Wednesday, February 27, 2013

SAMIR NA PHILIP KOTEY KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA UZITO WA 'MIDDLE'

    Philip Koyey akishushuana makonde na bondia Kelly Brook owa Uingereza

Na Mwandishi Wetu
Nchi ya Ghana iko katika hekaheka na bashasha za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey. Wawili hawa ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na barani Afrika kwa ujumla. Watakutana wakati wanapogombea mkanda wa IBF AMEPG uzito wa middle.
Muziki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye "musiki wa masumbwi" ulingoni wakati kila mmoja wake atakapoonyesha ulimwengu kuwa yeye ndiye bondia maarufu zaidi katika bara la Afrika uzito wa middle.
Pambano hili linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyalula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Mamamu wa rRis wa IBF Africa idara ya fedha.
Hivyo siku ya Machi 30, miamba hii miwili itakutana katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah!   
Nchi ya Ghana imejitokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa ngumi kwa iaka kadhaa na kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kuafuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!

No comments:

Post a Comment