Wednesday, February 27, 2013

NEW HIT FROM KING KAPITA FT GODZILLAH - KUNA TATIZO KWANI?


SAMIR NA PHILIP KOTEY KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA UZITO WA 'MIDDLE'

    Philip Koyey akishushuana makonde na bondia Kelly Brook owa Uingereza

Na Mwandishi Wetu
Nchi ya Ghana iko katika hekaheka na bashasha za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey. Wawili hawa ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na barani Afrika kwa ujumla. Watakutana wakati wanapogombea mkanda wa IBF AMEPG uzito wa middle.
Muziki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye "musiki wa masumbwi" ulingoni wakati kila mmoja wake atakapoonyesha ulimwengu kuwa yeye ndiye bondia maarufu zaidi katika bara la Afrika uzito wa middle.
Pambano hili linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyalula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Mamamu wa rRis wa IBF Africa idara ya fedha.
Hivyo siku ya Machi 30, miamba hii miwili itakutana katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah!   
Nchi ya Ghana imejitokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa ngumi kwa iaka kadhaa na kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kuafuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!

IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE MARCH 2


Bondia Ibrahimu Maokola akifanya mazoezi ya kupiga panch bag wakati wa kujiandaa na mpambano wake na Rajabu Majeshi utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa March 2  Mpambano huo utakua wa utangulizi kabla ya mpambano wa Maneno Osward na Japhert Kaseba.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, February 20, 2013

KAMA ZAMANI YA MWANA FA KUTOKA FEBRUARI 25, 2013Ile track iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki, KAMA ZAMANI kutoka kwa MwanaFA akiwashirikisha wakongwe wa burudani nchini, Kilimanjaro Band (NJENJE) pamoja na Mandojo & Domokaya sasa kutoka Tarehe 25 mwezi huu.
Kwa mujibu wa MwanaFA, alisema track hiyo itapatikana moja kwa moja katika mitandao mikubwa inayouza na kusambaza muziki duniani yaani iTunes, Amazon na Spotify na kuomba fans wake waupate huko.

NGOMA MPYA YA JCB & MOPLUS FT DOMO KAYA - NIENDE WAPI


Monday, February 18, 2013

NGOMA MPYA YA GRACE MATATA Ft OTUCK WILIAM - IMBA NAMI

Grace Matata ft. Otuck Wiliam
Song : Imba Nami
Produced by : Willie HD & Duke Gervalius
Studio: M Lab records.

Friday, February 15, 2013

MSANII GOLDIE AFARIKI


Goldie akiwa na Prezzo - enzi za uhai wake
***************

Mwakilishi wa nigeria katika shindano bba-2012,goldie amefariki masaa machache baada ya kuwasili nchini humo,taharifa zinasema muda mfupi baada ya kutua na ndege nchini nigeria.
Hhali ya msanii goldie ilibadilika ghafla, kufikia kukimbizwa hospitali ambako hakuchukuwa muda, alifariki dunia, usiku wa jana.
Rafiki wa karibu wa goldie, ambaye pia ni msanii kutoka nchini Kenya, CMB-Prezzo alitua mjini lagos-nigeria akitokea kenya, tayari kwa maandalizi ya tv-show ambayo ilikuwa ni project yake Prezzo na marehemu Goldie, inasemekana pia moja kati ya mipango ya marafiki hawa wawili, lilikuwepo swala la ziara ya kutembelea baadhi ya nchi za africa mashariki,i kiwemo tanzania, uganda na kenya, wakati dhumuni lilikuwa ni kuitangaza single mpya ya Goldie iitwayo -Skibobo
Goldie pia amefanya wimbo na msanii kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya 'AY' 

...MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEMA PEPONI-AMEN.

NGOMA MPYA YA SUMA MNAZALET FT DANNY JOE - AHSANTE


Sunday, February 10, 2013

VUMILIA - DUSHE DUSHE

MABONDIA FRANISIC MIYEYUSHO VS SADIK MOMBA KUPAMBANA PASAKA


Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka.

Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishina msuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka, wanashudia katikati ni Promota wa mpambano huo, Kaike Silaju na Makamu wa Rais wa PST, Aga Peter.
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com