Monday, September 30, 2013

J DEAL FT G'NAKO - NIIMBIE (Official Audio Release)

Download "Niimbie" wimbo toka kwa mkali ya R&B, J Deal au ukipenda "Jacob Deal" akiwa na Gnako the A City Kankara aka WaraWara. Wimbo ni category ya R&B toka studio za Noizmekah Arusha chini ya Producer Defxtro, kuusikiliza bofya HAPA na kwa mawasiliano zaidi check na J Deal kupitia +255 718 515 772

JIMMY MASTER FT KISUKE & SPAC DAWG - BADO NASO

Download "Bado Nahaso" wimbo wa JimmyMaster akiwa amemshirikisha Kisuke Matoke & SpacDawg mzigo toka studio za Noizmekah Arusha bofya HAPA kuisikiliza ngoma na kwa mawasiliano zaidi check na Jimmy Master aka Mnyampaa kwa nambari +255 655 499 318 powered by www.vmgafrica.com

BREAKING NEWS!!!!! MSANII NA MEMBA WA KUNDI LA WATEULE, MACK MALIK a.k.a SIMBA AFARIKI ASUBUHI HII

Msanii Na Producer Wa Music Wa Bongo Fleva Na Reggae Mack Malik Simba Amefariki Dunia Dakika 50 Zilizo Pita. Kaka Wa Marehemu Msafiri Masharubu Amesema Kuwa Alikuwa Akisumbuliwa Na Kuvimba Kwa Miguu Sana. Amefia Nyumbani Kwao Yombo. 
Mack Alikuwa Member wa Kundi la wateule na producer kwenye studio za Enrico Pale Sound Crafters. Tunazidi Kufuatilia Habari Zaidi

LORD EYEZ - ROHO ZINAWAUMA (Official Release)

Download Lord Eyes aka Lord Izzy Official full Song "Roho Zinawauma" HERE http://goo.gl/t9kDcB ikiwa ni Mkono toka Noizmekah Production Studios chini ya Producer Dx aka Defxtro, powered by www.vmgafrica.com

Thursday, September 26, 2013

JCB ft PROF JAY -DRIVE SLOW (MJ Recs) KIONJO SNIPPET

Pata kusikiliza kionjo cha JCB ft Professor Jay, wimbo unaitwa "Drive Slow" ikiwa ni kazi toka Mj Records chini ya MarcoChali, Download HAPA

Wednesday, September 25, 2013

1ST ANNIVERSARY OF THE LEGEND IS BACK

Sasa zimebaki siku 3 tu kabla ya kufika siku tunayoisubiri kwa hamu, The Legend is Back first anniversary. Project ilianza kwa support yenu na ni mwaka sasa tunatimiza kwa sapport yenu. Tulianza pamoja karibu tujumuike tutimize mwaka tukiwa pamoja. Siku hii muhimu itaambatana na shindano kali la disco dancing toka kwa mabingwa wa zamani kuiwakilisha Morogoro Maneno Ngedere na toka DSM Athuman Diga Diga. Vile vile wakali wa chacha Africa Mashariki Moddy Jazz B na Sunday Boy watachuana vikali. Utakuwa vilevile na special moment of silence kuwakumbuka malegendari wa disco waliotutangulia mbele ya haki ni j'mosi hii 28/9/2013 ndani ya isumba lounge. Wote mnakaribishwa


Tuesday, September 24, 2013

MSICHANA WA KIZUNGU ANAYEDAIWA KUONGOZA MAUAJI WESTGATE ADAIWA KUUWAWA KWENYE MASHAMBULIZIWakati mapambano bado yanaendelea dhidi ya wanamgambo wachache wa al Shabaab waliobaki ndani ya Westgate Mall, maofisa wa Kenya wamesema angalau al Shabaab watatu wameuawa katika harakati za kuokoa mateka
Taarifa zinasema mmoja wa magaidi hao ni mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa mwanamke huyo aliyetajwa ni Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White Widow” au “Mjane Mweupe” au “Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha anaripotiwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mume wa Samantha alikua mpiga mabomu wa kujitoa mhanga (suicide bomber) anayeitwa Germaine Lindsay ambaye baada ya kusilimu alitumia jina la Abdullah Shaheed Jamal.
Abdullah Jamal alikua ni mmoja wa magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga mabomu ya kujitoa mhanga katika treni tatu na kuua watu 56 nchini uingereza Julai 7, 2005 ambao unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7

MSANII MAY C, AACHIA WIMBO NA VIDEO YAKE YA RUDGALZ

  Download audio ya Rudgalz HAPA

Monday, September 23, 2013

BONDIA, ADAMU NGANGE AMTWANGA KWA K/O ISSA MATUMLA


Bondia Antony Mathias kulia akimpiga ngumi mfululizo bondia Ismail Ninja wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa kilimahewa chanika Kigogo Mathias alishinda kwa K,O Fresh Dar es salaam.

Bondia Adamu Ngange kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Issa Matumla wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya jumapili katika ukumbi wa Kilimahewa uliopo Chanika Kigogo Fresh Ngange alishinda kwa K,O ya raundi ya pili


Refarii Saidi Chaku kulia akimpa huduma ya kwanza bondia Issa Matumla baada ya kugalagazwa kwa ngumi na bondia Adamu Ngange

Bondia Antony Mathias AKIWA AMEBEBWA JUU JUU BAADA YA KUPATA USHINDI KWA k,O
Picha Zote na www.superdboxingcopach.blogspot.com

Sunday, September 22, 2013

HAPPYNESS ENOCK ANG'AA REDS MISS TANZANIA

Mkurugenzi wa masoko wa Tbl Kushilla Thomas akimkabidhi funguo za gari mshindi wa shindano la Red’s miss Tanzania 2013 mrembo Happiness Enock Watimanywa toka mkoani Dodoma  mara baaada ya kunyakua tajio hilo na kuwashinda washiriki wenzake 29  toka mikoa mbalimbali ambapo pamoja na gari lakini pia amepata kiasi cha shilingi milioni nane.

Redd’s miss Tanzania 2013 mrembo Happiness Enock Watimanywa toka mkoani Dodoma akiwa na washindi wa wenzake wa shindano la Redd’s miss Tanzania mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi kwenye shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani Cituy jijini  Dar Es Salaam,Kulia ni mshindi wa Pili Latifa Mohamed toka kanda ya Temeke na kushoto ni mshindi wa tatu Clara Bayo toka kanda ya Temeke


Friday, September 13, 2013

ILIVYOKUWA KWENYE UAANDAAJI WA VIDEO YA WIMBO, MWANAMBUZI YA WYNEM, VIDEO INAFANYWA NA KAMPUNI YA SULE'S INC.

Director, Sule Junior
Wynem akiwa na mrembo
Ass. Director, Alex Nyaganilwa (kulia) akielekeza jambo.
Bandago naye alikuwepo kushoo lav na Wynem.

Thursday, September 12, 2013

SHIWATA YAKABIDHI NYUMBA ZA WANACHAMA WAO KWA AJILI YA MAKAZI


Mkuu wa wilaya mstaafu, Bw. Henry Clemence akizungumza katika sherehe ya kukabidhi nyumba 38 za wasanii wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) katika kijiji cha Mwanzega, Mkuanga.

Mwandishi wa Habari, Josephine Joseph akionesha cheti alichokabidhiwa na SHIWATA mbele ya nyumba yake katika sherehe ya kukabidhi nyumba za wasanii, Mkuranga.

Mmoja wa wanachama wa SHIWATA, Emmanuel Ntumbii na mkewe wakipokea cheti cha kumilikishwa nyumba yake akishuhudiwa na wanachama wenzake.

Mwanachama huyu wa SHIWATA kulia ameamua kujijengea nyumba yake pole pole hapa akikabidhiwa cheti chake.
Mchezaji na Kepteni wa zamani wa Timu ya  Taifa Stars, Jella Mtagwa (kushoto) akipokea cheti cha nyumba aliyokabidhiwa na SHIWATA na eneo la robo ekari ambalo anatarajia kujenga nyumba kubwa

Wednesday, September 11, 2013

NOMA MPYA KUTOKA KWA PACHA THE GRE8 - VIJANA

Mc Pacha the great, mshindi wa pili (2nd runner Up) toka S.U.A season One akimshirikisha AdoraboMc, anadrop ngoma kwa jina "Vina" ,kazi ya hiphop ilosukwa pande za noizmekah productios na defxtro juu ya beat ya Moscow,pata kudownloadHAPA

Tuesday, September 3, 2013

MIYEYUSHO VS MOMBA SASA KUPAMBANA SEPTEMBER 29 MANZESE


Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akitunishiana misuri na Sadiki Momba wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika September 29 katika ukumbi wa Friends Coner Manzese Dar es salaam
Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
NA MWANDISHI WETU
MABONDIA Fransic Miyeyusho na Sadiki Momba wametambulisha mpambano wao wa kirafiki wa raundi 8 utakaofanyika katika ukumbi wa Friends Coner Manzese Dar es salaam
Akizungumza mmoja wa waratibu wa mpambano huo Ramadhanu Uhadi 'Rama Jah' amesema mpambano huo uliokuwa ukisubiliwa na mamia ya mashabiki wengi baada ya mabondia howo kutambiana kwa mda mrefu bila ya kuwepo na mpambano wao
ameongeza kwa kusema siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mingine ya utangulizi likiwemo ya vijana chpkizi na wakongwe vile vile watakuwepo
baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo katika utangulizi ni 
Mussa Sunga atakaemenyana na Fadhili Awadhi  raundi 6 uku bondia Iddy Mnyeke kotoka kambi ya Ilala akimenyana na Keis Amari  mpambano wa raundi 4 na Ambukile Chusa atapambana na Fadhili Kambi