Tuesday, October 30, 2012

WASANII WA ARUSHA WALIA NA SERIKALI

http://pamelamollel.files.wordpress.com/2012/10/dscf2217.jpg 
Meya wa manispaa ya Arusha (kushoto) akizungumza na baadhi ya wasanii wa jijini Arusha.
http://pamelamollel.files.wordpress.com/2012/10/dscf2218.jpg
Nakaaya Sumari (katikati) na wasanii wenzake wakiwa wanamsikiliza Meya wa jiji

 N a Mwandishi Wetu
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya na vikundi mbalimbali vya maigizo mkoani Arusha wamewataka  viongozi wa serikali kutowadharau na kuwashirikisha kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo jijini hapa
Hali hiyo imetokea wakati zikiwa zimebaki siku chache ili kufanyika uzinduzi rasmi wa Jiji la Arusha baada ya wasanii hao kudai kutoshirikishwa kwa lolote.
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake msanii wa muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari alisema kuwa wameshangaa sana kusikia kuwa msanii kutoka dar es salaam Diamond Platnum atakuja kutumbuiza  ilihali wao wapo na hawana taarifa yeyote.
Nakaaya alisema kuwa hawana tatizo na Nasibu Abdul (Diamond) ambaye amealikwa kuja kusherehesha uzinduzi huo ila walichokiona ni dharau kutoka kwa afisa Utamaduni wa manispaa kwa kutoonyesha ushirikiano na  badala yake wamepewa taarifa ya kufanya kitu juuya uzinduzi huo kama zima moto jana usiku baada ya wao kuulizia.
“Tumeshanga sana hii ni dharau wasanii wa arusha hatuheshimiki kabisa na tumeuliza ndo tunaambiwa eti tuandae kitu kwa ajili ya uzinduzi dah yani inakatisha tamaa sana alafu afisa utamaduni mwenyewe anatuona anatupotezea” alisema nakaaya.
 Hata hivyo Nakaaya alimpongeza  Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo kwa kutoa ushirikiano wake kwao na kuahidi kushirikiana nao kwa madai ya kilichofanyika ni makosa ya kibinadamu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wasanii mkoa wa arusha Hussein Sechonge alikemea vikali tabia hiyo kwa kuwa wasanii wana mchango mkubwa wa kufikisha ujumbe na kuwataka viongozi kuwa wazalendo.
Aidha walimtaka afisa utamadumi manispaa  Juma Sule kutoa ushirikiano kwa wasanii wa hapa kwa kuwa wao ndio wanajua kila kitu kuhusu manispaa na sio Diamond.
"tunamshangaa sana hapa kuna wasanii 70 sasa nashangaa kwenye mwenge aliletwa Juma Nature wakati wao wapo hapa na hawafahaamu kitu chochote sio vizuri” alisema Sechonge.
Hadi mida waandishi wanondoka eneo la tukio (ofisi za manispaa)  wasanii hao walikuwa  nje ya ofisi ya meya wakisubiri kujadiliana namna ya kufanya na kumaliza tofauti hiyo.

Monday, October 29, 2012

HUYU NDIYE FLORA MVUNGI WA H-BABA

H-Baba nasema anafurahia kuwa na mke kama FLORA MVUNGI niyo maana kaamua kumvisha Pete ya UCHUMBA.

HIVI NDIVYO MCHEZAJI WA COASTAL UNION, NSA JOB ALIVYO UMIA JANA KATIKA MECHI YAO NA JKT RUVU

Hapa ndio alipogongana na kipa wa JKT Ruvu
Hapa akitolewa nje ya Uwanja
Baadhi ya madaktari wa Timu wakimnyoosha mguu uliteguka
Akipelekwa kwenye gari kwa ajili ya kwenda hospitali
Hapa akiwa wodini baada ya kufikishwa hospitali

Picha zote kwa Hisahni ya gazeti la MWANANCHI

Friday, October 26, 2012

MBABE WA RAJABU MAOJA KUTETEA MKANDA WAKE DECEMBA 1.

Ndoshoko kulia akimsulubu mpinzanai wake
Helen Joseph

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 26, OCTOBA, 2012
Bondia kutoka nchini Namibia Gottlieb Ndokosho ambaye alimsambaratisha Mtanzania Rajabu Maoja katika raundi ya kwanza ya mpambano wao wa kugombea mkanda wa IBF Afrika katika uzito wa unyoya, atapanda tena ulingoni jijini Windhoek, Namibia kutetea mkanda wake kati ya mabondia watatu ambao walipendekezwa na IBF.
Mpambano huo utakaofanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia utatoa upinzani mkali sana kati ya mabondia hao wanaochipukia vyema.
Kati ya majina matatu yaliyopendekezwa na IBF limo jina moja na Mtanzania Fredy Sayuni ambaye anaishi jijini Dar-Es-Salaam. Wengine ni Patric Okine kutoka Ghana na David Kiilu kutoka nchini Kenya.
Wakati huo huo IBF imetoa kibali kwa bondia Helene Joseph wa Nigeria kutoka barani Afrika kupigania ubingwa wake wa dunia. Mpambano huo utawakutanisha Helen Joseph kutoka nchi ya Nigeria akikutana na bondia Dahianna Santana kutoka Dominican Republic huko Latin America ambaye ndiye bingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa unyoya (featherweight) kwa upande wa wanawake.
Mpambano huo utafanyika Decemba 1 katika jiji la San Domingo na litasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi.
Bondia Helen Joseph ameshapigana mapambano 13 na amepoteza mara mona wakati mpinzani wake Dahianna Santana amepigana mara 37 na kupoteza mara 6.

Imetolewa na:
*Uongozi*
*IBF Africa, Masharikim ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi*
*Dar-Es-Salaam*

Thursday, October 25, 2012

MDAU JACKLINE KATIKA POZI TOFAUTITOFAUTI AKISHOO LAV.

ALBAMU YA KINA KIREFU YA MANSU-LII, SASA IPO MTAANI

Mtu mzima  MANSU-LII akionyesha muonekano mzima kava la albamu yake ya KINA KIREFU. Albamu hii sasa ipo sokoni na inapatikana kwa Shilingi 3000/= za kitanzania.
Kwa yeyote anayehitaji apige +255 784 351 667, au +255 714 884 342.

TANZIA

FAMILIA YA  MAREHEMU MCHUNGAJI MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MZEE NSUBISI SAMUEL MWAKIPUNDA (MKURUGENZI WA ZAMANI WA IDARA YA MAELEZO)  KILICHOTOKEA SIKU YA JUMATANO TAREHE 24/10/2012.
MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU PUGU KINYEMWEZI DAR ES SALAAM.
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.
KWA MAWASILIANO ZAIDI
+255655994499
“BWANA AMETOA BWANA, AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE” 
AMENWednesday, October 17, 2012

BONDIA 'KING CLASS MAWE' AJIANDAA KUMKABILI SAIDI MUNDI WA TANGA

Bondia King Class

Kocha Super D (mbele)

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' mwishoni mwa wiki hii anaingia Kambini kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake mwingine baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kumtwanga bondia Jonas Segu wa Dar es salaam
King Class Mawe ataanza mazoezi mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kumkabiri bondia kutoka Tanga Saidi Mundi mpambano utakaofanyika 9 Desemba katika ukumbi wa PTA Sabasaba
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema anamuandaa King Class Mawe kwa ajili ya mpambano wake huo kwa kuwa yeye ni mtu wa ushindi kila wakati
Super D alisema bondia wake ataanza mazoezi kwa kuwa mpambano huo ni muhimu kwake kwani kwa sasa ndio kwanza anaonekana katika mapambano makubwa makubwa bondia huyo aliyewai kuwatwanga mabondia wakongwe nchini akiwemo Sako Mwaisege,Jonas Segu aliyemfulumushia kichapo cha paka mwizi na kukubalika kwa mashabiki
Amewaomba wadau mbalimbali kumpa sapoti na kamwe ato waangusha kwa kuwa yeye bila mashabiki na wadau awezi kuwa King amewataka wadau kuendelea kumpa ushirikiano walioutoa wakati wa mpambano wake wa mwisho ili aweze kufika mbali katika anga za masumbwi Duniani
Bondia huyo mwenye kuwa na rekodi ya kupiga wapinzani wake kwa K,O amesema mabondia wa Tanga anawaheshimu sana lakini kwa Said Mundi anataka kutoa mfano ili aweze kuendeleza kuweka jina lake juu katika anga za kimataifa ya mchezo wa Masumbwi

VIDEO MPYA KUTOKA KWA MABEST Ft JUX- SIRUDI TENA

Tuesday, October 16, 2012

ARUSHA INTERNATIONAL ART AND CULTURE FESTIVAL

Kutoka kushoto ni  Daz Knowledge kutoka S.U.A Arusha, IDEA AFRICA's Augustine (Kastrow) Namfua na Meneja Masoko wa K-Vant Gin  Mr. Goodluck Kway wakati wa walipokuwa wakiongea na waaandishi wa habari katika Hoteli ya   Arusha ' Arusha Hotel' Jana.

ARUSHA INTERNATIONAL ART AND CULTURE FESTIVAL

Kutoka kushoto ni  Daz Knowledge kutoka S.U.A Arusha, IDEA AFRICA's Augustine (Kastrow) Namfua na Meneja Masoko wa K-Vant Gin  Mr. Goodluck Kway wakati wa walipokuwa wakiongea na waaandishi wa habari katika Hoteli ya   Arusha ' Arusha Hotel' Jana.

Saturday, October 13, 2012

STEPS YATOA MSAADA SHULE YA BUGURUNI VIZIWI


Ofisa wa Kampuni ya Steps Entatainmenti, wasambazaji wa kazi za wasanii. Mbasha Mkilanya 'kulia' akigawa sehemu ya vyakula vilivyotolewa na Kampuni ya Steps kwa ajili ya watoto wa shule ya Buguruni Viziwi  Malapa Dar es salaam Kampuni hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika shule hiyo kwa ajili ya kuwa karibu na jamii inayowazunguka.
Ofisa wa Kampuni ya Steps Entatainmenti, wasambazaji wa kazi za wasanii. Mbasha Mkilanya 'kulia' akigawa sehemu ya vyakula vilivyotolewa na Kampuni ya Steps kwa ajili ya watoto wa shule ya Buguruni Viziwi Dar es salaam jana

Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Steps wakiwa pamoja na wanafunzi wa Buguruni Viziwi Malapa Dar es salaam jana.
Picha zote na www.burudan.blogspot.com

Friday, October 12, 2012

SUA EVENT EPISODE 9 (UJAMAA) SEASON 1


##########BACK TO THE SUA############

SUA EPISODE 9 SEASON 1

Episode inaitwa UJAMAA

Kama kawaida kwenye Utamaduni wetu wa HIPHOP
hakuna kiingilio.

Maalim Nash atakuwepo kuhamasisha Matumizi ya Kiswahili
katika uandishi...

Michoro,Mitindo Huru,Dj na MC...

STRICTLY HIP HOP.

TUKUTANE JUMAPILI PALEPALE MWISHO WA DALADALA
KIJENGE YA JUU.


###teamSUA###

Thursday, October 11, 2012

KANYE WEST AONGOZA KWA KUNYAKUA TUZO NYINGI BET 2012

Kanye West

Mtu mzima KanyeWest pamoja na kutokuwepo katika Usiku wa Tuzo za BET za Hip Pop 2012 lakini ndio msanii Rapa aliyeongoza kwa kuchukua tuzo nyingi kuliko wasanii wote katika Tuzo za BET zijulikanazo kama 'BET Hip Pop Awards 2012', Kanye amejinyakulia tuzo 7 ikiwapo Tuzo ya produza bora,  Mtu zima Kanye alichaguliwa kuwania tuzo 17 mwaka huu na yeye ndiye aliyeongoza kuwepo kwenye vipengele vingi mwaka huu '2012'.
List kamili ya Tuzo zilitolewa kama ifuatavyo;

1. Wimbo wa mwaka ni Ni-as in Paris wa Kanye West&Jay Z.
2.Video Director wa mwaka ni Hype Williams
3. Wimbo bora wa Kushirikiana yaani best Colabo ni Mercy wa Kanye West ft Big Sean, Pusha T na 2 Chainz.
4. Muandishi bora ni Kendrick Lamar
5. Tuzo nyingine ni Sweet 16:Best featurer Verse imekwenda kwa 2Chainz kupitia wimbo wa Mercy
6. Producer wa mwaka ni Kanye West
7. MVP yaani Most Voted Playlist, msanii ambaye ngoma zake zinapigwa sana kwenye redio na Televisheni ni Rick Ross
8. Tuzo ya Msanii mpya wa mwaka/Rookie of the year imekwenda kwa 2 Chainz
9. Msanii mwenye swag au staili bora ya Hip pop ni Kanye West
10. Impact Track yaani ngoma yenye mguso ni ngoma ya Daughters ya Nas
11. Msanii anayejituma kufanya kazi yaani Hustler of the year ni Jay Z.
12. CD ya mwaka imekwenda Jay Z na Kanye West 'The Throne'
12. Kanda Mseto ya mwaka yaani Mixtape Bora amechukua Meek Mill, 'Dreamchasers'
13. Best Live Perfomer ni The Throne, Kanye West na Jay Z.
14. Video Bora ya Hip Pop kachukua Drake , 'HYFR' aliyomshirikisha Lil Wayne
15. Ngoma inabang club sana ni Ni-as in Paris ya Kanye West na Jay Z
16. Dj bora wa mwaka ni Dj Khaled

MH. EDWARD LOWASSA AKUTANA NA A WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA 2012

 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimia na Msimamizi (Matron) wa warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012,Irene Karugaba wakati Warembo hao walipotembelea Nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Monduli ili Kupata Baraka zake.Mh. Lowassa aliwapokea warembo hao kwa furaha na kuzungumza nao machache juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 waliofika nyumbani kwake Monduli leo na kupata wasaa kwa kuzungumza nae mambo mawili matatu juu ya mafanikio ya Mashindano hayo na Maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa kenye picha ya pamoja na Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2012 pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania.
Picha Zote kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited

Monday, October 8, 2012

SERIKALI YASEMA SANAA SASA NI AJIRA RASMI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego akizungumza jambo wakati akifunga jukwaa la sanaa, Kushoto kwakwe ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kazi na Ajira ,  Haji Janabi.
********************************

Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema inatambua kwamba Sanaa ni ajira rasmi licha ya kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuratibu, uongozi na kupewa kipaumbele katika mipango ya kimaendeleo na Serikali.
Akiwasilisha mada ya Umuhimu wa Tasnia ya Sanaa katika kukuza Ajira nchini, katika Jukwaa la Sanaa, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kazi na Ajira,  bwana Haji Janabi amesema sanaa ina mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza upatikanaji wa nafasi za ajira na kipato.
“Kwa Tanzania iwapo tutatumia vyema uwepo wa ubunifu muafaka katika sekta ya sanaa zetu bila shaka tasnia  hii inaweza kuchangia sana upatikanaji wa nafasi za ajira na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuondoa tatizo la ajira hapa nchini,” alisema Janabi.
Janabi amesema kwamba pamoja na hivyo kuna changamoyo kubwa ya kiuratibu na kimuundo ikiwa ni pamoja na Serikali kutotoa kipaumbe katika masuala yanayohusu sanaa na wasanii pamoja na mgongano wa kimamlaka kati ya vyombo vinavyohusika na uratibu wa masuala ya sanaa.
Aidha amesema pamoja na nafasi nzuri ya kukuza ajira, ujio wa teknolojia umeanza kubana soko la ajira ya sanaa ambapo kwa sasa teknolojia inapunguza uhitaji wa watu katika ufanyikaji wa sanaa kwa akitolea mfano katika muziki ambapo vitu vingi vinafanywa na mtu mmoja hivyo kupunguza nafasi za watu wengine.
Pia amesema ili sekata hii iweze kuwa ajira nzuri zaidi ni muhimu kukaandaliwa viwango na vigezo kama ilivyo kwa fani zingine  ili kuwe na maradaja ya wafanyaji kazi kulingana na viwango vya umahiri na taaluma.

MPAMBANO MASUMBWI UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Friday, October 5, 2012

MDAU ANDREW CHALE KUSHEREHEAKEASIKU YAKE KWA STAILI YA PEKEE

Habari marafiki, Katika kuelekea siku yangu ya kuzaliwa, yaani October 21, natarajia kufanya yafuatayo.
(1)    October 6,nitatembelea moja ya kituo cha kulelea watoto na  kuwafariji.
(2)    October 7,nitatembelea  kambi ya wazee huko Kigamboni na kuwafariji
(3)    Otober 13,nitapata wasaha wa kukaa na watoto wa mtaani wa maeneo mbalimbali waliopo katikati ya jiji, hii ikiwemo kuwa nao kwa muda wa siku nzima, ikiwemo maeneo ya Posta,Kariakoo, gerezani,Jangwani na ferri (Hii ni kwa maeneo yote wanapopatikana waoto hawa.
(4)    October 14, nitakuwa kwenye fukwe za Kigamboni, na marafiki ambapo pia watakaojumuika siku hiyo watapata kufundishwa namna ya kuogelea kwenye maji, sambamba na kujiokoa endapo itatokea matatizo.
(5)    October October 20,nitatembelea Ocean Road kwenye wodi ya watoto na baadae nitaelekea Muhimbili kwenye wodi ya watoto na wamama wamama.
…October 21 nitaelekea kanisani na baada ya hapo ni kufurahia kwa pamoja na marafiki./
Ukiwa miongoni mwa #TEAM ANDREW CHALE# unakaribishwa sana usisite, kwani Andrew Chale, katika maisha yake hapa duniani anakutegemea wewe na ameishi miaka yote tokea saa 12,jioni, October 21,1985, alipozaliwa pale Muhimbili Hospital, mpaka leo hii amekuwa na kufikia hapa ameishi na wewe.
Kwa pamoja, Andrew Chale ambaye awali aliishi katika maisha ya taabu ikiwemo ya watoto wa Mtaani, na baadae kuachana na maisha hayo (Street children-3yrs) na baadae kuja kuishi na watu baki (2yrs) na maisha ya kujitegemea (7yrs) mpaka sasa muda huu.
Hakika kwa neema zake Muumba sina la kumrudishia zaidi ni asante, kwani licha ya kuwa na shida na taabu kila kukicha najikuta maisha yangu yanaongezeka mbali ya kutokuwa na kazi ambayo nalipwa mshahara, lakini nakula, kunywa,nalala,natembea nacheka na hakika wapo watu hapo hapo ambao wanalipwa mshahara na malupulupu hawaishi kwa raha wanaomba ni bora wafe…kwa mimi nasema ASANTE MUUMBA.
Ili kufanikisha hili ukiwa umeguswa na unahitaji kuungana name kwenye kushiriki ukiungana na na #Andrew Chale team#, unaweza kuwasiliana ama kuwakilisha mchango wako kupitia namba  kwa MP PESA ama TIGO PESA- 0719076376 ama 0767076376.
Pia kama utakuwa na vitu ikiwemo nguo ama vyombo ambavyo huvitumii  unaweza wasiliana nami ilikuweza kuvikusanya na kuwafikishia watoto na watu wasio jiweza.

UNAKARIBISHWA SANA.

KING CLASS MAWE AJIFUA KUMKABILI JONAS SEGU


Kocha wa mchezo wa Ngumi Habibu Kinyogoli kulia akimfua bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake na Jonas Segu October 14 Kati ukumbi wa Fransi Corne Manzese
Kocha wa ngumi wa kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli akimwelekeza jinsi ya kukwepa  bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake na Jonas Segu October 14 Katika ukumbi wa Fransi Corne Manzese
Kocha wa mchezo wa Ngumi Habibu Kinyogoli kulia akimfua bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake na Jonas Segu October 14 Kati ukumbi wa Fransi Corne Manzese 
Kocha wa mchezo wa Ngumi Habibu Kinyogoli kulia akimfua bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake na Jonas Segu October 14 Kati ukumbi wa Fransi Corne Manzese

Tuesday, October 2, 2012

BUSHOKE: NAPENDA KUSHIRIKISHA WASANII WAKALI

Na Elizabeth Edward
MWANAMUZIKI wa bongo fleva, Ruta Bushoke amesema anapenda kuimba na wasanii waliokwishatoka kwa sababu lengo lake kuu ni kutoka zaidi katika tasnia ya muziki.
Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, akiwa Afrika Kusini, Bushoke alisema kuwa wasanii waliokwishatoka wanamsaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kwa urahisi kazi zake za sanaa.
Alisema kuwa alishirikiana na wasanii mbalimbali wa kimataifa akiwemo Juliana Kanyomozi, Ngoni wa Uganda na wengie wengi tu walitoa baadhi ya nyimbo na zilizopendwa na mashabiku huku zikimuweka katika levo nyinginr kimuziki.
Msanii huyo ambaye aliwahi kufanya kazi za sanaa kwa miezi miwili nchini Uganda alisema kuwa ameamua kuweka maskani yake Afrika Kusini kwa kuwa nchi hiyo iko juu kimuziki.
Bushoke kwa sasa anakamilisha albam yake ambayo hata hivyo alikataa kuitaja jina wala atakapoizuindua kwa sababu mbalimbali. "Bado naendelea kuifanyia kazi siwezi kutaja jina wala uzinduzi," alisema.
Habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.