b..

B1

Wynem

animation

Saturday, December 18, 2010

KIFO CA ABUU SEMHANDO NI PIGO JINGINE KWENYE MUZIKI WA DANSI.


Mpiga dram wa siku nyingi wa Bendi ya Twanga Pepeta na bendi mbali mbali za hapa nchini,Abou Semhando a.k.a Baba Diana (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya pikipiki .Ajali hiyo imetokea maeneo ya Tanki Bovu,Mbezi baada ya kugongwa na gari akiwa katika pikipiki yake na kutumbukia mtaroni na kupelekea mauti kumfika.Msiba upo nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar.
Marehemu Abou Semhando (kulia) akiwa na mkongwe mwenzake Kanku Kelly katika msiba wa Dr. Remmy Ongala siku mbili zilizopita kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni.
Pikipiki ya Marehemu Abou Semhando aliyopata nayo ajali ilivyoonekana baada ya kupata ajali
Gari linalosadikiwa kuhusika na ajali hiyo likiwa mtaroni

Na John Kitime
 
Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari.
Marehemu Abou Semhando, maarufu kwa jina la 'Baba Diana', pia alikuwa mmoja wa waasisi na viongozi waandamizi wa The Affrican Stars 'Twanga Pepeta' kabla ya umauti kumfika. Bendi zingine alizopigia wakati wa uhai wake ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.
 
Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa Abou alikuwa mmoja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki yake

No comments:

Post a Comment