Monday, April 30, 2012

TBL YASHINDA TUZO YA USALAMA MAHALA PA KAZI SEKTA YA VIWANDA

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kushoto), akimkabidhi tuzo Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, baada ya kampuni hiyo kushinda masuala ya usalama mahali pa kazi, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama kazini duniani, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Makongoro Mahanga.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akimpongeza , Renatus Nyanda kwa niaba ya TBL.
Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Kabaka pamoja na baadhi ya washindi wa tuzo hizo.

CHEKA ALIVYOMGALAGAZA MAUGO BILA HURUMA

 
Baadhi ya Maraisi wa vyama vya mchezo wa Masumbwi Nchini wakiangalia mchezo wa Mada Maugo na Francis Cheka ubingwa wa IBF AFRIKA kutoka kushoto ni Rais wa TPBO,Onesmo Ngowi wa TPBC pamoja na Emanuel Mlundwa wa PST
Baadhi ya Marefarii kutoka Nnje ya nchi wakisubili kuchezasha mpambano wa ubingwa wa IBF Arika kati ya Mada Maugo na Francis Cheka
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wamekaa katika VIP wakiangalia mpambano
 
Ibrahimu Maokola kulia akipambana na Saidi Mbelwa Maokola alishinda kwa Point.Picha na www.superdboxingcoach
Mada maugo kushoto na Francis Cheka wakioneshana umwamba wa kutupiana masumbw
Cheka akipiga ngumi bila mafanikio uku mada akiludi nyuma kujiami
Francis Cheka akivalishwa mkanda wa ubingwa wa Afrika wa IBF baada ya kumchakaza Mada Maugo kwa TKO raundi ya 6

Meya wa Manspaa ya Ilala Jery Slaa akimkabidhi funguo ya gari bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa k.o raundi ya 6 

Thursday, April 26, 2012

LEO KINANUKA NDANI YA EMPIRE SPORTS BAR


CHEKA, KASEBA KUKUTANA SIKU YA SABASABA

Cheka akinia saini
kaseba akitia saini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com  

Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  amesaini mkataba wa kupigana na  bingwa wa kick Boxing. Japhet  Kaseba   katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi wanamtaka   kupigana  na yeye. "Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi yangu alisema Cheka. 
Kaseba nilimpiga kwa K.O tareha 3 October 2009 nilimpinga anataka tena wembe kwa ngua ngumi ni sehemu ya maisha yangu siwezi kukataa na mimi ndio napata ridhiki yangu humu hivyo nitahakikisha anaekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma nitaanza na Mada Maugo 28 April na huyo namuweka kama kipoloNae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya NchiMbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae;

Tuesday, April 24, 2012

SHINDANO LA KUIBUA VIPAJI LA KILI, LILIVYOKUWA DODOMA

majaji Kazini, hapa wakisikiliza muongozo kutoka kwa muendesha zoezi, Irene Kiwia, ambaye hayupo pichani, kutoka kushoto ni henry Mdimu, Joseph Haule, Queen Darleen, na Juma Nature
Mmoja wa washiriki Juma Madaraka akionesha ujuzi wake wa kuimba na kucharaza gitaa mbele ya majaji
Hawa ndio 20 bora waliokuwa wameingia katika fainali za mashindano hayo kutoka mkoani Dodoma
Washiriki wakipongezana baada ya tatu bora itakayowakilisha mkoa wa Dodoma kutajwa
Tatu bora, kutoka kushoto ni halima ramadhani, katikati ni Juma Madaraka na mwisho kabisa ni Issa Dubat
Washiriki wakifurahi pamoja baada ya washindi kutajwa

Na Mwandishi wetu
Baada ya siku mbili za usaili wa jumla ya washiriki 247 waliowania nafasi ya kupanda jukwaa moja na washindi wa tunzo za Kili wa mwaka 2012, hatimaye wawakilishi wa mkoa wa Dodoma wamepatikana jana mchana katika zoezi lililoonekana kuwa gumu kutokana na washiriki hao kuwa na vipaji vya hali ya juu vinavyofanana.
Katika zoezi hilo lililofanyika katika ukumbi wa Club maarufu mkoani humo inayojulikana kwa jina la 84, kati ya wasanii 247, ni wasanii watano tu wenye jinsia ya kike ndio walijitokeza kushiriki.
Kazi ya mchujo kwa wasanii hawa ilifanyika kwa takriban masaa 29 ambapo majaji wanne waliifanya, wakiongozwa na msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule, na mwanamuziki mwingine maarufu wa muziki huo Juma Kassim Nature, mshindi wa tunzo ya wimbo bora wa ragga kwa msimu huu Queen darleen na Mhariri wa Burudani wa Magazeti ya Mwananchi Communications.
Katika mchujo wa kwanza, jumla ya wasanii 200 waliondolewa katika mashindano, kisha wakabakia 47 ambao nao walipopita mbele ya majaji kwa mara ya pili, walijikuta wakiondoka 27 na kubakia 20 ambao waliingia katika fainali ya awali iliyofanyika siku iliyofuata.
Fainali nayo ilienda kwa michujo miwili ambapo katika mchujo wa kwanza, wasanii watano tu walibakia na mchuko wa pili ulipopita, wakabakia watatu ambao Jumamosi hii watakuwa ni wasanii wa awali kupanda katika jukwaa la tamasha kubwa la washindi wa tunzo za Kili mwaka huu ambapo kati yao, atakayeimba vizuri atadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro kuendeleza muziki wake na huyo pia atakuja kwenye tamasha kubwa la washindi litakalofanyika jijini Dar es salaam.
Akitangaza washindi, mmoja kati ya majaji walioonekana kuwa chachu ya mchuano huo henry Mdimu, aliwataja Halima Ramadhani, Juma madaraka na Issa Dulat kuwa ndio waliofanikiwa kufikia vigezo vya kuwa wasanii bora kabisa kutoka mkoani Dodoma kwa mwaka huu ingawa dhahiri vipaji vilionekana kuwa vingi kuliko walivyotegemea.
"Haikuwa kazi rafisi, ilikuwa inatupa wakati mgumu na kama sio maelekezo ya waandaaji huenda tungejikuta tu8nachukua hata watano baada ya watatu", alisema Jaji huyo baada ya shughuli kuisha.
Wiki hii mpambano utaendelea katika mkoa wa mwanza, ambapo Jumamosi, wasanii wa mkoa wa Mwanza watakuwa wakiisaka nafasi hiyo katika ukumbi wa Villa Park.

WASANII WA BONGOFLEVA WAPEWA DARASA

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha muziki wa asili nchini, Che Mundugwao akiongea na wadau wa Jukwaa la Sanaa (hawako pichani) wakati akiwasilisha mada iliyohusu Utunzi na Ubora Katika Tungo za Muziki. Kulia ni Maafisa kutoka BASATA, Aristide Kwizela na Agnes Kimwaga.
Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini, Mzee Kassim Mapili akichukua notisi ya kile kinachojadiliwa kwenye Jukwaa la Sanaa. Aliwaasa Wasanii kujifunza na utumizi wa ala katika muziki.
Mdau wakichangia mjadala kwa hisia

Na Mwandishi Wetu
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wameshauriwa kuwa na msimamo katika aina ya mahadhi ya muziki wanaoimba kuliko ilivyo sasa ambapo wengi wamekuwa wakichanganya na kushindwa kueleweka.
Wito huo umetolewa wiki hii na wadau wa Sanaa wakati wakiongea kwa nyakati tofauti kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo walisema kuwa, halil hiyo imeufanya muziki wetu ukose utambulisho na kushindwa kufanya vizuri kimataifa. “Wasanii wetu wamekuwa wakichanganganya mahadhi (aina) ya muziki wanaoimba.Leo anaimba reggae, kesho zouk mara muziki wa asili, hii inamfanya msanii asieleweke aina ya muziki anaoimba lakini pia tunakosa ubobezi kwenye aina hizi” alisema Che Mundugwao ambaye ni makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki nchini.
Aliongeza kuwa, kubadilika-badilika kwa wasanii kwenye aina ya muziki wanaoufanya si tu kumeufanya muziki wetu ushindwe kuvuma kimataifa bali pia unakosa utambulisho kwenye aina zingine za miziki zinazopatikana na kufahamika duniani kote.
“Muziki ni lugha ya Dunia, aina zake zinafahamika duniani kote.Tunachopaswa kufanya ni kutumia vionjo vya asili yetu ili kuleta utofauti. Tusipofanya hivyo tutaendelea kuwatumbuiza watanzaia wenzetu waishio ughaibuni tu na si kufanya matamasha ya kimataifa” alisistiza Che Mundugwao ambaye pia ni msanii wa muziki wa asili.
Mdau mwingine aliyefahamika kwa jina la Mbile Hango alionya kuwa, wasanii wetu wataendelea kuvuma kwa muda mfupi na kutoweka kama hawatazingatia taaluma na ubobezi katika aina fulani ya muziki.
Aliongeza kuwa, ni vigumu kwa wasanii kuimba kwa kunakiri muziki kutoka nchi za nje kama ile ya qwaito yenye asili ya Afrika Kusini halafu wategemee kupata fursa ya kuuza kazi zao nje na kushiriki matamasha ya kimataifa.
“Ukinakiri muziki kutoka nje maana yake huna kipya cha kupeleka nje, tutaendelea kuvuma humu humu ndani” alionya.
Mjadala wa wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa ulijikita kwenye Ubora katika Utunzi wa Tungo za Muziki

Monday, April 23, 2012

GARI LA CHEKA, MAUGO ILI HAPA

Msemaji wa Mpambano wa Ngumi kati ya Mada Maugo na Francis Cheka , Yasini Abdallah akionesha mkana na gari atakalopewa mshindi wa mpambano huo.
Johannes Lugenge kushoto na Promota wa Mpambano wa Mada Maugo na Francsis Cheka, Lucas Rutainurrwa wakionesha mkana wa Ubingwa wa I.B.F Afrika na gari atakalochukua bingwa wa mchezo huo Dar es salaam.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com 

Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gari watakalogombania  Mabondia Mada Maugo Na Francis Cheka  Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam. Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi. Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo. “Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike. 
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi. 
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .

Sunday, April 22, 2012

MRS KANARI KIPINGU ATEMBELEA KAMBI YA NGUMI KIBAHA NA KUTOA AHADI

MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. Zuwena Kibena ' Mama Kanari Kipingu' katikati akiwa katika picha ya pamoja na mabondia
MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. Zuwena Kibena ' Mama Kanari Kipingu' akikabidhi pesa ya maji  kwa Nahodha wa timu ya Taifa ya masumbwi Selemani Kidunda wachezaji wa timu hiyo jana
MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. zUWENA Kibena ' Mama Kanari Kipingu' kushoto akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Masumbwi alipotembelea kambi yao iliypo Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani juzi na kutoa ahadi mbalimbali kwa mabondia hawo.
MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. zUWENA Kibena ' Mama Kanari Kipingu' kushoto akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Masumbwi alipotembelea kambi yao iliypo Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani juzi na kutoa ahadi mbalimbali kwa mabondia hawo.
MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. Zuwena Kibena ' Mama Kanari Kipingu' akikabidhi pesa ya maji  kwa Nahodha wa timu ya Taifa ya masumbwi Selemani Kidunda wachezaji wa timu hiyo jana.
Picha zote  na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, April 20, 2012

HALI YA MSANII SAJUKI INATISHA, ANAHITAJI MSAADA.

Hizi picha zinamuonyesha Sajuki (mwenye miwani) akiwa katika hali aliyonayo sasa, hiyo ilikuwa katika hafla ya 40 ya kumtoa mtoto wao iliyofanyika aprili 15

Stori: Gladness Mallya
UKWELI ni kwamba, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ anaumwa.
Hali ya Sajuki imeendelea kuwa mbaya akidhoofu mwili siku hadi siku kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa. Aprili 15, mwaka huu Sajuki na mkewe Wastara Juma walifanya sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen ambayo ilihudhuriwa na waandishi wetu waliomshuhudia msanii huyo akiwa amedhoofu sana.
WASANII WAMTOLEA MACHOZI
Kabla ya kuugua, Sajuki alikuwa mwanaume aliyeshiba (mnene) na mwenye nguvu hivyo kutokana na hali yake ilivyobadilika na mwili kuwa mdogo, baadhi ya wasanii waliofika kwenye sherehe hiyo walijikuta wakimtolea machozi. “Jamani tuacheni utani, Sajuki anaumwa sana na anahitaji msaada na maombi yetu ili arejee kwenye hali yake ya kawaida,” alisema mmoja wa waigizaji wenzake.
SAJUKI KURUDI INDIA 
Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
WADAU TUMSAIDIENI SAJUKI
Kufuatia hali ilivyo, gazeti hili linaomba wadau tujitokeze kumchangia Sajuki fedha kwa ajili ya matibabu kupitia simu ya mkononi kwa kutuma kwenye Tigo Pesa namba 0713 666 113 au kwenye akaunti namba 050000003047 katika Benki ya Akiba Commercial yenye jina la Wastara Juma Issa.

Habari kwa hisani ya mtandao wa Global Publishers

Wednesday, April 18, 2012

MAWAKALA WA VYUO KUTOKA NJE GLOBAL EDUCATION LINK LTD CHAJIVUNIA UBORA WA UTOAJA WA ELIMU YA JUU .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kulia akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa vyuo kutoka nje Global Education Link. Bw. Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda la chuo hicho kwenye maonesho ya taaluma ya vyuo vikuu vya elimu ya juu katikati ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukulu Kawabwa na kushoto ni  Rahul Gupta Mwakilishi wa chuo cha  MMu.Picha na Mpiga picha Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal kulia akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa vyuo kutoka nje cha Global Education Link. Bw. Abdulmalik Mollel wakati alipotembelea banda la chuo hicho kwenye maonesho ya taaluma ya vyuo vikuu vya elimu ya juu katikati ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukulu Kawabwa.Picha na Mpiga picha Wetu

Tuesday, April 17, 2012

MABONDIA WA KAMBI YA ILALA WAJIFUA KWA AJILI YA MASHINDANO YA 10 BORA MAY 4

Mabondia wa Kambi ya Ngumi Ilala wakijifua kwa ajili ya mashindano ya kumi bora yatakayofanyika May 4 katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Dar es salaam.
Mabondia wa Kambi ya Ilala wakifanya Mazoezi ya Kichura chara kwa ajili ya kutafuta stamina na nguvu Mazoezi hayo yaliyokua yakitolewa na Kocha wa Kimataifa wa Mchazo wa Ngumi. Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kujiaandaa na mashindano ya kumi bora yatakayofanyika May 4 katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es salaam.

MAKAMU WA RAIS (TANZANIA) DK GHARIB BILAL ASAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU CHA KIFO CHA ALIYEKUWA RAIS WA MALAWI, DKT. BINGU WA MUTHARIKA LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maomboleo ya aliyekuwa Rais wa Malawi, Dkt. Bingu wa Mutharika, katika Ofisi za Ubalozi wa Malawi nchini, zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Aprili 17, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maomboleo ya aliyekuwa Rais wa Malawi, Dkt. Bingu wa Mutharika, katika Ofisi za Ubalozi wa Malawi nchini, zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Aprili 17, 2012. Kulia ni Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Flossie Asekanao Gomile-Chidyaonga. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais.

Monday, April 16, 2012

BREAKING NEWS: RUGE, SHIGONGO, ASHA BARAKA WAKABILIWA NA KASHFA YA KUCHAKACHUA FEDHA ZA MICHANGO MSIBA WA KANUMBA

Ruge (kushoto) akiwa na Shigongo (kulia)

MAJINA ya watu mashuhuri nchi hii, Erick James Shigongo na Rugemarila ‘Ruge’ Mutahaba- wote wakiwa ni wadau wa tasniya ya Habari yako hatarini kuingia doa.Kwa nini? Hiyo inatokana na kuwamo kwao kwenye Kamati ya mazishi ya mwigizaji Steven Charles Kanumba, ambayo imeingia kwenye kashfa ya kuchakachua michango ya msiba.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini leo vimeripoti kuwa, habari kutoka ndani ya familia ya Kanumba, imeituhumu Kamati hiyo kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele.Kamati ya Mazishi ilikuwa inaundwa  na Mwenyekiti Gabriel Mtitu, Makamu Mwenyekiti, Jacob Steven ‘JB’, Katibu, William Mtitu na Wajumbe Issa Mussa ‘Cloud’ (Mweka Hazina), Kimosa, Vincent Kigosi ‘Ray’, Single Mtambalike ‘Richie’, Dilesh Solanki, Millenne Happiness Magesse, Adele Kanumba (dada wa marehemu), Hartman Mblinyi, Ruge, Ally Choky, Simon Mwakifamba, Eric Shigongo, Steve Nyerere, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ na Mama Nassor, mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi Kanumba.Je, ukweli ni upi. Ni matarajio sasa wahusika wataibuka kujibu tuhuma hizi, hasa ikizingatiwa Kamati iliundwa na watu watu wazito kama Eric Shigongo, mmiliki wa Global Publisher, Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Clouds Media Group. 

PICHA YETU YA WIKI.

Picha hii mimi inanikumbusha wakati TOP BAND inaanza! wewe inakukumbusha wapi mdau!?

Sunday, April 15, 2012

NGOMA MPYA YA CHEGE - MWANAYUMBA

SUPER D ANZISHA PROGRAM YA KUTAFUTA MABONDIA KUMI BORA ITAKAYOANZA MAY 4

Kocha wa kambi ya
 Ngumi ya mkoa wa Ilala Kimichezo, Rajabu Mhamila,'Super D', ameanzisha programu maalum ya kuwafanyisha mazoezi mazitomabondia wake. 

Ameamua kuanzisha programu hiyo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuwana pumzi na nguvu kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani.
Akizungumza leo, Kocha huyo alisema kuwa mabondia wake watashirikikatika mashindano ya 10 bora yaliyoandaliwa na Kinyogoli Foundationyatakayofanyika May 4.
Alisema kuwa mabondia hao watazichapa katika mpambano wa aina yakeutakaofanyika mwezi ujao katika Ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.“Nimeanzisha programu ya aina yake kwa ajili ya kuwajengea uwezomabondia wangu ili waweze kuwa na pumzi za kutosha katika mashindanombalimbali” alisema.
nah! ila sio kiivyo! Super DAidha aliongeza kwa kusema wanaomba wadhamini kujitokeza kusaidi vitumbalimbali kwa ajili ya kufanikisha mchezo huo wa masumbwi kwakuwapatia vijana maja ata zawadi ndogo ndogo za kuwatia moyomashindano hayo yatakayowashirikisha vijana mbalimbali katika uzitotofauti yatakuwa na lengo la kuendeleza mchezo wa masumbwi NchiniMapambano yatakuwa mengi kwa kuwa vijana wengi wamejitokeza kujakujiandikisha kushiriki siku hiyo alisema Super D

NEW TRACK FROM ANAPITA - BARUA KWA MAMA.

Anapita, msanii wa miondoko ya AfroFusion anayewakilisha chuga kaskazini mwa Tz,sasa aja na "barua kwa mama" alorekodi pande za noizmekah.com kwa defxtro,asema "wimbo huu nimeuandika kutokana na maisha ya mjini jinsi yalivyo, vijana wengi tumekuja kutafuta na mama zetu wako mbali na sisi, kwa jinsi maisha yalivyo wakati mwingine mshiko wa kumpigia mother hauna, na wakati mwingine mama mwenyewe kijijini hana simu mpaka kwa jirani,kuna wakati hawa wamama hudhani kwamba tumewasahu halafu huku mjini tunakula bata lakini si kweli, ni utaftaji hapa na pale changanyia na panda shuka ya  gharama halisi ya maisha, pia kuna marafiki ambao kwa bahati mbaya mama zao washatangulia mbele za haki, nao hufikiria kuandika barua.Nawapenda mama zetu wote duniani kwasababu natambua umuhimu wao.Amani tele...

Thursday, April 12, 2012

BABA MZAZI WA LULU AFUNGUKA

Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini  Lulu Michael a.k.a Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba,  ameibuka na kueleza kushtushwa  sana na  taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake. Baba Lulu,  ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo,  Mkoani Kilimanjaro, anasema kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini  masikio yake baada ya kupata  taarifa za kifo hicho,  huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.
Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya  Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo. Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe  April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba  alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya  Midway  mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17. Bw Kimemeta  alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao  kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama  baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba. Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu. “Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na  kusaidia katika kupatikana  kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu  Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake” alisema. Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni  ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa  wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji. “Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa  Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia  alikuwa ni mpenzi  - nilishtushwa” alisema Kimemeta. Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa  kushindwa kuhudhuria mazishi  marehemu  Steven Kanumba  kuhofia usalama wake, na kusema  mazingira  yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole. Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.Kasema  kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla. 

MJUMBE WA YANGA AFARIKI DUNIA

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Wakili Theonist Rutashoborwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu ameaimbia bongostaz asubuhi hii kwamba bado wanawasiliana na familia ya marehemu ili kujua zaidi na saa 5:00 asubuhi watafanya Mkutano na Waandishi wa Habari.
Rutta ni mwanachama ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo kupata ufadhili wa Yussuf Manji mwaka 2006, kutokana na harakati alizoanzisha za Harambee ya Yanga kufuatia hali mbaya ya kifedha ndani ya klabu hiyo chini ya uongozi wa Francis Mponjoli Kifukwe enzi hizo.
Habari hii kwa hisani ya Dinah Ismail (mamapipiro.blogspot.com)

CECAFA YATUMA RAMBI RAMBI MALAWI

Rais Bingu wa Mutharika - Enzi ya uhai wake
BARAZA la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetuma salamu za rambi rambi kwa Shirikisho la Soka Nchini Malawi (FAM) baada ya rais wa nchini hiyo Dr Bingu wa Mutharika kufariki dunia. 
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye katika taarifa aliyoitoa alisema wamehuzunishwa na kifo hicho kilichotokea Alhamisi iliyopita kutokana na ugonjwa wa moyo kwenye Ikulu mpya ya Malawi iliyopo Mjini Lilongwe.
"Tunaomboleza na nyinyi na watu wa Malawi msiba huu mkubwa, ambapo tumepoteza mtu muhimu mwenye rekodi nzuri ya kuchapa kazi,"alisema Musonye.
Alisema,"tunasali ili watu wa Malawi ambao wapo pamoja na Cecafa wauchkue msiba huu kwa ustahimilivu mkubwa na waweze kupata rais mwingine kwa amani."
Pia alisema,"taarifa hii yangu ya maombolezo naomba imfikie mke wa rais, watoto wake, watu wa karibu wa familia na watu wa Malawi kwa ujumla."
Mwili wa Mutharika upo nchini Afrika Kusini na unatarajiwa kusafirishwa mpaka nchini Malawi kwa ajili ya mazishi Aprili 23 kwenye shamba lake huko Ndata Kusini mwa mji wa Thyolo.
Malawi ilikuwa mwanachama wa kamili wa Cecafa tangu mwaka 1970, lakini katika miaka ya 90 ilijiunga na Baraza la Vyama vya Soka vya Kusini mwa Afrika Cosafa.