Tuesday, December 28, 2010

M BAND KUKAMUA BUDHA BLUE LOUNGE KILA ALHAMIS

USIKOSE KUHUDHURIA SHOW KALI KUTOKA KWA M BAND KILA ALHAMISI PALE BUDHA BLUE LOUNGE KARIBU NA DK. KAIRUKI HOSPTAL. WASANII WAKALI WATATOA BURUDANI, NJOO UPATE LADHA YA KIPEKEE.

SIKU CHACHE BAADA YA SHINDANO LA UNIQUE MODEL


   
Mshindi wa Giraffe Unique Model, Asia Dachi (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo (unique model of the year 2010).Kulia ni mshindi wa pili, Diana Mainanson na mshindi wa tatu Mariam Rabii. shindani lilidhaminiwa giraffe ocean view hotel,channel ten,magic fm,Global pubishers,mohammed enterprises,Truworths,mtaakwamtaablog na uniqueentertz blog.

 Ikiwa ni siku chache 2u baada ya shindano hili kuisha kumetokea minong'ono mingi na stori zisizo na uhakika yote hayo ikiwa ni kuichafua timu nzima ya uandaaji wa shindano hili (Unique Entertainment). Mkurugenzi wa Unique Entertainment ametoa tamko lake akiwa kama kiongozi wa timu ya uandaaji.

Alianza hivi ".........Nawashukuru watu wote walionipa sapoti tangu mwanzo pale nilipozindua shindano, tukafika kwenye mchakato wa kuwapata washiriki, kuingia kambini mpaka hapa leo tumemaliza shindano, shukrani zangu ziende kwa vyombo vya habari, wadau kwa ushirikiano wao mzuri na sapoti kubwa niliyoipata kutoka kwa Bwana CHARLES BEKON kunidhamini kwa asililmia kubwa mpaka kufanikisha kulifikisha jahazi ukingoni mpaka kufikia kuwatangaza wanamitindo kumi katika soko a mitindo Tanzania ambao hawakuwepo kabisa kwenye ramani ya uanamitindo.

 Akiongelea kuhusu tuhuma za uchakachuaji wa matokeo Magesse alisema "........ukweli kuhusu tuhuma dhidi yangu na Unique Entertainment naweza kusema sio za kweli kabisa na hii ni kwa sababu tumegundua kama Unique model imeingiliwa na MAMLUKI na pia watu wanatumia pesa katika kunidhalilisha mimi na timu yangu. Naweza kusema kama mchezo huo mchafu tumesha ungundua."
Aliendelea Magesse kwa kusema ".....Nimesikitishwa na baadhi ya wanakamati wangu kuwa wasaliti kwa kupandikiza chuki kwa washiriki kuwahimiza waongee mambo ya uzushi na unafiki katika vyombo vya habari kwa lengo la kuniharibia shindano kwa kunivunjia uaminifu kwa jamii, wadau na wadhani kwa ujumla lakini kwa uwezo wa mungu nasema hilo nimeligundua na hawatafanikiwa kwa lolote.
.....TUMEKUWA NA MAMLUKI WENGI KATIKA MCHAKATO WA KUANDAA SHINDANO HILI KWANI TOKA AWALI TULIWAJULISHA WASHIRIKI NA VYOMBO VYA HABARI KUWA WAMEKUWA WAKITUMWA WATU MBALIMBALI KULETA MAMBO YA UZUSHI NA MAJUNGU HUKU WAKITUMIKIA NAFASI MBILI TOFAUTI
   Unique model ni shindano lililokuja kwa kasi lakini limeibua maadui wengi wanaolichukia shindano hili ikiwa hata wale wa ndani ya kamati kupeleka habari za uzushi katika vyombo vya habari mfano dhahiri katika  Gazeti la MWANACHI jumapili ya tarehe 26/12/2010  LILIANDIKA HABARI ZIMELETWA NA MMOA WA VIONGOZI WA SHINDANO LA UNIQUE MODEL.......jiulize sasa.. KIKULACHO KI NGUONI MWAKO, kama mtu anaweza kuandika habari ya kuchafua na kuituma kwenye vyoimbo vya habari je atashidwa kueneza maneno ya uzushi na kuwafatab chumbani washiriki waje kuongea maneno ambayo aliwashurutisha wayaseme kama alivyowapanga kuzungumza katika Televisheniya TAIFA (tbc1)

 MTU HUYU ALIDIRIKI KUWASHAWISHI MAJAJI KUSUSIA MAAMUZI NA KUWASHAWISHI WASHIRIKI KUFANYA FUJO NA KUGOMEA KILE KILICHOTANGAZWA PALE JUKWAANI KWANI WAO HAWAKUWA NA WAZO HILO LA KUFANYA FUJO (hii taarifa nmeipata kutoka kwa mmoja wa washiriki aliyekuwa nyuma ya jukwaa wakati mshindi wa kwanza hadi wa tatu wakiwa jukwaani)
 Magsse alimalizia kwa kusema "......WATANZANIA MIMI KAMA MWM/KITI WA KAMATI YA UANDAAJI WA SHINDANO HILI NAOMBA RADHI KWA YOTE YALIYOJITOKEZA ILA NAOMBA MTAMBUE KUWA KUNA MIKONO YA WATU WANAOTUMIA PESA, MAJUNGU, FITNA, UZUSHI NA KUWARUBUNI WASHIRIKI NA WATU WA KARIBU KUSAMBAZA MANENO YA UCHOCHEZI KUNIHARIBIA SHINDANO WABAKI PEKEAYO,I LA IPO SIKU UKWELI UTAJULIKANA TU KWA WATANZANIA WOTE...."
....INANIUMA SANA MTU KUMNUNUA MODEL WANGU AZUNGUMZE UONGO KATIKA MEDIA...HATA  YESU ALILETA UZIMA LAKINI ILIFIKA KIPINDI WATU WALIMTEMEA MATE, KUMDHIHAKI NA NA KUMDHALILISHA,KWANI BAADHI YA WATU HAO WALIONEKANA NI WENYE FURAHA SANA BAADA YA KUFANIKIWA MPANGO WAO AMBAO ULISUKWA KWA MUDA KADHAA NA KUWATUMIA WATU WA KARIBU YANGU KUFANIKISHA MKAKATI HUO

MCHANGO WANGU KATIKA SANAA YA MITINDO NI MKUBWA LAKINI NDO UMEFIKA WAKATI AMBAO JIWE MOJA KUKATAA KUKAA KATIKA JIWE JENZAKE, PIA MEDIA ZOTE MNATAKIWA KUBALANCE STORY ZENU SIO KILA MNACHOAMBIWA TU MNAPELEKA HEWANI....INA MAANA LEO MTU AKISEMA AKISEMA MAGESE NI MCHAWI MNARUSHA TU....!?? TAFUTENI EVIDENCE KWANZA NDO MRUSHE SIO MNACHAFUA TU WATU NA BIASHARA ZAO.

Monday, December 27, 2010

KAMA KAWA GAZETI LAKO LADIRA LIPO MITAANI LEO.

 
MPANGO MZIMA UKO MTAANI UKIWA UMESHEHENI HABARI ZA UHAKIKA KABISA. PATA NAKALA YAKO SAS.

Thursday, December 23, 2010

KARIBU KWENYE SHOW YA UNIQUE MODEL

CBH nae atakuwepo katika kuasindikiza washiriki wa shindano la kumtafuta mwanamitindo wa kipekee la UNIQUE MODEL 2010 litakalofanyika kesho pale Hoteli ya Giraffe Ocean Vew

Sunday, December 19, 2010

KWNYE RISECHI YA MTOTO WA KITAA PANDE ZA MADALE IMEGUNDUA BADO KUNA SHIDA YA MAJI SAFI.

Kama kwaida huu ndi usafiri wangu wangu wa kunifiksha kila ninapota kwenda (kwenye mizunguko yangu ya kawaida) mjini hapa.
Hiki ndio kisima kikuu cha maji wanayotumia watu madale, maji ya kisima hiki hutumika kwa kunywa baada ya kuchujwa kufulia na matumizi mengine ya nyumbani. Mtoto wa kitaa nilipita pande zile na nilzungumza na watu wawili watatu na kupata maoni yao.
Hawa ndio wananchi wa MADALE nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

BURUDANI YA WIKI NDIO HII HAPA. SIO LAZIMA MI KUISHI KAMA WEWE KUTOKA KWA WATENGWA.Hapa ni kikosi kizima cha WATENGWA kutoka kijenge ya juu A-town.

Saturday, December 18, 2010

KIFO CA ABUU SEMHANDO NI PIGO JINGINE KWENYE MUZIKI WA DANSI.


Mpiga dram wa siku nyingi wa Bendi ya Twanga Pepeta na bendi mbali mbali za hapa nchini,Abou Semhando a.k.a Baba Diana (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya pikipiki .Ajali hiyo imetokea maeneo ya Tanki Bovu,Mbezi baada ya kugongwa na gari akiwa katika pikipiki yake na kutumbukia mtaroni na kupelekea mauti kumfika.Msiba upo nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar.
Marehemu Abou Semhando (kulia) akiwa na mkongwe mwenzake Kanku Kelly katika msiba wa Dr. Remmy Ongala siku mbili zilizopita kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni.
Pikipiki ya Marehemu Abou Semhando aliyopata nayo ajali ilivyoonekana baada ya kupata ajali
Gari linalosadikiwa kuhusika na ajali hiyo likiwa mtaroni

Na John Kitime
 
Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari.
Marehemu Abou Semhando, maarufu kwa jina la 'Baba Diana', pia alikuwa mmoja wa waasisi na viongozi waandamizi wa The Affrican Stars 'Twanga Pepeta' kabla ya umauti kumfika. Bendi zingine alizopigia wakati wa uhai wake ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.
 
Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa Abou alikuwa mmoja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki yake

UMABE ARTS COMPANY WATOA WIMBO WA HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA. TAZAMA WIMBO HUO HAPA CHINI.


SONG: MERRY CHRISTIMASS AND HAPPY NEW YEAR BY UMABE COMPANY (AUDIO)

ARTIST: Ndyamukama, Kajubi, Kita, Azma, Sir J, Lady Shani & G Fulla

Friday, December 17, 2010

HAWA NDIO WASHIRIKI WA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010.

Shindano hili ltafanyika katika hotel ya Giraffe Ocean Vew hotel tarehe 24/12 2010 kwa kiingilio cha Tsh. 20,000/= viti vya kawaida na Tsh. 30,000/= kwa viti maalum. OFFER ya punguzo la bei ya vyakula na vinywaji siku ya tukio! Tiketi zitaanza kuuzwa jumatatu ya tarehe 20/12/2010 na zitpatikana  duka la nguo la Truworths (mlimani city), Global publisher (bamaga), Giraffe Ocean Vew hotel (Africana / kunduchi) na stears (posta).

AJALI MCHA KWEUPEEEE!


Hap ni kwenye mataa ya mwenge. sijui walikuwa hawaonani!?

WASHIRIKI WA GIRAFFE UNIQUE MODEL WAENDELEA NA MAZOEZI KAMBINI.

Hapa wakifanya mazoezi ya kucheza mziki
Hapa wakipata mafunzo ya kutmbea (cat-walk) kutoka kwa mwalimu wao Victoria Martin.
Hapa wakipata maelezo jins ya kuingia kwenye jukwaa
Baada ya kumaliza mazoezi wailpata picha ya pamoja
Huyu ndie Christina Peter aliomba apige picha ya pekeake

Tuesday, December 14, 2010

UZINDUZI WA KAMBI YA WASHIRIKI WA SHINDANO LA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010

 
Mratibu wa shindano Bw. Methuselah Magese akizungumza na waandishi wa habari
Muwakilishi kutoka Mohamed enterprisses Zeinul Mnzige akizungumzia ni jinsi gani wamevutiwa na shindano mpaka kampuni yake ikaamua kudhamini shindano hilo
Zeinul Mnzige (kulia) akikabidhi zawadi ya vitenge kwa Mratibu mkuu wa Giraffe Unique Model,Methuselah Magese ikiwa ni moja ya zawadi zitakazokabidhiwa kwa warembo hao.

UNIQUE MODEL ni shindano la kutafuta wanamitndo wenye sifa za kipekee. Kwa mwaka huu limepewa jina la Giraffe unique model kutokana na Hoteli ya Giraffe Ocean vew ambayo iko katika hadhi ya nyota nne kuwa mdamini mkuu wa shindano hili.
Lengo la kuweka kambi ni kuwakusanya washiriki sehemu moja na kuwapa elimu kuhusu masuala mbalimbali yahnayo husu mitindo, maadili na namna ya kuishi na jamii yenye tabia tofautitofauti. Kwa upande wa unique entertainment lengo lake ni kuinua na kuendeleza vipaji vya sanaa ya uanamitindo hapa nchini.
Hiki ni kitu kipya tumekuja nacho kutokana na utafiti tuliofanya na kugundua soko la mitindo hapa nchini na hata nje ya nchi linahitaji wanamitindo wa aina gani ili kila mtu avutiwe na tasnia hii ndio maana unique entertainment tumeamua kutengeneza wanamitindo mabao watakidhi na watakua bora katika soko la uanamitndo kwa hapa nchini.
Shindano hili litafanyika 24th desemba siku ya ijumaa kuanzia saa mbili usiku ambapo tutakua pia na burudani kutoka kwa wasnii mbalimbali wa kizazi kipya na kiingilio kitakua ni tsh. 20,000/= kwa viti vya kawaida na tsh. 30,000/= kwa viti maalum.
Kwa upande wa udhamini tukimuacha Giraffe ocean Vew Hotell kama mdhamini mkuu pia tunao wadhamini kama Robbialack paints, Mohamed enterprises, Channel Ten, Global Publishers, Truworths, Ally Rehemtullah, Galacha wear mtata kwa mtaa blog na uniqueentertz blog.
Kwa kumalizia tu ni kwamba tiketi za tukio zitaanza kupatikana muda wowote kuanzia leo na tunatarajia zitakua zikipatikana katika vituo mbalimbali kama vile Truworths (mlimani city), Global publisher (bamaga), Giraffe Ocean Vew hotel (Africana / kunduchi) na stears (posta).

Kuhusu UNIQUE ENTERTAINMENT

UNIQUE ENTERTAINMENT ni kampuni iliyesajiliwa kisheria nchini Tanzania chini ya BASATA kufanya kazi za mitindo na burudani.
Kwa mawasiliano zaidi:
e-Mail: uniqueentertz@yahoo.com
web: www.uniqueentertz.blogspot .com
Tel: +255 714 796 622, +255 769 378 747

Mratibu wa shindani wa Giraffe Unique Models 2010

Methuselah Magese

Sunday, December 12, 2010

EXCLUSIVE: DR. REMYY ONGALA AMETUTOKA.


Msanii mahiri na mkongwe Dk. Remy amaga dunia usiku wa kuamkia leo. watanzania wote wameguswa na kifo chake kutokana na Remy kuwa kipenzi cha watu.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPOONI AMINA.

GAZETI LAKO LA DIRA YA MTANZANIA LIPO MTAANI LEO HII, PATA NAKALA YAKO SASA.
Kama kawaida gazeti lako la kila wiki linalotolewa na DIRA MEDIA GROUP leo lipo mtaani kwa tsh. 400/- pata nakala yako upate kujua kinachoendelea ndani ya nchi yako na hata nje ya nchi kupitia waandishi waliobobea katika kuandika habari za kiuchunguzi na zenye uhakika. ndani ya gazeti la DIRA utapata habari za kisiasa, kiuchumi, kijamii, michezo na burudani.

Saturday, December 11, 2010

KILIMANJARO STARS ILIVYOIPGA UGANDA JANA.

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakishangilia kutinga fainali baada ya kuwatungua Uganda kwa penati 5-4 katika gemu lililopigwa jioni ya leo pale neshno stadiumu.Kilimanjaro Stars itakutana na Ivory Coast katika fainalo ya mashindano ya Tusker Challange Cup siku ya jumapili pale pale Neshno.
Furaha ya Ushindi.
John Boko wa Kilimanjaro Stars akiribu kutapa kucheka na nyavu lakini hakufaniliwa.kwa kweli gemu la leo lilikuwa ni la kuvutia na lenye msisimko mkubwa sana.hadi mwisho wa mchezo,Kilimanjaro Stars iliibuka kidedea kwa kuinyuka Uganda bao 5-4 na kuwafanya stars kutinga fainali bila longolongo.
Mrisho Ngassa akifanya vitu vyake mbele ya beki wa Uganda,Walusimbi Godfrey.
Refarii wa mchezo wa jana, Davies Omweno akipiga stori mbili tatu na makiwa wa Kilimanjaro Stars, Juma Kaseja pamoja na Odongkala Robert wakati wa kupigiana petati kwa timu zote mbili.
Wapiganaji wa BBC walienda laivu bila chenga katika libeneke lao.
Kila Mtanzania amefurahia usindi wa Stars jana.
Kitu wavuni huku Kipa wa Uganda akisindikiza kwa macha.
Wazee wa kazi wakiwakilisha.
Stars jana ilikuwa na full shangwena rahaaaaa.....

Friday, December 10, 2010

WASHIRIKI WA SHINDANO LA GIRAFFE UNIQUE MODEL WATEMBELEA MLIMAN TV NA KUFANYA KIPINDI CHA MITINDO NA UREMBO NA MWANADADA SHIKNA OTHMAN.

Hili ndio gari kutoka Gioraffe ocean vew hotel ambalo washirki walitumia katika safari za hapa na pale mjini
Hapa washiriki wakiwa mlimani city ambapo walitembelea kabla ya kwe mlimani tv.
Sarari ya kwenda mlimani tv iliannza.
Hatimae wakafika mlimani tv
Kabla ya kuanza kipindi washirki walijipiga ma mek up ya kutosha na kipindi kikaanza.
Kipindi kilirikodiwa dizaini hiyo.
Baada ya kumaliza kurikodi kipindi watu walijiachia na kamera ya mtoto wa kitaa.