Thursday, August 30, 2012

KITU CHA TAMADUNIMUZIKI KESHO PALE NEW MSASANI CLUB


WASANII WATAKIWA KUIJENDELEZA KITAALUMA

Mkufunzi wa masuala ya aundaaji wa Filamu kutoka taasisis ya Sanaa na uandishi wa Habari (IAMCO) Ngalimecha Ngahyoma, akizungumza jambo katika Jukwaa la Sanaa, kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego

Na Mwandishi Wetu
Wasanii wa nchini wametakiwa kujiimarisha katika masuala ya taaaluma ili waweze kufanya kazi zenye ubora na zinazokidhi mahitaji  ya soko la ndani na nje ya nchini.
Akizungumza katika Jukwaa la Sanaa jana, mkufunzi wa masuala ya uandaaji wa filamu hapa nchini Ngalimecha Ngahyoma amesema kumekuwa na matatizo mengi katika uandaaji wa kazi za filamu hapa nchini kutokana na wasanii kutokuelewa misingi ya uandaaji wa filamu.
“Kuna maeneo ya msingi ambayo yanahitaji watu kubobea ili kuyafanya kwa utimilifu, na hakuna njia ya mkato ni lazima kuyapata shuleni kwa maana lazima mtu ufundishwe. Wasanii wengi wanatumia vipaji vyao, lakini matokeo ya kufanya mambo kwa vipaji ndiyo haya ambayo yanatupa filamu zenye matatizo katika maeneo mbalimbali,” alisema.
Alisema ni muhimu kwa wasanii kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuanza kuandaa kazi kitaalamu ili kufanya kazi zilizobora na kwamba ni vyema kutumia wataalam katika maeneo yote yanayohitaji utalaam badala ya mtu mmoja kufanya kazi zote.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego, amesema suala la taaluma alikwepeki katika kutengeneza kazi zenye ubora na kuwasisitiza wasanii kujiunga na vyuo kupata utaalam katika fani zao.

Monday, August 27, 2012

TOP 10 YA MADEM WENYE MATAKO MAKUBWA HLLYWOOD

No. Jenifer Lopez
Anautajiri wa dola milioni $250 ,jinsi gani alipata hu utajiri,?? Nikutokana na uigizaji wake, Mfanyabiashara na kazi yake ya uimbaji. J-lo ni mwanada maaraufu mwenye maumbile makubwa ya makalio, ambayo yanafanya ashikile nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wanawake maarufu Hollywood. Inarepotiwa kuwa mataka yake ameya weka bima ya dola milioni $27. Anapenda kujivunia kuonyesha assets yake hiyo kwenye magazines cover ya Stuff magazine mwaka 2001. Ambalo ni moja ya magazine iliyoweka histori ya rekodi ya gazeti lilouza kuliko. Kiukweli hilo tako limegharimu maelfu ya dola na sio chini ya hapo. Matako mengine ya nakuja na kuondoka lakini kwa Jlo atatumia kila kitu kulinda tako lake. Lol

No.2 Kim Kardashian
Anautajiri wa dola milioni $35, jinsi alivyo upata huo utajiri, ?? utajiriwake umetokana , umodel, uigizaji, mwanamkemfanyabiashara, Television Personality, na socialite. Anachukuwa nafasi ya pili kuwa ni mwanamke mwenye Tako kubwa Hollywood, nalilionekana sana kwenye s*x tape ambayo alikuwa nimmoja ya maboyfriend wake maarafu sana. Naalishazushiwa kuwa matako yake ni yakutengeza lakini yeye alikataa akasema no way its real.

3. Beyonce.
Anamiliki utajiri wa dola milioni $300 milioni. Jinsi gani alivyotengeneza utajiri?? Dada huyu anaingiza pesa zake kwa kuwa muandishi mzuri wa nyimbo, rekodi Producer, muigizaji, umodel, mvumbuzi wa mavazi, na ni mfanyabiashara. Anajiita “b**t-y-l-i-c-i-o-u-s” . Nahuyu anachukua nafasi ya 3 kwa kuwa na matako makubwa Hollywood

No. 4 Serena Williams
Anautajiri wa dola miliobi $85, nautajiri wake unatokana na uchezaji wa Tennis as Professional. Na nimaarufu kwa kwa kuwa na tako kubwa kwenye tennis, lakini kutoka kwa serena mwnyewe anasema kuna mwanamke mwenye matako makubwa kuliko yangu huko nje nikisimama nae ni aibu tu.

No. 5 Nicki Minaj


Anautajiri wa dola milioni $14 ambao umetokana na uandishi wa mistari yake na rapa, mwanadada huyo anapenda sana kuongelea kuhusu tako kila wakati, hata kwenye interview iliotokea New York post Nicki Minaj alikuwa anaongela kuhusu ruma za utengezaji wa matako yake. “absolutely not” said Nicki Minaj alipokuwa anaulizwa kuhusu matako ya kutengeneza , “people will pick anything to talk about , and that happens to be the thing at the moment’’. Alisema Nicki Minaj.

No.6 Vida Guerra
Anautajiri wa dola milioni 2.5 na amazitengeza kupitia kazi yake ya umodel. Wakati hajulikani kama wanawake wengine waliopo kwenye orodha yetu, Nyuma kwa Vida kunamilikiwa na dunia, alishinda FHM’s Best B*tt , kwenye the world award na sio mara moja. Ni model, muimbaji na mwigizaji lakini anajivunia kwa kujilikana kwa umbo la mwili wake. Kiukweli ameshinda tuzo ya best b*tt mara mbili .

No.7 Nicole “Coco” Austin
Anautajiri wa dola milioni 4 kutokana na umodel, reality Tv Personality , web personality. Hakuna wasi wasi wowote kuwa Mke wa Ice T , Nicole Coco Austine anajivunia mwili wake sana. Anapenda kupost picha za makalio yake sana kwenye Twitter,

No.8 Buffie Carruth
Buffie Carruth vile vile anajulikana kwa jina la Buffie The Body or simply Buffie, ni model kutokea Athens, Georgia anajulikana kunekana kwenye posing za hip hop zinaendana na magazine na kuonekana kwenye video za hip hop. Shukuru kwa model kama Buffie The Body the Big Booty” comple imefagia Us nzima nao inelekea to getting out of control.

No.9 Jessica Biel
Anautajiri wa dola milioni $ 18 , amepatamafanikio hayo kwa kuwa muigizaji, model na mwimbaji , anachukua nafasi ya 9 kwa kuwa na makalio makubwa kwa wanawake maarufu. Alianza kucheza kwenye tv kama mtoto wakike wa muhubiri. Lakini umaarufu wake ulitoke bada yakupiga picha ya utupu kwenye Gear Magazine akiwa na umri wa miaka 17.

10. Sofia Vergara
Anamiliki utajiri wa dola milioni 14, na utajiri huo unatokana na uigizaji, modeling , mtangazaji wa television na mjasiriamali. Ni muigiza wa modern family amefungasha kila mahali. Ni mdada mwenye kipaji, mzuri na ana makalio mazuri yenye mvuto sana. Ame shikilia namba tatu kwenye Askmen.com 99 Most Desirable Women wa 2011

Friday, August 24, 2012

SUMA MNAZALET: OSTAZI JUMA (MTANASHATI) SIO MAFANYAJI KAZI, ANAPENDA SIFA NA KUUTAKA USTAA KWA NGUVU

Sababu muhimu kuliko zote ya kujitoa kwa OSTADH JUMA NA MUSOMA MTANASHATI, na sio kufukuzwa kama alivyowadanganya waTANZANIA ni hii hapa. Nilienda mtashati kwa ajili ya kuhitaji usimamizi thabiti wa kazi zangu ili niweze kufika mbali na kutambulika zaidi EAST AFRICA,AFRICA na dunia kiujumla ndo maana nikaingia mtanashati! ckufata ela za OSTADH JUMA, baada ya kuingia nikagundua kwmba kwa ostadh juma akuna hilo.
Ila lililopo sio kazi bali OSTADH JUMA anahtaji zaidi u STAR, UMAARUFU na kujulikana TANZANIA zaidi hta ya wasanii. hilo niligundua pale 2 ambapo hata ukiiimba nyimbo na R KERRY au LIL WAYNE alaf ujamtaja OSTADH JUMA NA MUSOMA au kumuandika kwnye video iyo NYIMBO AIPOKEI, hvyo nikaona hapa akuna kazi zaidi ya kumpa SIFA M2.
La pili! OSTADH JUMA yuko tayari kumwaga hata million 10 kwa wa2 wa media ili aonekane tajiri na asifiwe kwnye vyombo vya habari na wakati huo huo msanii una shoot video ya laki 4 low quality vp utaweza kumfikia m2 kama AY anaye shoot video million 30, vp utaweza kupigwa kwnye vi2o vya kimataifa na kujulikana africa na dunia kama CHANEL O, MTV, TRACE na vinginevyo wakati una video ya miyeyusho! kwa hilo pia nikagundua mtanashati akuna kazi ila sifa 2. kama mwanamuziki nnayejitambua nahitaji kufika mbali siwezi kukaa sehem kama hiyo kwani video za laki 4 mi mwnyewe nilikuwa nafanya na kampuni yangu ya MEGA PIX 20.
M2 kama PNC awezi kuliona hilo wala kujitoa kwa sbb chumba anacholala kodi kalipa ostadh juma na dogo janja pia inabidi amtetee ostadh juma kwa sbb asipofanya hivyo atakosa pa kulala, kula na atarudi ARUSHA so lazima wamtetee ostadh juma na kunikandamiza mimi ili waendelee kuwa mjini! ila OSTADH JUMA ANAZINGUA na sbb anazotoa kuhusu mimi na MANAGER MANENO ni za uongo anatengeneza mazingira ya kujisafisha. kuhakiki hilo angalia video zote za wa2 wa mtanashati zinakoshutiwa ni sehem za laki 4 so kwa hali iyo m2 utaenda wapi? kaona bolingo wa2 awasikilizi sana so hta akipaishwa jina alikui sana akaona bola atumie wabongo fleva ili a HIT TZ na kafanikiwa kwa ilo ila kwa kazi akuna. na hta uo mkwanja so kiivyo kama watanzania mnavyosikia mi mwnyewe nilikuwa najua kama nyie, ila kuna mengi ukiingia ndo utayajua! 
CKO MTANASHATI NIMEJITOA ananitishia kunionyesha kuwa yeye ndo OSTADH JUMA anamtishia manager maneno ila ndo mziki NAHITAJI SUPPORT YENU NA UKWELI NDIO UO! DOGO JANJA, PNC NA AMAZON wamepangwa yakusema ili wapotoshe ukweli.. haha hahaa chunguza niliyoyasema mi msanii wa watanzania so ostadh juma.
DOGO JANJA NA PNC NDO WAMEKUWA WASEMAJI BAADA YA KUPANGWA WAKATI MI NAONGEA NA OSTADH JUMA. KWELI NJAA NOMA! JANJA ANASAHAU MI MSANII KAMA YEYE ILA OSTADH JUMA SO MSANII. na nimemuandikia mashairi kwnye watasubri ya MTANASHATI na ile ya waanga wa meli! si angeandikiwa na OSTADH.
HII PIA AMEIANDIKA KATIKA UKURASA WAKE (SUMA MNAZALETI) WA FACEBOOK.

KOCHA MZONGE HASANI AWANOWA MABONDIA WA TIMU YA TAIFA

Makocha wa timu ya Taifa wakiwaonesha mabondia jinsi ya ngumi zinavyopishanishwa wakati wa mchezo kushoto ni Hasani Mzonge na Edward Luyakwipa
Hasani Mzonge akimwelekeza mmoja wa Mabondia wa Timu ya Taifa jinsi ya kupishanisha ngumi wakati unapigana. 
Unatakiwa mkono wako unyoshe hivi ndivyo anavyosema Kocha wa mchezo wa ngumi Hasani Mzonge kulia wakati alipokuwa anafundisha mabondia wa timu ya Taifa.
Kocha wa mchezo wa ngumi Hasan Mzonge akiwaelekeza mabondia wa timu ya taifa ya masumbwi jinzi ya kupiga ngumi zilizonyooka wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika katika GMY ya Gmykhana Klabu.
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Thursday, August 23, 2012

ABDALLAH BULEMBO AJITOSA KUWANIA UENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA YA CCM

KATIBU mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamis Suleiman Dadi (kulia) akimkabidhi fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo Majura ambaye pia ni mdau mkubwa wa michezo nchini.
********************
MDAU wa michezo nchini Abdallah Majura Bulembo amejitosa kuwania uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Bulembo ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (MRFA) na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alichukua fomu hizo na kuzirejesha jana hiyohiyo.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hizo, Bulembo alisema kwamba amelazimika kuwania nafasi hiyo ili kuifanyia makubwa jumuiya hiyo kwani ni mwanachama halali wa CCM na mwenye sifa hivyo anawajibu wa kuwania nafasi yoyote inayomfaa kwa lengo la kuendeleza mikakati iliyopo ndani ya jumuiya hiyo.
Hata hivyo, Bulembo ambaye katika uchaguzi uliopita aligombea nafasi hiyo na kushika nafasi ya pili nyuma ya Balozi Athuman Juma Mhina ambaye sasa ni marehemu, alisema ataweka wazi mikakati yake pindi atakapopitishwa na halmashauri kuu ya CCM.
Bulembo anakuwa mgombea wa saba kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ambapo awali wanachama waliojitosa ni pamoja na John Edward Machemba, Said Ramadhan Bwanamdogo, Salim Hamis Chikago, Jasson Samson Rweikiza, Alfred Joseph Mwambeleko na Alphonce John Siwale.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Hamis Suleiman Dadi,alisema zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu wa nafasi mbalimbali katika jumuiya hiyo lililoanza  Agosti 22 litafikia tamati Agosti 29 mwaka huu.
Alisema mbali na nafasi ya uenyekiti, tayari baadhi wa wanachama wamejitokeza kuchukua fomu za  kuwania nafasi mbalimbali za uongoizi katika jumuiya hiyo kwa upande wa Bara na Visiwani.
Alizitaja nafasi nyingine ni pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Bara na Zanzibar, Wajumbe wa Kamati Kuu Wazazi kwa upande wa Bana na Visiwani, Jumuiya ya Wazazi kwenda Umoja wa Wanawake (UWT) na  Jumuiya ya Wazazi kwenda Umoja wa Vijana (CCM).

HABARI/PICHA  http//:dinaismail.blogspot.com

DK. MWAKYEMBE AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA BANDARI NA WASAIDIZI WAKE

Dk. Mwakyembe
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.
Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.
Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.
Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.
Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na inami na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.
Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.

MAGAZETINI SIKU YA LEO

MDAU ALLY KINDOILE APENYA USAILI KRFA, UCHAGUZI SASA KUFANYIKA SEPTEMBA 9

Kidole (kushoto) akisalimiana na mmoja kati ya wagombea wenzake.

Na Mwandishi Wetu

USAILI  kuwania nafasi ya uongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro (KRFA), umefanyika mapema leo Agosti 22,  chini ya Mwenyekiti wake Dr. Haule na kushuhudia viongozi mbalimbali wakichaguliwa huku mdau wa michezo na aliekuwa Mjumbe wa Villa Squad, Ally Kindoile, kupenya kwenye usaili huo.
Katika usaili huo ulioshuhudiwa na wadau mbalimbali wa michezo, ulifanyika katika ofisi za Manispaa ya Moshi,  ambapo nafasi ya Mwenyekiti waliopita ni pamoja na Godluck Moshi  na Charles Mchau, Makamu Mwenyekiti Shaban Mwalimu  na nafasi ya Katibu Mkuu msaidizi kwenda kwa Ally Kindoile.
Aidha nafasi zingine walizopita wadau hao wa soka wa Mkoa wa Kilimanjaro, majina na nafasi zao kwenye mabano ni Kusianga Kiata (Mhani), Distin Kilua  na Abdala Husein (Wajumbe Mkutano Mkuu).
Wengine ni Keneth Essau  na Amri Kiula (Wawakilishi wa Vilabu), Denis Joseph Msemo, Cuthbert Mushi  na Nassor Muchi (Wajumbe Kamati  ya  utendaji) na Salma Omari Mndaira (Mwakilishi TWFA).
Katika hatua hiyo, Uchaguzi wake unatarajia kufanyika Septemba 9,Ulili, Mkoani humo.
Hata hivyo, Ali Kindoile alipozungumza na waandishi wa Habari, muda mfupi baada ya usaili huo, alishukuru kwa kupita kwake na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kuinua soka la Mkoa  huo, ambapo mipango yake mbalimbali anatarajia kushirikiana na wagombea wenzake pindi watakapofanikiwa kwa pamoja kupata nafasi hiyo hiyo Septemba 9.
“Tunaomba ushirikiano na umoja ili kufika mbali katika soka letu, umoja wetu ndio tutasaidia soka la mkoa huu” alisema Kindoile.
Kindoile licha ya kuwa mdau wa michezo, aliwahi kuchezea timu mbalimbali zikiwemo Simba B na Idrisa Fc, kwa sasa ni mdau mkubwa wa timu ya Kilimanjaro Rangers ya mkoani humo na amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vijana kwenye soka.
Uchaguzi huo awali ulitakiwa kufanyika Agosti 28,  ambapo sasa umesogezwa mbele mpaka hapo Septemba 9.

Tuesday, August 21, 2012

BREAKING NEWS: MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA YATENGUA UBUNGE WA DR LALALY KAFUMU

Aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Dk Dalali Kafumu, aliyechukuwa Ubunge kwenye uchaguzi mdogo uliopita baada ya Rostam Aziz (CCM) kujiuzulu wadhifa huo. Igunga imeingia katika sura mpya baada ya Mahakama Kuu ya Kanda ya Tabora kutengua ubunge wake leo hii. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Mary Shangali

Monday, August 20, 2012

OSWARD AMGARAGAZA MATUMLA


Bondia Rashidi Matumla (mwenye bukta nyeusi)  akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika ukumbi wa Dar live Maneno alishinda kwa point.
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, August 19, 2012

NI ZAMU YA MABONDIA ZOLA D NA MCHUMIATUMBO UZITO WA JUU


Bondia David Michael Mlope (Zola D – King) akitunishiana msuli na Alpjonce Joseph (Mchumiatumbo) wakati wa upimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya idi pilikatika Uwanja huo huo wa Chuo cha Bandari Temeke.

Bondia David Michael Mlope (Zola D – King)  akipima uzito leo kwa ajili ya mpambano wa idi pili utakaofanyika katika Uwanja huo huo wa Chuo cha Bandari Temeke

Bondia Alpjonce Joseph (Mchumiatumbo) akipima uzito.
Mtangazaji wa kituo cha ITV Amir Masareakimuhoji Bondia David Michael Mlope (Zola D – King).
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

ALLY REHEMTOLLAH: USAILI WA ‘ENCHANTED JUNGLE’ AGOST 26

BAADA ya kimya cha muda mrefu, mbunifu wa mitindo Ally Remtulah amevunja ukimya na kuelezea dhamira yake ya kufanya onyesho la kwanza mwaka huu, litakalofanyika katika hoteli ya Serena ya jijini Dar es salaam
Onyesho hilo litakalofahamika kama enchanted Jangle, litafanyika September 24 mwaka huu, huku likitoa nafasi kwa watu mbalimbali kushuhudia toleo lake jipya litakalofahamika kama AR 2013.
Ally Remtulah alisema, onyesho hilo litakuwa tofauti kabisa na maonyesho mengine yaliyowahi kufanyika nchini, kwani ukiachilia mbali tofauti ya mavazi pia kuna utofauti mkubwa wa mandhari alisema.
“Imezoeleka kuona ‘stage’ za kawaida zikitumiwa kuonyesha mavazi lakini kwangu mimi mambo yatakuwa ni tofauti kidogo, kwani ukumbi nitakaotumia utatengenezwa mithili ya mwitu hivi na hivyo kuleta muonekano wa kipekeee” alisema mbunifu huyo
Remtulah aliongeza kuwa wanamitindo wenye viwango vya juu watakuwepo kuonyesha toleo lake hilo. Na usaili wa wanamitindo watakaoshiriki utafanyika Agosti 26 mwaka huu.
Wataalamu wa mambo ya mitindo watakuwepo katika usaili huo, kuchagua wanamitindo mahiri watakaopanda stejini kwenye onyesho hilo.
Katika onyesho hilo pia kutakuwepo na onyesho maalum la vito vya tanzanite ambapo watanzania watapata wasaa wa kujionea na kununua vito vinavyotengenezwa na madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee alisema.
Hili ni onyesho la nne kuandaliwa na mbunifu huyu. Maonyesho yake yaliyotangulia ni pamona na ‘Prism Break’, ‘Temptation’ na ‘Delectable’
Habari kwa hisnai ya Gazet la mwananch 'starehe'

Friday, August 17, 2012

BONDIA SANDE KIZITO TOKA UGANDA AWASILI KUMKABILI RAMADHANI SHAURI SIKU YA IDI PILI

Bondia Sande Kizito wa Uganda
Bondia Sande Kizito wa Uganda kulia akiwa na kocha wake Bogere Francis baada ya kuwasili.
Bondia Sande Kizito katikati akiwa amewasili katika jiji la Dar es salaam usiku wa leo akitokea Uganda kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauri siku ya Idi pili kushoto ni mwenyeji wake aliyempokea Yasini Abdallah 

Thursday, August 16, 2012

AIRTEL YATANGAZA SHULE 93 ZA SEKONDARI ZITAKAZO FAIDIKA NA MRADI WA VITABU.

Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano (katikati), Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi (kulia) na Bw Masozi Nyirenda, wakionyesha vitabu vilivyotolewa na Airtel
Mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla maalum ya Mradi na droo ya
kugawa Vitabu kwa Shule za Sekondari ijulikanoyo kama ‘ AIRTEL SHULE YETU’ iliyofanyika katika ofisi za Airtel. Kulia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi, Hawa Bayumi na kushoto ni Ofisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda.

Na Mwandishi wetu
Dar as Salaam, Airtel Tanzania, imeendeleza dhamira yake katika kuboresha elimu kwa kuchezesha droo iliyochagua shule za sekondari  93
zitakazo faidika na mradi wa vitabu wa Airtel wa kusaidia jamii unaojulikana kama  Airte shule yetu kwa  mwaka 2012 -2013. Akiongea katika mkutano na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Airtel Kitengo cha Mawasiliano Bi, Beatrice Singano Mallya alisema “Mwaka huu, Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia elimu kwa kuzipatia vitabu shule  za sekondari 93.
Mradi huu utafaidisha shule 3 kutoka katika kila mkoa Tanzania bara na visiwani.
Shule 93 zilizochaguliwa ni matokeo ya droo iliyochezeshwa na kuzichagua shule hizo kutoka shule 3,000 zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu Tanzania kuwa ni shule ambazo zina uhitaji mkubwa wa vitabu na kushauri  ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa Airtel shule yetu.
“Toka tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka saba iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi ya shule 1000 za sekondari zilizopo Tanzania bara na visiwani  kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa  yote  na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya Tanzania.
Mwaka huu vitabu tunavyogawa vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 110, hivyo kila shule  iliyopatikana kwenye droo hii watapata Vitabu alisema Mallya.
Bi Mallya aliongeza kwa kusema “tumefanya kazi kwa pamoja na Mamlaka ya elimu na Wizara ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mahitaji ya vitabu kwa shule zote zitakazoingia kwenye Mradi huu wa Shule yetu tunayatimiza kwa  kuwapatia vitabu vya mitaala ya  masomo yao kama ilivyopendekezwa na Wizara” 
“Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwa kutoa misaada mbalimbali ili kuisaidia jamii hapa Tanzania  hasa kwa kuchangia sekta ya elimu kwa kuwapatia vitendea kazi vikiwemo Vitabu  kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Mwaka jana pia Airtel ilisaidia Vitabu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 104 tsh  kwa  shule za sekondari kwa kupitia  droo iliyohusisha jumla ya shule 502″ alisema Bi, Mallya.

Nae Afisa Mkuu Mwandamizi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw Masozi Nyirenda aliongea kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ulimu (TEA) alisema “Mamlaka ya Elimu Tanzania tunawashukuru sana Airtel kwa dhamira yenu ya kusaidia jamii kwa kuinua kiwango cha elimu hapa nchini” Mradi wa Airtel Shule Yetu ni mradi mzuri sana kwa jamii yetu kwa kuinua kiwango cha elimu  na maisha ya watanzania”.
Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo watanzania wote pamoja na waalimu mtakaopokea vitabu hivi vya mradi wa Airtel Shule yetu tuvitunze na kuvitumia vizuri ili kuunga mkono jitihada za Airtel katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu hapa nchini” aliongeza kwa kusema Bw, Nyirenda.
Mbali na  shule 93 za sekondari zitakazofaidika na mradi huu wa vitabu mwaka huu,  pia Airtel Tanzania imeshamaliza kukarabati shule ya msingi ya Kiromo iliyopo nje kidogo ya jiji la DSM kando kando na barabara ya bagamoyo  ilichaguliwa mwaka jana 2011 huku mipango mingine ya mwaka huu ikiendelea ili kupata shule nyingine itakayofaidika kwa kujengwa na kukarabatiwa na Airtel shule Yetu.
Airtel bado itaendelea kushirikiana wizara ya elimu kwa wadau wengine kuweza kushiriki katika kuinua kiwango cha elimu hapa Tanzania.

Wednesday, August 15, 2012

BONDIA RASHIDI MATUMLA AJIFUA KWA KINYOGOLI KWA AJILI YA MPAMBANO WA IDI MOSI


Kocha  Mkongwe wa mchezo wa Masumbwi nchini  Habibu Kinyogoli 'kushoto' akimfua bondia Rashidi Matumla wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Matumla anajiandaa na kupambana na Maneno Osward siku ya Idi mosi.

Kocha  Mkongwe wa mchezo wa Masumbwi nchini  Habibu Kinyogoli 'kushoto' akimfua bondia Rashidi Matumla wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Matumla anajiandaa na kupambana na Maneno Osward siku ya Idi mosi litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live .
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com