b..

B1

Wynem

animation

Tuesday, December 28, 2010

SIKU CHACHE BAADA YA SHINDANO LA UNIQUE MODEL


   
Mshindi wa Giraffe Unique Model, Asia Dachi (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo (unique model of the year 2010).Kulia ni mshindi wa pili, Diana Mainanson na mshindi wa tatu Mariam Rabii. shindani lilidhaminiwa giraffe ocean view hotel,channel ten,magic fm,Global pubishers,mohammed enterprises,Truworths,mtaakwamtaablog na uniqueentertz blog.

 Ikiwa ni siku chache 2u baada ya shindano hili kuisha kumetokea minong'ono mingi na stori zisizo na uhakika yote hayo ikiwa ni kuichafua timu nzima ya uandaaji wa shindano hili (Unique Entertainment). Mkurugenzi wa Unique Entertainment ametoa tamko lake akiwa kama kiongozi wa timu ya uandaaji.

Alianza hivi ".........Nawashukuru watu wote walionipa sapoti tangu mwanzo pale nilipozindua shindano, tukafika kwenye mchakato wa kuwapata washiriki, kuingia kambini mpaka hapa leo tumemaliza shindano, shukrani zangu ziende kwa vyombo vya habari, wadau kwa ushirikiano wao mzuri na sapoti kubwa niliyoipata kutoka kwa Bwana CHARLES BEKON kunidhamini kwa asililmia kubwa mpaka kufanikisha kulifikisha jahazi ukingoni mpaka kufikia kuwatangaza wanamitindo kumi katika soko a mitindo Tanzania ambao hawakuwepo kabisa kwenye ramani ya uanamitindo.

 Akiongelea kuhusu tuhuma za uchakachuaji wa matokeo Magesse alisema "........ukweli kuhusu tuhuma dhidi yangu na Unique Entertainment naweza kusema sio za kweli kabisa na hii ni kwa sababu tumegundua kama Unique model imeingiliwa na MAMLUKI na pia watu wanatumia pesa katika kunidhalilisha mimi na timu yangu. Naweza kusema kama mchezo huo mchafu tumesha ungundua."
Aliendelea Magesse kwa kusema ".....Nimesikitishwa na baadhi ya wanakamati wangu kuwa wasaliti kwa kupandikiza chuki kwa washiriki kuwahimiza waongee mambo ya uzushi na unafiki katika vyombo vya habari kwa lengo la kuniharibia shindano kwa kunivunjia uaminifu kwa jamii, wadau na wadhani kwa ujumla lakini kwa uwezo wa mungu nasema hilo nimeligundua na hawatafanikiwa kwa lolote.
.....TUMEKUWA NA MAMLUKI WENGI KATIKA MCHAKATO WA KUANDAA SHINDANO HILI KWANI TOKA AWALI TULIWAJULISHA WASHIRIKI NA VYOMBO VYA HABARI KUWA WAMEKUWA WAKITUMWA WATU MBALIMBALI KULETA MAMBO YA UZUSHI NA MAJUNGU HUKU WAKITUMIKIA NAFASI MBILI TOFAUTI
   Unique model ni shindano lililokuja kwa kasi lakini limeibua maadui wengi wanaolichukia shindano hili ikiwa hata wale wa ndani ya kamati kupeleka habari za uzushi katika vyombo vya habari mfano dhahiri katika  Gazeti la MWANACHI jumapili ya tarehe 26/12/2010  LILIANDIKA HABARI ZIMELETWA NA MMOA WA VIONGOZI WA SHINDANO LA UNIQUE MODEL.......jiulize sasa.. KIKULACHO KI NGUONI MWAKO, kama mtu anaweza kuandika habari ya kuchafua na kuituma kwenye vyoimbo vya habari je atashidwa kueneza maneno ya uzushi na kuwafatab chumbani washiriki waje kuongea maneno ambayo aliwashurutisha wayaseme kama alivyowapanga kuzungumza katika Televisheniya TAIFA (tbc1)

 MTU HUYU ALIDIRIKI KUWASHAWISHI MAJAJI KUSUSIA MAAMUZI NA KUWASHAWISHI WASHIRIKI KUFANYA FUJO NA KUGOMEA KILE KILICHOTANGAZWA PALE JUKWAANI KWANI WAO HAWAKUWA NA WAZO HILO LA KUFANYA FUJO (hii taarifa nmeipata kutoka kwa mmoja wa washiriki aliyekuwa nyuma ya jukwaa wakati mshindi wa kwanza hadi wa tatu wakiwa jukwaani)
 Magsse alimalizia kwa kusema "......WATANZANIA MIMI KAMA MWM/KITI WA KAMATI YA UANDAAJI WA SHINDANO HILI NAOMBA RADHI KWA YOTE YALIYOJITOKEZA ILA NAOMBA MTAMBUE KUWA KUNA MIKONO YA WATU WANAOTUMIA PESA, MAJUNGU, FITNA, UZUSHI NA KUWARUBUNI WASHIRIKI NA WATU WA KARIBU KUSAMBAZA MANENO YA UCHOCHEZI KUNIHARIBIA SHINDANO WABAKI PEKEAYO,I LA IPO SIKU UKWELI UTAJULIKANA TU KWA WATANZANIA WOTE...."
....INANIUMA SANA MTU KUMNUNUA MODEL WANGU AZUNGUMZE UONGO KATIKA MEDIA...HATA  YESU ALILETA UZIMA LAKINI ILIFIKA KIPINDI WATU WALIMTEMEA MATE, KUMDHIHAKI NA NA KUMDHALILISHA,KWANI BAADHI YA WATU HAO WALIONEKANA NI WENYE FURAHA SANA BAADA YA KUFANIKIWA MPANGO WAO AMBAO ULISUKWA KWA MUDA KADHAA NA KUWATUMIA WATU WA KARIBU YANGU KUFANIKISHA MKAKATI HUO

MCHANGO WANGU KATIKA SANAA YA MITINDO NI MKUBWA LAKINI NDO UMEFIKA WAKATI AMBAO JIWE MOJA KUKATAA KUKAA KATIKA JIWE JENZAKE, PIA MEDIA ZOTE MNATAKIWA KUBALANCE STORY ZENU SIO KILA MNACHOAMBIWA TU MNAPELEKA HEWANI....INA MAANA LEO MTU AKISEMA AKISEMA MAGESE NI MCHAWI MNARUSHA TU....!?? TAFUTENI EVIDENCE KWANZA NDO MRUSHE SIO MNACHAFUA TU WATU NA BIASHARA ZAO.

No comments:

Post a Comment