Tuesday, December 14, 2010

UZINDUZI WA KAMBI YA WASHIRIKI WA SHINDANO LA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010

 
Mratibu wa shindano Bw. Methuselah Magese akizungumza na waandishi wa habari
Muwakilishi kutoka Mohamed enterprisses Zeinul Mnzige akizungumzia ni jinsi gani wamevutiwa na shindano mpaka kampuni yake ikaamua kudhamini shindano hilo
Zeinul Mnzige (kulia) akikabidhi zawadi ya vitenge kwa Mratibu mkuu wa Giraffe Unique Model,Methuselah Magese ikiwa ni moja ya zawadi zitakazokabidhiwa kwa warembo hao.

UNIQUE MODEL ni shindano la kutafuta wanamitndo wenye sifa za kipekee. Kwa mwaka huu limepewa jina la Giraffe unique model kutokana na Hoteli ya Giraffe Ocean vew ambayo iko katika hadhi ya nyota nne kuwa mdamini mkuu wa shindano hili.
Lengo la kuweka kambi ni kuwakusanya washiriki sehemu moja na kuwapa elimu kuhusu masuala mbalimbali yahnayo husu mitindo, maadili na namna ya kuishi na jamii yenye tabia tofautitofauti. Kwa upande wa unique entertainment lengo lake ni kuinua na kuendeleza vipaji vya sanaa ya uanamitindo hapa nchini.
Hiki ni kitu kipya tumekuja nacho kutokana na utafiti tuliofanya na kugundua soko la mitindo hapa nchini na hata nje ya nchi linahitaji wanamitindo wa aina gani ili kila mtu avutiwe na tasnia hii ndio maana unique entertainment tumeamua kutengeneza wanamitindo mabao watakidhi na watakua bora katika soko la uanamitndo kwa hapa nchini.
Shindano hili litafanyika 24th desemba siku ya ijumaa kuanzia saa mbili usiku ambapo tutakua pia na burudani kutoka kwa wasnii mbalimbali wa kizazi kipya na kiingilio kitakua ni tsh. 20,000/= kwa viti vya kawaida na tsh. 30,000/= kwa viti maalum.
Kwa upande wa udhamini tukimuacha Giraffe ocean Vew Hotell kama mdhamini mkuu pia tunao wadhamini kama Robbialack paints, Mohamed enterprises, Channel Ten, Global Publishers, Truworths, Ally Rehemtullah, Galacha wear mtata kwa mtaa blog na uniqueentertz blog.
Kwa kumalizia tu ni kwamba tiketi za tukio zitaanza kupatikana muda wowote kuanzia leo na tunatarajia zitakua zikipatikana katika vituo mbalimbali kama vile Truworths (mlimani city), Global publisher (bamaga), Giraffe Ocean Vew hotel (Africana / kunduchi) na stears (posta).

Kuhusu UNIQUE ENTERTAINMENT

UNIQUE ENTERTAINMENT ni kampuni iliyesajiliwa kisheria nchini Tanzania chini ya BASATA kufanya kazi za mitindo na burudani.
Kwa mawasiliano zaidi:
e-Mail: uniqueentertz@yahoo.com
web: www.uniqueentertz.blogspot .com
Tel: +255 714 796 622, +255 769 378 747

Mratibu wa shindani wa Giraffe Unique Models 2010

Methuselah Magese

No comments:

Post a Comment