Wednesday, December 1, 2010

WASHIRIKI WA GIRAFFE UNIQUE MODE;L WATAMBULISHWA LEO.Mwalimu wa warembo wanaoshiriki katika shindano la Giraffe Unique Model,Hidaya Maeda akiongea katika mkutano wa kutambulishwa warembo hao kwa waandishi wa habari uliofanyika leo katika hoteli ya Giraffe Ocean View,Kunduchi jijini Dar.

Mkurugenzi wa kampuni ya Unique Entertainment,Methusule Magesse akizungumza katika mkutano huo pamoja na kuwatambulisha washiriki wa shindano ya Giraffe Unique Model katika hotel ya Giraffe Ocean View Jijini Dar leo.

Meneja Mwajili wa Giraffe Ocean View Hotel,Elsis Mtenga akiongea kwa niaba Mkurugenzi mkuu wa Hotel hiyo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel Giraffe Ocean View,Kunduchi Jijini Dar.

Baadhi ya Washiriki wa shindano la Giraffe Unique Model wakiwa katika pozz wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika hotel ya Giraffe Ocean View,Kunduchi jijini Dar.

wanahabari wakiwa mzigoni leo.

UINQUE ENTERTAINMENT Kampuni inayoandaa shindano la GIRAFFE UNIQUE MODEL leo imeamua kutangaza majina ya warembo watakaoshiriki katika fainali za shindano hilo.

Warembo hao wako kumi (10) na wanatarajiwa kupanda jukwaani katika fainali za shindano hilo zitakazofanyika tarehe 24-12-2010 kwenye Hoteli ya Girrafe Ocean View iliyoko Kunduchi Beach.

Lengo likiwa ni kuwatambulisha pia majaji wetu ambao ambao kwa imani yetu tunaamini wataweza kutufanyia kazi nzuri itakayoturidhisha. warembo wenyewe pamoa ja mashabiki watakaohudhuria katika onyesho hilo

Washiriki wetu hao kumi ni Dora Mhando, Ritha Samwel, Bilkis Suleiman, Asia Dachi, Neema Purity Walele, Careen Suleiman, Caroline Mwakasaka, Diana Manason, Mariam Rabii na Jacline Jiabe.

Majaji wetu watakua ni Ally Rehemtulah, Miriam Gerald, Steven Kanumba, Victoria Martin na Asia Idarus

Pia tanapenda kuwatangaza wadhamini wetu kuwa ni Giraffe Ocean Vew Hotel, Robialack Paint, Global Publisher blog ya uniqueentertz.blogspot.com ambayo ndio inayotoa habari zetu kwa haraka zaidi na kuweza kuwafikishia wadau na Chanel Ten televisheni.No comments:

Post a Comment