Monday, January 9, 2012

MACHWEO KUZINDULIWA JUMAPILI.

Ile filamu ya kibongo inayozungumzia mambo mengi yanayomkuta msanii wa kizazi kipya pindi anapoanza harakati za kukuza au kuendeleza muziki kwa ujumla iliyopewa jina la machweo itazinduliwa juma pili ya tarehe 15 pale maisha club. 
Filamu ihii ambayo imechezwa na mastaa kibao na wadau wa huu muziki wa kizazi kipya (bongo fleva) wote kwa pamoja wameweza kuiwasilisha vyema dhamira yao katika kuieleza jamii kile kinachoendelea katika tasnia nzima ya muziki wa kibongo.
Akizungumza na MTOTO WA KITAA mwongozaji wa filamu hiyo, Adamu kasale alisema kila kitu kimeshakuwa sawa na kinachosubiriwa ni tukio tu la uzinduzi mabalo litafanyika siku ya jumapili pale maisha clab. "napenda kusema kuwa kila kitu kimekamilika, na kinachosubiriiwa ni siku tu ya kuizindu" 
"Pia filamu hii imekuja kivingine kabisa kutokana na kuwa tofauti sana na filamu nyingine kutokana na aina ya uigizaji mpaka upigagaji wa picha." aliongeza kasale.
Kasale pia aliwataja wasanii walioshiriki katika filamu hiyo  kuwa ni mzee Abby Sykes, Snare, Buff G, Bandago, Fid Q, Stev RnB, Suka na wengine kibao
katika uzinduzi huo kasale alisema kutakuwepo pia na shoo kali kutoka kwa wasanii wa bongo fleva ambao wataongozwa na Farid Kubanda a.k.a Fid Q

No comments:

Post a Comment