Wednesday, January 11, 2012

BREAKING NEWS: MZEE KIPARA HATUNAE TENA.

Msanii Mkongwe katika tasnia ya Maigizo/Filamu hapa nchini, Fundi Saidi kwa jina la kisanii alijulikana kama Mzee Kipara amefariki leo asubuhi, nyumbani kwake, Kigogo Mbuyuni-Kinondoni,  jijini dar.
Mzee kipara ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1922, huko Bongoni mkoani Tabora, alikuwa kisumbuliwa na matatizo ya miguu kukosa nguvu, alikuwa hawezi kusimama  mwenyewe, sambamba na umri nao huenda ulichangia kwa maradhi hayo na mengineyo, hali iliyokuwa ikimlazimu kutumia muda  mwingi kitandani, wakati mwingine alishindwa kutoka nje mpaka watu watokee kumtoa nje ili kuota jua ama kupunga upepo.
SULE'S INC. & ENTERTAINMENT, BLOG YA MTOTO WA KITAA, WASANII NA WADAU WOTE WA SANAA NA BURUDANI TUNATOA POLE KWA FAMILIA YA MZEE KIPARA NA WOTE WANAOHUSIKA NA MSIBA HUU

No comments:

Post a Comment