Sunday, August 5, 2012

PREZZO MSHINDI WA PILI SHINDANO LA BIG BROTHER AFRICA 2012

Msanii wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Flava, kutoka nchini Kenya Prezzo (pichani kushoto) akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa ndani ya Jumba la BBA Afrika, baada ya kuibuka kidedea katika nafasi ya pili ya shindano hilo la  Big Brother StarGAME 2012 , lililomalizika usiku wa kuamkia leo. 
Prezzo alitangazwa kuwa mshindi wa pili nyuma ya Keagan kutoka nchini Afrika ya Kusini ambaye aliibuka kidedea katika nafasi ya kwanza na kutwaa Taji la Big Brother StarGAME 2012 na dola za Kimarekani 300,000, ambazo ni sawa na milioni 460 za kitanzania, huku Prezzo, pia akiambulia na kuteuliwa kuwa Balozi wa One Campaign na kupata nafasi ya kuwa mmoja kati ya Wasanii watakaohudhuria katika jukwaa na Shoo kubwa ya mkali Jay Z itakayofanyika nchini Marekani hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment