Saturday, August 21, 2010

WASANII BADO WANAENDELEA KULIZWA TU!

Hapa wasanii wakiwa kwenye gari wakielekea huko kijijini

Sasa ndio wamefika kijijini na kuanza kutafuta wahusika

Baada ya kila kitu wasanii wakaamua kupata picha ya pamoja na baadha ya wanakijiji

Tamko la Serikali ya Mkoa wa Pwani kwamba, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliouziwa mashamba katika Kijiji cha Manzenga, Kata ya Visegese Wilayani Mkuranga, wametapeliwa, limewatoa machozi baadhi ya mastaa ambao ni miongoni mwa waathirika, Risasi Jumamosi linashuka nayo.

Mpango mzima wa ishu hiyo tangu mwanzo uko hivi, wengi wa mastaa baada ya kupata taarifa hizo waliangua vilio huku wengine wakishindwa kujua la kufanya.

Awali, ilitolewa taarifa na uongozi wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (Shiwata) juu ya kuwepo kwa mpango wa kuanzisha kijiji ambacho wataishi mastaa katika huku ikielezwa kuwa, walengwa ni wasanii, waandishi wa habari, wachezaji na wengineo.

Taarifa hiyo alieleza kwamba, kwa mtu ambaye angehitaji kuwa sehemu ya mpango huo alitakiwa kufika katika ofisi za shirikisho hilo akiwa na picha mbili za pasipoti, shilingi 25,000 kwa ajili ya ada ya kujiunga na shirikisho, 500 ya kitambulisho na 10,000 kwa ajili ya gharama ya kupatiwa eneo.

Aidha, baada ya wanachama hao kutoa kiasi hicho cha shilingi 35,500 ilidaiwa kuwa, baadaye walitakiwa tena kutoa shilingi 6,000 ufafanuzi ukiwa ni kwamba, shilingi 4,000 kwa ajili ya gharama ya kupimiwa kiwanja na shilingi 2,000 nauli ya kwenda eneo la tukio.
“Tulipokamilisha taratibu zote na kupewa risiti za malipo, tulichukuliwa, tukapiga vishoka kwenye magari na kuelekea Visegese, tulipofika huko tukaoneshwa maeneo yetu na kurejea Dar tukiwa na matumaini ya kwamba tumepata,” alisema mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Hata hivyo, baada ya zoezi la awamu hiyo lililofanyika miezi kadhaa iliyopita, hivi karibuni tangazo hilo tena lilitolewa kwa watu mbalimbali wakiweno mastaa ambapo taratibu zilikuwa kama za mwanzo, tofauti ikiwa kiasi cha pesa walichotakiwa kutoa kwani wao walitakiwa kutoa shilingi 53,500.

Ikaelezwa kuwa, baada ya kukamilika kwa taratibu zote, Jumamosi iliyopita kundi la watu wakiwa katika magari kibao walianza safari kuelekea eneo la Visegese tayari kwa kugaiwa viwanja hivyo.

miongoni mwa wasanii waliokuwa katika msafara huo ni pamoja na Besta Prosper, Laurence Marima ‘Marlaw’, Estelina Peter Sanga ‘Linah’, Rashidi Makwilo ‘Chid Benz’, Stara Thomas, Nasib Abdul ‘Diamond’, Mwasiti Almasi, Ali Salehe Kiba ‘Ali Kiba’, Ambwene Yesaya ‘A.Y, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Jacqueline Wolper, Khadija Shabani ‘Keisha’, Hafsa Kazinja na wengineo.
Pia ilidaiwa kuwa, walikuwepo pia watangazaji maarufu wa vituo mbalimbali vya Televisheni na Radio kama vile Abdallah Mwaipaya, Milard Ayo na Godwin Gondwe (ITV), Salma Msangi (Channel 10), Anold Kayanda, Adam Mchomvu, Dina Marious, Gea Habib (Clouds), Khadja Shaibu ‘Dida’ (Times) na wengineo.
Hata hivyo, baada ya mastaa hao pamoja na watu wengine kukabidhiwa maeneo yao na kapakia ndinga kurejea Dar, siku nne baadaye uongozi wa Wilaya ya Mkuranga ulitoa tamko lililowafanya mastaa hao kupigwa na butwaa.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Henry Clemence alisema kuwa, wote waliogaiwa viwanja katika eneo hilo wametapeliwa kwani Mwenyekiti wa kijiji hicho aliliruhusu SHIWATA kumiliki maeneo hayo kinyume na taratibu.

Alisema kuwa, alishangaa mwishoni mwa wiki iliyopita kuona watu wapatao 1,000 kutoka Dar wakifika katika kijiji hicho wakiwa na magari mengi wakidai wameletwa na taasisi hiyo kukabidhiwa mashamba ambayo wametawafutiwa bila ya Tarafa, Kata na Halmashauri ya wilaya hiyo kujua.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema kuwa, watu waliouziwa maeneo hayo hawaruhusiwi kufanya chochote kwakuwa viwanja hivyo vina matatizo ya mipaka kati ya kijiji hicho na cha jirani kiitwacho Msorwa.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Kasim Twalib ‘Ticha’ alithibitisha kuwepo kwa mpango huo na kudai kuwa, hakuna mazingira ya kutapeliwa kwa watu waliuziwa maeneo katika kijiji hicho bali kuna matatizo yaliyojitokeza na kwamba wanajaribu kuyashughulikia.

No comments:

Post a Comment