Sunday, August 29, 2010

CUF NAO WAZINDUA KAMPENI ZAO JIJI DAR!

Baada ya chama cha mapinduzi na chadema kuzindua kampeni zao jijini Dar es salaam sasa na cuf nao wawazindua rasmi 

Prof. Lipumba akisalimiana na Mh. Hamad Rashid mmoja wa wanachama na viongozi waandamizi wa CUF
 
Mwenyekiti wa CUF na mgombea urais wa chama hicho cha wananchi, Prof. Ibrahim Lipumba akisalimia wanachama wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya chama hicho katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar

Sehemu ya umati wa wana CUF waliohudhuria mkutanoni hapo

Saturday, August 28, 2010

JESHI LA WANANCHI LATOA TAHADHARI KWA WAKAZI WA DSM NA PWANI.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wakazi wa Pwani na Dar es salaam kutokuwa na hofu yoyote kufuatia zoezi la majaribio ya ulizaji wa ving’ora likalofanyika tarehe 31, Agosti, 2010.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ leo jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa ving’ora hivyo ambavyo hulizwa wakati wa hatari vitafanyiwa majaribio kwa siku mbili mfululizo nyakati za asubuhi pia ikiwa ishara ya sherehe za JWTZ kutimiza miaka 46 tangu lilipoanzishwa zinazoendelea katika kamandi ya wanamaji Kigamboni .

Taarifa hiyo imeeleza kuwa majaribio hayo ya siku mbili yatatafanyika tarehe 31, Agosti 2010 saa 12 asubuhi katika kambi ya Jeshi Lugalo na kufuatiwa na majaribio mengine yatakayofanyika tarehe 1, Septemba 2010 saa 12 asubuhi Makao makuu ya Jeshi Upanga.

Aidha, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linawafahamisha wananchi kutokuwa na hofu yoyote ya mlio wa ving’ora hivyo wakati wa majaribio kufuatia kuwa salama na kulizwa kwa malengo maalum

Friday, August 27, 2010

TAMASHA LA WATOTO YATIMA KUFANYIKA LEADERS IDDI PILI.


Mkurugenzi wa PSET, Osman Kazi akizungumzia bonanza ambalo amaenadaa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya watoto yatima siku ya Idd pili katika viwanja vya leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wataandaliwa michezo na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula na vinywaji.Kushoto kwake ni Bi Mwanaisha Magambo wa New Life Orphanage. Kulia ni Mwakilishi wa Royal Palm Seraphin Lusala.

Kazi ameomba wadau wenye moyo mwema na walio na haja ya kuchangia watoto hao wajitolee kwa vitu mbalimbali vinavyoweza kufanikisha siku hiyo ikiwa ni pamoja na uandaaji ambako vinahitajika vyakula, vinywaji vitamu, vifaa vya michezo na hata fedha ili kufanikisha.

Kikubwa ni watu kujitokeza na kujumuika na watoto hao pamoja na familia zao katika siku ya tukio ili kuifanya iwe ya mafanikio zaidi. Hotel Movenpick Royal Palm imejitolea ukumbi wa mikutano na vinywaji kwa jili ya maandalizi.

WASIOSAJILIWA MARUFUKU KUFANYA SHUGHULI ZA SANAA NCHINI.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


USHIRIKI WA WASANII WASIOSAJILIWA KWENYE TUNZO NA MATUKIO YA SANAA NCHINI

Baada ya BASATA kusimamia na kuratibu uanzishwaji wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini ambayo ni Shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu), Shirikisho la Muziki Tanzania, Shirikisho la Sanaa za Maonyesho na Shirikisho la Sanaa za Ufundi kwa lengo la kuvipa nguvu vyama vya wasanii na kuvipa umoja kitaifa,Baraza linapeleka nguvu kwenye urasimishaji wa sekta ya sanaa ikiwa ni pamoja na wadau wote wanaojihusisha na sekta hiyo hususan wasanii.

Kwa mujibu wa Sheria na. 23 ya Bunge ya mwaka 1984, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepewa jukumu la kutambua na kusajili wadau wa Sanaa, kumbi zote za burudani Tanzania Bara na wasanii wote ikiwa ni pamoja na kutoa vibali vya kufanya shughuli za Sanaa.

Lengo ni kuzifanya shughuli za sanaa kufanyika katika mazingira rasmi na ya kufuata sheria za nchi pia kuwatambua wasanii wote nchini kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi yetu.Ikumbukwe kwamba, kufanya shughuli za sanaa bila kusajiliwa na kupewa kibali na BASATA ni kuvunja sheria za nchi na hivyo kustahili adhabu.

Faida za kurasimisha sekta ya sanaa hususan kwa wasanii

1. Kuendesha shughuli za sanaa kwa mujibu wa Sheria za nchi ili kuepuka usumbufu.

2. Kutambulika kwa shughuli ya msanii binafsi, kikundi, Chama nk. hivyo kufanya kazi kihalali.

3. BASATA kama shahidi wa Jamhuri hutoa utambulisho/uthibitisho kwa msanii, kikundi au chama halali mahali popote panapohitajika kwa mfano wakati wa kufungua akaunti benki, kupata VISA, pasi ya kusafiria, mikopo kwenye asasi za fedha, msaada au ushahidi mahakamani.

4. Ikihitajika kuweka ulinzi wa kisheria wa kazi za sanaa,kwa mfano wa Hakimiliki na Hakishiriki.

5. Kuingilia kati pale makubaliano/mikataba ya msanii, kikundi, chama nk. inapokiukwa na kuripotiwa katika Baraza.

6. Kushauri na kutoa mafunzo ya sanaa.

7. Kutafutiwa masoko na/au kuunganishwa na masoko, wasanii na fursa mbalimbali zinapojitokeza.

BASATA linawaagiza waandaaji wa matukio ya sanaa nchini (Tunzo za Sanaa/matamasha/maonyesho) kuhakikisha wanafanya kazi na wasanii waliosajiliwa tu na inapotokea kufanya vinginevyo basi muandaaji wa tukio husika na msanii atawajibika moja kwa moja.

BASATA linatoa hadi tarehe 31 Oktoba, 2010 kwa wasanii na wadau wote nchini kujisajili vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwazuia wasanii pia wadau wasiosajiliwa kushiriki tunzo/matamasha/Matukio ya Sanaa.

Ghonche MateregoKATIBU MTENDAJI, BASATA.

MCHANGO KWA AJILI YA UJENZI WA MSIKITI

Bismillahir Rahmanir Rrahim

Amesema Allah S.W: Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni kama mfano wa punje moja iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke pana punje mia. Na allah humzidishia amtakaye (zaidi kuliko hivi) na Allah ni mwenye wasaa mkubwa (na) mwenye kujua. Suratil Baqarah (2:261)

Uongozi wa masjid munawar Jang'ombe kwa Maharuki - Zanzibar, unawatangazia waislamu wote bara na visiwani kuchangia katika upanuzi wa msikiti kwa kuwasilisha michango yao moja kwa moja msikitini au kupitia benki ya watu wa Zanzibar A/C 0212 0602 8457
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na uongozi kwa namba 0777 450 140/238 927

Wasalaam.

MISS TZ 2009 MIRIAM GERALD ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WAATHIRIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI

VODACOM MISS TANZANIA 2009, MIRIAM GERALD AKIMKABIDHI MSAADA WA VYAKULA NA FEDHA KATIBU MKUU WA KITUO CHA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI CHA TUMAINI KILICHOPO ARUSHA, RICHARD LAIZER IKIWA NI MAADHIMISHO YAKE YA SIKU YA KUZALIWA ALIYOFANYIKA JANA. KWA NIABA YA WATOTO WANAOSOMA KATIKA KITUO HICHO NI MTOTO SWEETMERCY EMMANUEL ALIYEPOKEA KWA NIABA YA WENZAKE.

CHEKI VIDEO MPYA YA FA NA AY FT HARDMAD - NAMBA 1.

WASHIRIKI WA VODACOM MISS TANZANIA WAKIWA MONDULI MKOANI MANYARA.

Paulina Lowasa dada wa Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowasa, akiwapa mkono wa kuwatakia heri Warembo wa Vodacom Miss Tanzania alipokutana nao Wilayani Monduli mkoni Arusha jana na kuwapa zawadi ya vikoi vya kimaasai warembo wote 30. Warembo hao wanatembelea Kanda ya Kaskazini kuangalia vivutio vya Utalii nchini.

  
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wasichana Maasai iliyopo Monduli Mkoani Arusha wakati wa rembo hao walipotembelea shule hiyo jana wakiwa katika ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.

  
Mkurugenzi wa Lino Interanational Agency, Waandaaji wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Hashim Lundenga akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya wasicahana Maasai ya Mkoani Arusha jana wakati warembo wa Vodacom Miss Tanzania walipoitembelea shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi.

  
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimkabidhi chandarua Mria Charles, mmoja wa wagonjwa katika Hospitali ya Mto wa Mbu Mkoani Manyara jana wakati warembo hao walipombatana na Balozi wa Kampeni ya Malaria Haikubaliki Mwasiti Almas (watatu kulia). Warembo wa Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.

 
Mshiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010,akigawa chandarua kwa mmoja wa wakazi wa Mto wa Mbu Mkoani Manyara jana katika utekelezaji wa Kapeni ya malaria. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutuio vya Utalii na kuhamasisha Utalii wa Ndani Nchini.

FRANCIS CHEKA KUCHEZA FILAMU YA HISTORIA YA MAISHA YAKE!!


 BINGWA wa masumbwi Tanzania Francis Cheka anatalajia kuonekana duniani kote kupitia filamu maalum itakayohusu historia ya maisha yake tokea utoto mpaka mafanikio katika mchezo huo hapa nchini

.
Akiongea na waandishi wa habara jijini Dar es Salaam, mtayalishaji wa filamu hiyo hapa nchini kupitia kampuni ya Real Peoples Enterprises (RPE) Amon Ntevi alisema kampuni yake ipo katika hatua ya mwisho kupiga picha maeneo mbalimbali ikiwa ni sambamba na kuingiza matukio aliyofanya ndani nje ya Tanzania kwenye masumbwi.
“Filamu hii itakua ya pekee na ya kwanza kutengenezwa kwa hapa nchini ambapo itaonyesha uhalisia wa bondia Cheka tokea alipokua kijana mdogo na maisha aliyopitia hadi mafanikio katika mchezoo wa ngumi hapa nchini’ alisema Amon.
Pia alisema kuwa watanzania na washabiki wake duniani kote watapata kumjua kwa undani kupitia filamu hiyo itakayojaa simulizi na vitendo kutoka kwa Cheka mwenyewe.
“Wengi wanamuona Cheka kama bondia lakini hawajamjua kwa undani zaidi hivyo kupitia filamu hiyo wataweza kumjua kwa undani ni pamoja na kuingiza matukio ambayo washabiki hawakuwai kuyaona.
Kampuni ya RPE, inayojishuhurisha na matangazo, uchapishaji na utengenezaji wa ‘video documentary’ mbalimbali, kwa filamu hiyo itakuwa ni ya kipekee hapa nchini na watu watafurahia.
Aidha, alisema kuwa filamu hiyo inatalajiwa kuzinduliwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro siku ya Idd Pili ambapo Cheka atakua na pambano kali dhidi ya bondia wa Uganda Sebyala Med.

HAPPY B'DAY MWAMBA WA KASKAZINI.

Hongera kaka kwa kutimiza miaka kadhaa na leo ikwa ndio siku na tarehe yako ya kuzaliwa.
Wtu wako na wadau wote wa burudani wanakutakia HAPPY B'DAY na pia wanakutakia maisha marefu yenye mafanikio ili uendelee kuwapa burudani

Wednesday, August 25, 2010

ANGALIA PICHA ZA SHOW YA BENJAMIN WA MAMBO JAMBO NCHI FINLAND NA ETHIOPIA.

Hapa Benja alikuwa akisikilizia nyuma ya steji kabla hajapanda jukwaani.

Hapa bana kazi ikaanza akiwa na madansa wake ambao ni kutoka kundi la sanaa za asili la Sanaa sana
Mpango mzima uliendelea mpaka hapo akawa anawauliza wapiga vyombo vipi tuendelee au mmechoka?!


HII NI NYINGINE TENA  CHINI ETHIOPIA

Hapa anasema na mashabiki
Hapa mshkaji anakamua kinoma
Chki mchizi alivyokuwa na  mzuka

Monday, August 23, 2010

MAMBO YA KCB HAYA!

Mwenyekiti wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa akimkabidhi zawadi ya begi Mwanaidi Ibrahim ambaye alikuwa mmoja wa washindi wa michuano ya wazi ya gofu iliyodhaminiwa na benki hiyo katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana. Nyuma ni kepteni wa mchezo huo Joseph Tango. (Mpiga picha Wetu).
Mwenyekiti wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa (Katikati) akimkabidhi Zainab Ibrahim zawadi fimbo ya mchezo wa gofu baada ya kuwa mshindi wa michuano ya wazi ya mchezo huo kwa upande wa wanawake iliyodhaminiwa na benki katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Gofu nchini (TGU) Dioniz Malinzi (Mpiga picha Wetu).
Mwenyekiti wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya wazi ya gofu yaliyodhaminiwa na benki hiyo.
Vikombe na baadhi zawadi za washindi wa mchezo wa gofu
Mchezaji wa Gofu ambaye pia ni mwanachama wa Dar es Salaam Club, Tayana William, akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya wazi ya mchezo huo yaliyodhaminiwa na Benki ya KCB na kufanyika katika viwanja vya Gymkhana.
Christina Manyenye Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Jamii KCB kulia pamoja na wafanyakazi wenzie.


Saturday, August 21, 2010

WASANII BADO WANAENDELEA KULIZWA TU!

Hapa wasanii wakiwa kwenye gari wakielekea huko kijijini

Sasa ndio wamefika kijijini na kuanza kutafuta wahusika

Baada ya kila kitu wasanii wakaamua kupata picha ya pamoja na baadha ya wanakijiji

Tamko la Serikali ya Mkoa wa Pwani kwamba, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliouziwa mashamba katika Kijiji cha Manzenga, Kata ya Visegese Wilayani Mkuranga, wametapeliwa, limewatoa machozi baadhi ya mastaa ambao ni miongoni mwa waathirika, Risasi Jumamosi linashuka nayo.

Mpango mzima wa ishu hiyo tangu mwanzo uko hivi, wengi wa mastaa baada ya kupata taarifa hizo waliangua vilio huku wengine wakishindwa kujua la kufanya.

Awali, ilitolewa taarifa na uongozi wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (Shiwata) juu ya kuwepo kwa mpango wa kuanzisha kijiji ambacho wataishi mastaa katika huku ikielezwa kuwa, walengwa ni wasanii, waandishi wa habari, wachezaji na wengineo.

Taarifa hiyo alieleza kwamba, kwa mtu ambaye angehitaji kuwa sehemu ya mpango huo alitakiwa kufika katika ofisi za shirikisho hilo akiwa na picha mbili za pasipoti, shilingi 25,000 kwa ajili ya ada ya kujiunga na shirikisho, 500 ya kitambulisho na 10,000 kwa ajili ya gharama ya kupatiwa eneo.

Aidha, baada ya wanachama hao kutoa kiasi hicho cha shilingi 35,500 ilidaiwa kuwa, baadaye walitakiwa tena kutoa shilingi 6,000 ufafanuzi ukiwa ni kwamba, shilingi 4,000 kwa ajili ya gharama ya kupimiwa kiwanja na shilingi 2,000 nauli ya kwenda eneo la tukio.
“Tulipokamilisha taratibu zote na kupewa risiti za malipo, tulichukuliwa, tukapiga vishoka kwenye magari na kuelekea Visegese, tulipofika huko tukaoneshwa maeneo yetu na kurejea Dar tukiwa na matumaini ya kwamba tumepata,” alisema mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Hata hivyo, baada ya zoezi la awamu hiyo lililofanyika miezi kadhaa iliyopita, hivi karibuni tangazo hilo tena lilitolewa kwa watu mbalimbali wakiweno mastaa ambapo taratibu zilikuwa kama za mwanzo, tofauti ikiwa kiasi cha pesa walichotakiwa kutoa kwani wao walitakiwa kutoa shilingi 53,500.

Ikaelezwa kuwa, baada ya kukamilika kwa taratibu zote, Jumamosi iliyopita kundi la watu wakiwa katika magari kibao walianza safari kuelekea eneo la Visegese tayari kwa kugaiwa viwanja hivyo.

miongoni mwa wasanii waliokuwa katika msafara huo ni pamoja na Besta Prosper, Laurence Marima ‘Marlaw’, Estelina Peter Sanga ‘Linah’, Rashidi Makwilo ‘Chid Benz’, Stara Thomas, Nasib Abdul ‘Diamond’, Mwasiti Almasi, Ali Salehe Kiba ‘Ali Kiba’, Ambwene Yesaya ‘A.Y, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Jacqueline Wolper, Khadija Shabani ‘Keisha’, Hafsa Kazinja na wengineo.
Pia ilidaiwa kuwa, walikuwepo pia watangazaji maarufu wa vituo mbalimbali vya Televisheni na Radio kama vile Abdallah Mwaipaya, Milard Ayo na Godwin Gondwe (ITV), Salma Msangi (Channel 10), Anold Kayanda, Adam Mchomvu, Dina Marious, Gea Habib (Clouds), Khadja Shaibu ‘Dida’ (Times) na wengineo.
Hata hivyo, baada ya mastaa hao pamoja na watu wengine kukabidhiwa maeneo yao na kapakia ndinga kurejea Dar, siku nne baadaye uongozi wa Wilaya ya Mkuranga ulitoa tamko lililowafanya mastaa hao kupigwa na butwaa.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Henry Clemence alisema kuwa, wote waliogaiwa viwanja katika eneo hilo wametapeliwa kwani Mwenyekiti wa kijiji hicho aliliruhusu SHIWATA kumiliki maeneo hayo kinyume na taratibu.

Alisema kuwa, alishangaa mwishoni mwa wiki iliyopita kuona watu wapatao 1,000 kutoka Dar wakifika katika kijiji hicho wakiwa na magari mengi wakidai wameletwa na taasisi hiyo kukabidhiwa mashamba ambayo wametawafutiwa bila ya Tarafa, Kata na Halmashauri ya wilaya hiyo kujua.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kuwa, watu waliouziwa maeneo hayo hawaruhusiwi kufanya chochote kwakuwa viwanja hivyo vina matatizo ya mipaka kati ya kijiji hicho na cha jirani kiitwacho Msorwa.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Kasim Twalib ‘Ticha’ alithibitisha kuwepo kwa mpango huo na kudai kuwa, hakuna mazingira ya kutapeliwa kwa watu waliuziwa maeneo katika kijiji hicho bali kuna matatizo yaliyojitokeza na kwamba wanajaribu kuyashughulikia.

FA, AY KUWAWRUSHA WAKENYA LEO.

Kkuanzia kushoto ni Mwana FA, projuza Hammy B kutoka B-Hits na AY

Wanamuziki Mwana FA na AY watawarusha mashabiki wao wa nchini kenya leo katika tamasaha la KICC jijini Nairobi. nina imani kuwa watu wangu wa pande za nairobi wamefurahia uwepo wa hawa vijana maana kazi zao kila mmoja anazijua. 

KIKWETE 2010 OFFICIAL SITE.


Ninafuraha kubwa xana kuwafahamisha kuwa Tanzania tumepiga hatua katika mambo ya utandawazi. Habari njema zilizopo kwa asasa hizi:- kwamba tovuti maalumu na rasmi ya Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. M. Gharib Bilal sasa inapatikana kwenye mitandao:


Ukitembelea tovuti hii maalumu ya Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 utapata habari mbalimbali kama vile:

Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.

Mafanikio katika sekta mbalimbali.

• Sera na Malengo 2010 – 2015.

• Ratiba za kampeni.

• Hotuba maalumu.

• Matoleo ya Habari.

• Video na picha.

• Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.

Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.

“ TUKISHIRIKIANA TUTAFIKA MBALI ZAIDI”

Thursday, August 19, 2010

WALIMBWENDE WA VODACOM MISS TANZANIA KUANZA ZIARA LEO

Mkurugenzi wa Miss Tanzania bw. Hashimu lundenga akimtambulisha Mlezi wa kambi mbi ya Vodacom miss TanzaniaMlezi akionge na warembo pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa na kukaribishwa Wanaofuatia katika picha ni Hashim Lundenga Mkurugenzi Miss Tanzania, Bosco Majaliwa Katibu Mkuu Miss Tanzania na Charles Bekon Mkurugenzi wa Giraffe Ocean View Hotel.


warembo wakisikiliza kile wanachoambiwa na mlezi wao huku wakipgwa picha mbili tatu na waandishi pamoja na wapiga pcha.

 

Kaka mkubwa John bukuku kutoka blog ya fullshangwe akipata msosi baada ya kazi nzito ya kuwapiga picha walimbwende. 

Warembo wakipata chakula cha mchana kwa pamoja


Warembo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutoka kwenye utambulisho wa mlezi wao.


Walimbwende wanawania taji la Vodacom Miss Tanzanialeo wamesafiri ka ajili ya kuanza ziara mikoa ya kaskazini ambapo wataweka kambi mjini Moshi na hatimaye Arusha na baadae Tanga.
Hayo yalisemwa na meneja mawasiliano wa vodacom bi Nector Pendaeli Foya jana katika pale Hoteli ya Girafe ambapo ndipo kambi ya miss Tanzania ilipo. “mamiss wetu wataondoka kesho kwenda moshi na arusha ambapo warembo watafanya shughuli za kijamii, na huko watakaa kwa muda wa wiki moja” alisema Nector Foye.

Pia mkurugenzi wa Miss Tanzania bw. Hashimu Lundenga alitumia muda huo kumtambulisha kwa warembo na waandishi wa habari ndg. Emanuel Olemaiko kama ndio atakae kuwa mlezi wa kambi ya Vodacom Miss Tanzania

Akiongea mara baada ya kukaribishwa na kutambulishwa Ndg. Ole Naiko aliwaasa walimbwende hao wapendane na waishi kwa kushikiana wakiwa kambini nahata pale anapotangazw mshindi basi wasio shinda wasikasirike kwa maana katika mashindano ni lazima apatikane mshindi, pia Olemaiko aliishauri kamati ya Miss Tanzania kuendeleza shughuli za kijamii kupitia mshindi wa Miss Tanzania.

Ole Naiko amesema anafurahishwa sana na mkataba uliosainiwa na pande mbili zote Kamati ya Miss Tanzania na warembo washiriki wa shindano hilo na ameongeza kuwa warembo hao watangaze vyema utalii wa Tanzania kwani mrembo wa Vodacom Miss Tanzania ndiyo kioo cha Tanzania katika fani hiyo na kielelezo cha nchi kwa hiyo ni vyema wakawa na tabia njema.


NATURE AWAASA WASNII KUBADILIKA

Juma Kasim Nature

Baba Levo

"Nature" amewataka wanamuziki na wasanii wote nchini Tanzania kujali dhamana yao katika jamii,

Nature amesema "Wasanii na wanamuziki nchini wanayo nafasi kubwa ya kuibadili jamii na kuifanya iwe na maadili mema na kuendeleza utamaduni wake."

"Iwapo wasanii na wanamuziki hapa nchini watakumbuka wajibu wao na kuitekeleza kazi yao, jamii itanufaika,"alisema Nature.

"Ninawakumbusha wasanii na wanamuziki wenzangu hapa nchini kuachana na mazoea, Tuchape kazi kwa mujibu wa kazi yetu ya kuielimisha jamii yetu ya Kitanzania."

Mmoja wa wasanii wa kundi la TMK Wanaume Halisi maarufu kwa jina "Baba Levo" amesema wasanii na wanamuziki wengi wamejisahau kuwa hao ndio kioo cha jamii."
Kutokana na wasanii na wanamuziki kutembea sehemu mbalimbali wanaweza kuwa kiunganishi kizuri cha maendeleo kwa jamii iwapo hawatakuwa na roho za uchoyo.

WADAU WA SEKTA YA HABARI WAKUTANA KUJADILI UCHAGUZI MKUU 2010!!

Wadau wa sekta ya habari nchini wakipiga kura kupitisha baadhi ya maamuzi yatakayozingatiwa na vyombo vya habari kama mwongozo wa maadili kwa vyombo vya habari katika kutoa taarifa za uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini mwezi Octoba 2
Baadhi ya wadau wa sekta ya habari wakichangia masuala mbalimbali kuhusu Mwongozo wa maadili ya vyombo vya habari katika kutoa habari za uchaguzi mkuu wa 2010 leo jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kutoa habari zisizopendelea upande wowote ,zenye ukweli na yenye kujali uchunguzi wa hoja.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO akiongea na wadau wa sekta habari leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa kujadili mwongozo wa maadili ya vyombo vya habari katika kutoa taarifa za uchaguzi mkuu 2010. Pamoja na mambo mengine amewataka kuheshimu Uhuru wa vyombo vya habari uliopo nchini kwa kuepuka kuandika habari za uchochezi na matumizi ya lugha zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

KWA HISANI YA JOHN BUKUKU http://www.fulshangwe.blogspot.com/ 

Wednesday, August 18, 2010

ANGALIA VIDEO YA KAFARA HAPO CHINI.

Miss Vodacom Tanzania kudhaminiwa kwa Bil 1/-
Hapa warembo wakiwasili mjenggoni Hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam

 Mkurugenzi mtendaji wa Hoteli ya Girraf  Charles Bekoni (kushoto) akiwakaribisha walimbwende kambini hotelini hapo, kulia ni  Afisa Udhamini wa Vodacom, Ibrahim Kaude
Baadhi ya washiriki wakiwa katika ukumbi wa mikutono katika hoteli ya Giraf  kwa ajili ya utambulisho na kukaribishwa kambini hapo.

 Walimbwende wote kwenye picha ya pamoja.


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imesema kuwa, mwaka huu itatumia takribani shilingi Bilioni 1/- ili kufanikisha udhamini wa shindano la Miss Vodacom Tanzania kuanzia ngazi ya awali hadi siku ya fainali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kambi ya warembo wa Miss Vodacom Tanzania iliyoanza juzi jijini Dar es Salaam, Afisa Udhamini wa Vodacom, Ibrahim Kaude alisema fedha hizo zitatumika kwa kazi mbalimbali ikiwemo usafiri wa warembo ndani na nje, mavazi siku ya fainali na gharama zingine.

Aidha Kaude aliwataka warembo hao kuzingatia maelekezo ya walimu na masharti ya kambi hiyo ili kulifanya shindano la kumtafuta mlimbwende wa mwaka huu kuwa lenye msisimuko kama yalivyo matarajio ya Vodacom Tanzania.

“Hongereni kwa kufikia katika hatua hii, najua safari imekuwa ndefu tangu ngazi ya vitongoji hadi leo katika kambi ya Miss Vodacom Tanzania. Msikate tamaa kwani mwisho wa siku mmoja kati yenu ndiye atakayeibuka kuwa mlimbwende atakayeliwakilisha taifa kwenye medani za kimataifa,” alisema Kaude.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Giraffe Charles Bekoni alisema wamejiandaa kuwapa huduma bora washiriki hao ili waweze kukamilisha matarajio yao ya kuwa warembo wa kimataifa.

“Katika kipindi chote mtakachokuwepo hapa naamini mtafurahia huduma zetu na mtaondoka mkiwa na historia nzuri juu ya hoteli yetu na yote mliyoyapata,” alisema Bekoni.

Naye matroni wa walimbwende hao Gladys Shao alisema kwa jinsi alivyowaona washiriki inaashiria kwamba shindano la mwaka huu halitabiriki na hivyo kuleta ushindani mkubwa miongoni mwa warembo.

“Kwa mwaka jana tetesi zilienea kuwa Miss Vodacom Tanzania anayemaliza muda wake Miriam Gerald angeweza kuwa mshindi na kweli ilitokea. Lakini kutokana na kufanana kwa vigezo na warembo wenye sifa kwa washiriki wa shindano la 2010/11 ni wazi upinzani utakuwa mkali,” alisema Shao.

Warembo 31 walioanza kambi inayofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe ni Esther Dennis, Gloria Kaale kutoka kanda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shadia Mohamed (Mbeya), Furaha David (Ruvuma), Mary Kagali (Iringa) kanda ya nyanda za juu kusini.

Wengine ni Bahati Chando, Salma Nwakalukwa (Dar City Center) na Consolata Lukosi (Tabata) kanda ya Ilala, Frola Florence, Mary Adam (Morogoro), Angelina Ndege (Lindi) kanda ya Mashariki, Alice Lushiku, Irene Hezron (Dar Indian Ocean) na Amisuu Malik (Sinza) wanaoiwakilisha Kinondoni. Pia wamo Genevieve Emmanuel, Anna Daudi na Britney Urassa (Chang’ombe) kutoka Temeke.

Washiriki kutoka kanda ya Kaskazini ni Glory Mwanga (Arusha), Prinsca Mkonyi (Kilimanjaro) na Jally Murei. Ambapo kutoka kanda ya Chuo Kikuu Huria (OUT) ni Gloria Mosha na Christine Justine.

Kutoka elimu ya juu ni Flora Martin, Pendo Sam (IFM), Rachel Sindbad (UDOM), Fatma Ibrahim (Mara), Buduri Ibrahim, Margareth Godson (Shinyanga) wa kanda ya ziwa na Willemi Etami, Wande Masegese (Dodoma) na Pili Issa wanaoiwakilisha kanda ya Kati.