Saturday, May 7, 2011

MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA 2010/2011 NI MWANAIDI HASSAN

Mtoto wa kitaa (Sule Junior) Nikifuatilia mchongo mzima wa utoaji wa tunzo za TASWA


Mgeni rasmi,Makamu wa Rais akisoma hotuba fupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tuzo za kumsaka Mwanamichezo Bora 2011,ambazo zimedhaminiwa na kampuni ya bia ya Seren
geti (SBL).

Mgeni rasmi,Makmau wa Rais
,Dr Gharib Bilal pamoja na Waziri wa Vijana,habari,utamaduni na michezo Mh.Emmanuel Nchimbi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi waliojinyakulia zawadi mbalimbali usiku wa huu kwenye hafla ya tuzo za TASWA zilizothaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti.

Mgeni rasmi,Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal akimkabidhi tuzo kwa mchezaji wa jumla Bi.Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa netiboli katika timu ya JKT Mbweni.Mwanaidi ndiye alijijinyakulia gari aina ya Toy
ota GX 100,iliyotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndiyo waliokuwa wadhamini wakuu wa tuzo hizo za kumsaka mwanamichezo bora wa Mwaka zilizoratibiwa na TASWA,kusho ni Waziri wa Vijana,habari,utamaduni na michezo Mh.Emmanuel Nchimbi akishuhudia tukio hilo.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa,akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali mara baada ya kuipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal,Mh Mkapa amesisitiza kuwa uwanja huo unapaswa uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa, akipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA) kimempa mzee Kkapa tuzo hiyo maalum ya heshima, kutokana na mchango wake katika michezo hasa ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa,Mh Mkapa amesisitiza uwanja huo uendelee kutunzwa vyema ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi vijavyo,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda. Katika utoajiwa tuzo hizo mchezaji wa jumla ni Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa Netball katika timu ya JKT Mbweni.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa akipeana mkono wa pongezi na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti Breweries Ltd,Teddy Mapunda kwa kudhamini tuzo hizo za kuwapa heshima na kuwathamini wanamichezo wetu hapa nchini.Anaeshuhudia kwa nyuma ni Mgeni Rasmi,Makamu wa rais Dr Gharib Bilal.

Mwenyekiti wa bodi ya Serengeti (SBL),Mzee Marck Boman akimkabidhi tuzo mchezaji bora wa kiume wa timu ya Yanga Shadrack Nsajigwa.

Meza Kuu ikiwa imechangamka,hapa ilikuwa ikifurahia jambo kutoka jukwaani.

Mwenyekiti wa chama cha Michezo (TASWA),Juma Pinto akizunguma mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia uto
aji tuzo kwa wanamichezo mbalimbali akiwemo na mwanamichezo bora kwa ujumla usiku huu ndani ya hotel ya Movernpick,jijini Dar.


No comments:

Post a Comment