Saturday, January 7, 2012

JOKATE KWANGU NI KAMA DADA TU - DIAMOND


Diamond alianza mwaka vibaya mara baada mkesha wa mwaka mpya kusherekea akiwa Mahabusu huko mkoani Iringa, Na siku ya Jumapili alipata dhamana na kuweza kuondoka kwa usafiri wa gari ndogo ya kukodi na kuja Jijini Dar es salaam ili kuweza Kuzindua albamu yake, ndani ya Maisha Club, Wakati akiwa katika uzinduzi wake aliruhusu mashabiki ku uliza maswali moja kati ya swali alilojibu na ambalo watu walitegemea kupata majibu yake ni kuhusiana na sakata la nani ni mpenzi wake kati Jokate na Wema... bila kuficha alisema "wema ndio wangu Jokate ni kama dada yangu... Baada ya kauli yake hiyo umekamilisha ule uvumi kuwa wao ni wapenzi ila kuna baadhi ya wadau wanasema kuna kitu ambacho kiko nyuma ya pazia ni kipi hicho? 

.......KAZI KWAKO.......

No comments:

Post a Comment