b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, January 31, 2012

AJALI TEGETA YASABABISHA FOLENI.

Nipo mitaa ya tegeta leo........
Kama akwaida ya barabara zetu hazipitishi saa nzima bila kutokea ajali!..........
Hapa ni Tegeta Kibaoni ambapo ajali hii imetokea mida hii ya saatisa na nusu alasiri (15:35)

Monday, January 30, 2012

RITA DOMINIC NDANI YA BIFU ZITO NA STEPANIE OKEREKE

MWIGIZAJI Stephanie anazidi kupata maadui baada ya Rita Dominic kuingia kwenye listi ya watu wanaompinga baada ya kupewa shavu nene katika tasnia ya filamu Nollywood.
Awali Stephanie aliyekua rafiki mkubwa wa Gienevieve Nnaji waliingia katika bifu baada ya Stephanie kupewa shavu hilo na yeye kupigwa chini.
Kisa cha kutokuwa na maelewani kwa wasanii hao ni kitendo cha Stephanie kuteuliwa kuwa kiunganishi kati ya wasanii na rais wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan.
Gienevieve alipinga uteuzi huo akisema hawawezi kufanya kazi na rais halafu mtu wa katikati awe msanii huyo akidai kuwa bado mchanga.
Rita naye ameibuka na kusema kuwa anataka kuonana na rais lakini suala la eti kupitia kwa Okerekea analipinga kwa kuwa msanii huyo ni mdogo sana kwake.
"Stephanie ni nani hapa Nollywood, eti nikitaka kuwasiliana na rais lazima nimuone yeye, huyo aliyemteua hana akili hata kidogo," alisema Rita.

MISS KISWAHILI ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA


MISS Kiswahili Tanzania, Rehema Fabian amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa aina ya pekee ambapo amejumuika na Watoto Yatima wa Kituo cha Kuwama kilichopo Mwenge Jijini Dar es Salaam
Akizungumza na mtandao huu Rehema amesema nimefanya hivi ili kuikumbusha jamii haswa Warembo wenzangu na Mastaa kwa ujumla kuwa kuna wenzetu ambao wanahitaji faraja ya pekee na haswa tunapowashirikisha furaha zetu kama hiviWatu wengi wanapokuwa na furaha binafsi hujumuika na ndugu ama marafiki na kufanya makamuzi ya kufa Mtu lakini pia tunapowakumbuka hawa ambao hawamjui Mama wala Baba ni jambo jema mbele ya jamii na kwa Mwenyezi Mungu pia
Rehema Fabiani ni Mrembo anayeshikilia taji la Miss Kiswahili Tanzania kwa sasa,wito wake kwa jamii ya watanzania na haswa kwa watu wenye uwezo ama nafasi tuwakumbuke watoto Yatima amesema Rehema

Sunday, January 29, 2012

CHEKA AMSHINDA NYILAWILA KWA POINT!


Francis Cheka akinyosha mikono juu baada ya kuibuka mshindi na refarii Nemes Kavishe huku Bondia Kalama Nyilawila akiwa haamini matokeo hayo.

Bondia Francis Cheka (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Kalama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro mwishoni mwa wiki cheka alishinda kwa 
pointi.
  
 Askari wa usalama wakiendeleza ulinzi wakati wa mpambano huoo jana
Bondia Ibrahimu Class (kushoto) akipambana na Venasi Mponji wakati wa mpambano wa utangulizi walitoka droooo Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com.

SERENGETI LAGER YAZINDUA NEMBO YENYE MUONEKANO MPYA WA DHAHABU, LAKINI BURUDANI ILEILE.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko B. Joyce Mapunjo katikati akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kampuni ya bia ya Serengeti mara baada ya kuzindua rasmi bia ya Serengeti katika muonekano wa Dhahabu, uzinduzi uliofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam na kuhudguriwa na wadau mbalimbali na wageni waalikwa.
Kutoka kulia ni Emilian Rwejuna meneja masoko (SBL) Mark Tyro Mkurugenzi wa Usambazaji, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Viwanda, Biashara na Masoko Joyce Mapunjo, Mkurugenzi mtendaji wa (SBL) Richard Wells na kushoto ni Zohra Moore Meneja wa Huduma IPP wakipozi kwa picha huku wakiwa wameshikilia chupa mpya ya Serengeti Lager iliyo katika muonekano wa Dhahabu
Chupa mpya ya Serengeti Lager yenye muonekano wa wa Dhahabu ikiibuka kutoka katika maji mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana usiku.
Shamrashamra zikiendelea wakati nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager ikizinduliwa jana.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko B. Joyce Mapunjo akizungumza katika uzinduzi huo
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza katika uzinduzi huo wakati alipomkaribisha mgeni rasmi.
Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akizungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika taifa kupitia bia ya Serengeti Lager.
Mark Tyror Mkurugenzi wa Usambazaji kulia na Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti wakionyesha nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager.Mrembo wa Serengeti Lager akipozi kwa picha na huku akionyesha Nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager
Mkurugenzi wa Usambazaji Mark Tyro kushoto akipozi kwa picha na marafiki zakeKutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti na Mwisho ni Meneja wa Mahusiano kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela
Hapa ilibaki burudani tu.
Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akiongea na mkurugenzi wa Extra Bongo Kamalade Ali Choki , kulia ni Meneja Masoko wa (SBL) Emilian Rwejuna.
Hapa mzuka ukapanda kidogo lakini yote ilikuwa burudani na uzinduzi wa muonekano wa Dhahabu katika burudani ileile ya Serengeti Lager.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
Kikundi cha ngoma za asili kikitoa burudani katika uzinduzi huo.
Dada Ritah Mchaki meneja wa bia ya Tusker katikati akipozi na wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti hebu wacheki pozi lao.
Mdau Bahati Singh kutoka kampuni ya bia ya Serengeti yeye ilikuwa mishemishe tu ili kuhakikisha mambo ya uzinduzi yanakwenda sawa.
Mikakati ikipangwa hapa Meneja wa kiinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo katikati anaonekana akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Richard Wells kushoto, huku akimsikiliza pamoja na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Emilian Rwejuna kulia.
Rapa mahili wa Extra Bongo Maarufu kama Furgason akighani huku akmsikilizia mnenguaji mahiri wa bendi hiyo Aisha Madinda wakati alipokuwa akicheza.
Huo ndiyo muonekano wa dhahabu wenyewe kama unavyoonekana.
Wanenguaji wa bendi ya Extra Bongo wakifanya vitu vyao jukwaani.
Wadau kutoka R$R wakiwajibika kazini.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo

BRAND NEW VIDEO! SUMA MNAZALETI ft MABESTE & BEN POL. TAFAKARI.. WATCH IT!!

Saturday, January 28, 2012

MAMBO YA MAANDALIZI YA WIKIEND.......

Hii ni pande za kawe mitaa ya kwa joseph pale.

Friday, January 27, 2012

UJUMBE KUTOKA KWA MWANAHARAKATI OSCAR AYOUB

Oscar Ayoub akiwa anapika madude.
Oooiiih!guy wtraap? let now 'n 4 all time extract from our body-music as a dentist extracts a stinking tooth all those decadent stooges versed in antivirus album.you are dentists ov dic music,u hv 2 do u'r proffesion in making musical revolution.,our 2ru musicians are not those intoxicated opresions,exploitation,inhuman proffesion but ze 2ru musicians are those who speak language of people lyk antivirus group who put forward people's interest and humanity.dat viruses"they hv bitten the finger with which their mother fed them"they deserve to be hanged.mandela said"no easy walk to freedom".

Thursday, January 26, 2012

PINDA: SIFIKIRII KUGOMBEA URAISI 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ikulu, Dar es Salaam jana. Picha na Emmanuel Herman


Ramadhan Semtawa
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amezungumzia mambo muhimu kumi na moja yanayogusa nchi kwa sasa yakiwemo ya kiuchumi na kisiasa huku akiwashangaa wanaotumia nguvu nyingi kuwania nafasi ya urais akisema hawajui mzigo mkubwa wa kuongoza taasisi hiyo.Katika mkutano wake na wahariri na wawakilishi wao uliofanyika ofisini kwake Dar es Salaam jana, Pinda alisema: “Kwa dhati sifikirii kugombea nafasi hiyo ya juu kwani ni mzigo mkubwa.”Alisema kuna watu wanautaka urais kwa nguvu na kuhoji kama wanajua mzigo mkubwa uliopo katika taasisi hiyo au wanafurahia mazingira yake ili wakanufaike kiuchumi na kibiashara.“Kuna watu wanautaka kweli urais... wanautaka kwelikweli, lakini kuutaka na kuupata ni vitu tofauti. Sijui kama wanautaka ili wawatumikie Watanzania au kwa sababu tu ya mazingira mazuri yaliyopo pale ili waweze kufanya biashara au wanufaike kiuchumi.”Alisema mtu anayejua mzigo mkubwa uliopo Ikulu kamwe hawezi kuutaka kama baadhi wanavyofanya: “Wakati mwingine huwa nikienda Ikulu namwambia ndugu yangu Rais pole. Ikulu ni mzigo mkubwa.”

Wednesday, January 25, 2012

KOZI YA MCHEZO WA NGUMI KIMATAIFA YAMALIZIKA KIBAHA MKOA WA PWANI

Mkufuzi Mkuu wa Makocha wa ngumi toka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani Joseph Diouf, akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa , Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa ufungaji wa mafunzi hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani, kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini Makore Mashaga
Makocha wakiwa na Vyeti Vyao
Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya chezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani Jana.

MAPENZI YAMLIZA ROSE NDAUKA

Msanii wa filamu nchini Tanzania Rose Ndauka  amesema kuwa anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Love Me’.
Ndauka akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema kuwa filamu hiyo itaonesha muonekano mpya wa Afrika ambapo hakutakuwa na matukio ambayo yanaweza kuchafua maadili.
Alisema kuwa filamu hiyo itaonesha matukio mengi kama vile mapenzi, usaliti na matukio mengine mengi ambayo yatakua ni fundisho kwa jamii. 


“Nipo katika mchakato wa kuitoa filamu yangu niliipa jina la  ’Love Me’, ambayo itakuwa ya kiafrika zaidi kwani watu wengine wamezoea kusema kwamba filamu zetu tunacheza kama wazungu hivyo sasa wategemee ujio tofauti kabisa,” alisema.
Sambamba na hilo msanii huyo aliwaomba mashabiki wake kuitafuta filamu hiyo pindi itakapokuwa sokoni kwani itaonyesha maisha halisi ya mapenzi na matukio mengine mengi ya kisisimua .

Sunday, January 22, 2012


Kocha wa Tmu ya JKT, Saidi Omari 'Gogo Poa' (kushoto) wakioneshana ufundi wa kutupa makonde na Kocha wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' wakati wa mazoezi ya vitendo yanayoendelea Kibaha Mkoa wa Pwani leo kwenye kozi ya kimataifa ya mchezo wa ngumi.


Kocha mchezo wa ngumi wa Timu ya Ashanti pamoja na Timu ya Mkoa wa Kimichezo Ilala. Rajabu Mhamila'Super D' (kushoto) akitupiana makonde na kocha wa Mkoa wa Pwani, Gaudence Uyaga wakati wa mazoezi kwa vitendo kwa makocha hawo ambao wapo katika kozi ya