya mazoezi ili kuweza kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Siku hiyo katika Viwanja vya Posta kutakuwa na gym kumi na mbili zilizo maarufu ambazo zitashiriki na kutakuwa na wakufunzi kumi ambao wataongozwa na mkufunzi wa kimataifa SAAS,” alisema, huku akidai mtu anatakiwa kwenda tu kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.
Alisema, lengo kuu kuu la bonanza  ni kuhamasisha jamii nzima kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga umoja imara wa gym zilizopo nchini.
Consolata alisema, katika kuhakikisha bonanza hilo linakuwa bora na la kufana jumla ya gym kumi na mbili zitashiriki ambazo ni Better Life, Genessis ya Kijitonyama, Segerea Gym, Rio Gym,Genessis ya Kimara, Azula ya Mikocheni na Serena Gym.
Alisema pia baa zilizoshinda katika kuchoma nyama katika mashindano yaliyofanyika hivi karibuni za Fyatanga ya Tegeta na Kisuma Bar ya Temeke, zitaonyeshana umwamba kwa kuchoma nyama bomba kwa kipindi chote hicho.
“Tumeweka burudani za kila aina kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya kufurahisha kama soka, netiboli, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, Sehemu za watoto kuchezea pia na zawadi nyingi toka Vita Malt zitakuwepo.”
NaYe Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TBL, Edith Mushi alisema mbali na hayo kutakuwa na burudani mbalimbali toka kwa bendi African Stars ‘Twanga Pepeta’ na msanii mkali wa Hip hop, Roma Mkatoliki sambamba na burudani nyingine nyingi kwa kipindi chote cha tamasha.
“Hii ni siku ya familia napenda kuwajulisha watanzania wote na wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na familia zao siku ya Jumamosi, hakutakuwa na kiingilio chochote na vinywaji vyote toka TBL vitakuwepo.
“Lakini pia watu wa kawaida na wa rika zote siku hiyo hakutakuwa na kikwazo chochote cha kufanya mazoezi, kwani ni bure kabisa, hivyo nawashauri tufike kwa pamoja ili tuweze kupata pia ushauri mbalimbali juu ya kupunguza uzito na aina ya mazoezi yanayotakiwa,” alisema.
Vita Malt ni kinyaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).'THE NIGHT OF THE LEGEND'


Wednesday, August 21, 2013

BANX KUDONDOSHA NGOMA MPYA TAREHE 1 SEPTEMBA.

Tarehe Moja Mwezi wa Tisa 2013, Banx atadrop "Excellent" ikiwa ni mkono toka Noizmekah Studios akishirikiana na Defxtro alopita Verse moko, Pata Kionjo/Snippet HAPA 

Sunday, August 18, 2013

MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA WAVUKA LENGO

http://2.bp.blogspot.com/-3USyFZ0ObHs/UhFPOnoKTiI/AAAAAAAADRE/qtqnU35Ryh4/s1600/100_0753.JPG


Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza na waandishi wa habari jana kutoa takwimu za makusanyo ya damu kwa mwezi Aprili mpaka Juni mwaka huu ambapo ulivuka malengo kwa asilimia 111 kutoka chupa 36,278 mpaka 38,948. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Masoko na Uhusiano Bi. Rayah Hamad  (Picha na Mpiga picha maalum).


PRESS RELEASEMPANGO wa Taifa wa Damu Salama umevuka lengo la makusanyo ya damu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa kukusanya chupa za damu 38,948 ambazo ni asilimia 111 ikilinganishwa na chupa 36,278 zilizokusanywa kutoka Januari hadi Machi mwaka huu.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Damu Salama, Bw. Rajab Mwenda akizungumza jana Dar es Salaam alisema kanda inayongoza kwa uchangiaji ni Mashariki na Kanda ya Ziwa.
Alisema mafanikio hayo yametokana na uanzishajiwa mpango wa damu salama wa  kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari  katika jamii na kushirikisha wadau.
 Bw. Mwenda alisema maadhimisho ya siku ya wachangia Damu duniani ambapo lengo la kukusanya chupa za Damu 8,500 kutoka kanda sita za mpango wa Taifa wa damu salama liliwekwa na mpango ulifanikiwa kukusanya jumla ya chupa 8,683
Alisema Mpango wa Damu salama kushirikiana na wadau mbalimbali kama asasi za kiraia  nayo imeongeza makusanyo ya damu toka vituo vidogo vya kuchangia damu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,  Morogoro na Dodoma kutoka chupa za damu 2,560 mpaka chupa 3,151 kufikia Aprili hadi Juni mwaka huu.
Aliwaomba wadau kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya jamii na vipeperushi.
Bw. Mwenda alisema ushirikiano ni mdogo kati ya wahamasishaji wa Mpango  wa damu salama na viongozi wa Taasisi mbalimbali, matumizi mabaya ya damu kidogo inayopatikana katika hospitali zetu na miundo mbinu hafifu hususan barabara mbovu wakati wa ukusanyaji  na usambazaji wa damu.
Alisema changamoto nyingine ni uuzwaji wa chupa za damu kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa hospital ambao si waaminifu hivyo kukatisha tamaa wachangia damu kwa hiari.
Bw. Mwenda alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianzisha Mpango wa Taifa wa Damu Salama mwaka 2005 ili kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha kwa wote wanaohitaji.
Alisema shughuli za mpango ni pamoja na uhamasishaji jamii kuhusu uchangiaji damu wa hiari, ukusanyaji upimaji na usambazaji wa damu salama mahospitalini.
“Mpango wa Taifa wa Damu salama unafanya kazi kwa kushirikianana kitengo cha kuzuia magonjwa (CDC)  na wadau wengine wa Chama cha Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)” alisema Bw. Mwenda.
Alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama uliweka lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) katika damu iliyokusanywa asilimia 1.1 kwa kipindi Aprili- Juni ikilinganishwa na asilimia 1.2 kipindi cha Januari hadi Machi baada ya kujikita katika suala la uhamasishaji na kutoa damu toka kwa jamii ambayo ni salama, kuboresha dodoso la wachangiam damu na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na wachangiaji kujiepusha na tabia hatarishi ili wawe wachangiaji wa kujirudia.

JINSI POLISI WALIVYOWADHIBITI MAJAMBAZI PALE ILALA JANA ASUBUHI


PICHA KWA HISANI YA BLOG YA HABARI MPASUKO

Friday, August 16, 2013

PICHA ZA UFUSKA ZA MSANII MANAIKI SANGA ZANASWA AKIFANYA UFUSKA NA MADEMU TOFAUTITOFAUTIMtandao mmoja nchini  umefanikiwa kunasa picha mbalimbali za aibu za msanii chipukizi na mwanamuziki Manaiki Sanga akifanya ufuska wa kutisha na wanawake tofauti tofauti hali inayoonesha ameazimia kujitoa muhanga juu ya gonjwa hatari la ukimwi linalotishia dunia nzima.
 Habari za uhakika toka kwa chanzo chetu kilichotushushia shehena za  picha hizo kilisema msanii huyo ambae pia ni anaigiza pamoja na kundi  la Ze Komedi la East Afrika Tv tangu apate jina amekuwa akijihusisha  na vitendo viovu vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwarubuni mabinti  kupiga nao picha za aibu kwa lengo la kutafuta jina na amekuwa akitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanikisha suala hilo. 
Aidha katika hali nyingine msanii huyo aliyetamba sana kwenye filamu  ya Love Position, Tikisa na nyinginezo amekuwa akitumia gari yake  kufanyia ufusika  hadharani....

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Wednesday, August 14, 2013

OFFICIAL VIDEO, SAIGON - RUDIA

WASANII WA MOSHI, GAZA CROSS WAJA NA 'MASOJA'

Kundi chipukizi toka Moshi Town, Gaza Cross na wimbo wao wa "MASOJA" mahadhi ya Dancehall/Kwaito wakiwakilisha vema muziki wa kaskazini Duniani kote,pata kuusikiliza HAPA

Friday, August 9, 2013

SALAMU ZA IDD LFTIR KUTOKA TIMU NZIMA YA SULE'S INC. & ENTERTAINMENT


Kwa kuwa sisi wote ni ndugu, Timu nzima ya wafanyakazi wa SULE'S INC. & ENTERTAINMENT wanatoa salamu za siku kuu ya IDD LFITIR kwa wadau wote Blog hii na kampuni kwa jumla.
Mungu awape mwongozo katika kusherehekea siku kuu hii.
IDD MUBAARAK.

Wednesday, August 7, 2013

'THE LEGEND IS BACK' NI KAMA KAWA PALE ISUMBA LOUNGE / JOLLIE CLUB

Legends dont speak much cause we believe action speaks louder than words, come join the legends @isumba lounge (jollies club) this eid and dance to ur favourite tunes from the 80's to the late 90's, behind the 1 and 2 DJ John Dillinga aka the Legend is Back, DJ Fast Eddy and DJ Young Kelvin. Party starts on eid eve 2 the 2nd eid. Doors open 9pm, entry on the 1st eid 10k b4 mid midnight 15k after mid night dont miss it.


Tuesday, August 6, 2013

MAJEMBE YA KASKAZINI (FIDO VATO & BOU NAKO - MI NAJUA

Majembe ya Kaskazini Bounako & FidoVato wanarudi tena na Hardcore hiphop Joint kwa jina "Mi Najua" ikiwa ni mkono wa Defxtro toka Noizmekah studios, remix ya pini hili litakuja mwezi ujao wakiwemo Mcs wengine JCB na Moplus, kwa sasa Majembe wanajipanga na Video Kadhaa za ngoma zao hivyo mashabiki wakae mkao wa kuburudika na kuelimika,Pata kuusikiliza wimbo huu na kudownload HAPA