Monday, January 30, 2012

RITA DOMINIC NDANI YA BIFU ZITO NA STEPANIE OKEREKE

MWIGIZAJI Stephanie anazidi kupata maadui baada ya Rita Dominic kuingia kwenye listi ya watu wanaompinga baada ya kupewa shavu nene katika tasnia ya filamu Nollywood.
Awali Stephanie aliyekua rafiki mkubwa wa Gienevieve Nnaji waliingia katika bifu baada ya Stephanie kupewa shavu hilo na yeye kupigwa chini.
Kisa cha kutokuwa na maelewani kwa wasanii hao ni kitendo cha Stephanie kuteuliwa kuwa kiunganishi kati ya wasanii na rais wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan.
Gienevieve alipinga uteuzi huo akisema hawawezi kufanya kazi na rais halafu mtu wa katikati awe msanii huyo akidai kuwa bado mchanga.
Rita naye ameibuka na kusema kuwa anataka kuonana na rais lakini suala la eti kupitia kwa Okerekea analipinga kwa kuwa msanii huyo ni mdogo sana kwake.
"Stephanie ni nani hapa Nollywood, eti nikitaka kuwasiliana na rais lazima nimuone yeye, huyo aliyemteua hana akili hata kidogo," alisema Rita.

No comments:

Post a Comment