Tuesday, May 31, 2011

BRASIL FILM FESTIVAL BADO INAENDELEA LEO PALE GOLDEN TULIP


Ndugu Waandishi wa Habari, Wanamziki na Marafiki wote,

          Tunayo heshima kubwa kuwaalika kwenye Onyesho la pili la Tanz Cine Brazil Festival-Brazilian Film Festival Tanzania, siku ya jumanne May, 31st Golden Tulip Hotel, saa 11.00 jioni hadi saa 07.00 usiku.
          Tanz Cine Brazil Festival- kwa mara ya pili itaonyesha Sinema nzuri za Brazili hapa Tanzania, pamoja na kufanya majadiliano na kubadilishana utaalam mbalimbali na Wanasanaa wa hapa nchini.Mwezi huu vilevile kutakuwa na majadiliano na Film Directing, itakayo ongozwa na Monoca Monteiro,  Chuo kikuu cha Dra es Salaam.
        Ufunguzi wa hii sherehe ya wazi ni June, 3rd  Makutano, ambapokutakuwa na Bralian band Pandero Repique Duo na muziki wa Tnzania Mulfred. June 4th kutakuwa na onyesho la picha kwenye TV ya nje, Makutano kuanzia 07 jioni., na 8th Nafasi Art Space sinema maarufu ya Brazil; City of God, Usikose. 
Pia utaweza kuonana na Producer kutoka Brazili Pandeiro Repique Duo na utweza kuuliza maswali ya matembezi yao.

Monday, May 30, 2011

Sunday, May 29, 2011

HAPPY B'DAY MTU MZIMA MARCO CHALI

http://2.bp.blogspot.com/-yDUGgRCvL2U/TeHptFKZxUI/AAAAAAAASzE/fjrtIS8BBWQ/s1600/217626_1994390463524_1356305629_2357582_6618930_n.jpg 
Leo ni tarehe ya kuzaliw mtu mzima Marco Chali Producer mahiri kabisa kutoka pal MJ Record

Thursday, May 26, 2011

MAKING VIDEO YA KUDADADEKI YA MALFRED

Hii ni moja tu ya seting ilivyokuwa pale sehemu ya tukio
Huyu nio Directo wa hii video kutoka OUTCOME
Directo Frank kutoka OUTCOME akifanya vitu vyake
Mpango mzima ulikuwa hivi!
Hapa Malfred alijiacha na warembo.

Wednesday, May 25, 2011

MALARIA IS DANGEROUS

WASHIRIKI WA MISS UNIVERSE WAPEWA SOMO NA VODACOM


Mtaalam wa  mawasiliano na bidhaa wa Vodacom Tanzania  Joel Bendera akifafanua jambo kwenye semina maalumu   ya kampuni hiyo kwa washiriki wa Miss universe,katikati Ofisa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo Elihuruma Ngowi,Mtaalamu wa maswala ya habari wa Vodacom Matina Nkurlu,shindano hilo linategemea kufanyika  mwishoni mwa mwezi huu na limedhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mshiriki wa shindano la Miss Universe Yacoba Assengu akifafanua jambo mara baada ya kuulizwa na waandishi wa habari katika semina maalum iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kwa washiriki hao kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo, shindano hilo linategemea kufanyika  mwishoni mwa mwezi huu lenye warembo 20 na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi akielezea jambo kwa baadhi ya washiriki wa shindano la Miss Universe wakati wa semina ya washiriki hao kujifunza mambo mbalimbali ya kampuni hiyo ,wapili kutoka kushoto Mtaalam wa maswala ya habari Matina Nkurlu,shindano hilo linategemea kufanyika  mwishoni mwa mwezi huu lenye warembo 20 na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa shindalo la Miss Universe wakiwa kwenye semina fupi iliyoandaliwa na Vodacom kwa ajili ya washiriki hao kujifunza mambo mbalimbali ya huduma za kampuni hiyo inazofanya, shindano hilo linategemea kufanyika  mwishoni mwa mwezi huu lenye warembo 20 na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

BRASIL FILM FESTIVAL BADO INAENDELEA.

TETEMESHA REC. YAJIPANGA KUTAMBULISHA VIPAJI VIPYA KWENYE GEMU LA MUZIKI WA BONGO.

C-SIR MADINI, sanii anaetambulishwa wakati huu

Huu ni ujumbe kutoka TETEMESHA RECORD! "Mambo vipi,

Nachkua nafasi hii kukushkuru sana kwa support unayoendelea kutupatia kiukweli bila mchango wako hatuwezi fika popote.
Sisi kama TETEMESHA RECORDZ tumejiwekea malengo ya kuwa tunajaribu kutafuta wasanii wachanga kabisa lakini wenye vipaji na kuwapika kisha kuwatambulisha katika music industry hapa TZ.
Tulianza na HUSSEIN MACHOZI, akafuata SAJNA na sasa ni zamu ya msanii mwingine mpya C-SIR MADINI kutoka Mwanza.
Huyu tunaemtambulisha sasa jina lake kamili ni PETER MPONEJA, na jina lake lingine la nyumbani ni MASISA, hilo MASISA lilikuwa jina la babu yake, na kutoka katika hilo ndio akaamua kulifupisha kuwa SISA na ndilo anatumia katika muziki lakini katika matumizi ya Muziki litakuwa likiandikwa C-SIR. ila kwa ukamilifu wake tunaomba mumpokee kwa majina mawili yaani C-SIR MADINI.
Huu ndio wimbo wake wa kwanza kutoka, na utakuwa katika album yake ya kwanza ambayo bado tunaendelea kuirekodi. Video ya wimbo huu imekwishafanyika chini ya ADAM JUMA wa NEXT LEVEL na itatoka siku chache zijazo."

SONG'S DETAILS
Track Name: KIFUNGO HURU
Artist: C-SIR MADINI
lyrics composed by: C-SIR MADINI, KID BWOY & JOSEFLY
arranged by: C-SIR MADINI & KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ

Tuesday, May 24, 2011

MAJIBU YA EPPA YAANAZA KUTEMA


....FARIJALA HUSSEIN NA RAJAB MARANDA....

    Hukumu ya kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetolewa leo kwa
   Farijala Hussein na ndugu yake Rajabu   Maranda,wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela ambapo pia wametakiwa kurudisha fedha hizo kwa Serikali
     Jopo la majaji watatu likiongozwa na Mh Saul Kinemela,limewatia hatiani kwa mashitaka nane yanayowakabili shitaka la kwanza lilifutwa kwa kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha hilo,Kwa kosa la pili mshitakiwa wa kwanza pekee atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela,kosa la tatu na la nne 
    washitakiwa wote watatumikia adhabu ya miaka mitano,kosa la tano mshitakiwa wa pili pekee atatumikia adhabu ya miaka miwili jela huku Kosa la sita washitakiwa wote kwa pamoja watatumikia adhabu ya miaka miwili jela na kosa la saba na la nane wote watatumikia adhabu ya miaka mitatu jela," alifunguka Hakimu Mgeta

Monday, May 23, 2011

WASHIRIKI WA MISS UNIVERSE WALIPOTEMBELEA OFISI ZA VODACOM

Meneja wa Bidhaa wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda akisalimiana na baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Miss Universe walipotembelea makao makuu ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ambaye ni moja ya mdhamni wa shindano hilo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam
Mmoja wa warembo wa Miss Universe akipata maelekezo kutoka Omary Kilumanga ambaye ni Afisa wa Kitengo cha Mauzo kwa njia ya simu wa Vodacom Tanzania wakati washiriki wa shindano hilo lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Kitengo cha Huduma kwa Wateja Laurent Ivo akiwaonesha baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Miss Universe jinsi mfumo wa kitengo hicho unavyofanya kazi wakati washiriki wa shindano hilo lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam

Sunday, May 22, 2011

ILIVYOKUWA KWENYE BRASIL FILM FESTIVAL MITAA YA KAWE.

Hapa ni Timu nzima ya NGO ya UNGANA TUJENGE BAADAE YETU (UTUBAYE) ikiwa kwenye maandalizi ya kufunga Projecto kwa ajili ya kuonesha filamu za kibrazil
Hili ndio nyomi lililojitokeza kwenye zoezi zima la kuangalia filamu 
Baada ya kumaliza kuangalia filamu watoto wa mtaa waliachiwa mziki mnene na kama kawa waliruka debe mpaka kikaeleweka.
Baada ya mambo yote dada Lucy aliongea na ITV kushukuru ubalozi wa Brazil kwa kuleta hili zoezi mitaa ya kawe
Na baadae SUle junior Ikawa zamu yangu kuongea na wadau na kuweza kuwashukuru ubalozi wa brazil kilea kilchofanyika!
Hii ndio timu ya UTUBAYE kuanzia kushoto ni Alex Peter Nyaganilwa (Excutive secretary), Salum Suleiman Lyeme (Chairperson), Jerry Joseph na Dymond Asangalwisywe
Balozi Mdogo wa Brazil, Ronado Vieira akiwa na wadau 
\Salum suleiman (Katikati) akiwa na balozi mdogo wa brazil, Ronado Vieira na mwananchi wa kawada!
Na hii ndio NEMBO aya NGO yetu

Friday, May 20, 2011

BREAKING NEWS….. SHEIKH YAHYA HUSSEIN HATUNAE TENA!!


 
Sheikhe Yahya Hussein Enzi za uhai wake

Mtabiri maarufu wa mambo ya Nyota afrika mashariki na Kati Sheikhe Yahya Hussein Amefariki dunia Leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. 
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya Lugalo. kwa taarifa zaidi kuhusiana na Msiba wake na habari zaidi juu ya kifo hicho tutawaletea hapa hapa endelea kuwa nasi na utafahamu zaidi. 
Blog hii inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, wananchi wote wa Tanzania kutokana na msiba huu mkubwa.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na ujasiri wanafamilia yake katika kipindi hiki kugumu cha kuomboleza hadi kuzikwa kwa mwenzetu Sheikhe Yahya Hussein.
SULE'S INC. & ENTERTAINMENT na timu nzima ya blog ya mtoto wa kitaa inatoa pole kwa ndugu jamaa na waislamu wot kwa kuondokewa na ndugu yao kipenzi.
INNA LILLAHI WA INNA-ILAHI RAAJIUUN

Thursday, May 19, 2011

USIKOSE KWENYE BOB MARLEY DAY 2011


BOB MARLEY DAY  - 2011
- Yes Reggae Massive ..Waandaaji Wakali wa matamasha ya reggae nchini wanawaletea tamasha la kumuenzi Mfalme Wa Reggae BOB MARLEY
-Tamasha hilo litafanyika siku ya j moss tarehe 21 May 2011 ndani ya  HUNTERS BEACH-KIGAMBONI
-Katika kunogesha maazimisho hayo kutakua na maonesho ya kazi za sanaa asilia ambayo yataanza saa sita mchana na baadae ikifwatiwa na live performance kali kutoka bendi za  wasanii mahiri wa Reggae wakiwemo
JHIKO MAN and AFRIKABISA BAND,MZUNGU KICHAA,RAS NGWANDUMI ,BUMMIJAH,RAS MIZIZI na MACHIFU BAND.Pia Kutakuepo na mshindi wa tunzo ya msanii bor.a wa reggae nchini,HARD MAD. Bila kusahau Surprise show kutoka kwa wasaani waalikwa.
- Kama hiyo haitoshi…zitapigwa mixing kali za reggae kutoka kwa  Reggae djs Mahiri akiwamo JA BLAZE,CRUCIAL YUSS along side KAKA MALIK
Kumbuka ni tarehe 21 May  ndani ya HUNTERS BEACH-KIGAMBONI na tamasha litaaza toka sa sita mchana mpaka majogoo.Ebaneeee..hii si ya kukosa.Tamasha hili limezaminiwa na 100.5 TIMES FM,TANZANIA RASTAFARIAN MOVEMENT na JAHRO SOUND

AMA KWELI POMBE SIO CHAI

Mshiriki wa Kinyang’anyiro cha Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian ‘Video Queen’, amekumbwa na aibu ya karne baada ya kufakamia pombe na kulewa tilalila.
Tukio hilo lilijiri katika Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumamosi ambapo kulikuwa na shindano la kumsaka Miss Dar City Centre 2011-12.

LIBENEKE JIPYA LA KONA YA MATUKIO


Tunapenda kulitambulisha wadau wote  libeneke jipya la KONA YA MATUKIO  ambapo nia na lengo kubwa ni kuleta matukio yanayotokea kila siku katika Jamii yetu na Duniani kwa Ujumla..pia kutakuwa na Matukio ya papo kwa hapo yaniBreaking News Endelea kuwepo kila muda kujua nini kitatokea