b..

B1

Wynem

animation

Monday, February 22, 2016

KOCHA SUPER D AWAKILISHA LAMBILAMBI ZA WADAU KWA FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED CHIBUMBUI



Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT MuttaRwakatare katikati akimkabidhi Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' mchango uliotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya lambilambi ya marehemu Mohamed Chibumbui kilichotokea  Mkoa wa Mtwara Wilaya ya Masasi kushoto ni katibu Mkuu wa shirikisho hilo Makole Mashaga


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi mama mzazi wa marehemu Mohamed Chibumbui  Hadija Likamba ubani uliotolewa na wadau mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka Tanzania Boxing Fans pamoja na chama cha ngumi za ridhaa BFT katikati ni Baba mzazi Said Chibumbui Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekabidhi fedha za lambilambi kwa wafiwa wa bondia Mohamed Chibumbui ambaye alikuwa anachezea timu ya taifa ya mchezo wa masumbwi nchini
Chibumbui  aliefaliki feb 10 alikuwa anasumbuliwa na ugojwa wa kisukari na alizikwa feb 13 katika  kijiji cha Mihima kata ya Namupa Tarafa ya Mtama wilaya ya Lindi Mkoa wa Lindi
Bondia Mohamed Chibumbui aliezaliwa April 24 mwaka 1988 
Alianza kujifundisha mchezo wa masumbwi mwaka 2003 akiwa chini ya kocha  Juma Urungu 'Mkebezi' na timu ya mavituzi baada ya hapo aliamia timu ya polisi kisha timu ya JKT na mwisho mapaka kifo kinamkuta alikuwa akichezea timu ya Magereza.
Akizngumza wakati wa kupokea ubani uho uliotolewa na wadau mbalimbali wa masumbwi wakiongozwa na
Rais wa Shilikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT  na Tanzania Boxing Fans  'TBF' inayowakutanisha wadau mbalimbali  kwa njia ya mtandao wa Watsap Group mama wa marehemu 
Hadija Likamba ameshukuru kwa kufikiwa na lambilambi hiyo kutoka kwa wadau wa mchezo wa ngumi nchini na kuzidi kuwaombea duwa ili mchezo wa ngumi usonge mbele
Nae baba wa marehemu Said Chibumbui amewashukuru wadau wote na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega ambapo watakaa kikao kwa ajili ya alobaini ya marehemu na kufikishiwa taharifa
Marehemu alimuowa Ratifa Adrea june  7 mwaka 2008 na kubahatika kupata watoto wawili  mmoja ni Alhaj Mohamed Chibumbui (7) na Abubakari Mohamed Chibumbui (2) jumla marehemu ameacha watoto wawili na mke mmoja 
aliongeza kwa kusema kuwa shughuli nzima ya alobaini itafanyika nyumbani alipozaliwa marehemu tndika azimio tambukareli eneo la maputo .