Saturday, January 14, 2012

UZINDUZI WA FILAMU YA MACHWEO KUFANYIKA MAISHA CLUB KESHO.

MACHWEOni muda ambao jua linazama, Hii inamaanisha ni mwisho wa siku 
na si mwisho wa maisha.
Machweo ni kipindi muhimu ambacho mtu anapata nafasi ya kuyaangalia na kuyatafakari yale yote yaliyotokea siku nzima ili kesho yake iwe siku mpya kweli.
Nchi yetu iko katika kipindi hicho ,Sasa tumetimiza miaka hamsini ya uhuru Tanzania bara ambayo tunaweza kuhesabu kama siku moja.Tumefanya mambo mengi ya kukumbukwa, ya kizalendo,kishujaa,tumekosea,tumejifunza, tumeishi katika nyakati tofauti katika sekta tofauti za kimichezo ,kibiashara ,kisiasa,kiuchumi,kiutamaduni ,tumapita katika majanga makubwa tofauti tofauti na mambo mengine mengi tu kwa ujumla. Ndio maana leo tunakila sababu ya kuongelea mustakabali wa nchi yetu,kwa siku za mbeleni .
Kuuliza wapi tunaelekea is not a crime. ndani ya hii miaka hamsini ya uhuru wa nchi yetu ulizaliwa muziki uliochukua nafasi kubwa ya mioyo ya vijana.muziki wa bongo flava au mziki wa kizazi kipya.
Tumeshuhudia ukipita katika nyakati tofauti kabla haujakubalika mpaka ukaja kukubalika kabla haujawa biashara mpaka umekuwa biashara ,tumeshuhudia wanamuziki wakija,wakikua na kisha kupotea na wengine kufanikiwa.tumeshuhudia wakitokea watengenezaji wa muziki(ma-producer) wauzaji wa muziki , wasambazaji ,watumiaji wa muziki ambao ni wateja, kukua kwa media mbalimbali,waandishi wa habari ambao ndio wadau wakubwa katika muziki huu.tumeshuhudia watu wakilumbana ,makundi yakivunjika ,wadau wakipotea au kuhama kambi ,wasanii wakihangaika na serikali kufumbia macho misingi imara inayotakiwa kuwepo ili kila mmoja afaidike na tasnia hii.
Nadhani sasa ni wakati muafaka wa kulizungumzia hilo.kwani idadi kubwa ya wasanii inatoka katika familia za chini,tunawaomba wadau wetu,makampuni mbalimbali yanayo saidia tasnia hii kukua,waandishi wahabari,maproducer,wasambazaji,mapromota waonyeshe uwezo wao katika kusaidia tasnia hii.
Muziki huu ni kama familia iliyokosa walezi .ajira nyingi zinaweza kuletwa na muziki huu iwapo mpango wa serikali wa kuleta ajira kwa vijana ukalitazama suala hili kiundani. ni vizuri serikali nayo itulinde watuandalie mazingira mazuri katika sanaa hii.sisi kama wasanii tunajitahidi sana na tunaomba watuunge mkono.washabiki watuunge mkono pia kwani ni wadau wakubwa katika hili..
na katika kufanikisha hili tumewaandalia filamu inayokwenda kwa jina la "machweo"ambayo pia ina soundtrack kuonyesha hisia zetu juu ya muziki huu.tunawaomba na nyinyi muonyeshe hisia zenu.tarehe 15/01/2012 tumeandaa uzinduzi wa filamu hiyo pale maisha club kuanzia saa mbili usiku mpaka usiku wa manane.kiingilio kitakuwa sh 5000.
Filamu ya machweo itakuchukua katika safari nzima ya msanii BOKA MC ambaye alikuwa na ndoto za kuishi maisha yake kupitia muziki.Ndoto zake zinapotezwa na mazingira yaliyopo katika muziki huo hapa nchini .huku umri wake ukiwa unapotea,hana elimu ,hana hela za kujikimu yeye na familia yake.anatokea DJ FLASHA na kulisimamia swala hilo kupitia kindi chake cha PIGA KELELE kilichokuwa kinaruka kila jumamosi mchana.filamu hii inaibua hisia na mwamko mpya kwa wasanii wengi wanaotaka kutoka na waliotoka ila wakakata tamaa.
Kauli mbiu ya filamu ya machweo ni "FURAHA YA MAISHA SI KUTOKUANGUKA BALI NI KUSIMAMA KILA PALE UNAPOANGUKA"
filamu hii imetengenezwa na BONTA ARTS PRODUCTION pamoja na BLOOD BROTHERS.

No comments:

Post a Comment